Mradi wa Ufugaji wa ng'ombe

Ni Wapi napoweza kupata maziwa kwa ajili ya kuuza hapa dar. Iwe nje kidogo ya mji ili bei iwe poa kimtindo.
 
Naomba kujua kwa mwenyewe uzoefu na ufugaji wa ng'ombe wa kisasa tafadhari anipe uzoefu.
 
Mimi nimewahi kunenepesha ng'ombe baadaye kuwaleta pale Mnada wa Pugu. Nilijuta sana na sitarudia tena maishani.
 
MIMI NAOMBA KUFAHAMU YAFUATAYO

1. NI AINA GANI YA NG'OMBE WA MAZIWA ANAYEWEZA KUTOA MAZIWA YA KUTOSHA KWA MIKOA YENYE JOTO KAMA LINDI NA MTWARA

2. NG'OMBE HAO WANAPATIKANA WAPI KWA KARIBU NA BEI ZAKE (MAKADIRIO)

3. ILI WAWEZE KUENDELEA KUTOA MAZIWA YA KUTOSHA, WAPATE AINA GANI YA CHAKULA.

Nina mpango wa kuanza huu ufugaji na mtaji ninao.. Nataka nianze huu mradi mwishon mwa mwaka huu 2018.

Ushauri tafadhali.
 
Long time no contribution on this topic. It's a high time we heard from someone or people dealing in this area as the need is high.
 
MIMI NAOMBA KUFAHAMU YAFUATAYO

1. NI AINA GANI YA NG'OMBE WA MAZIWA ANAYEWEZA KUTOA MAZIWA YA KUTOSHA KWA MIKOA YENYE JOTO KAMA LINDI NA MTWARA

2. NG'OMBE HAO WANAPATIKANA WAPI KWA KARIBU NA BEI ZAKE (MAKADIRIO)

3. ILI WAWEZE KUENDELEA KUTOA MAZIWA YA KUTOSHA, WAPATE AINA GANI YA CHAKULA.

Nina mpango wa kuanza huu ufugaji na mtaji ninao.. Nataka nianze huu mradi mwishon mwa mwaka huu 2018.

Ushauri tafadhali.
Mkuu ng'ombe wa maziwa wapo aina nyingi ila kwa hapa Tanzania common breed ni Ashire, Fresian na Jersey. Wakati mwingine unakuta kutokana na kutoelewa kwa wakulima hizi breed zimezaliana pia kwahiyo unaweza kupata mchanganyiko wa hizo breed. Ng'ombe wanaongoza kwa utoaji wa maziwa ni Fresian wakifuatiwa na Ashire na Jersey ni wa mwisho. Kila mmoja hapo anafaida zake na asara zake. Fresian wanatoa maziwa mengi kama ukiwalisha vizuri lakini maziwa yake yana fat content kidogo ukilinganisha na wengine. Pia ni warahisi sana kushikwa na magonjwa especially maeneo ya joto au kama utawafuga huria. Ashire yeye ana maziwa mengi pia lakini siyo mengi kama Fresian ila maziwa yake yana fat yahani mafuta zaidi. Pia uwezo wake wa kukabiliana na magonjwa ni mkubwa kidogo ukilinganisha na Fresian. Pia anakula chakula kidogo kulinganisha na fresian .Jersey wanaumbo dogo kidogo kwa hizo aina nyingine mbili wao faida yao ni kuwa na uwezo wa kutoa maziwa ambayo yanakiwango kikubwa cha fat. Yahani maziwa yake ni futa futa yanakaribiana na ya ng'ombe wa kienyeji lakini pia ni mengi lakini siyo kama ya wenzie hapo juu. Pia kutokana na kuwa na mwili mdogo wanakula chakula kidogo kulinganisha na hao wawili hapo juu. Pia wanauwezo wa kupambana na hali ngumu kidogo. Kimsingi ng'ombe wa maziwa wote siyo rafiki wa ufugaji holela kama wale wa kienyeji .hivyo ukiamua kufanya mradi wa ufugaji wa ng'ombe wa kisasa epuka kuwazururisha kama wale wa kienyeji. Kama unataka kuwachunga hakikisha unawachunga kwenye eneo ambalo unachunga wewe tu. Yahani shambani kwako ambapo hawakutani na wengine. Pia ufuate ushauri wa kitaalam hasa kinga na matibabu. Ng'ombe hawa inapendeza zaidi ukiwafuga kwenye eneo ambalo ni confined. Maeneo ya pwani wanafugwa pia. Kuna aina nyingine ya ng'ombe ambao kwa asili ni ng'ombe wa kienyeji huko india wanaitwa Sahiwal. Hawa nao wana maziwa mengi kiasi lakini hawafikii wale watatu juu. Ila hawa wanamudu kwa kiasi fulani mazingira magumu. Hawa pia wanapatikana tanzania ila maeneo ya mpakani na Kenya Namanga kwasababu hii breed inafungwa pia kenya. Kenya wapo mbali sana kwenye issue ya ufugaji kwasababu serikali yao inasupport sana wakulima na wanaimport mbegu nzuri kutoka nje ya nchi. Jambo lingine unalotakiwa kuelewa ni kwamba utoaji wa maziwa kwa hawa ngombe wote wa kisasa unategemea sana malisho mazuri na huduma nzuri mtu anazo mpatia ng'ombe wake.
Kwa ushauri zaidi juu ya ufugaji wa ng'ombe unaweza kuwasikiana nami kwa email hii judicate2010@gmail.com.
 
Helow habari wana jf
Nahitaji nianze ufugaji wa ng'ombe wa maziwa nimeona sana tija sana hivyo nilihitaji nifaham mambo yafuatayo:

Mbegu ipi nzuri na yenye kustahimili ugonjwa

Ndama wa kuanza kufugwa hughalimu kiasi gan cha PESA

Nahitaji kufuga songea wapi nitapata ndama wa kuanza kufuga

Wataalam nijuzeni jinsi ya ujengaji wa banda

Asanteni sanaa
 
AINA ZA NG’OMBE WA MAZIWA

Kuna aina nyingi za ng’ombe wa maziwa ambao hutofautishwa kwa sifa zifuatazo;

-Umbo, mahali alipotokea.
-Rangi ya ngozi
-Uzalishaji wa maziwa nk.

Zaidi kabisa kuna aina kuu mbili ambazo ni; “Bos taurus” na “Bos indicus”.

Bos taurus inahusisha: Friesian, Ayrshire, Brown Swiss, Guernsey and Jersey na wengine wengi kama vile (Red Dane, Swedish Red and White, Holstein Friesian nk.)

Bos indicus inahusisha: Sahiwal, Red Sindhi, Kenana, Criolo, Tharpakar nk.

1. FRIESIAN/FRESHIANI

-Asilia yao ni holand.

-Hutambuliwa kwa kuwa na rangi nyeupe na nyeusi.

-Uzalishaji bora wa maziwa (7800l/mwaka).

-Walikuwa maalum kwa ajili ya kutengenezea “cheese”.

2. AYRSHIRES

-Wanatambuliwa kwa kuwa ana rangi nyekundu na nyeupe.

-Wanatoa maziwa yenye wastani wa fati 4%.

-Huzalisha maziwa yenye fati nyingi (5400l/mwaka).

3. JERSEYS

-Asili yao ni visiwa vya jersey katikati ya Uingereza na Ufaransa.

-Wanatambuliwa kwa kuwa na rangi mtambuka wa nyeusi na kahawia.

-Maziwa 5700l/mwaka.

-Maalum kwa ajili ya utengenezaji wa “butter”.

KUHUSU UNUNUZI WA HEIFER/MTAMBA.

Siku zote hatushauri mfugaji atafute mtamba mbadala kwa sababu zifuatazo;

-Hawapatikani kwa urahisi na kama wakipatikana ni ghali sana.

-Hatari ya kuingiza magonjwa shambani kwako.

-Ugumu wa kufuatilia historia ya wazazi.

-Hakuna mfugaji anaeweza kuuza mtamba wake bora.

JE WAJUA Kila mwaka ng’ombe wengi wa maziwa wanaondolewa katika shamba kwa sababu mbalimbali ???

Zifuatazo ni sababu kuu;

-Uzalishaji mdogo wa maziwa

-Magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambikiza (TB).

-Matatizo ya uzazi

-Kuuzwa au kuchinjwa tu bila sababu maalum.

HIVYO USHAURI NI KWAMBA, SI KILA MTAMBA UNAOUZWA NI BORA HIVYO ZINGATIA SANA KUOMBA TAARIFA NA KUMBUKUMBU ZA MTAMBA PINDI PALE UTAKAPO ENDA KUNUNUA MTAMBA.

Kuhusu upatikanaji wake kwa huko songea sijafahamu ila Njombe kuna shamba moja kubwa la serikali lipo maeneo ya kitulo pale utapata mtamba mzuri kwa bei nzuri..
 
Upo tayari kwa somo?

Je unajua kwamba, Ng'ombe mmoja anaweza kutoa maziwa Lita 30 kwa siku?

Umejiandaa kuwa mfugaji?
Ng'ombe wanapatikana, Pure breed.
Jersey, Friesian, Fleckvie etc.

Somo litakuja.

0737212132!!

IMG-20190607-WA0023.jpeg
IMG-20190607-WA0018.jpeg
IMG-20190607-WA0033.jpeg
IMG_20190607_095013_390.jpeg
IMG-20190607-WA0031.jpeg
 
Back
Top Bottom