Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

M

MZAWA JF

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2014
Messages
2,360
Points
2,000
M

MZAWA JF

JF-Expert Member
Joined Apr 4, 2014
2,360 2,000
Zipo pia boss,tuwasiliane ili uzione baadhi ya tulizo install
Mkuu samahani kwa hili swali, naskia samaki wasipobadilishiwa Maji kwa muda Fulani wanakufa kwa kukosa hewa. Sasa kwa Dodoma ambapo Maji ni ya shida nikifuga si nitatumia pesa nyingi kuliko mapato?
 
M

Malo2

New Member
Joined
Jul 1, 2019
Messages
2
Points
20
M

Malo2

New Member
Joined Jul 1, 2019
2 20
Samaki wa biashara mara nyingi hufikia market size ktk kipindi cha miezi sita (sato zaidi). Kimsingi unatakiwa kuangalia ukuaji wa samaki wako kila wakati ili wafikie market size, sato wanaweza kufikia size hiyo bila taabu sana ukilinganisha na kambale, nikipata muda wa kambale nitauweka hapa. Kama unafuga kwa matumizi binafsi,size inayopendeza macho yako ndio nzuri.


Bwawa la saruji unaweza kulitumia kwa kufugia samaki pia,lakini sharti uwaone watalaam ili wawe na wewe kuanzia ktk hatua za ujenzi. Kumbuka virutubisho toka ardhini haviwezi kuwafikia samaki kirahisi kupitia kuta za saruji.
Kuna mabwawa ya mabanzi na karatasi. Kwa mbeya naweza kupata karatasi wapi kwa anayejua ndg zangu?
 
F

Fideline

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2011
Messages
202
Points
225
F

Fideline

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2011
202 225
Knowledge is power. Get knowledge and increase in wealth. Fish farming is never a shortcut to wealth. You either learn the rudiments and remain in the business or move out of the business for lack of knowledge. farming is ever dynamic. The more you know the better for you.


Tanzania Eco-farm, kwa mara nyingine tena inakuletea somo juu ya ufugaji wa samaki kitaalamu. Bandiko hili leo litazungumzia kuhusu chakula cha samaki, uandaaji na ulishaji.

Upatikanaji wa chakula cha samaki hapa tanzania bado ni changamoto kubwa inayowakumba wafugaji wengi hapa tanzania. Chakula kimekuwa cha gharama kubwa sana kiasi kuwa ufugaji umekuwa biashara inayohitaji mtaji mkubwa sana. Na wengine wamejikuta wameshindwa kufanikiwa kukuza samaki wao kufikia ukubwa unaotakiwa tokana na kushindwa kupata mtaji wa kutosha kulisha samaki wao. Nimeona wafugaji wengine wamekuwa wakijitengenezea chakula wanyewe bila hata ya kufata fomula inayotakiwa kuandaa chakula cha samaki chenye virutubisho muhimu vinavyohitajika kukuza samaki.

Hivi leo ningependa kuzungumzia uandaaji wa chakula cha samaki aina ya kambale kwa gharamu nafuu sana na kufata formula ya kitaalamu katika uandaaji na kuweza kukuza samaki kwa haraka sana.

Crude Protein (CP) ni kirutubisho muhimu kinachohitajika katika chakula cha samaki ili aweze kukuwa, kuwa na afya njema na kumuwezesha asipatwe na magonjwa kirahisi. Husaidia uzalishaji wa hormones na chemical reactions katika samaki na huweza kubadilishwa kuwa sukari au mafuta katika mwili wa samaki endapo kutakuwa na upungufu wa aina nyingine za virutubisho. Bila protein, nutrients nyingine haziwezi kutumiwa/ kufanya kazi au kuwa na umuhimu katika ukuaji wa samaki.

Crude protein ( CP) ni kiasi au kipimo cha protein kilichomo kwenye chakula cha samaki. Kipimo chake huelezewa katika percent (%). Samaki aina ya kambale ili kuweza kukuwa vizuri, chakula chake kinatakiwa kiwe na CP kati ya 35% had 48% kutegemea na ukubwa au stage aliyopo katika ukuaji. Jinsi anavyozidi kukuwa ndivyo kiasi cha CP kinapungua kuhitajika katika chakula chake.

Hivyo basi, Mfugaji kabla ya kuandaa chakula cha samaki anahitaji ajue kiasi cha CP kinachotakiwa kiwe katika chakula cha samaki.

JINSI YA KUKOKOTOA KIASI CHA CP.

Kiasi cha CP katika chakula kinakokotolewa kwa formula rahisi ifuatayo.
CP = ( x/100)y
Where X= asilimia ya CP ya kiungo ( ingradient)
Y= kiasi cha kiungo (ingradient) kg

Baadhi ya Viungo muhimu katika chakula cha samaki vinavyopatikana hapa Tz ni:
Dagaa 65% cp
Uduvi 70cp
Mahindi 8% CP
Mashudu 31% CP
Damu 74% CP
Pumba za mchele laini 12% CP
Soya 47% CP
Karanga 30% CP
Permix

MFANO.
Nahitaji 41% CP katika Kg 100.

CP 35kg pumba za mahindi: 12/100 x 35= 4.2%
CP 20 kg soya:47/100 x 20 = 9.4%
CP 20kg ya karanga : 48/100 x 20/1 = 9.6%
Cp from 25kg fishmeal: 72/100 x 25/1 = 18%.

Hivyo basi jumla ya CP kutokana na mchanganyiko apo juu utakuwa ni:
4.2+9.4+9.6+18 = 41.2%

Mfano wa mchanganiko hapo juu unaweza gharimu kati ya 100,000tsh had 130,000tsh kutegemea na msimu, na eneo husika. Maana yake 1kg ya chakula ni kati ya 1000 had 1300. Hapa ni kuwa gharama imeshuka zaid ya 50% kama ungekuwa unanunua chakula kilichotengenezwa tyari ambacho bei huwa 3000 had 5000 kwa kg.

Huu mchanganiko pia Mkulima anaweza utengeneza na kuwa katika mfumo wa pellets kwa kutumia njia za kienyeji.

View attachment 975215
Tanzania Eco-farm. Ltd inatoa huduma mbalimbali katika secta ya Ufugaji wa samaki kuanzia ujenzi wa mabwawa, ushauri, mafunzo, vifarannga na masoko. Huduma zetu ni bure na bidhaa ni nafuu kabisa. 0759741303 kwa mawasiliano zaid.

Unakaribishwa katika Group letu la whatsup ambalo tunatoa mafunzo ya kitaalamu juu ya ufugaji wa samaki, mbegu, chakula na msoko.
UFUGAJI SAMAKI KIBIASHARA
mkuuu upo vizuri.Ubarikiwe
 
M

mysterious user

New Member
Joined
Feb 15, 2019
Messages
3
Points
45
M

mysterious user

New Member
Joined Feb 15, 2019
3 45
Asanteni sanaa wakubwa kwa kushare this great idea with us...me ni kijana mdoogo ambae nnavutiwa sana na hii business though sijaanza kuifanya bado, nlikua nauliza kwa mtaji wa 500k mpk 700k unaruhusu kuanza na samaki kama wangapi ivi sato?
 
Ailars David

Ailars David

Senior Member
Joined
Jul 6, 2017
Messages
118
Points
195
Ailars David

Ailars David

Senior Member
Joined Jul 6, 2017
118 195
Mkuu samahani kwa hili swali, naskia samaki wasipobadilishiwa Maji kwa muda Fulani wanakufa kwa kukosa hewa. Sasa kwa Dodoma ambapo Maji ni ya shida nikifuga si nitatumia pesa nyingi kuliko mapato?
Kuna mifumo mingi ya kiufugaji
Una weza tumia recirculating system n mfumo ambao maji yanazungushwa na kuchujwa na kurudishwa tena ni mifumo kama RAS na Aquaponics! Ipo iliyo rahisi kabisa na ya garamah na fuu inasaidia sana kuepuka garama Za maji
 

Forum statistics

Threads 1,336,170
Members 512,562
Posts 32,529,430
Top