Wadau,
Poleni kwa kazi. Nina maswali mawili ambayo ninaomba mnisaidie
1. Nimekuwa nikijaribu kufuatilia kanuni za ufugaji bora wa Sungura katika maeneo ya joto kama DSM. Nimevutiwa sana na ufugaji huu, ila kuna jambo moja ambalo bado sijalipatia ufumbuzi. Hivi kwa hapa Tanzania soko la Sungura lipo wapi hasa?
2. Kuna huyu mtu anaitwa Bennet (anamiliki Mitiki blog), ana info nzuri sana za kilimo. Kuna yeyote anayeweza kuniunganisha nae? Nimejaribu sana kumtumia e mail kwa e mail yake niliyo ikuta katika blog yake but in vain. Kwa aliye na mawasiliano nae naomba aniunganishe nae tafadhali.
Reason ni kuwa ninahitaji kujiingiza katika kilimo, kwa mkulima ninayeanza nafikiri ni vizuri sana nikawa karibu na mtu kama yeye for guidance
Wasalaam
MICHANGO,USHAURI KUTOKA KWA WADAU
--------
-------
Poleni kwa kazi. Nina maswali mawili ambayo ninaomba mnisaidie
1. Nimekuwa nikijaribu kufuatilia kanuni za ufugaji bora wa Sungura katika maeneo ya joto kama DSM. Nimevutiwa sana na ufugaji huu, ila kuna jambo moja ambalo bado sijalipatia ufumbuzi. Hivi kwa hapa Tanzania soko la Sungura lipo wapi hasa?
2. Kuna huyu mtu anaitwa Bennet (anamiliki Mitiki blog), ana info nzuri sana za kilimo. Kuna yeyote anayeweza kuniunganisha nae? Nimejaribu sana kumtumia e mail kwa e mail yake niliyo ikuta katika blog yake but in vain. Kwa aliye na mawasiliano nae naomba aniunganishe nae tafadhali.
Reason ni kuwa ninahitaji kujiingiza katika kilimo, kwa mkulima ninayeanza nafikiri ni vizuri sana nikawa karibu na mtu kama yeye for guidance
Wasalaam
MICHANGO,USHAURI KUTOKA KWA WADAU
Usiingie kwenye ufugaji huu kichwa kichwa, jitahidi kupata information muhimu kwanza, nitakupa kwa ufupi kwa kuwa sina muda sasa:-
1. Angalia usije kuuziwa sungura wetu wa kienyeji hawa hata ufuge vipi hawafiki kilo 5/6
2. Sungura bora ambao ni rahisi kupatikana hapa afrika nashariki ni New Zealand White California White na EA White or Kenya White
3. Ukitaka kufanikiwa zaidi na ufugaji huu, tenga madume peke yake na majike peke yake na pindi jike anapokuwa kwenye heat muhamishie kwenye kiota cha dume na baada ya "mounting" after a day or two mrudishe kwenye kiota chake
4. Sungura wako akisha jifungua make sure after three weeks unamtenganisha na watoto wake na baada ya muda atarudi tena kwenye heat kwa uzao mwingine.Mambo ni mengi na muda sina kwa sasa.
Ufugaji mwema
Kabla hujaamua kufuga sungura hakikisha ya kwamba umejitoa na una muda wa kuwahudumia wanyama waha, ufugaji wao si rahisi kama vile ukifuga paka au mbwa, sungura wanahitaji uangalizi na hassa kwenye usafi kwa sababu ni rahisi kwao kupata maradhi yatokanayo na mazingira mabaya na machafu
Mabanda
Kuna aina mbili za mabanda ya kufugia kwanza ni yale ya kuwafungia ndani muda wote bila kutoka nje na ya pili ni ile ya pili ni nusu nusu yaani wanakuwa na mabanda na wanaweza kutoka nje kwenye ua maalum, katika aina zote mbili ni muhimu kuhakikisha hakuna upenyo wa kuruhusu panya kupita kwa sababu huwa wanakula watoto wa sungura.
Ufugaji wa ndani
Ufugaji wa nje
- Usitumie banda la kioo (aquarium) kwa sababu halina hewa ya kutosha na ni vigumu kusafisha
- Sakafu ya nyavu za waya ni nzuri zaidi ila hakikisha hakuna sehemu zenye ncha kali inayoweza kuwaumiza sungura, kwani wakumia ni mpaka wapone wenyewe au umchinje kwa sababu ukitumia dawa za antibiotic sungura hana uwezo wa kuzimeng’enya na kuisha mwilini mwake, siku ukimchinja atabakia na dawa na hata ukinusa nyama yake utahisi harufu ya dawa
- Ukubwa wa banda usipungue mita 4 * 2 kwa kila sungura mmoja, likiwa kubwa zaidi ni vizuri
- Chini kuwekewe matandazio kama nyasi kavu au maranda ya mbao, lakini maranda yatokanbayo na miti yenye mafuta kama mi-pine na mikaratusi hayafai, wawekee kipande cha blanket au taulo la zamani kwa ajili ya kulalia na kujifungulia hasa kwa wazazi
- Ni muhimu kuwawekea sehemu ya kujificha mara wanapohisi hatari, unaweza kutumia mbao, box gumu au plastiki
Maji
- Sehemu yote izungushiwe wavu wa kuku kuzuia panya kuingia na wanyama wengine kama paka, mbwa, mwewe nk
- Upande mmoja uwe na mabanda, sehemu ya chakula na maji pamoja na kivuli kwa ajili ya sungura kupumzika
- Futi moja chini ya udongo kuwe na zege kuzuia sungura kuchimba na kwenda mbali
- Eneo la wazi liwe huru na hatari zote za sumu kama dawa za kuulia wadudu au mbolea, pia majani yaliyoota yasiwe ni yale yenye sumu (waone wataalamu wakushauri au ng’oa yote)
Tumia mabakuli ya kigae, plastiki au jengea kwa saruji, maji yabadilishwe kila siku na vyombo visafishwe kila siku
Chakula
Wapewe majani, mabaki ya mboga za jikoni baada ya kuchambuliwa, pia unaweza kuwawekea pumba au chakula cha kuku (growers mash) kwenye vyombo maalum kama chakula chenye virutubisho (concentrates)
Usafi
Kila siku jaribu kuondoa uchafu kama vyakula vilivyo mwagika, na kinyesi kilichoganda kwenya matandazio, fagia na kubadili matandazio angalau mara moja kwa wiki, manyoya ya sungura mzazi yasiondolewe hii huonyesha kwamba anakaribia kujifungua watoto
Meno
Wakati mwingine meno ya mbele hukua sana na kumsababishia usumbufu wakati wa kula, waone wataalam ukiona ni marefu zaidi na yanahitaji kupunguzwa, dalili kuu ni sungura kushindwa kula kwa zaidi ya masaa 12
Miguu
Miguu ya sungura si kama ya wanyama wengine, nyayo zake zimefunikwa kwa manyoya, angalia ukiona yananyonyoka kuna tatizo chunguza, kucha zake nazi huhitaji kupunguzwa zikikua sana
Ubebaji
Usimbebe kwa kutumia masikio yake huwa wanaumia sana, shika ngozi nyuma ya shingo kama paka ukitaka kumbeba
Dawa
Wapewe dawa ya minyoo kama piperazine kila baada ya miezi mitatu, dawa za wadudu kama akheri powdeer zinyunyuziwe kwenya mabanda yao kuzuia viroboto, usiwape dawa nyingine bila ushauri wa kitaalamu
--------
Aina za Sungura
Mfugaji anahitaji kutambua sungura ambao atatumia kama mbegu kwa kuzalisha wengine wa hali ya juu.
Ni vyema kutenga sungura wangali wadogo wakiwa miezi minne kwa wa kike na miezi sita kwa sungura wa kiume yaani kabla hawajaanza kuzaa.
Baada ya kupandisha kwa mara ya kwanza na wanapopata mimba sungura hao wa kike ni vyema kuwatenga na kuwaweka katika chumba chao maalum ili kuanzisha kizazi kingine.
Kuna aina mbali mbali wa sungura lakini wanagawanywa mara mbili kwa matumizi.
Moja ni kwa matumizi ya ngozi yake kwa kutengeza kofia, mifuko, na mishipi
Pili kuna aina ya sungura ambao hufugwa kwa kuzalisha nyama. Mfano wa aina ya sungura wa ngozi ni “Angora” ambaye manyoa yake ni marefu.
Na kwa sungura wanaofugwa kwa nyama ni aina ya sungura ambao hukua haraka, uzito wa sungura wa nyama ni kutoka kilo mbili hadi kilo tano. mfano Califonia White na Newzealand White, Chinchila Flemish Giant, Flemish Fender.
Faida za kufuga sungura
Kulingana na wataalam, sungura ni mnyama rahisi wa kufuga hana gharama kubwa. Sungura akitunzwa vyema inavyostahili haugui kwa urahisi na pia lishe yake ni rahisi kupatikana.
Chakula cha sungura ni kama nyasi, mamboga kama vile sukuma wiki, spinarch, karoti, na pia unaweza kununua chakula halisi cha sungura kutoka maduka ya vifaa vya wanyama.
Wataalam wanashauri mfugaji akaushe chakula cha sungura ili asikojoe ovyo na pia kukinga magojwa ya tumbo.
Nyama ya sungura ni tamu na wale ambao wameila huilinganisha na nyama ya kuku. Kulinagana na wataalam ni nyama nyeupe ambayo haina mafuta ya cholestrol na hiyvo wataalam wa lishe bora huhimiza matumizi ya nyama ya sungura kwani ni bora kwa afya.
Ufugaji wa sungura ni kitengo kidogo cha ustawi wa mifugo kwa minajili ya kuongeza uzalishaji wa nyama ya sungura, na pia kwa mapato. Kama mnyama yeyote sungura anahitaji utunzaji mwema ili waweze kuzalisha kwa wingi.
Pia anahitaji kujengewa chumba maalum na kuangaliwa kila siku na kuhakikisha usafi wa vyumba hivi. Na kama watoto wa binadamu pia sungura wanahitaji kupewa chakula kisafi cha hali ya juu kilicho na madini ya protini na kalsham na pia kupewa maji masafi.
-------
SOKO
Soko la sungura lipo kubwa sana, shida ni kumaintain soko kwani watu wengi hufuga sungura kati ya 5 hadi 30, kwa mfano hivi majuzi hoteli moja hapa ilihitaji kilo 500kg za nyama ya sungura kila wiki na walikuwa tayari kuingia mkataba wa mwaka mzima. Hakuna mtu hata mmoja aliyejaribu, sasa jamaa wanaagiza toka China na Ujerumani
Wakuu Malila na Ngamba, heshima kwenu wakuu! nadhani taarifa ya kuwa kuna Hoteli wanahitaji supply ya nyama ya sungura ni njema na inahitaji kupewa uzito wa aina yake. Kama ipo Hoteli moja, basi huenda zikawepo kadhaa zenye uhitaji huo ila wenyewe wanaumia kimyakimya.
Jaribu kufikiria, umetoka "out" na Mamaa. Halafu huyu Mhudumu Mrembo, nadhifu, sauti ya Malaika, anakuuliza "Sir, would you like Sungura Stew for starters, Sir, Madam?" Mzee, hapo vipi?
Hii huenda ikawa fursa nyingine ya kuchangamkia kabla Wake hawajavamia. Soko likivamiwa na hao washikaji ni ngumu kuwatoa huwa wanang'ang'ania kama ruba!
Siku chache zilizopita kuna Mdau katangaza hapa jamvini kutafuta mtu wa ku-supply kuku 30 kwa wiki (kama sikosei) lakini cha kushangaza hadi siku kadhaa baada ya tangazo hakuna mdau yeyote aliyejitokeza angalau hata kufukuzia fursa hiyo.
Nadhani kuna haja ya kufuatilia fursa hii na kupeana taarifa. Binafsi nina ziara ya mbugani Serengeti hivi karibuni. Nitaulizia hilo pamoja fursa nyingine.