Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Mimi nipo Dar.
Sijui kama mtaweza kutika Arusha hadi Dar kwa ajili ya kuunganisha liner tu

Bwawa limeshachimbwa.

Liner zimeshanunuliwa tayari.

Shida ni kuziunganisha

Samahani mkuu. Unaweza kunielekeza zinapopatikana liner kwa Dar?
 
Wakuu msaada vipimo vya bwawa la samaki 5000,upana,kina na urefu.
 
Nimelielewa somo mkuu na asante sana kwa elimu sasa je nikitaka kambale wazaliane natakiwa kufanya nini ili wazaliane?
 
Knowledge is power. Get knowledge and increase in wealth. Fish farming is never a shortcut to wealth. You either learn the rudiments and remain in the business or move out of the business for lack of knowledge. farming is ever dynamic. The more you know the better for you.


Tanzania Eco-farm, kwa mara nyingine tena inakuletea somo juu ya ufugaji wa samaki kitaalamu. Bandiko hili leo litazungumzia kuhusu chakula cha samaki, uandaaji na ulishaji.

Upatikanaji wa chakula cha samaki hapa tanzania bado ni changamoto kubwa inayowakumba wafugaji wengi hapa tanzania. Chakula kimekuwa cha gharama kubwa sana kiasi kuwa ufugaji umekuwa biashara inayohitaji mtaji mkubwa sana. Na wengine wamejikuta wameshindwa kufanikiwa kukuza samaki wao kufikia ukubwa unaotakiwa tokana na kushindwa kupata mtaji wa kutosha kulisha samaki wao. Nimeona wafugaji wengine wamekuwa wakijitengenezea chakula wanyewe bila hata ya kufata fomula inayotakiwa kuandaa chakula cha samaki chenye virutubisho muhimu vinavyohitajika kukuza samaki.

Hivi leo ningependa kuzungumzia uandaaji wa chakula cha samaki aina ya kambale kwa gharamu nafuu sana na kufata formula ya kitaalamu katika uandaaji na kuweza kukuza samaki kwa haraka sana.

Crude Protein (CP) ni kirutubisho muhimu kinachohitajika katika chakula cha samaki ili aweze kukuwa, kuwa na afya njema na kumuwezesha asipatwe na magonjwa kirahisi. Husaidia uzalishaji wa hormones na chemical reactions katika samaki na huweza kubadilishwa kuwa sukari au mafuta katika mwili wa samaki endapo kutakuwa na upungufu wa aina nyingine za virutubisho. Bila protein, nutrients nyingine haziwezi kutumiwa/ kufanya kazi au kuwa na umuhimu katika ukuaji wa samaki.

Crude protein ( CP) ni kiasi au kipimo cha protein kilichomo kwenye chakula cha samaki. Kipimo chake huelezewa katika percent (%). Samaki aina ya kambale ili kuweza kukuwa vizuri, chakula chake kinatakiwa kiwe na CP kati ya 35% had 48% kutegemea na ukubwa au stage aliyopo katika ukuaji. Jinsi anavyozidi kukuwa ndivyo kiasi cha CP kinapungua kuhitajika katika chakula chake.

Hivyo basi, Mfugaji kabla ya kuandaa chakula cha samaki anahitaji ajue kiasi cha CP kinachotakiwa kiwe katika chakula cha samaki.

JINSI YA KUKOKOTOA KIASI CHA CP.

Kiasi cha CP katika chakula kinakokotolewa kwa formula rahisi ifuatayo.
CP = ( x/100)y
Where X= asilimia ya CP ya kiungo ( ingradient)
Y= kiasi cha kiungo (ingradient) kg

Baadhi ya Viungo muhimu katika chakula cha samaki vinavyopatikana hapa Tz ni:
Dagaa 65% cp
Uduvi 70cp
Mahindi 8% CP
Mashudu 31% CP
Damu 74% CP
Pumba za mchele laini 12% CP
Soya 47% CP
Karanga 30% CP
Permix

MFANO.
Nahitaji 41% CP katika Kg 100.

CP 35kg pumba za mahindi: 12/100 x 35= 4.2%
CP 20 kg soya:47/100 x 20 = 9.4%
CP 20kg ya karanga : 48/100 x 20/1 = 9.6%
Cp from 25kg fishmeal: 72/100 x 25/1 = 18%.

Hivyo basi jumla ya CP kutokana na mchanganyiko apo juu utakuwa ni:
4.2+9.4+9.6+18 = 41.2%

Mfano wa mchanganiko hapo juu unaweza gharimu kati ya 100,000tsh had 130,000tsh kutegemea na msimu, na eneo husika. Maana yake 1kg ya chakula ni kati ya 1000 had 1300. Hapa ni kuwa gharama imeshuka zaid ya 50% kama ungekuwa unanunua chakula kilichotengenezwa tyari ambacho bei huwa 3000 had 5000 kwa kg.

Huu mchanganiko pia Mkulima anaweza utengeneza na kuwa katika mfumo wa pellets kwa kutumia njia za kienyeji.

Screenshot_20181223-113753_Instagram.jpeg

Tanzania Eco-farm. Ltd inatoa huduma mbalimbali katika secta ya Ufugaji wa samaki kuanzia ujenzi wa mabwawa, ushauri, mafunzo, vifarannga na masoko. Huduma zetu ni bure na bidhaa ni nafuu kabisa. 0759741303 kwa mawasiliano zaid.

Unakaribishwa katika Group letu la whatsup ambalo tunatoa mafunzo ya kitaalamu juu ya ufugaji wa samaki, mbegu, chakula na msoko.
UFUGAJI SAMAKI KIBIASHARA
 
mkiu naomba unieleweshe hapo juu umesema cp ya soya ni 30% ila kwenye mfano inaonyesha cp ya soya ni 47% ( value ya x)
Hii 47 imetoka wapi huku mwanzoni umeandika 30%?
 
mkiu naomba unieleweshe hapo juu umesema cp ya soya ni 30% ila kwenye mfano inaonyesha cp ya soya ni 47% ( value ya x)
Hii 47 imetoka wapi huku mwanzoni umeandika 30%?
Haya sasa mathematician wamekuja watu na comb zao
 
mkiu naomba unieleweshe hapo juu umesema cp ya soya ni 30% ila kwenye mfano inaonyesha cp ya soya ni 47% ( value ya x)
Hii 47 imetoka wapi huku mwanzoni umeandika 30%?
Ni mechanganya. Soya meal ina CP kati ya 47% had 49%. Ilichanganya ya soya ya karanga.

Asante kwa marekebisho. Umeonesha upo makini mkuu. Vzuri sana
 
Back
Top Bottom