salmin siraj
Senior Member
- Oct 10, 2017
- 198
- 204
- Thread starter
- #21
Hizi mbegu zimesambaa maeneo tofauti tanzania ukitafuta zinapatikana sjui unapatikana wap mkuu?tunazipatia wapi hizo mbegu mkuu?
Hizi mbegu zimesambaa maeneo tofauti tanzania ukitafuta zinapatikana sjui unapatikana wap mkuu?tunazipatia wapi hizo mbegu mkuu?
Kama upo mkoa tofauti na dar es salaam zaid nakushauri uchukue breed aina ya friesian wanafnya vzr kwenye baridi baridiJe, kama nahitaji Ng'ombe kwa ajili ya maziwa. Utanishauri kuchukua breed gani kati ya Friesian, Jersey na Ayshire?
Mungu akujalie katika kutimiza ndoto zakoNiko lindi wilayan nachingwea sehem nilipo ni sehemu yenye nyasi za kutosha na mifugo ni michache acha nikope benki nianze kufuga mshahara wangu naona haunitoshi mola anijalie
Aina ya boran inapatikana zaid kanda ya kati na kaskazini hapa tzsalmin siraj,
..ng'ombe aina ya Boran wanapatikana wapi hapa Tz?
..pia unaweza kutueleza bei yao kwa mfano dume wa boran aliyetayari kupanda ni bei gani?
..au jike wa boran mwenye mimba anauzwa bei gani?
salmin siraj,
..ng'ombe aina ya Boran wanapatikana wapi hapa Tz?
..pia unaweza kutueleza bei yao kwa mfano dume wa boran aliyetayari kupanda ni bei gani?
..au jike wa boran mwenye mimba anauzwa bei gani?
Umetisha aisee tall mnyamaHabari zenu ndugu zangu wajf leo nimeamua kuanzisha hii thread inayohusu ufugaji wa ng'ombe wa kisasa /maziwa kwa minajiri ya kujaribu kusolve changamoto mbalimbali zinazowakumba wafugaji wa sector hii kupitia uzoefu wangu mashambani na shuleni (SUA) hivo karibuni tusharee mawazo tupate kujifunza njia na namna tofauti ya kuzitatua hizi changamoto kitaalamuna kiasili ili ufugaji huu uweze kua yenye tija kwetu na jamii kiujumla.
Tuanze mwanzo kabisa kujua aina ya ng'ombe wa maziwa na sifa zake mbalimbali.
Friesian
Sifa
-Hawa ni wale wenye rangi meusi na nyeupe (rangi yeyote inaweza kutawala kuliko nyingine).
-Wana maumbo makubwa kuliko aina (breed) nyingine.
-Wanasifa ya kuwa na uwezo wa kutoa maziwa mengi kuliko aina nyingine zote za ng'mbe wa kisasa.
-Kutokana na kua na umbo kubwa wanafaa pia kutumika kama ngombe wa nyama.
Changamoto
-Sio wastahimilivu wa magonjwa hasa magonjwa ya kupe na ndorobo.
-Wanamahitaji makubwa ya chakula kutokana na kua na uzito mkubwa .
-Sio wastahimilivu kwenye mazingira ya joto sababu ni rangi nyeusi inaakisi joto zaid ya rangi nyingine.
Arshire
-Hawa wanamchanganyiko wa rangi nyekundu na nyeupe .
-Wanaumbo la wastani ukilinganisha na friesian (ni wakubwa kuliko aina ya jersey na guernsey.
-Ni wastahimilivu wa mazingira magumu mfano maeneo yenye joto.
-Kinga kwa maginjwa ipo juu ukilinganisha na fresian.
-Pia Wanatoa maziwa mengi yenye wastani asimilia 4% ya fatty(mafuta).
Changamoto
-Wanamatumizi makubwa ya chakula na maji.
Guernsey
-Hawa wanataka kufanana na arshire ila wao wanaumbo madogo na rangi zao ni kama njano hivi au red yenye brown ilochanganyika na rangi nyeupe
Sifa
- Wanatoa maziwa ya wastani ukilinganisha na arshire na friesian
- Maziwa yao yana asilimia ya fatty (mafuta ) 4.3%
- Mahitaji ya chakula ni wastani
Changamoto
- Awatoa kiasi kikubwa cha maziwa kama friesian na arshire
Jersey
- Sura zao ukiziangalia ni kama dish (sura kama imebonyea) na macho ya prominent (yametoka nje)
- wanaumbo dogo zaid kuliko aina nyingine.
- Wanatoa maziwa mazuri zaidi, mazito yenye kiasi kikubwa cha mafuta(fatty 4.8%)
- wako very fertile (uwezo mkubwa wa kushika mimba na kuzaa kuliko aina nyingine .
- Wanamature haraka sana (kupevuka).
Changamoto
-Wanatoa kiasi kidogo cha maziwa kuliko aina nyingine za ng'mbe wa waziwa
Aina nyingine zitumikazo ni
1. Brown swiss
2. Mpwapwa breed
Note
Ng'ombe wetu wengi Tanzania ni crossbreed yani ni mchanganyiko wa mbegu za kisasa na kitanzania sio pure breed.
Kuna breed moja wanaita Fleckvieh, inaonekana kufanya vizuri zaidi ya jamii nyingine kwenye utoaji wa maziwa na kuhilimi hali ngumu ya maisha ikiwa pamoja na kula chakula kichache pamoja na kuhimili vema baadhi ya magonjwa. Hii breed unaiongeleaje?
Hio ni friesian ndo katika zile picha nimeweka inamabaka muesi na meupe lakini ukwel kutokana na ngozi yao kua nyeusi na ngombe anaenekana zaidi na maadui kama kupe na ndorobo hivo wanatabia ya kupata magonjwa mara kwa mara hata hivo wanatoa maziwa mengi na ukipata friesian alochanganyika na ngombe wa asili kama boran unaweza kupata matokeo chanya kwenye kuzuia magonjwa na kupata maziwa ya kutosha.
Mkuu Fleckvieh ni jamii ama breed inayojitegemea. Ni maarufu sana Australia na hata jirani zetu kenya wameanza kuifuga kwa miaka mingi tu. Jaribu KuigoogleHio ni friesian ndo katika zile picha nimeweka inamabaka muesi na meupe lakini ukwel kutokana na ngozi yao kua nyeusi na ngombe anaenekana zaidi na maadui kama kupe na ndorobo hivo wanatabia ya kupata magonjwa mara kwa mara hata hivo wanatoa maziwa mengi na ukipata friesian alochanganyika na ngombe wa asili kama boran unaweza kupata matokeo chanya kwenye kuzuia magonjwa na kupata maziwa ya kutosha.
Mkuu Fleckvieh ni jamii ama breed inayojitegemea. Ni maarufu sana Australia na hata jirani zetu kenya wameanza kuifuga kwa miaka mingi tu. Jaribu Kuigoogle
..mbona sijakusikia ukimzungumzia ng'ombe wetu aliyeboreshwa aina ya KONGWA?
..hivi ng'ombe wa kongwa ana sifa na ubora gani kulinganisha na ng'ombe wa kienyeji, au wanaotokea nje kama Boran, Sahiwal, Ankole, etc?
Mkuu swali zuri ila ni hivi hakuna breed inayoitwa kongwa bali kongwa beef ni brand ya kongwa ranch wao wanasifa ya kuzalisha nyama yenye ubora wake hapa tz na breed inayopatopatikana wa wingi kongwa ni boran hata pale ruvu ranch wanatumia brand kongwa beef ila breed zilizopo mule ni tofauti tofauti ila hasa borani wapo kwa wengi. Nyongeza pale dodoma mpwampwa kunakituo kituo cha utafiti wa mifugo wanabreed yao inaitwa mpwampwa breed yenye sifa zote za maziwa mengi na nyama ya ubora na ya kutosha
Asantee ndugu mimi ntaendelea kile nlichokua nacho kwa nguvu zote...nashukuru sana kwa elimu hii uliyonipa.
..MUNGU akuzidishie elimu na maarifa zaidi ili uendelee kutoa kwa wengine.