Mbona hata 1000 (buku) unatajirika? Ingia sokoni majira ya jioni au alfajiri bei ya bidhaa iko chini.

DAY1
Nunua Tikiti zima la 1000 ( buku), nenda sehemu yenye uhitaji katakata pata vipande 5. Jero isevu.

500× 5= 2500

DAY2
Nunua matikiti 2 kwa 2000 na mia tano itumie tu.

Katakata tena safari hii utakuwa na vipande 10.

500× 10 = Sh. 5000

DAY3
Nenda nunua tikiti 5.

Hapa kila tikiti 1 vipande 5 ×5 = 25
500×25 =7,500

DAY 4
Tikiti 8 kwa nikimaanisha 7500 + 500 uliyosevu DAY1 = 8000.

This time tikiti 8 utapata vipande 40
40 × 500 = 20,000

DAY 5
Tikiti 20
Utapata vipande 100

100×500= 50,000

DAY6
Tikiti 50
Utapata vipande 5 × tikiti 50= 250
Vipande 250 × 500 = 75,000

DAY 7
Nenda kachukue tikiti 75 na fungua kijiwe kingine weka kijana afanye internship.

Hapo utakuwa na vipande 375 ukiuza kwa bei yetu 500 unapata Sh. 187500/=

Wiki inayofuata kuwa constant tu kwamba

Kila siku unachukua tikiti 100 za bukubuku kwa Sh. 100,000. Ile 87,500 isevu.

Tikiti 100 kwa wastani wetu wa kila tikiti moja vipande 5 na unauza kwa 500.

Kila siku utakuwa unauza vipande 500 unapata Sh. 250,000/=.

250,000 × siku 30 (mwezi1) = 7,500,000

7,500,000 × mara miezi 12= 90,000,000

Kipato chako kwa mwaka kitakuwa Sh. 90,000,0000.

Huna mtaji wa 1000 (Buku!) Unasubiri nini kuanza.
Mkuu vipi....million 90 ishaingia?
 
Wadau kwema, mimi kama kijana, nimeamua kujikita kwenye ujasiliamali, nimeanza biashara kua kuuza kuku wa kienyeji ambao nawatoa Dodoma na Singida, natafuta soko mwenye connection tafadhali tujuzane hapa.

Bei zanfu ni kuanzia elfu 13 hadi 17 kwa kuku mmoja kutegemeana na uzito wa kuku husika.

Naomba kuwasilisha
 
Changanya kufuga na kuku weupe peee! wa dawa, wabongo ni waumini na ni washirikina ni usipime hata wachungaji watakuja, watanunua nyekundu, nyeusi, blue, kijani ikibidi wapake rangi kabisa upate faida chapchap!

then nunua fuso peleka Congo DRC, wa kienyeji ni wagumu hawafi kirahisi, fanya kwa mtindo huo huo UONE hautarudi bongo, kwa unono wa faida! Dogo lazima uwe mbunifu ambao wengine hawana! unasikia?
 
Wadau kwema, mimi kama kijana, nimeamua kujikita kwenye ujasiliamali, nimeanza biashara kua kuuza kuku wa kienyeji ambao nawatoa Dodoma na Singida, natafuta soko mwenye connection tafadhali tujuzane hapa.

Bei zanfu ni kuanzia elfu 13 hadi 17 kwa kuku mmoja kutegemeana na uzito wa kuku husika.

Naomba kuwasilisha
Upo DSM sehemu gani
 
Hata mm nitakupigia nikitafuta masoko

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli ndugu mm ninafuga kuku waw kienyeji mwaka sass nilianza na kuku 30 niliwatoa tabora wakafa na magonjwa wakabaki 12 , baada ya kufanya uchunguzi ya jinsi ya kuwafuga ili kupata faidi Hadi sasa Nina kuku wakienyeji wengi tu na nishauza sana , Cha msingi ukitaka faida inabidi uwafuge kisasa uwawekee chakula kizuri chenye virutubisho vyote kulingana na umri wao utaona kama huajapata faidi sio unawaacha wazunguke tu mitaani alafu unakaa kutegemea faida
 
Nakushauri ufuge wa kisasa - Layers. wa kienyeji it takes time na faida si kubwa vile unavyodhani - nitafute nikupe ushauri wa bure - meanwhile angalia kazi hii hapa

Hawa wako 900, wanatoa Tray 24 kila siku kila Tray 5000- Chakula chao ni kilo 125 approx Tshs 55,000/-

Mtaji wa kuanzia unahitaji kuwa na not less than 6m before you start production. Kama unataka mchakato mzima sema nitakutumia database yangu.

Send me database please
 
Mkuu hii sishauri mtu aifuate maana ataumia sana kama anategenea kuku haohao, binafsi nilitenga laki 4 nikanunua kuku wa miezi 2 kwa shs 3500 kijijini walikuwa kama 23 hivi, nikajipanga chakula kizuri plus,chanjo zote maana banda lilikuwepo.

kuku walikufa wengine kwamagonjwa ambayo umewapa chanjo wakabaki 15 hivi ndo walivuka salama wakawa wakubwa wote tetea nikanunua jogoo 1 kwa 15.

hapo kuna vifaranga kufa kutokana na sababu fulani kuna kuku kutolalia vizuri unakuta mayai 12 anatotoa 3.....sema naahukuru kipato ninacho so nawahudumia ila sijapata profit yoyote zaidi ya nyama tu.

Kutotoa wanatotoa ila kunachangamoto sana kuvivusha vifaranga kwenda kwenye stage ya 2.
Unapoteza muda. Huwezkufuga kuku wa kienyeji kwa ktumia intensive manahement. Only what u can get is loss.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom