Ufugaji wa kisasa wa Sungura: Ushauri wa masoko na faida za ufugaji

Kuna jinga limemuingiza mjini boss wangu eti alime michai chai soko lake ni noma duniani.Bossi wangu kalima heka kumi kwa sasa jamaa halionekani boss wangu kawa mwehu kila siku na majani ya michai chai kwenye gari lake tunapewa ofisini na siku hizi tumembadili jina tunamuita BOSS MICHAI CHAI
Daah. Huyo jamaa ana dhambi sana. Boss wako nae ana uwezo mdogo wa kuchambua mambo! Michaichai ukiikuta sokoni ama barabarani, siku zote muuzaji ikimdodea, jioni anaitupa. Hawezi kurudi nayo nyumbani. Sa hapo kuna soko gani?
 
Hao watu wa sungura wamemkamata jirani yangu, kanambia wamefundishwa kanisani. Nimejaribu kumnasihi aachane na hii kitu, kagoma. Alianza vzr kufuga kuku. Kaphase out kuku, kaingiza sungura. Namuangalia anavohangaika kuwakatia majani sungura wake.... Daaah. Kaambiwa Sungura watauzwa Kenya kabla kuoelekwa ulaya!
 
Kuna jinga limemuingiza mjini boss wangu eti alime michai chai soko lake ni noma duniani.Bossi wangu kalima heka kumi kwa sasa jamaa halionekani boss wangu kawa mwehu kila siku na majani ya michai chai kwenye gari lake tunapewa ofisini na siku hizi tumembadili jina tunamuita BOSS MICHAI CHAI
Ila wabongo kwa kuwadanganya wenzao ni noma unakumbuka ufugaji wa kwale
 
Kwa mimi binafsi jinsi nilivyo ni kwamba kila mfugo unaowezekana kufuga mimi huwa nafuga huwa sisubiri kusikiliza kwa mtu kwa upande wa sungura huwa nawapenda kwasababu ufugaji wake ni rahisi sana na hauna gharama,ni kuwatengenezea banda zuri harafu unanunua mbegu hapo unaweza anza na wawili tu dume na jike na baada ya hapo utapata sungura wengi sana baada ya muda mufupi hadi utashangaa.
Chakula chake hununui unang'oa majani unawawekea ni bure kabisa na mabaki ya vyakula wao wanagonga kwa wale wenye mashamba na bustani yale majani ya kupalilia unayakusanya unawawekea wanagonga vizuri ambayo wewe ungeyatupa.
Hawaumwi kizembe na wala huwezi poteza gharama kununua dawa.

Sasa ninamaana mtu unaweza kuwafuga kwa mapenzi yako kwasababu hawana gharama ikitokea mtu anawahitaji unaweza muuzia (hapa huwa wanajitokeza sana kununua wakisha jua tu unao sungura)na vile vile unaweza watumia wewe mwenyewe wakakupunguzia gharama za kitoweo(hapo wewe ni mboga za majani na kitoweo cha nyama ya bure hiyo utaamua wewe uchome ,ukaange na nk)

KWA WENYE SHAMBA NA BUSTANI.
sasa hivi samadi inauzwa sasa wewe sungura watakupatia samadi nyingi bure na mkojo utakaotumia kunyunyiza kwenye mimea yako .

USISIKILIZE ETI NGOJA NIPATE SOKO LA MKUPUO WEWE ANZA KUFANYA FAIDA ZA HICHO KITU UTAZIPATA MBELE NA UTASHANGAAA.

Mfano,kuna watu huwa wanabeza hata wale bata wa kienyeji kwamba hawana soko kama wanavyobeza sasa kwa sungura lakini kuna watu wanafanya biashara ya kuchinja na kupaki nyama ya bata vizuri na kuziuza kama kuku kitu ambacho kinawezekana kwa nyama ya sungura nimeweka picha hapo chini.

Angalizo hizo picha sio za kwangu nimechukua kwa mjasiliamali yuko Dar.View attachment 726571View attachment 726572
Couldn't agree more mkuu, mimi ni juzi tu nimeanza ufugaji wa sungura, nimeanza na wawili, na nikipata hela natia bata mzinga, nikipata tena nachimba bwawa la samaki. The thing about me, nafanya ufugaji for passion hua sifikirii kwanza habari za masoko.
 
Hivi sungura hali michaichai?, kama wanakula inaweza saidia kwa bosi michaichai kupata soko la kilimo chake
 
Umehamasishwa kufuga? Au umeshauriwa? Wewe unatakiwa kutafakari mwenyewe Je hiwa unaona Sungura wakiuzwa.mtaani kama kuku au mbuzi? Au usha tembelea ndugu jamaa na marafiki ukakyta wamepika nyama ya Sungura? Kama ni hapana kwa nini?

Shida yetu huwa ni uvivu ila kufanya utafiti ni simple sana
 
ukijua soko nistue na mimi ndugu, umri ushaenda hivi siwezi tena kuingia pori na kuwatoa nduki.
 
Umecoment nini? Shida ya Humu siku hizi mizaha ni mingi sana kupita kiasi ni tofauti na zamani. Zamani ilikuwa ni nadra kukutana na Coment za mizaha kama hii

mi mnunuzi wa kula tu, si mfugaji maana nawahitaji pia kwa ajili ya nyama si kufuga, ningekuwa bush huko nisingekuja kuandika chochote hapa, ningezama pori, ila huku town utawatoa wapi? ukimuona afugwa huyo...sasa nasema hivi atakayesema wauzwa wapi, ndicho nachosubiri katika uzi wako...mkuu japo uzi ni wako inabidi ukubaliane na wachangiaji wa kila aina...mimi si mfugaji wala muuzaji mimi ni mlaji
 
kweli tunazungumzia Sungura wa Bushi au Sungura wa Kufugwa?
 
Kuwa watu humu wanachukulia hili jukwaa kama Facebook au instagram.
Nasikitika sana Kuona hakuna aliye elewa huu uzi.
 
Personally kuna kipindi nilifanya utafiti kuhusu viability ya ufugaji huu. NIlichokiona kuhusu soko ni kwamba masoko yapo nje ya nchi specifically mahoteli/migahawa mikubwa huko nje hasa nchi kama Jamaica ambapo huko wakulima wanaofuga Sungura wanauza nyama kwenye hayo mahoteli kwa kilo hadi (kwa Shilingi yetu ni Roughly elfu ishirini na kidogo).

Changamoto hapo kwa hiyo ni kuwa itahitaji mzalishaji mkubwa mwenye mtaji wa mabilioni hivi au ni ama wawepo wafugaji wengi wenye umoja kwamba wajikusanye wawe wanazalisha sungura wa kutosha. Mfano kusafirisha kontena moja gharama yake ni milioni 9 roughly, na hapo kujaza kontena moja la nyama ya Sungura ina maana wameshachinjwa Sungura zaidi ya 8000 na zaidi kitu. Ukatokea umoja wa wafugaji wakazalisha kwa kiwango cha kutosha itahitaji pia uwepo wa middlemen wenye mitaji ambao wanaiweza biashara wanunue sungura kwa wafugaji wachinje na kusafirisha nje ya nchi.

Labda mamalishe na migahawa ya hapa nchini wawe wanapika nyama ya Sungura ndio huo ufugaji utakua biashara, Maana walaji wa Sungura nchini napo ni wachache na hapo hapo Sungura hizo zinanunuliwa na kuchinjwa wakati wa sikukuu tena n.k
All in all nihitimishe kwa kusema kuwa hii ni Biashara ngumu, ataeiweza labda ni mtu mwenye mtaji na kipawa cha uwezo wa kibiashara na ubunifu wa hali ya juu.
 
Good
 
Sungula ni mfugo mzuri sana mim pia nimefuga nilianza na watano hadi sasa nina sungula 64 kwenye upande wa soko lipo vizuri kwa mkoani morogoro sungura anapimwa kwa kilo kilo moja sh 15000 kwa kawaida nyama ya sungura akiwa amechingwa makadilio ni kilo mbili adi na robo pia kuna muda huwa dili waweza ukauza sungula mmoja 40000 iyo inakuwaga mwezi wa sita adi wa nane pia sungura anaitaji matunzo je wew upo wapi
 
mm ni
mi mnunuzi wa kula tu, si mfugaji maana nawahitaji pia kwa ajili ya nyama si kufuga, ningekuwa bush huko nisingekuja kuandika chochote hapa, ningezama pori, ila huku town utawatoa wapi? ukimuona afugwa huyo...sasa nasema hivi atakayesema wauzwa wapi, ndicho nachosubiri katika uzi wako...mkuu japo uzi ni wako inabidi ukubaliane na wachangiaji wa kila aina...mimi si mfugaji wala muuzaji mimi ni mlaji
mm ninao nauza wako weng 2
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom