Ufugaji wa Nguruwe: Fahamu faida, hasara na mbinu bora za ufugaji

SIKUBALIANI NA HESABU ZAKO.
Kwa Nini unasema gharama ya chakula ni sh.1,000,000 ?!!au kwa sababu wewe una shamba ekari 30 za kulima maboga na alizeti ili kuwalisha?!nguruwe mdogo wa kuanzia mwezi mmoja anakula wastani wa kilo 2 kwa siku.atakapofika umri wa kubeba mimba mpaka kujifungua ni wastani wa kuanzia kilo 6 mpaka 10 kwa siku kutegemea na ukubwa wake,akifika wakati wa kunyonyesha atahitaji nusu kilo ya ziada kwa Kila mtoto mmoja anayenyonyeshwa,kama Ana watoto 10 piga nusu kilo Mara 10 alaf ongeza na kilo zake anazokula Kwa siku...ndo umpe ale kwa ujumla kwa siku moja.sasa nguruwe hao 20 ambao wote ni majike na unataka wazae watoto 160 kwa mwaka mmoja!!! Ambao na wenyewe wanahitaji kula Tena!! FIKIRI MARA MBILI.na kabla hujamuuza lazima umpe chakula Cha ziada ili afikie walau kilo 200
Mbaya zaidi umuuze kwa sh.200,000 (laki 2) baada ya kumlisha mwaka mzima!heheh utapata HASARA ya kukutosha.
Hata kama gunia la pumba ni sh.10,000 tu
Na kumbuka nguruwe Hali pumba peke yake Kuna na mchanganyiko wa vyakula na lishe nyingine ambazo ni lazima apate .
Bado madawa na chanjo za kuzuia magonjwa.
Bado vifo vya watoto anaozaa,na kama unawafuga maeneo yenye joto,vifo vinaweza ongezeka zaidi.
Hiyo Milioni 1 haifai kwa lolote kulisha nguruwe.
Na kumbuka jinsi muda unavyozidi kwenda rate ya kuzaa kwa nguruwe huwa inapungua kutokana na genetically reasons kwa hiyo si rahisi kupata nguruwe 1500 kwa miaka 3 la sivyo matajiri wote wakubwa duniani wangekuwa wafugaji wa nguruwe!!! Wafugaji wakuku tu wenyewe wanajua gharama ya chakula ni almost 50% ya pesa zote..sembuse nguruwe.
Sahau kuhusu mil.300 in 3 years!!!
Usitupe False hopes!!!
GET YOUR FACTS STRAIGHT.
Chakula cha nguruwe sio less ya 70% ya gharma nyingine asee! Labda kama kuna sehemu unakusanya makombo ya vyakula
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom