Ufugaji wa Nguruwe: Fahamu faida, hasara na mbinu bora za ufugaji

Hakufuga kibiashara.... haukuwa na hasira ya uwekezaji.... haukufata taratibu sahii.... mwanzo mgumu.


Note:

Tafuta mbegu sahihi... mara nyingi hupatina mission kwa watasha.

Eneo la kutosha na lenye maji na sehemu ya bustani.

Nunua stock ya kudumu ya vyakula mbalimbali... na tengeneza rough garden ya carbage n.k kwa ajili ya mifugo...

Toa chanjo ma tiba kila inapohitajika....

Usipende kuuza nguruwe au vifaranga kila unapopata shida...

Maximum... ukianza na nguruwe 20... ndani ya miaka miwili utakuwa na nguruwe 200 wa umri tofauti...

Utauza mia kwa gharama zaidi ya million 50.

Misosi ni million 10 tu.

Unapata vp hasara.

Sent from "La -Vista"
Watu wanafuga kienyeji afu wanataka faida,kitimoto ni formula tena ya kuwapishanisha na target ni uwingi kinyume na hapo ni hasara
 
Mimi ni mfugaji kwa miaka minne sasa Avatar yangu inanitambulisha pia. Sijaona faida ya mnyama huyo isipokuwa hasara. Ana gharama za malisho na rahisi sana kudumaa...Kwa ufupi hachelewi kukosewa katika ukuaji.

Unaweza kujaribu ukajionea mwenyewe ingawa wengi humu ambao hawafugi watakuja kukupa ushauri wa kwenye vitabu.
Mimi kwa sasa nafuga kama huduma si faida tena kwakuwa mabanda nilishayajenga ya kisasa hayawezi kukaa hivi hivi.
Utakuwa unakosea kwenye kanuni za ufugaji bora.Kwanza elewa kuwa faida kubwa ktk ufugaji wa huyu mjamaa ipo kwenye watoto, hivyo hakikisha kuwa unafuga nguruwe anayezaa Sana,kuanzia kumi na kuendelea,watoto watasaidia kupunguza running cost yao. Baada ya hapo jitahidi kupata mbegu inayokua haraka na yenye HFC-ratio kubwa. (High Feed Conversional ratio). Angalau basi kwa haya yatakusaidia.
 
Mimi ni mfugaji wa nguruwe ndo nimeanza ufugaji huu nina nguruwe 9 majike 7 madude 2 naomba mwenyewe elimu nzuri juu ya ufugaji huu na idadi nzuri ya kuanza nayo anisaidie ili niweze kupata faida.
 
Karibuni sana katika ufugaji wa nguruwe nina banda kubwa la mabanzi bagamoyo kiromo lenye tayari umeme wa solar na maji ya kisima na tank lenye litre 5000ltr.ninakodisha 650,000 kwa mwezi.atakayekuwa interested tunapenda tuingie mkataba wa mwaka moja.mawasiliano zaidi whatssap 0756661761 au 0627840045.karibuni sana.





















 
Mm hawa wadudu nawafuga..na kwa kwl ninawaheshimu sn...
Wafugaji wengi wanakata tamaa sababu wanafanya ufugaji km ni shughuli ya kupoteza muda...hata kama wewe ni muajiriwa,wekeza juhudi zako nyingi ktk ufugaji unaoufanya...tusikate tamaa..ht huko makazini kuna makandokando yake ambayo kimsingi hatuyakatii tamaa sababu mwisho mwezi tuna uhakika...
Ukitaka kuona faida ya nguruwe fuga wengi...ili ukiuza uione hela yake...
Lkn pia usitegemee tuu kuwauza wakiwa hai...ongeza thamani...tengeneza soseji..
Niko mbioni kuingia ktk soko la soseji maana huku kwa uchunguzi nilioufanya bd hakuna competition kubwa sn...
Kwa yeyote mwenye ABC Za utengenezaji wa soseji tutafutane

Sent using Jamii Forums mobile app
Great idea. Ninafikiria hivyo hivyo. Kwa mwanza.Kimsingi ukienda nchi za wenzetu utaona watu wanafurahia nyama hapa kwetu tunauziwa mifupa. Ukiweza kuongea thamani ukatengeneza pork products like sausage...beacon...pork ribs na fillets unauza.
 
Uko kama mimi yaani. Bora yako labda ni karibu na nyumbani.... mimi ni mbali kidogo na home. Sasa ukute chakula kimeisha, (nimeajiri zee sumbufu ndo linawahudumia.) Litapiga simu hata saa 8 ya usiku au lipate matatizo ya familia yake. Utatamani kulia.... mpaka saivi nawaona nguruwe kama simba
pole sana mkuu! Kama naliona hilo zee linavyokusumbua kudai msosi
 
Mm hawa wadudu nawafuga..na kwa kwl ninawaheshimu sn...
Wafugaji wengi wanakata tamaa sababu wanafanya ufugaji km ni shughuli ya kupoteza muda...hata kama wewe ni muajiriwa,wekeza juhudi zako nyingi ktk ufugaji unaoufanya...tusikate tamaa..ht huko makazini kuna makandokando yake ambayo kimsingi hatuyakatii tamaa sababu mwisho mwezi tuna uhakika...
Ukitaka kuona faida ya nguruwe fuga wengi...ili ukiuza uione hela yake...
Lkn pia usitegemee tuu kuwauza wakiwa hai...ongeza thamani...tengeneza soseji..
Niko mbioni kuingia ktk soko la soseji maana huku kwa uchunguzi nilioufanya bd hakuna competition kubwa sn...
Kwa yeyote mwenye ABC Za utengenezaji wa soseji tutafutane

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hongera sana kwa ufugaji wako na inaonekana unao uzoefu mkubwa kwenye hii biashara. Mimi ndo najiandaa kuanza ufugaji. Je unaweza kunipa mawili matatu juu ya banda zuri la kufugia?
 
Biashara ya nguruwe uifugiw maporini au vijijini gharama ya matunzo au malisho ni ndogo..kwa mjini haina maslahi kupotezeana mda na kupoteza pesa zako..
Nakushauri fuga kuku walipa zaidi kuliko biashara ya nguruwe au ng'ombe.
Angekuwa anakula majani hiyo hoja yako inekuwa na mashiko sasa ngurue alacho hupatikana mjini ukimfuga bush huoni itakuwa garama kusafirisha chakula?
 
Habari mpenzi ,msomaji leo nataka nikuoneshe vitumuhimu katika ufugaji wa nguruwe kwa kua ni moja kati ya wanyama wenye faida sana.




“Ufugaji wa Nguruwe ni lazima uwe wa kisasa ili kupata nguruwe bora.
Jamii nyingi hapa Tanzania huchukulia nguruwe kama mnyama mchafu na asiyefaa kuwa karibu naye na hata kwa matumizi kama lishe. Zaidi, nyama yake inapendwa na haina madhara kwa afya na inapendekezwa kuliwa zaidi kuliko nyama nyekundu. Unaweza kuanzisha mradi wa nguruwe kwa gharama ndogo lakini baada ya kipindi cha miezi tisa tu ukaanza kujipatia kipato kutokana na ufugaji huo.

Ufugaji
Nguruwe hawa itaji mtaji mkubwa sana ili kuwafuga,hata wakulima wadogo wanaweza kumudu kufuga nguruwe kwa kua huitaji mtaji mkubwa sana ili kuwa fuga na pia huleta faida kubwa pale wanapo fiki hatua ya kuya wakubwa

BANDA
Nguruwe wanahitaji kuwa na banda lililojengwa kwa sakafu ya zege au ukachanganya mchanga na siment unaweza chagua kulingana na uwezo wako
. Ukubwa wa banda unategemeana na idadi ya nguruwe unaotaka kufuga. Mita 3 kwa mita 2.5 zitawaweka nguruwe 8-10 wanaonenepeshwa kwa soko au nguruwe jike mmoja na nguruwe ndume mmoja.

CHAKULA
Uzuri wa nguruwe hua hawana gharama kubwa sana katika kuwalisha. Unaweza kuwalisha kwa kutumia majani laini ya aina mbalimbali,pumba.napia unaweza kuwalisha na mashudu aina ya Wheat Poland,au mabaki ya chakula chabinadamu.japo kua kunakua na aina maalum kwa ajili ya chakula kwa ajili ambacho unaweza kuwalisha kilo 1-2 kwa siku


KUPANDISWA
Nguruwe wakike yan sow ka lugha ya kitaalam anapandishwa pale anapo ingi kwenye joto kama mnyama yoyote yule.
na unaweza kujua kama ameingia kwenye joto pale anapokua msumbufu/lestless, anakua anawapanda wenzae,uteute mweupe unatoka kwenye uke wake,na pia vulva inabadilika nakua nyekundu.

KUZAA
Nguruwe hubeba mimba kwa kipindi cha siku 114 yan miez mitatu na na siku kadhaa.
Nguruwe mmoja ana uwezo wa kuzaa watoto 6 hadi 14 kwa mara moja. Watoto wa nguruwe (piglets) huanza kula chakula cha kawaida wanapofika umri wa mwezi mmoja na nusu mpaka miezi miwili. Endapo nguruwe watapata matunzo mazuri, baada ya miezi 6 wanakuwa na uzito kati ya kilo 50-70 na wanaweza kuuzwa.


JINSI YA KUWATUNZA
Baada ya nguruwe kuzaa anatakiwa kupatiwa chakula na maji ya kutosha cha kutosha na ili kupata maziwa ya kutosha kwa ajili ya watoto wake. Watoto wa nguruwe wachomwe sindano ya madini ya chuma (Iron injection) baada ya siku2 au3 toka kuzaliwa. Hii ni muhimu sana vinginevyo wanaweza kufa wote. Kata meno (tooth clipping) baada ya miezi mitatu. Unaweza kuhasi madume (castration) baada ya miezi miwili.


BAADHI YA MAGONJWA YA NGURUWE
Kila siku magonjwa mengi kwa binadamu na wanyama yanatokea.lakinm kunamagonjwa ambayo kama mfugaji lazima uyajue kwakua ndio yanayo jitokeza.


UGONJWA WA MIGUU NA MIDOMO
Ugonjwa huu huathiri midomo na miguu ya nguruwe.
Ni ugonjwa ambao hushambulia nguruwe mara kwa mara hasa wasipokuwa na matunzo mazuri. Ugonjwa wa miguu na midomo, hudhoofisha nguruwe kwa haraka sana, ikiwa ni pamoja na kupungua uzito.


Chanjo: Chanjo yake huitwa FMD VACCINATION nautolewa kila baada ya mwaka mmoja

Dalili,dalili zake miguu na midomo ya nguruwe inabadilika na pia nguruwe anadhoofika
Tiba: Ugonjwa huu hauna tiba halisi. Inapotokea nguruwe wakawa wameshambuliwa kinachofanyika ni kutibu magonjwa nyemelezi kwa kutumia antibiotics.


HOMA YA NGURUWE(SWINE FEVER)
Ugonjwa huu unasambaa kwa kasi kama mmoja akiambukizwa wengine pia wataambukizwa na kufa

Dalili, nguruwe anakua na vidonda na vitu kama vibarango mwili mzima pia mdomo na masikio yanabadilika rangi nakua mekundu.
Chanjo: Ugonjwa huu hauna chanjo wala tiba. Kinachofanyika mlipuko unapotokea ili kuwa salama ni kuwateketeza nguruwe wote walioathirika na kuanza upya. Unaweza kuteketeza kwa kuwachoma moto.


Muhimu: Baada ya kuwateketeza nguruwe wagonjwa, safisha banda kisha nyunyiza dawa aiana ya Acon au Ectomin, na uache banda wazi kwa kipindi cha wiki moja kabla ya kuweka nguruwe wengine kwa kua huu ni viral disease


UGONJWA WA MAPAFU (PNEUMONIA)
Ushambulia sehemu za koo na mapafu ya nguruwe,Ugonjwa huu husababishwa na bacteria (Secondary bacterial), joto kupita kiasi, vumbi na gesi inayotokana na madawa makali.

Dalili, nguruwe hukooa na kupumua kwa shida sana
Tiba: Homa ya mapafu kwa nguruwe inatibika kwa kutumia antibiotics. Pamoja na kuwaweka wanyama sehemu safi, isiyo na baridi kali au joto la kupitiliza kiwango.


KIMETA(ANTHRAX)
Huu ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria wanaojulikana kama Bacillus anthracis, wadudu hawa wanabaki kuwa hai kwa muda mrefu na wanaweza kuwa kwenye udongo wakiwa hai kwa kipindi cha miaka mingi

Tiba: Unaweza kutibu nguruwe wako kwa kutumia dawa aina ya Penisilin au Oxytetracycline.


Muhimu:nguruwe alie kufa kwa kimeta usimshkew kabsa kwa sababu hata binadamu anaupata huu ugonjwa, chimba shimo mbali na watu mwagia mafuta ya taa ndani ya hilo shimo kisha fukia mzoga.,
dalili ya nguruwe alie kufa kwa kimeta damu hua aigandi na pia hata nzi hawasogei kwenye mzoga kwa hiyo kua makini.


AINA ZA NGURUWE

Largewhite



characteristics

  • hii ndio aina kubwa kabsa kuliko aina zote tatu
  • anakua na mwili mweupe pote
  • masikio yake yamesimama wima
  • ni mama mzuri
  • anakua na mdomo mbinuko
landress

characteristics
  • anakua mweupe pia au anaweza kua na mabaka meusi
  • ni mkubwa kuasi
  • masikio yake yamelala
saddleback



characteristics
  • anakua mweusi ila anakua na mkanda mweupe shingoni
  • pia ni mpole
  • anamasikio ya kulala
  • anakua mkubwa kiasi

natumaini umejifunza kitu kwa elimu zaidi usisite kunitafuta
rubabaimani@gmail.com
+255764148221
+255653882567
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom