Ufugaji wa Mbuzi wa maziwa

abuusamira

Member
Dec 5, 2012
29
45
Habari zenu wakuu.

Poleni sana kwa huzuni mliyonayo kuhusu makinikia. Ama baada ya hayo nije kwenye mada.

Nina nia na dhamira ya kutekeleza mradi wa ufugaji wa mbuzi wa kisasa wa maziwa, hivyo basi ninaomba msaada wenu wa taarifa juu ya sehemu ambapo nitaweza kupata mbegu bora ya hawa mbuzi,ima saanen au togenbag,au aina yeyote ile ya mbuzi wa maziwa, pia ninaomba kujua kwa sasbei ya mbuzi hawa ipoje.

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa michango yenu mtakayotoa, kwani itakuwa ni mwanga mkubwa kwangu na sababu kubwa ya kufanikiwa kwa mradi wangu.

Habarini wapendwa wangu, naombeni msaada nina uhitaji wa mbuzi wa maziwa kwa ajili ya kufuga nitawapataje? Nipo Mwanza
Habari wadau nimeanza kufuga mbuzi kwa kununua mbuzi 20 ila ningependa kupata ushauri zaidi jinsi ya kuwatunza,madawa pamoja na chanjo zao
 

MR HELOO

Member
Jun 13, 2017
22
75
Ahsante sana mkuu
Mkuu ukifanikiwa naomba utoe mrejesho hapa ili na sisi member wengine tujue ni namna gani tunaweza pata, ikiwezekana weka na bei uliyoipata huko.

Pia nina swali , je mbuzi wa maziwa wanalipa kuliko ng'ombe wa maziwa au? ni lita ngapi mbuzi wa maziwa anaweza toa kwa siku kadiri ya uchunguzi wako?

ASANTE.
 
Sep 15, 2017
18
45
Jamani wana jamvi wenzangu kama kuna mtu anaweza kunisaidia kwa upande wa mawasiliano niwasiliane nao moja kwa moja naombeni msaada tafadhali.
 

Nsuri

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
1,015
2,000
Maziwa ya mbuzi ni mazuri na yana nguvu sana, pia ni muhimu sana kwa watu wenye upungufu wa kinga mwilini. Mdau ukipata na mimi niambie ninunue hta wawili.
 

kawombe

JF-Expert Member
Mar 26, 2015
4,064
2,000
Habarini wapendwa wangu, naombeni msaada nina uhitaji wa mbuzi wa maziwa kwa ajili ya kufuga nitawapataje? Nipo Mwanza
Mm niliagiza kutoka kwa jamaa flani wa morogoro wako nao wengi Sana. Project yao ni kubwa sana nilikutana nao 7 7 D.S. M mwaka huu baazi ya mbegu zao katika picha.sema bei zao nazo zimechangamka kiasi.SORRY PICHA ZIMEGOMA KUWEKWA HAPA KUTOKANA NA TATIZO LA MTANDAO.
Wasiliana na huyu jamaa anaitwa!!
Mr.KOBELO
0652210477
 

chama2chawa

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
736
500
dodoma wilaya chamwino kuna mama anao na huwa anawauza nilimjua siku za nanenane kwenye maonyesho....kwa mwaka 2014 alikuwa anauza kuanzia laki na nusu kwa mbuzi mwenye mimba.Contact zake nilipoteza ila naimani umepata pakuanzia, ukiwa makini kumtafuta utampata
 

OMEGA

JF-Expert Member
Jul 12, 2011
694
250
Mimi nina mbuzi wa maziwa bleed kama mbili tofauti na nafanya zero grazing,tatizo mbuzi walitoa maziwa kidogo mwanzoni lakini sasa hivi hawatohi maziwa wakati chakula wanashiba,tatizo ni nini?
 

sawariya

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
359
250
dodoma wilaya chamwino kuna mama anao na huwa anawauza nilimjua siku za nanenane kwenye maonyesho....kwa mwaka 2014 alikuwa anauza kuanzia laki na nusu kwa mbuzi mwenye mimba.Contact zake nilipoteza ila naimani umepata pakuanzia, ukiwa makini kumtafuta utampata
Laki na nusu mwenye mimba? Huyu atakua kienyeji kama wanaopatikana vingunguti
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom