Mwongozo wa ufugaji wa kisasa wa Mbuzi wa nyama na maziwa

Dodoma sehemu gani mkuu? Ungetaja na jina la hiyo taasisi. Hapa JF ni mahali pa uwazi na ukweli mambo ya kuficha ficha majina haisaidii
 
Habari zenu wakuu.

Poleni sana kwa huzuni mliyonayo kuhusu makinikia. Ama baada ya hayo nije kwenye mada.

Nina nia na dhamira ya kutekeleza mradi wa ufugaji wa mbuzi wa kisasa wa maziwa, hivyo basi ninaomba msaada wenu wa taarifa juu ya sehemu ambapo nitaweza kupata mbegu bora ya hawa mbuzi,ima saanen au togenbag,au aina yeyote ile ya mbuzi wa maziwa, pia ninaomba kujua kwa sasbei ya mbuzi hawa ipoje.

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa michango yenu mtakayotoa, kwani itakuwa ni mwanga mkubwa kwangu na sababu kubwa ya kufanikiwa kwa mradi wangu.

Habarini wapendwa wangu, naombeni msaada nina uhitaji wa mbuzi wa maziwa kwa ajili ya kufuga nitawapataje? Nipo Mwanza

Habari wadau nimeanza kufuga mbuzi kwa kununua mbuzi 20 ila ningependa kupata ushauri zaidi jinsi ya kuwatunza,madawa pamoja na chanjo zao
 
Kama bado ujafanikiwa cheki n huyu mdau kwa msaada zaidi.
2e2dd702347d3cc808950d9fca7e0102.jpg
ab883567bee27db3160bf761261ea8cc.jpg
 
Ahsante sana mkuu

Mkuu ukifanikiwa naomba utoe mrejesho hapa ili na sisi member wengine tujue ni namna gani tunaweza pata, ikiwezekana weka na bei uliyoipata huko.

Pia nina swali , je mbuzi wa maziwa wanalipa kuliko ng'ombe wa maziwa au? ni lita ngapi mbuzi wa maziwa anaweza toa kwa siku kadiri ya uchunguzi wako?

ASANTE.
 
Jaribu kwenda pale mpwapwa kuna taasisi ya serikali niliwahi kukuta aina zaidi ya tano za mbuzi na sifa zao. wenda wakawa na mbegu za aina hiyo.
Mpwapwa mbali mkuu aende Mbande kama unatoka DsM ukimaliza lanchi kabla ya kufika Mbande mkono wa kulia kuna kibao kina maelezo yote. Fuata barabara utawakuta. Zamani walikuwa wanauzwa laki mbili kwa mbuzi ila ni wa kisasa sio wa kienyeji kama wa kwangu.
 
Mpwapwa mbali mkuu aende Mbande kama unatoka DsM ukimaliza lanchi kabla ya kufika Mbande mkono wa kulia kuna kibao kina maelezo yote. Fuata barabara utawakuta. Zamani walikuwa wanauzwa laki mbili kwa mbuzi ila ni wa kisasa sio wa kienyeji kama wa kwangu.
Upo mkoa gani mkuu?
 
Mpwapwa mbali mkuu aende Mbande kama unatoka DsM ukimaliza lanchi kabla ya kufika Mbande mkono wa kulia kuna kibao kina maelezo yote. Fuata barabara utawakuta. Zamani walikuwa wanauzwa laki mbili kwa mbuzi ila ni wa kisasa sio wa kienyeji kama wa kwangu.
Bei yake ya sasa hivi ni Laki tatu, na maziwa yake ni dawa kwa watu wenye maradhi ya sukari.
 
Mbuzi kuzaa mapacha wanne wanafanyiwa dawa mimi ninayo ni ya kiboko, ukichapa viboko vitatu wanazaa watatu na ukichapa vinne wanazaa wanne. Ila mara nyingi huwa nachapa mwisho viboko vitatu labda wawe wakubwa sana kwa umbo ndo unachapa vinne. Usiweke mbele tamaa ya kuzaliwa ndama wenhi ambao mama yao atashindwa kuwanyonyesha kwa kuwatoshereza hivyo kufa kwa njaa au magonjwa kutokana na kuwa na utapiamulo.

Kwanza mie huwa siamini hatika miujiza, kwahiyo suala la kuchapa viboko siliamini maana ni kama muujiza. Suala la kuzaa mapacha ni la kibaiolojia na urithi na si la kimiujiza. Jambo la pili, nakubaliana na wewe kuwa wasipopata matunzo mazur wanaweza kufa kutokana na kutokula vizuri. Lakini nilishawahi kuwafuga na nilikuwa nawatunza vzr tu. Kwahiyo sina ttz na matunzo ninachohitaji ni mbegu hiyo.
nimekaa kidogo mkoa wa kigoma, mkuu ana point ya msingi
tena sio tu kuwachpa bakora kuna njia tofauti tofauti za kupata watoto wawili na kuendelea, muhimu ni kukaa na wazee wa mji wakupe somo tena bure tu
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom