Ufugaji wa Nguruwe: Fahamu faida, hasara na mbinu bora za ufugaji

741ff5d5963a9097fd5f7fdbce4771ef.jpg
 
soko la nguruwe linalipa sana. me najivunia sana kuwa mfugaji. chakula ni chamuhimu sana.

awali sikuzingatia chakula lkn baada ya kuanza kuzingatia aisee hii midude inazaa.

nilianza na nguruwe 4 lkn hadi sasa nina 48 na wengine kama 200 niliuza
9003fc9787d32d305875e1b43a4a3766.jpg
 
Tangu 2009wazazi wang wamekua wakifuga nguruwe kwa mazoea, tupo (mahina) mwanza.
Now nimeludi nyumbani (mwanza) nataka nifanye revolution ya ufugaji nyumbani kwetu.
Kuna nguruwe majike 8 wanalishwa pumba za mchele two times a day.
Wengine manyoya yao yamesimama matumbo yameshuka.
Tu endelee kupeana updates za nguruwe
Hao wanaminyoo wachome sindano za ivermactin
 
View attachment 324772

- Nguruwe watoto 20 @ 20000 = 400000
- Banda la mabanzi=1,000,000
- Chakula = 1,000,000
- Dawa= 200000

After 1yr: Nguruwe 20 watazaa vitoto kama 160,utachakuwa vitoto jike 100,
mama zao wote watauzwa, huku shambani kwetu nguruwe
mkubwa ni Tsh 200,000 tu, utapata 4,000,000.

After 2yrs: Nguruwe 100 wanaweza kuzaa 700. Kati ya 700 chagua majike 500,(unaweza kuuza watoto dume ukanunua jike).

Year 3: Nguruwe 500 watazaa watoto 3500, chagua watoto 1500 tu
Kutoka hapo unamentein Number 1500, kila mwaka unaweza kuuza
watoto zaidi ya 3000, na nguruwe wakubwa 1500.
1500*200000= Tsh 300,000,000/= kwa mwaka
Nusu ya hiyo pesa ni gharama zingine, unabaki na 150mil.
Welcome to the club

Kabla hujajitumbukiza kaone mifano, au nenda sokoine ukaonane na wataalamu.

Kila mwaka nalima Mahindi, alizeti, maboga ekari 30 kwa ajili ya chakula cha nguruwe tu.

Nakupenda saana mpwa..









==========

USHUHUDA

======================================================

Naomba namba yako ya simu
 
Nguruwe hata umuweke wapi minyoo haitomuondoka hatta siku moja. Huyu mnyama anakula mavi yake mwenyewe Vipi utaweza kumuepusha na minyoo kwa kutumia hizo drinkers?
Kichwa cha muharabu si rahisi kuelewa jambo. Hata kikielewa bado kinakuwa kizito kukubali
 
Mkuu Mzizimkavu sitetei kula nguruwe ila naongea kitu ambacho watu wote wanatakiwa wakijue. Mimi siongei pumba, nitake radhi tafadhali we ni mtu wa heshima kwenye hili jukwaa. Kwenye life cycle ya tinea kuna host wawili, nguruwe na binadamu au mnyama yeyote anayekula nyama ya nguruwe. Nguruwe anakula majani au uchafu wenye mayai ya taenia ambayo yataanguliwa tumboni mwake. Lavae watapierce kwenye utumbo na kuingia kwenye mfumao wa damu mpaka kwenye misuli,maini,figo,ubongo nk ambavyo vitaliwa na binadamu na kugeuka na kuwa adult worms ndani ya utumbo wa binadamu. Hao wadudu wataendelea kuwepo tumboni na kufyonza nutrients na kusababisha matatizo mengine ya tumbo. Watataga mayai na pingili zitatolewa kupitia mavi ambayo ukinya popote yanasombwa na maji na cycle inaanza tena. Ikitokea binadamu akala mayai kupitia mboga, maji, matunda yataanguliwa tumboni mwake na cysticerci watakaa kwenye maini, uboogo, figo, misuli ya binadamu. Hii ndo inaleta cysticercosis ambayo husababisha kifafa. Kula nyama kunasababisha mzunguko uendelee na chance za kupata cysticercosis kuongezeka lakini siyo ukila nyama unapata cysticercosis badala yake unapata taeniasis. Ndo maana nikasema usishangae mtu asiyekula nguruwe kupata ugonjwa huo katika maeneo yenye prevalence kubwa. Naomba unisome vizuri na kunielewa.!

Bana weee nguruwe watu wana ogopa ila ukimwi hawaogopi pia wake za watu wana kula dunia hii

Mi kitimoto nimeanza kula tangu mtoto ila sijawai kumbana na ugonjwa
 
Kichwa cha muharabu si rahisi kuelewa jambo. Hata kikielewa bado kinakuwa kizito kukubali
Maneno ya Busara kutoka kwa fundi wa chupa!
Teh teh teh.

Endelea kushona hizo kabati kamanda. Siku ukianza kushona suruali tuwasiliane.
Ahsanta.
 
Kwa muda nimetafuta formula ya chakula kwa ajili ya kulisha nguruwe bila mafanikio. Leo nimefanikiwa kupata hii formula toka chuo cha kilimo na mifugo Tengeru, Arusha. Kutengeneza kilo 100 changanya hivi

Pumba ya mahindi 40kg
Pumba ya ngano 35kg
Mashudu ya alizeti 15kg
Dagaa waliosagwa 5kg
Chumvi 1kg
Pig mix 1kg
Mifupa iliyosagwa 1kg
Chokaa 2kg


Mchanganyiko huu ni kwa nguruwe wa umri wote.
Tafadhali share kama una formula tofauti kwa ulishaji wa nguruwe


Piglets 0.5kg/day.
Weaners 1.0 kg/day
Growers 1.5kgs/day
Finishers 1.5 - 2kgs/day.
Pregnat and lactating sow 3 kgs/day
Boar 2.5 kgs/day.

~piglets ni watoto wa nguruwe,
~weaners ni nguruwe walioachishwa kunyonya (after 8 weeks of age), ~Growers ni nguruwe wanaokuwa (4months of age),
~Finishers ni nguruwe walofikia umri wa kutolewa/kuchinjwa ( 7-9months of age). ~Sow ni nguruwe jike ambae ameshazaa na
~boar ni nguruwe dume ambaye hajahasiwa.
 
  • Thanks
Reactions: Kop

Similar Discussions

Back
Top Bottom