Ufugaji wa Nguruwe: Utaalam na Masoko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufugaji wa Nguruwe: Utaalam na Masoko

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Amoeba, Oct 27, 2009.

 1. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  IMG-20150929-WA0025.jpg

  - Nguruwe watoto 20 @ 20000 = 400000
  - Banda la mabanzi=1,000,000
  - Chakula = 1,000,000
  - Dawa= 200000

  After 1yr: Nguruwe 20 watazaa vitoto kama 160,utachakuwa vitoto jike 100,
  mama zao wote watauzwa, huku shambani kwetu nguruwe
  mkubwa ni Tsh 200,000 tu, utapata 4,000,000.

  After 2yrs: Nguruwe 100 wanaweza kuzaa 700. Kati ya 700 chagua majike 500,(unaweza kuuza watoto dume ukanunua jike).

  Year 3: Nguruwe 500 watazaa watoto 3500, chagua watoto 1500 tu
  Kutoka hapo unamentein Number 1500, kila mwaka unaweza kuuza
  watoto zaidi ya 3000, na nguruwe wakubwa 1500.
  1500*200000= Tsh 300,000,000/= kwa mwaka
  Nusu ya hiyo pesa ni gharama zingine, unabaki na 150mil.
  Welcome to the club

  Kabla hujajitumbukiza kaone mifano, au nenda sokoine ukaonane na wataalamu.

  Kila mwaka nalima Mahindi, alizeti, maboga ekari 30 kwa ajili ya chakula cha nguruwe tu.

  Nakupenda saana mpwa..

  ==========

  USHUHUDA
  ======================================================
   
 2. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Mpwa hii bonge ya deal hata mate yananitoka ila tatizo mimi imani yangu inaniambia nguruwe ni haramu kabisa. lakini hiyo hela naitaka tena sana tu.
   
 3. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  hii ni yenyewe mzee, ndg yangu mmoja ameomba nimpelekee, nimeona ni bora niiweke hapa hadharani faida kwa wote. kupanga ni kuchagua kaka, ila sikushauri uende kinyume na imani. na hiyo bei ya nguruwe ni huku shambani kwangu, mjini sijui bei, mm naona maroli yanakuja tu.
   
 4. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  i like it!
   
 5. Magpie

  Magpie Member

  #5
  Oct 28, 2009
  Joined: Aug 26, 2009
  Messages: 70
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  dada kaka hilo bonge la dili,watu tunashinda maofisini masaa 10 kwa siku ila kwa mwaka hata ata mil 30 hatufikishi kweli bora kujiajili tu.sasa kaka hicho kijiji gani mbona husemi yaani umenipa mzuka mbaya i must try that this year
   
 6. S

  Simplelady Member

  #6
  Oct 28, 2009
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa interested sana na ushauri wako nami ningependa kujaribu hilo deal. Jambo moja linanisumbua ni jinsi ya kupata sehemu ya kufugia, kama kuna mtu ana idea mashamba ya bei nafuu pembezoni mwa Dar es salaam naomba msaada.
   
 7. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Sasa mtani nina maswali kadhaa hapa.
  1. Nguruwe anachkua muda gani hadi kuuzwa, umri
  2. Nguruwe 500 wakubwa + watoto 3000 wanahitaji wapagazi wangapi
  3. Je kama sina shamba la kulima chakula cha nguruwe mikakati inakaa vipi
  4. Nguruwe 500 wakubwa + watoto 3000 wanahitaji eneo la ukubwa gani kuwajengea mabanda (zizi)
  5. Soko la nguruwe watoto na wakubwa liko vipi
  6. Je kuna magonjwa yoyote hatarishi kwa nguruwe ambayo yanaweza maliza zizi zima.

  MJ
   
 8. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #8
  Nov 5, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  1.Nguruwe anachukua miezi 6 mpaka 12 mpaka kufikia uzito wa kutosha (inategemeanan na malisho)
  2.Inategemeana na nafasi yako, ukiwa upo pale full time, wapagazi watatu ni more than enough (kumbuka usipokuwapo watu wanakuwa na uzembe flan). mimi nnao sita chini ya usimamizi mkali.
  3.inategemea uko wapi. huku kwetu hata kama haulimi gunia la pumba za mahindi ni Tsh 10,000/=! mashudu ya alizeti gunia ni 20,000/=!
  4. Ekari moja wanakaa kwa amani yote. ni vizuri kuwa mbali na makazi ya watu.
  5. inategemea uko wapi. kwangu mm nauwezo wa kuuza nguruwe 200 kwa mwezi bila shida. watoto inasumbua kidogo kwa sababu wananunua wafugaji, ukitaka kuwauza kwa urahisi wakuze mpaka miezi mitatu hv.
  6. Minyoo na ukurutu. Kikubwa ni chanjo na usafi wa hali ya juu KILA SIKU (nguruwe ni msafi sana akitunzwa, wa kwangu nikimkuta sebuleni nacheka tu-ni WASAFI kama pet)

  Nguruwe wanahitaji usimamizi wa karibu sana, uwajue kwa namba ili uweze kufuatilia maendeleo yao kila asubuhi. Ukiona mnyama mmoja amezubaa mwite doctor haraka sana. usiachie wasaidizi kila kitu, kuwa makini na kuhakikisha wanapata milo miwili ya kutosha bila kusahau vegs. nguruwe wanapenda maji-usiwanyime starehe ya kwa kuwabananisha hawatanenepa vya kutosha. Nguruwe ana uwezo wa kuzaa mara mbili kwa mwaka. Mimi sijasoma kilimo na mifugo, ni ubishi tu na kuthubutu vilivyoletwa na maisha magumu. MUHIMU UKUBALI KUKAA SHAMBA, JF UIPATE KWA TTCL NA SOLLAR!
   
 9. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hoja yako imekaa kaa blank cheque hivi..

  Nwy, wajasiriamali wengi wanasema nguruwe wanalipa sana kwa sababu wanazaa watoto wengi na haichukui muda kuwakuza. Sijui kaa nimesaidia ktk hiyp aspect.
   
 10. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #10
  Mar 3, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  kwa kufuga inalipa mbaya!!
  kwa kuuza kama kitoweo inalipa mbaya - sio buchani lakini, uwe unanunua mwenyewe na unachinja na kukaanga mwenyewe.
   
 11. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #11
  Mar 3, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  anachukua muda gani mpaka kufaa kuuza?
   
 12. K

  Kabengwe JF-Expert Member

  #12
  Mar 4, 2010
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nadhani mdau anataka kujua mchanganuo mzima wa ufugaji wa nguruwe, key issues za ku-take into consideration kama unataka kufuga huyu mnyama!
  Wanaojua tunaomba watumwagie data hapa!
   
 13. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #13
  Mar 4, 2010
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kuna thread ya Amoeba alichanganua vizuri sana yaani ilinitia moyo sana, hawa nadhani nikianza shambani nitawafuga, search au mpm ni nzuri hiyo thread.
   
 14. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #14
  Mar 4, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Inaitwaje?
   
 15. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #15
  Mar 4, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  katika kutafuta tafuta nimekutana na blog fulani inaitwa MITIKI,hapo amaefafanua kila kitu hadi aina na vikorokoro vyote vya jinsi ya kuwafuga nguruwe,anayetaka aitembelee atafaidika.
   
 16. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #16
  Mar 4, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180

  Umeikuta ni post ya lini ama weka link hapa maana nimefika kule sikuiona ingawa nimekutana na vitu vingine vizuri
   
 17. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #17
  Mar 4, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  sorry mkuu, nimechelewa kidogo kuingia pm, hivyo msg yako nimechelewa kuijibu.
  Biashara ya ufugaji wa mnyama yeyote inahitaji research na uangalifu wa kutosha, hapa kwenye thread yangu nilieleza kwa haraka tu sababu ya muda. Hata hivyo kama uko srz tafadhali tembelea kwa mtaalamu yeyote wa wanyama aliye karibu nawe, ningependa kuandika kwa undani na kirefu, lakini muda hauniruhusu ndg yangu.

  jaribu kucheki hapa https://www.jamiiforums.com/matangazo-madogomadogo/42162-anza-hivi-mpwa-wangu.html
   
 18. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #18
  Mar 4, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  nimeshindwa kuweka link ila ni post ya Friday, September 25, 2009,kasearch UFUGAJI WA NGURUWE utaipata.
   
 19. K

  Koba JF-Expert Member

  #19
  Jan 17, 2011
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  safi sana ndugu Amoeba,watu lazima wale kila siku no matter what.
   
 20. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #20
  Jun 15, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  wadau nataka nianze ufugaji wa nguruwe wa nyama dsm...sijui chochote kuhusu hawa jamaa ila wanalipa ile mbaya.....give me tips,plz.
   
Loading...