Ufugaji wa Nguruwe: Fahamu faida, hasara na mbinu bora za ufugaji

Amoeba

JF-Expert Member
Aug 20, 2009
3,289
781
1591269151625.png


- Nguruwe watoto 20 @ 20000 = 400000
- Banda la mabanzi=1,000,000
- Chakula = 1,000,000
- Dawa= 200000

After 1yr: Nguruwe 20 watazaa vitoto kama 160,utachakuwa vitoto jike 100,
mama zao wote watauzwa, huku shambani kwetu nguruwe
mkubwa ni Tsh 200,000 tu, utapata 4,000,000.

After 2yrs: Nguruwe 100 wanaweza kuzaa 700. Kati ya 700 chagua majike 500,(unaweza kuuza watoto dume ukanunua jike).

Year 3: Nguruwe 500 watazaa watoto 3500, chagua watoto 1500 tu
Kutoka hapo unamentein Number 1500, kila mwaka unaweza kuuza
watoto zaidi ya 3000, na nguruwe wakubwa 1500.
1500*200000= Tsh 300,000,000/= kwa mwaka
Nusu ya hiyo pesa ni gharama zingine, unabaki na 150mil.
Welcome to the club

Kabla hujajitumbukiza kaone mifano, au nenda sokoine ukaonane na wataalamu.

Kila mwaka nalima Mahindi, alizeti, maboga ekari 30 kwa ajili ya chakula cha nguruwe tu.

Nakupenda saana mpwa..

UZOEFU WA UFUGAJI WA NGURUWE WENYE FAIDA

Natambua wapo watu wengi ambao imani zao zinaruhusu wanatamani kufanya mradi wa ufugaji nguruwe wenye faida.Labda wengine wamejaribu bila mafanikio.Kwa uzoefu wangu ( refer thread yangu Mbegu nzuri ya nguruwe sasa inapatikana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers ndivyo waweza fanya kupata mfanikio.

1. Kwanza tambua hii ni agri-business,basi kama business nyingine inahitaji usimamizi wa kutosha. Watu hudhani ukianzisha mradi na kuweka kijana wa kuwalisha basi unangojea faida tu. Ni vema ukaelewa mahitaji ya hao wanyama (chakula,usafi,malazi,tiba na jinsi ya kuzuia magonjwa) na wewe sasa ndio uwe mwalimu wa herdman wako

2. Tambua faida inatokana na aina bora ya mbegu na malezi. Nia ni kuwalea wanyama wakue kufikia uzito wa soko kwa muda mfupi.Kwa kawaida nguruwe huuzwa kwa nyama akiwa na uzito kuanzia 50kg. Shambani kwangu huuzwa kuanzia miezi 5.

3. Waangalizi(herdmen) ni watu muhimu sana kwako.Ni lazima wafundishwe vizuri na maslahi yao yaangaliwe kwa makini.

4. Nguruwe akiugua atibiwe mara moja. Nguruwe ni mnyama ambae haugui kirahisi akilelewa vema unless kama kuna outbreak ya ugonjwa(kama swine fever). Mara mojamoja huugua inabidi herdman awe na uwezo wa kugundua mapema na mnyama apewe tiba mara moja. Ukiwalea vizuri muda mwingi wanahitaji chanjo tu za minyoo na ukurutu.

5. Nguruwe walishwe ration(balanced feed) sio pumba tu au masalia ya jikoni. Tambua mahitaji ya chakula ya nguruwe (protein,wanga,mafuta,madini,vitamin) na hakikisha mchanganyiko unaofaa kwa umri husika wa nguruwe.Shambani kwangu chakula kikuu ni mahindi/mtama,pumba za mahindi na mpunga,mashudu ya alizeti, ambayo tunalima hapo shamba.Pia huchanganya madini (nguruwe mix) na mifupa/chokaa

6. Tambua gharama kubwa ya ufugaji ipo kwenye chakula (atleast 70%). Kwa wastani nguruwe mkubwa anahitaji 2kg/siku. Kwa hiyo kumlea nguruwe mmoja hadi miezi 6 anahitaji 240kg(miezi 2 ya kwanza huwa ananyonya)

(a) ukininunua chakula ambacho tayari kimechanganywa gharama ni kama tshs 600/kg
(b) ukinunua vyakula na kuchanya mwenyewe gharama ni kama tshs.400/kg
(c) Ukilima vyakula na kuchanganya mwenyewe gharama ni kama tshs 150-250/kg

Hizo ni gharama za wastani kwa morogoro na Dar es salaam.Utaona kama waweza kulima mazao kwa ajili ya mifugo wako gharama inapungua sana. Nguruwe hula pia vyakula vingine kama mihogo,majani,viazi vitamu,maboga etc. Angalia vyakual rahisi kwa mazingira unayofuga. Faida yako ipo kwenye kuuza nguruwe wa nyama. Wanunuzi wa mbegu sio wengi na sio consistent. Kwa hiyo itakuchukua a minimum ya miezi 6 kuanza kupata faida kutoka kwenye mradi wako.Huu ndio ukweli. Lengo ni kuuza idadi fulani ya nguruwe Kila mwezi. Kwa mfano ingalau nguruwe 20 kila mwezi.Unadhani unahitaji nguruwe wangapi kwa wakati mmoja kufanikisha hilo???

8. Soko la nguruwe ni kubwa na linazidi kukua. Walaji wengi wapo Dar es salaam. Waweza kuuza live hapo shambani au ukapeleka mwenyewe machinjioni inategemeana na soko lipo mbali kiasi gani. Nguruwe wa miezi 6 anaweza kukuingizia tshs.200,000-300,000 kutegemea na namna ulivyouza na uzito 9.Unaanzaje kufuga kibiashara? Mfano.

(a) Faida ndani ya miezi 6,na kuuza nguruwe 20 kila mwezi.
Nunua nguruwe jike wenye mimba uzao wa 2 ; wa2 mimba miezi 3;wa2 miezi 2 na wa2 mimba mwezi1,wa2 ambao ndiowamepandwa na wa2 wenye umri wa miezi 6. Nunua kwa mfugaji mwenye mbegu inayoanza kuzaa mapema.

Ukinunua wa uzao wa kwanza namba inakuwa nguruwe 3 badala ya 2 kwa sababu uzao wa kwanza watoto ni wachache,6-9.Pia unahitaji dume mzuri mwenye umri wa miezi 8 au zaidi.Kwa namna hii kila mwezi nguruwe wa2(au 3) watazaa watoto sio chini ya 20. Utaanza kuuza mbegu ndani ya miezi

2.Na baada ya miezi 6 utauza nguruwe sio chini ya 20 kila mwezi kwa nyama
Nguruwe jike mwenye mimba waweza kumpata kwatshs350,000-400,000
Mauzo 4-6m kila mwezi. Neti profit itategemeana na gharamaza chakula kama nilivyo ainisha awali.

Shambani kwangu tunawaachisha watoto kunyonya wakiwa na week6 na jike hupata joto na kupandwa tena ndani ya siku 3-7. Hivyo nguruwe wetuhuzaa mara 2.5 kwa mwaka. Watoto huwauza wakiwa na miezi 2 kwa 45,000-60,000 kutegemeana uzito

(b) Kama utaanza kufuga nguruwe watoto wenye miezi 2?!
Ina maana utaanza kuuza nguruwe wa nyama baada ya miezi isiyopungua 14.

Pia utahitaji kuwafanya nguruwe wako wapate mimba kwa groups ambayo inahitaji uzoefu wako na herdman. Utahitaji pia dume lenye umri wa miezi12 au zaidi. Pia kwa mtu anaeanza ufugaji inasumbua kidogo. Lakini ni nafuu kidogo interms of upfront capital though gharama za ufugaji zinaWEZA kuwa kubwa. Utahitaji kuanza nao wengi pia ili kupata faida na utahitaji kufuga muda mrefu kama nilivyoeleza hapo juu.

Kama una mpango wa muda mrefu na mtaji wa kugharamia chakula na mengineyo kwa muda mrefu,hii ni namna nzuri pia.

Kwa mtu anaetaka kufuga kibiashara,mie humshauri option 8(a) hapo juu
Shambani kwangu Morogoro kwa sasa nguruwe wa 2 au 3 wanazaa kwa mwezi. Kuanzia November nguruwe 5-7watazaa kwa mwezi.

Hope hii itawasaidia watakaopenda kujaribu hii project. Ni muhimu kutembelea mfugaji halisi kupata uzoefu kabla ya kuanza ufugaji.

NYONGEZA1
Mojawapo ya vitu watu wanakosea wakati wa kuanza ufugaji wa nguruwe ni uchaguzi wa mbegu bora.Wengi anapotembelea mtu anaefuga na kukuta nguruwe wakubwa wanapata hamasa bila kuuliza maswali muhimu yatakayomsaidia kujua kama mbegu anayoona inafaa.

Mtu anaefuga kibiashara huwa na:majike na dume(au madume kutegemea na idadi ya majike).Lengo ni kuzalisha nguruwe wa kutosha watakaokua haraka na pia kuwa na nyama nzuri(isiyo na mafuta mengi) wakati wa kuuza akiwa na miezi 6 au 7.Ni vema basi ukjua sifa za jike na Dume!

Dume:iwe mbegu inayokua haraka na kuzalisha nyama nzuri.unapochagua asiwe na ulemavu wowote na awe na matiti 12 au zaidi. Large white,duroc,hampshire na crosses zake zinafaa.Ukiweza kupata first cross za duroc au hampshire ni wazuri zaidi kuwatumia kama terminal sire(dume wa kuzalishia nguruwe wako wa mauzo)

Jike:awe kutoka mbegu zinazozaa watoto wengi na pia uwezo mzuri wa kulea watoto.Awe na matiti 12 au zaidi.ni vema kutoka kwenye crosses za largewhite na landrace.Pia saddle back na crosses zake.

Kwa leo ni hayo.nitaendelea ku-update hii thread ninapokuwa na muda kwa topic mbalimbali.Ninatambua kuna breeds nzuri zaidi kama camborough,etc.nilizoelezea hapo ni breeds unazoweza kupata kirahisi humu nchini.

mawasiliano:0789412904,simu isipopokelewa andika msg ,utapigiwa

Pia angalia Mbegu nzuri ya nguruwe sasa inapatikana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

HABARI ZA 2016.
NNA WATAKIA UFUGAJI WENYE MAFANIKIO WALE WOTE WALIONUFAIKA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE NA UZI HUU!2016 UWE MWAKA WA NEEMA KWENU!

Mfumo wa Pig Innovation Production System (PIGS)

Wakati nnafikiria namna nafuu ya kufuga nguruwe wengi kwa wakati mmoja nikakutana na mfumo unaitwa Pig Innovation Production System (PIGS).

Mfumo huu bunifu unatumiwa sana philipines kwa kuwa mnamuwezesha nguruwe kufanya vitu anavyopenda kufanya naturally ambavyo ni rooting,wallowing na socialization.Ili nguruwe akue haraka na kuwa productive lazima apate chakula na mazingira muafaka.

PIGS ina manufaa yafuatayo
1.Ni nafuu sana ujenzi wake
2.Humpa nguruwe mazingira natural kuweza kukua vema
3.Huwezesha wananyama wengi kukaa sehemu moja
4.Ni rahisi kufanya usafi na mabanda hayana harufu

Shambani kwangu hutumia mfumo huu kuzalisha market pigs i.e nguruwe nnao wakuza na kuwauza kwa nyama.

Katika mfumo huu nguruwe mmoja huhitaji mita za mraba 1-1.5,Hivyo banda la 5mx5m lilaweza kulea nguruwe 15-20.

Hivi ndivyo linavyojengwa(angalia picha ya kwanza)

1.msingi wa tofali au mawe na miti/mabanzi.

2.upande mmoja kwa upana wa 30cm na partition za 25-30cm ni vya kulishia chakula ili kila mnyama apate nafasi

3.upande wa pili ni bwawa la kuogea la upana wa 0.7-1m ili nguruwe akitaka kujipooza anafanya hivyo

4.katikati panachimbwa 60cm-100m na kujazwa mapumba/malamba au nyasi Kwa ajili ya wanyama ku root au kupumzika

Mfumo huu ni very cost effective,banda la namna hiyo hujengwa kwa around 1.5m shambani kwangu.Ni matumaini yangu itawasaidia wanaopata shida ku design banda ufugaji nguruwe kwa ajili ya mauzo

Picha za Banda langu

Baada ya kupata idea ya ufugaji kitimoto hapa JF niliamua kutafuta zaidi namna ya ufugaji wa hawa kitimoto.

Niliamua kwanza kutembelea wafugaji wa kuu wa kitimoto hapa morogoro, ambao ni SUA , Magereza Kingulwira na Pangawe kwa Mkorea.

Nilivutiwa zaidi na Mkorea wa pangawe kwani yeye anafuga kiasili na kutunza mazingira. baada ya hapo niliamua kuingia mtandaoni na kuona huko korea wanafugaje hawa kitimoto.

wanafuga bila ya kuweka sakafu , chumba anachoishi huanza kwa kuchimba chini cm 100 - 120 na humo ndani ya shimo unaweka majani makavu, pumba za mpunga na randa za mbaokwa kuchanganya ujazo wa cm 30 -40 na nguruwe huishi juu ya mchanganyiko huu,hapo hakutakuwa na harufu ya aina yeyote toka ndani ya banda.

Pia ufugaji huu hauhitaji usafishaji wa banda kwani kinyesi hujichanganya na mchanganyiko uliowekwa huja kutolewa baada ya miaka 3 kwa kupata mbolea iliyobora kabisa kwa kilimo cha aina yeyote.

View attachment 131822

Kwangu mimi nilianza na ngutuwe 30. kumi madume ya kuchinja, 2 madume ya mbegu na 18 majike ya kuzalisha na mpaka sasa yote yanamimba tayari. hapa nakuonyesha ufugaji huu ulivyo kwa namna mbalimbali.

View attachment 131831View attachment 131834View attachment 131836View attachment 131835View attachment 131838View attachment 131839View attachment 131840View attachment 131841View attachment 131842View attachment 131843View attachment 131844View attachment 131846View attachment 131849View attachment 131848View attachment 131847

Pamoja na kuwa mpaka sasa ninamuda wa miezi 6 ya ufugaji lakini nimeona tofauti kadha katika ufugaji wa aina hii

1. Gharama ndogo za uendeshaji kwani mpaka sasa nina mfanyakazi mmoja tu na anawamudu vizuri

2. zaidi ya kuchoma dawa za minyoo hakuna dawa nyingine ninazowapa na hawajapata gonjwa lolote hii ni sababu ya kuishia kiasili kwa kunusa udongo ambao wakolea wanasema unampunguzia magonjwa

3. Naishi ndani ya kijiji na nimezungukwa na watu wa dini na imani tofautitofauti lakini sijawahi pata lalamiko lolote kwani hakuna halufu inayotoka na nivigumu hata kwa bahati mbaya nguruwe kutoka nje maana anaishi ndani ya shimo.

4.Nimeweza vuna maji mengi toka kwenye paa la nguruwe na kuhifadhi zaidi ya lita 100,000

5. Kwakuwa pia nalima ninauhakika wa mavuno mazuri yanayotokana na mbolea ninayopata kwenye kitimoto hawa kiasi cha kuweza kuwalisha kwa mwaka mzima.

kwa manufaa haya naweza sema mazingira yangu nayatunza vizuri kutokana na ufugaji wa aina hii
Ebarhad

Ugonjwa wa Nguruwe unaosababishwa na tegu (cysticercosis)

Tegu (Tapeworm) ni aina mojawapo ya minyoo inayosababisha ugonjwa unaojulikana kitaamu kama Cysticercosis na hii inatokana na kuwepo kwa viuvimbe vingi ndani ya viungo vya mwili vilivyojaa majimaji. Aina ya tapeworm

inayosababisha ugonjwa huu inajulikana kwa jina la kisayansi kama Taenia solium. Hatua ya lava iitwayo cysticercus ndiyo yenye madhara na ndo kiini cha jina la ugonjwa huu. Tegu wakubwa ambao mara nyingi wana urefu zaidi ya mita

moja hukaa kwenye utumbo mwembamba lakini ni mara chache sana wanaweza wakasababisha ugonjwa. Madhara yaletwayo na ugonjwa huu ni makubwa ikiwemo ya kiuchumi kwa vile nyama ya nguruwe mwenye ugonjwa hutupwa yote, lakini pia ugonjwa huleta mdhara makubwa umpatapo mwanadamu. Ugonjwa huu upo sehemu mbalimbali za

Tanzania na madhara yake yamekuwa ni makubwa situ kwa wafugaji bali hata kwa walaji wa nyama ya nguruwe. Tafiti nyingi sana zimefanywa na wataalamu kutoka SUA katika kitivo cha tiba ya mifugo na kubaini uwepo wa ugonjwa huu hasa maeneo ya Mbulu, Mbeya, Iringa, Morogoro na mengine mengi tu. Ugonjwa huu uko karibu maeneo yote duniani isipokuwa haujawi kuripotiwa katika maeneo ya Pasifiki pekee.

UENEAJI WA UGONJWA HUU
Ugonjwa huu unasababishwa na tegu (Taenia solium) wakiwa katika hatua ya lava, na nguruwe anaupata ugonjwa huu anapokula chakula kilichochanganyikana na kinyesi cha binadamu chenye mayai ya tegu. Wakati mwanadamu

anaupata ugonjwa huu anapokula nyama ya nguruwe yenye ugonjwa huu ambayo haikupikwa vizuri au kwa bahati mbaya akimezaa mayai ya tegu kutoka katika vyakula vilivyochanganyikana na uchafu wenye mayai ya tegu. Mzunguko mzima wa maisha ya tegu ni kama inavyoonekana kwenye kielelezo hapa chini.



Kulingana na kielelezo hapo juu utabaini kuwa kwa asilimia kubwa kinachofanya ugonjwa huu unendelee kushamili katika maeneo ambapo ugonjwa huu upon i kutokana na nguruwe kula kinyesi cha binadamu. Hivyo ufugaji huria wa nguruwe (kuwaacha wajitautie wenyewe chakula) pamoja na watu kujisaidia hovyo bila kutmia choo ni michango dhahili ya ugonjwa huu nan i maeneo ambayo yanapaswa kurekebishwa ili kuzuia mwendelezo wa ugonjwa huu.

DALILI ZA UGONJWA

a) Dalili kwa nguruwe


Kwa bahati mbaya ugonjwa huu una dalili chache sana kwa nguruwe na mara nyingi si rahisi kuziona nguruwe akiwa hai, hivyo huonekana wakati amechinjwa. Uumuhimu wake ni kule kumpata hasa mwanadamu na kupelekea kukataliwa

hata nyama ya nguruwe na hivyo kuwa hasara kwa mfugaji. Dalili za ugonjwa huu hasa ugonjwa ukiwa kwa nguruwe wengi ni kama zifuatazo;

-Mfumo wa fahamu na misuli huwa huvurugika
-Kuwepo kwa malengelenge katika maeneo kutolea haja kubwa na chini ya ulimi
-Afya hudhoofika
-Mapigo ya moyo hushindwa kufanya kazi


Lava wakiwa chini ya ulimi wa nguruwe

Ukimchinja nguruwe
Ukimchinja nguruwe unaweza kuona uvimbe uliojaa maji yenye malengelenge wenye ukubwa wa milimita 5-8 kwa milimita 3-5. Maji yake huwa na rangi ya kahawia au waridi na wakati mwingine kichwa cha lava huonekana kama nukta nyeupe. Na viuvimbe hivyo vinaweza kuonekana maeneo yafuatayo;

-Kwenye moyo

-Ulimi

-Misuli ya mashavuni, mabegani, koromeo, kiwambo kinachotenganisha mapafu na tumbo na misuli ya mbavuni na shingoni.

-Mara chache viuvimbe vinaweza kuonekana kwenye ini, bandama, ubongo na tezi.


Nyama ya nguruwe ikiwa imejaa vijiuvimbe maeneo mbalimbali[/TD]


Moyo wenye vijiuvimbe vingi vyenye majimaji ndani

b) Dalili za ugonjwa kwa binadamu

Mwanadamu aliyepata tegu wakubwa mwilini mwake ataanza kutoa mayai kwenye kinyesi kuanzia wiki ya 8 hadi 12. Na tegu wakubwa huweza kuishi ndani ya mwili wa binadamu wakitoa mayai na vipingiri vilivyopevuka kupitia kinyesi kwa muda wa miaka 30. Hii ni hatari sana kwa usambazaji wa ugonjwa. Dalili za ugonjwa huanza kujitokeza kuanzia wiki

moja au miaka kumi na kuendelea tangu awapate hao tegu na mara nyingi lava wakiwa wanakufa.
Mwanadamu awapo na tegu wakubwa mwilini mwake huwa si rahisi sana kutambua, shida huanza anapokuwa na lava.

Mara chache tegu akiwa tumboni mwa binadamu dalili zisizo maalumu kama kuwa mkali bila sababu (anawaka), kupoteza hamu ya kula, kupunua uzito na maumivu ya tumbo, kuharisha na kufunga choo zaweza kujitokeza.

Dalili za ugonjwa huu kwa mwanadamu zaweza kuwa kali kutegemea eneo ambalo lava (vijiuvimbe) wapo ndani ya mwili. Na ni mara chache vijiuvimbe vinaweza kufika sentimita 1-2 hasa kwenye ubongo wa mwanadamu.

-Misuli: Vijiuvimbe kwenye misuli katika maeneo mbalimbali ya mwili kwa kawaida havionyeshi dalili zozote, isipokuwa mabonge ya uvimbe waweza kuyatambua kwa kubonyeza ngozi.

-Macho: Vijiuvimbe vinaweza kuwa vinaelea kwenye macho na kusababisha macho kutokuona vizuri na hata kutenganisha mboni ya jicho.

-Ubongo na uti wa mgongo: Vijiuvimbe hivi vya ugonjwa vikiwepo kwenye ubongo na uti wa mgongo huwa na dalili kama kuuma kichwa, kizunguzungu, kuchanganyikiwa, kuyumbayumba (kukosa urari) na kasha kufa. Kwa muda mrefu

maeneo mengi hapa nchini na kwingineko barani Afrika wamehusianisha ugojnwa huu na ushirikina hasa mgonjwa unapoenda kichwani na kupelekea kwenye ugonjwa wa kifafa. Hapa ndipo hatari kubwa ya ugonjwa huu, kifafa na kifo kwa mwanadamu.

Kifafa-Ni kawaida ya lava kwenda kwenye mfumo wa fahamu wa binadamu na hasa maeneo ya ubongo. Larva hukaa kwenye ubongo kwa muda mrefu sana kwani hulindwa na kizuizi damu-ubongo. Lakini kwasababu ya lava kufa na kuleta madhara kwenye ubongo dalili za kifafa huanza kuonekana


Uvimbe chini ya ulimi wa mwanadamu mwenye ugonjwa

Jinsi ya kuutambua ugonjwa
-Dalili zilizotajwa hapo juu zitasaidia kuutambua ugonjwa huu zikiunganishwa na za kimaabara.

-Kwenye maabara uchunguzi wa kinyesi cha mwanadamu kuangalia uwepo wa mayai ya tegu kwa kutumia darubini hufanyika.

-Larva wakiwa kwenye ubongo wa binadamu njia za kitaalamu zaidi hutumika kama MRI au CT brain scan. MRI ndicho kipimo chenye uhakika kwani kinauwezo wa kuonyesha hatua ya uvimbe, mahali ulipo na mabadiliko yake. Lakini gharama kubwa za kipimo hiki na gharama za kununua mashine yenyewe imefanya matumizi yake kuwa kwa nchi chache tu ambazo tena ugonjwa huu kwao si tatizo.

Matibabu ya ugonjwa huu
Matibabu ya ugonjwa huu yanalenga hasa tegu wakubwa, kwa wadogo wakiwa ndani ya viuvimbe vyenye ngozi isiyorushu dawa kupita huwa ngumu.

Kwa nguruwe: Nguruwe watibiwe kwa kutumia dawa ya minyoo ( Oxfendazole ndiyo dawa inayopendekezwa kutumika kuua tegu na lava-ushauri wa mtaalamu ni muhimu)

Kwa binadamu: Ukiwa nje ya mfumo wa fahamu si wa kutisha na hivyo hauhitaji matibabu maalumu. Dawa za minyoo zinatumika hata kwa wenye lava walio kwenye mfumo wa fahamu japo uponyaji wake si wa uhakika. Lava wakiwa kwenye mfumo wa fahamu upasuaji ili kuondoa uvimbe hushauriwa ufanyike. Lakini matibabu mengine hufanyika yatakayosaidia kushusha dalili za kifafa kabla ya upasuaji kufanyika.

Njia za kuzuia ugonjwa huu

Nguruwe
: Nguruwe wafugiwe ndani ya mabanda na wasiruhusiwe kutembea nje ya banda
-Wapatiwe dawa za magonjwa ya minyoo angalau kila baada ya miezi mitatu
-Nguruwe wakaguliwe na wataalamu wakati wa kuwachinja na wale wote watakaopatikana na ugonjwa waharibiwe.​
-Chakula na maji wanayopewa nguruwe yawe ni masafi​
Mwanadamu: Hakikisha nyama ya nguruwe inapikwa kwa ukamilifu, epuka kula nyama isiyopikwa vizuri. Kuwa makini na kiti moto ambacho sasa ni maarufu sana hapa nchini. Lava wanaweza kufa kwa kuweka nyama kwenye friza nyuzi -10 kwa siku 4 au kupika katika nyuzi 45 hadi 50 kwa dakika 15 hadi 20.​
-Mboga za majani zioshwe na kupikwa vizuri hasa maeneo ambako wanatumia mbolea ya​
nguruwe au nguruwe wanazurula ovyo​
-Hakikisha unanawa mikono kwa maji safi na sabuni mara utokapo chooni na kabla ya kuandaa chakula(Usafi kwa ujumla)​
-Hakikisha vyombo unavyotumia ni safi kwa ajili ya kitimoto na hata matumizi ya kawaida nyumbani​
-Hakikisha matuzi ya choo nyumbani yanafanyika ipasavyo na epukuka kujisaidia sehemu isiyo na choo.​
-Hakikisha unapima choo chako angalau mara moja kila baada ya miezi mitatu ili kujua hali yako kwa magonjwa ya minyoo​
-Tumia dawa za minyoo angalau kila baada ya miezi mitatu ili kutibu magonjwa ya minyoo ambayo hayajaanza kuonyesha dalili. Kama eneo lina watu wengi wenye minyoo hii utibuji wa pamoja utasaidia kuzuia mzuko wa maisha ya tegu (Praziquantel na Albendazole zimependekezwa zitumiwe-ushauri wa daktari muhimu).​
Kumbuka: Mwanadamu ndiye mwenye mchango mkubwa wa kuhakikisha ugonjwa huu unazulikika hivyo elimu ya kutosha kupambana na huu ugonjwa inahitajika kwa kiasi kikubwa sana. Maeneo kama ya Mbeya na Mbuyu​
yameonyesha kuwa ufugaji huria/holela wa nguruwe umechangia kwa kiasi kikubwa sana kwa ugonjwa huu kushamili maeneo hayo ikiwa ni pamoja na kutotumia choo.​
Kwa maeneo yenye minyoo aina ya tegu, kutibu binadamu na nguruwe kwa wakati mmoja ndiyo njia pekee ya kuondokana na huu ugonjwa.​
HAYA TENA KWA WALAJI WA KITOMOTO KAZI KWENU MCHANGA WA PWANI HUO MIMI SIMOOOOO

==========

USHUHUDA
Ufugaji wa nguruwe ulivyonipa utajiri na kujitegemea

Habari wanaJF
,
Tafadhali kwa wale wasiopenda jina hilo hapo juu samahani sana.

Mimi nimefuga nguruwe, nilianza nikiwa niko chuo kikuu mwaka wa pili pale UDSM kwa mtaji wa shilingi 500,000/=

Nilianza kujenga zizi kwa shilingi laki tatu tu na nikanunua makinda ya nguruwe mawili jike na dume kila mmoja sh. @40,000 (mradi niliufungua nyumbani mkoani Kigoma). Fedha zilizobakia nilitafuta mfanyakazi wa kuwalisha hao nguruwe. Nilimlipa sh. 40000 kwa mwezi. Kati ya laki 5, zilibaki 80,000 ambazo nilianza kwa kunulia chakula cha nguruwe.

Baada ya hapo nguruwe niliwapandisha wakazaa watoto 10. Kati ya hao madume yalikuwa 4 na jike 6. Baada ya hayo makinda kukua sikuuza makinda ya jike. niliamua kupanua mradi hivyo nilipanua zizi! Hapo ilikuwa baada ya miezi tisa tu.

Baada ya kupanua mradi niliuza madume 3 nikanunua vyakula (maharage yaliyooza na mashudu) ya kulishia nguruwe waliobakia.

Baada ya miezi 18 nguruwe waliongezeka baada ya kuzaa tena (yale majike 6 na dume 1). Nikaendelea kupanua zizi maana nilijikuta nina nguruwe 30. Kumbuka nguruwe sita wote walizaa. Mmoja makinda 6, mwingine 5, mwingine 5 mwingine 4 mwingine 7 na mwingine 2, na lile dume 1. Jumla nguruwe 30.

Nazidi kupanua mradi na chuo nimeshamaliza kwa sasa nasimamia mwenyewe!

Hakika kwa sasa mimi ni tajiri!

Amini usiamini mimi sio masikini tena!

siku njema.
===

Utangulizi
Utunzaji wa nguruwe mara nyingi hutegemea aina ya nguruwe, njia na aina ya ufugaji. Kwa mfano nguruwe jike anayefugwa kwa ajili ya kuzaa anahitaji kutunzwa tofauti na wale wanaonenepeshwa kwa ajili ya nyama. Kadhalika nguruwe wanaweza kufugwa ndani ya banda au nje, kutegemea na ukubwa wa shamba, fedha zilizopo kwa shughuli za ufugaji na aina ya nguruwe.

Utunzaji wa Nguruwe Dume
Achaguliwe dume mwenye sifa bora ikiwa ni pamoja na kutokuwa na kilema au ugonjwa wowote. Dume aliyechaguliwa, atenganishwe na majike ili kuepusha kupanda wakati usiotakiwa. Inabidi nguruwe huyu asinenepeshwe, kwa hiyo alishwe chakula bora kiasi cha kilo mbili hadi tatu kwa siku. Vile vile apewe maji kila siku.

Kama anapanda chini ya mara tatu kwa wiki, alishwe kilo mbili na nusu na kama anapanda zaidi ya mara tatu, alishwe kilo tatu kwa siku. Ikiwa dume ni dhaifu, aongezewe nusu kilo ya chakula na kama amenenepa sana apunguziwe nusu kilo ya chakula kwa siku. Ni muhimu awe na eneo la mita mraba 9.3 ilikuwezakupata mazoezi ya mwili. Ikiwa sehemu ya kupanda imetenganishwa eneo livve la mita mraba saba.

Nguruwe dume anaweza kutumika kwa kupandajike akiwa na umri wa miezi minane hadi tisa. Kwa umri huu anaruhusiwa kupanda jike moja kwa juma. Afikiapo miezi 10 anaruhusiwa kupanda majike mawili hadi matatu kwa juma. Akiwa na umri wa mwaka mmoja au zaidi ana uwezo wa kupanda jike mmoja kila siku kwa majuma mawili hadi matatu, kisha apumzike kwa muda wa majuma mawili. Dume wakubwa wasitumike kupanda jike wadogo kwani wanaweza kuleta madhara kama vile kuwavunja mgongo.

Ni vizuri nguruwe dume mmoja apande jike 15 hadi 20 kwa mwaka. Dume akizeeka au kuwa na ubovu wa miguu, achinjwe mara moja. Ni muhimu dume aogeshwe kwa sabuni na dawa zinazoweza kuua wadudu na vijidudu vinavyoweza kusababisha magonjwa. Banda na vifaa vinavyotumika visafishwe kila siku.

Utunzaji Wa Nguruwe Jike
Ili mfugaji aweze kupata mazao mengi na bora hana budi kuchagua nguruwe jike mwenye sifa zinazotakiwa. Nguruwe huyu ni vizuri awe amezaliwa na mama anayezaa watoto wengi, mwenye kutoa maziwa mengi na mtunzaji mzuri wa watoto. Tabia hizi zinarithiwa hata navizazi vingine vijavyo. Vile vile awe na afyanzuri na chuchu nyingi zisizopungua 12.

Nguruwe jike anaweza kuzaa akiwa na umri wa miezi mitano hadi sita. Ili kumzuia asibebe mimba mapema, ni vizuri atenganishwe na dume afikiapo umri huo.

Afikiapo miezi nane hadi tisa au akiwa na uzito wa kilo 130 ahaweza kupandishwa. Kabla ya kupandishwa nguruwejike apewe kilo 2.5 hadi tatu za chakula kwa siku. Nguruwe asipelekwe kwa dume mpaka atakapoonyesha dalili zajoto.
Maelezo zaidi unaweza pata kupitia
 
Nguruwe watoto 20 @ 20000 = 400000
Banda la mabanzi=1,000,000
Chakula = 1,000,000
Dawa= 200000
After 1yr: Nguruwe 20 watazaa vitoto kama 160,
utachakuwa vitoto jike 100,
mama zao wote watauzwa, huku shambani kwetu nguruwe
mkubwa ni Tsh 200,000 tu, utapata 4,000,000
After 2yrs: Nguruwe 100 wanaweza kuzaa 700
Kati ya 700 chagua majike 500,(unaweza kuuza watoto dume ukanunua jike)
Year 3: Nguruwe 500 watazaa watoto 3500, chagua watoto 1500 tu
Kutoka hapo unamentein Number 1500, kila mwaka unaweza kuuza
watoto zaidi ya 3000, na nguruwe wakubwa 1500
1500*200000= Tsh 300,000,000/= kwa mwaka
Nusu ya hiyo pesa ni gharama zingine, unabaki na 150mil.
Welcome to the club

Kabla hujajitumbukiza kaone mifano, au nenda sokoine ukaonane na wataalamu.
Kila mwaka nalima Mahindi, alizeti, maboga ekari 30 kwa ajili ya chakula cha
Nguruwe tu.


nakupenda saana mpwa,

Mpwa hii bonge ya deal hata mate yananitoka ila tatizo mimi imani yangu inaniambia nguruwe ni haramu kabisa. lakini hiyo hela naitaka tena sana tu.
 
Mpwa hii bonge ya deal hata mate yananitoka ila tatizo mimi imani yangu inaniambia nguruwe ni haramu kabisa. lakini hiyo hela naitaka tena sana tu.

Hii ni yenyewe mzee, ndg yangu mmoja ameomba nimpelekee, nimeona ni bora niiweke hapa hadharani faida kwa wote. kupanga ni kuchagua kaka, ila sikushauri uende kinyume na imani. na hiyo bei ya nguruwe ni huku shambani kwangu, mjini sijui bei, mm naona maroli yanakuja tu.
 
Nguruwe watoto 20 @ 20000 = 400000
Banda la mabanzi=1,000,000
Chakula = 1,000,000
Dawa= 200000
After 1yr: Nguruwe 20 watazaa vitoto kama 160,
utachakuwa vitoto jike 100,
mama zao wote watauzwa, huku shambani kwetu nguruwe
mkubwa ni Tsh 200,000 tu, utapata 4,000,000
After 2yrs: Nguruwe 100 wanaweza kuzaa 700
Kati ya 700 chagua majike 500,(unaweza kuuza watoto dume ukanunua jike)
Year 3: Nguruwe 500 watazaa watoto 3500, chagua watoto 1500 tu
Kutoka hapo unamentein Number 1500, kila mwaka unaweza kuuza
watoto zaidi ya 3000, na nguruwe wakubwa 1500
1500*200000= Tsh 300,000,000/= kwa mwaka
Nusu ya hiyo pesa ni gharama zingine, unabaki na 150mil.
Welcome to the club

Kabla hujajitumbukiza kaone mifano, au nenda sokoine ukaonane na wataalamu.
Kila mwaka nalima Mahindi, alizeti, maboga ekari 30 kwa ajili ya chakula cha
Nguruwe tu.


nakupenda saana mpwa,
Nimekuwa interested sana na ushauri wako nami ningependa kujaribu hilo deal. Jambo moja linanisumbua ni jinsi ya kupata sehemu ya kufugia, kama kuna mtu ana idea mashamba ya bei nafuu pembezoni mwa Dar es salaam naomba msaada.
 
Nguruwe watoto 20 @ 20000 = 400000
Banda la mabanzi=1,000,000
Chakula = 1,000,000
Dawa= 200000
After 1yr: Nguruwe 20 watazaa vitoto kama 160,
utachakuwa vitoto jike 100,
mama zao wote watauzwa, huku shambani kwetu nguruwe
mkubwa ni Tsh 200,000 tu, utapata 4,000,000
After 2yrs: Nguruwe 100 wanaweza kuzaa 700
Kati ya 700 chagua majike 500,(unaweza kuuza watoto dume ukanunua jike)
Year 3: Nguruwe 500 watazaa watoto 3500, chagua watoto 1500 tu
Kutoka hapo unamentein Number 1500, kila mwaka unaweza kuuza
watoto zaidi ya 3000, na nguruwe wakubwa 1500
1500*200000= Tsh 300,000,000/= kwa mwaka
Nusu ya hiyo pesa ni gharama zingine, unabaki na 150mil.
Welcome to the club

Kabla hujajitumbukiza kaone mifano, au nenda sokoine ukaonane na wataalamu.
Kila mwaka nalima Mahindi, alizeti, maboga ekari 30 kwa ajili ya chakula cha
Nguruwe tu.


nakupenda saana mpwa,

Sasa mtani nina maswali kadhaa hapa.
1. Nguruwe anachkua muda gani hadi kuuzwa, umri
2. Nguruwe 500 wakubwa + watoto 3000 wanahitaji wapagazi wangapi
3. Je kama sina shamba la kulima chakula cha nguruwe mikakati inakaa vipi
4. Nguruwe 500 wakubwa + watoto 3000 wanahitaji eneo la ukubwa gani kuwajengea mabanda (zizi)
5. Soko la nguruwe watoto na wakubwa liko vipi
6. Je kuna magonjwa yoyote hatarishi kwa nguruwe ambayo yanaweza maliza zizi zima.

MJ
 
Sasa mtani nina maswali kadhaa hapa.
1. Nguruwe anachkua muda gani hadi kuuzwa, umri
2. Nguruwe 500 wakubwa + watoto 3000 wanahitaji wapagazi wangapi
3. Je kama sina shamba la kulima chakula cha nguruwe mikakati inakaa vipi
4. Nguruwe 500 wakubwa + watoto 3000 wanahitaji eneo la ukubwa gani kuwajengea mabanda (zizi)
5. Soko la nguruwe watoto na wakubwa liko vipi
6. Je kuna magonjwa yoyote hatarishi kwa nguruwe ambayo yanaweza maliza zizi zima.

MJ

1.Nguruwe anachukua miezi 6 mpaka 12 mpaka kufikia uzito wa kutosha (inategemeanan na malisho)
2.Inategemeana na nafasi yako, ukiwa upo pale full time, wapagazi watatu ni more than enough (kumbuka usipokuwapo watu wanakuwa na uzembe flan). mimi nnao sita chini ya usimamizi mkali.
3.inategemea uko wapi. huku kwetu hata kama haulimi gunia la pumba za mahindi ni Tsh 10,000/=! mashudu ya alizeti gunia ni 20,000/=!
4. Ekari moja wanakaa kwa amani yote. ni vizuri kuwa mbali na makazi ya watu.
5. inategemea uko wapi. kwangu mm nauwezo wa kuuza nguruwe 200 kwa mwezi bila shida. watoto inasumbua kidogo kwa sababu wananunua wafugaji, ukitaka kuwauza kwa urahisi wakuze mpaka miezi mitatu hv.
6. Minyoo na ukurutu. Kikubwa ni chanjo na usafi wa hali ya juu KILA SIKU (nguruwe ni msafi sana akitunzwa, wa kwangu nikimkuta sebuleni nacheka tu-ni WASAFI kama pet)

Nguruwe wanahitaji usimamizi wa karibu sana, uwajue kwa namba ili uweze kufuatilia maendeleo yao kila asubuhi. Ukiona mnyama mmoja amezubaa mwite doctor haraka sana. usiachie wasaidizi kila kitu, kuwa makini na kuhakikisha wanapata milo miwili ya kutosha bila kusahau vegs. nguruwe wanapenda maji-usiwanyime starehe ya kwa kuwabananisha hawatanenepa vya kutosha. Nguruwe ana uwezo wa kuzaa mara mbili kwa mwaka. Mimi sijasoma kilimo na mifugo, ni ubishi tu na kuthubutu vilivyoletwa na maisha magumu. MUHIMU UKUBALI KUKAA SHAMBA, JF UIPATE KWA TTCL NA SOLLAR!
 
Nadhani mdau anataka kujua mchanganuo mzima wa ufugaji wa nguruwe, key issues za ku-take into consideration kama unataka kufuga huyu mnyama!
Wanaojua tunaomba watumwagie data hapa!
Kuna thread ya Amoeba alichanganua vizuri sana yaani ilinitia moyo sana, hawa nadhani nikianza shambani nitawafuga, search au mpm ni nzuri hiyo thread.
 
Inaitwaje?

sorry mkuu, nimechelewa kidogo kuingia pm, hivyo msg yako nimechelewa kuijibu.
Biashara ya ufugaji wa mnyama yeyote inahitaji research na uangalifu wa kutosha, hapa kwenye thread yangu nilieleza kwa haraka tu sababu ya muda. Hata hivyo kama uko srz tafadhali tembelea kwa mtaalamu yeyote wa wanyama aliye karibu nawe, ningependa kuandika kwa undani na kirefu, lakini muda hauniruhusu ndg yangu.

jaribu kucheki hapa https://www.jamiiforums.com/matangazo-madogomadogo/42162-anza-hivi-mpwa-wangu.html
 
wadau nataka nianze ufugaji wa nguruwe wa nyama dsm...sijui chochote kuhusu hawa jamaa ila wanalipa ile mbaya.....give me tips,plz.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom