Mradi wa Ufugaji wa ng'ombe

Mwaka juzi nilinunua Ng'ombe anayeaminika kuwa ni fresian kwa kuwa alikuwa na mabaka. Nikaambiwa ni mtamba mwenye mimba ya miezi3 na anatarajiwa kutoa maziwa kuanzia Lita 10 kwa Siku na kuendelea.

Baada ya kuchukua, baadae ilibainika hana mimba na ikabidi kumpandisha tena. Akashika mimba ila akawa na tatizo la kizazi, akatibiwa hivyo hivyo hadi akazaa. Hata hivyo anatoa maziwa chini ya Lita 4 kwa Siku pamoja na kupewa huduma za premier !

Ila ana umbo kumbwa na anavutia kweli
Mazingira ya Dar changamoto kubwa kwenye hawa mifugo ni joto, joto husemekana kupunguza kiwango cha utoaji maziwa kwa ng'ombe iwapo umemtoa sehemu ya baridi....
Mtaalamu ataelezea vizuri akikuja..
 
Dume anahusika vipi na kutoa maziwa ?hii ndio Mara ya kwanza kujua hii
ka ulikuwa hulijui hilo ndo hivyo mkuu, kitaalamu sijui namna ya kulielezea ila wataalamu wa mifugo husema hilo nyakati zote, na ukiwauliza watakwambia, ila naweza elezea kitaalamu uzao ulopatikana na dume huyo namna utakavyokuwa mbovu katika uzalishaji. mtoto atakayezaliwa atakuwa anaurithi usio na maziwa maana kachukuwa vinasaba kwa baba yake
 
Uzoefu wa 4 years kwa mlioko Dar usinunue hawa Ng’ombe utajuta. Nilinunua 4 , 2016 kwa milioni 8 wote wamekufa na watoto wao. Kwa Dar hawatoi zaidi ya lita 5 kwa siku. Wanakua na gharama kubwa kuwatunza kama yai. Tafuta chotara tena nenda Kibaha ndio wanasurvive Dar. Mtakaonunua hawa mlete mrejesho.
Mfugaji wa kawaida anashauriwa kufuga chotara ambaye anakua na sifa Kati ya hao fresian ambao ni wa Western countries uko pamoja na baadhi ya ng'ombe zetu apa.
Ao fresian wako vizuri sema mazingira ya apa kwetu hayawafai kwa hiyo utatumia gharama nyingi afu return ndogo.Mpwapwa breed ni wazuri Kama unaweza kuwapata Hawa ndio wana shauriwa kwa apa bongo.
Sema tuu serikali yetu haitaki kuwekeza katika hii sekta, ni sekta nyeti Sana sema tumeamua kuwaachia wamasai na wasukuama ambao wao wanaiendeaha for fun...
My take tuache kufanya Mambo kienyeji.Unakuta mtu anafuga ng'ombe mmoja au wawili wa tatu.. hii haitatutoa hata siku moja.Inabidi watu wa ache ubinafsi waweze kukaa pamoja na kufanya Jambo la maana.Kufuga ng'ombe ni iwekezaji na ni science pia, Kama huna ujuzi wa haya mambo waone wataalamu na wazoefu wakuelekeze out of that tutaendelea tu kupata lita3 kwa siku.
 
Mazingira ya Dar changamoto kubwa kwenye hawa mifugo ni joto, joto husemekana kupunguza kiwango cha utoaji maziwa kwa ng'ombe iwapo umemtoa sehemu ya baridi....
Mtaalamu ataelezea vizuri akikuja..

Mkuu hilo sio tatizo hata kidogo, kuna ngombe wazuri tu wanafanya vizuri kwenye maeneo ya joto mfano fleckvieh..pia kama unafugia maeneo ya joto fuga chotara..mfano borani+friesian = chotara utakalopata hapo litakupa tija nzuri saana...Mtembelee JK MSOGA..utaona anavyofuga kwa tija...na ili ngombe wakupe 70% ni proper management na 30% ni feeding
 
Mwaka juzi nilinunua Ng'ombe anayeaminika kuwa ni fresian kwa kuwa alikuwa na mabaka. Nikaambiwa ni mtamba mwenye mimba ya miezi3 na anatarajiwa kutoa maziwa kuanzia Lita 10 kwa Siku na kuendelea.

Baada ya kuchukua, baadae ilibainika hana mimba na ikabidi kumpandisha tena. Akashika mimba ila akawa na tatizo la kizazi, akatibiwa hivyo hivyo hadi akazaa. Hata hivyo anatoa maziwa chini ya Lita 4 kwa Siku pamoja na kupewa huduma za premier !

Ila ana umbo kumbwa na anavutia kweli
Kujua breed ya mfugo unaotaka kuwekeza ni jambo muhimu sana...iwe Ngombe, Nguruwe, Kuku nk.

Fertile ONE upatikanaji wake hapa nchini ni shida kiogo, Mashamba mengi hawana Parents stock ... ni mwendo wa kuuziana uziana tu hivyo hivyo...
 
Uzoefu wa 4 years kwa mlioko Dar usinunue hawa Ng’ombe utajuta. Nilinunua 4 , 2016 kwa milioni 8 wote wamekufa na watoto wao. Kwa Dar hawatoi zaidi ya lita 5 kwa siku. Wanakua na gharama kubwa kuwatunza kama yai. Tafuta chotara tena nenda Kibaha ndio wanasurvive Dar. Mtakaonunua hawa mlete mrejesho.
Kibaha wapi mkuu?
 
Du aha ha a we manzese kweli ufugaji haukufai
ufungaji unahitaji muda hasa kwa wakati huu, kumhasi Mbuzi ni jambo jema lakini inahitaji vilevile chakula cha kutosha ili aweze kunenepa, haitoshi hivyo tu ila dawa nazo zinahitajika kuuwa wadudu na viroboto, kupe na vimelea vingine, kumfanya Mbuzi aweze kuwa kukua vizuri, lakini vilevile banda lao linahitaji kuwa safi zaidi.
 
Kitaaluma Mimi ni mtaalam wa Animal science and production.
Njoo DM unijuze unachotaka kufahamu kuhusu ng'ombe wa maziwa na tutajua tusaidiane vipi..!?
nyocksie, naomba unielimishe kuhusu Ng'ombe aina ya Nyakore ,changamoto zake na namna ya kuwafuga lakini vilevile namna ya ukamuaji maziwa. nitashukuru Mtaalam
 
Si kila dume linafaa kwa mbegu, kumbuka dume moja laweza kuhudumia majike mpaka 250 kwa mwaka kama litatumika kitalaamu ( kama sijakosea). Pili dume likihasiwa ( ng`ombe, mbuzi nk) linakuwa haraka na kunenepa sana ktk muda mfupi. Kwa njia hii mkulima anaweza kupata faida haraka. Tunahitaji majike zaidi kuliko madume ktk ufugaji, hata kuku, jogoo ni mmoja kwa matetea matano.
Kwa kuongezea, dume lililohasiwa nirahisi kulitunza(wanakua wapole) kuliko wale wasio hasiwa, na ni kwa utaratibu wa wamarekani hua hawapendi nyama ya ng'ombe yenye harufu ya testerone (hormone inayozalishwa na korodani) hivyo ndo maana wanashauri ng'ombe wahasiwe Kama hawatumiki kwa ajili ya upandishaji
 
Kama kuna mtu anauza ng'ombe wa maziwa chotara au kuna sehemu anajua wanapouzwa kwa Dar es salaam,Pwani na Morogoro tuwasiliane.
 
Mambo vipi wakuu. Ninaomba anayefahamu minada ya mbuzi katika mikoa ya jirani especially Tanga, Morogoro (?), na Dodoma hasa siku za Ijumaa, Jumamosi, na Jumapili anifahamishe please. Kama una information nyingine yeyote kuhusu hili ambayo unadhani inaweza kusaidia unaweza kuchangia. Suggested Format: Mkoa-> Kijiji-> Siku-> Extra info (e.g. range ya bei, quality ya mbuzi, gharama za kusafirisha etc). Asanteni sana.

*On a second thought, nimeona kwamba watu wengine wanaweza kuwa interested na minada hiyo katika mikoa mingine na siku zingine. So, feel free to share the info regardless of the day and the region.
Relax kuna bonge la soko linakuja Namanga kuna kiwanda kinaanzia wa sita mwakani .mmarekani kainvest 11 mil $ ,ni neema
 
Kiwanda hiki kinachokuja ni cha kutengeneza nini??
kununua mbuzi,ngombe ,nguruwe na kuku wa kienyeji kwa ajili ya usindikaji wa mazao mbalimbali ya nyama ikiwemo fillets,sausages ,seasoned meat etc kwa ajiri ya kuuza masoko ya nje kiko km 5 kutoka mpaka wa namanga
 
Kama unaenda Longido au?
kununua mbuzi,ngombe ,nguruwe na kuku wa kienyeji kwa ajili ya usindikaji wa mazao mbalimbali ya nyama ikiwemo fillets,sausages ,seasoned meat etc kwa ajiri ya kuuza masoko ya nje kiko km 5 kutoka mpaka wa namanga
 
Malila huu mpango wa kufuga ng'ombe wa nyama na mimi ninao kilichobaki sasa hivi nikuanza utekelezaji tu by 2013 nadhani mradi utakuwa hewani.. lakini mimi nafikiria kufuga ng'ombe wa nyama wa kisasa.. niliona kwa bwama ASAS aisee ng'ombe anakwenda mpaka kg 1000 within a year baada ya castration. ASAS anaimport mbegu kutoka Denmark na kuzihifadhi kwenye vacuum tanks na alisema pia anaziuza kwa wafugaji wengine.
Hawa wakienyeji tatizo ukuaji wake kidogo unachukua muda mrefu lakini kama utapenda unaweza kupata mbegu nzuri ya ng'ombe wakubwa kutoka kanda ya ziwa i.e shinyanga
Hizo ni mbegu za ng'ombe wa nyama au wa maziwa?
Utaalamu wa kupandisha ng'ombe kwa chupa (AI) ni mdogo sana
Mi nafuga na lastly niliamua kununua dume
 
Kuna Aiana Fulani ya Ngo'ombe wako Kenya,wanatoa lita 40 kwa siku, ila kuwatoa kule si kazi ya kitoto,
Hiki kitu tatizo ni wizara ya mifugo na kilimo wana tatizo hapa kwetu.
Yaan ninafuatilia nataka kununua dume moja la ng'ombe kwenye ranch fulani IPO Kenya nataka niboreshe shamba langu.
Vibali ni mgogoro usiopimika. Ila sekta ya mifugo bila kuwa na breed za kibiashara utachemka.

Maana kwenye ufugaji wa ng'ombe kuna fursa kubwa tatu; maziwa, nyama na kama ukiwa na breed nzuri ni Ujazaji wa Mitamba (hii ndio inalipa ingawa ni uwekezaji mrefu). Hii sekta inakuwa sana ingawa serikali haijaweza kutenga hata maeneo ya wafugaji wadogo au wa kati hasa wale wa zero grazing.

Nenda kwa watu wa Mipango miji angalia master plan zao hawaoneshi kabisa kuwa labda hapa wafugaji madogo au eneo la wafugaji wa kati hivi wanaweza kufugia hanna wao ni makazi biashara na fremu tu.

Mi nilinunua shamba kwa madhumuni hayo, wamekuja kupima vimetoka viwanja vya makazi 39 na mibarabara kibao kwahiyo hata sielewi nafanyaje.

Hii sekta ukiitolea macho vizuri inakutoa kwakuwa kila uchao matumizi ya mazao yapatikanayo kwa mifugo ni yanahitajika hasa nyama na maziwa

Asante
 

Attachments

  • IMG-20190917-WA0002.jpg
    IMG-20190917-WA0002.jpg
    83.4 KB · Views: 38
Nilisikia South Africa wanauza ng'ombe dume wa fleckvieh anauza $ 15,000 ambayo ni sawa na kama Tshs 35,000,000 za kitanzania. Wale ng'ombe ni dual purpose na wanaimili sana maisha ya baridi kali na Joto kali pia na ulaji wao sio mkubwa
Hii bei inazidi vitoyota rush au vanguard zinazosumbua hapa mjini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom