Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Wadau naomben mnijulishe bei ya chakula cha samaki kwa kilo, aina za chakula na vinapatikana wapi panapoaminika kwa Dar es salaam
 
Na kiukwel biashar ya samaki imekuwa ngumu sana, ni ipi bei ya Jumla ya samaki aina ya sato kwa kilo hapa Dar
 
Utangulizi

Kitu muhimu cha kuzingatia wakati wa ufugaji wa samaki ili kuongeza uzalishaji ni kuwalisha samaki chakula ambacho kipo kamili (balanced diet). Mfugaji hapo nyumbani unaweza kutengeneza chakula chako hapo nyumbani kama upon a malighafi zifuatazo pumba za mahindi pamoja , mashudu , dagaa,pumba za mchele katika mchanganyiko maalamu ambao utatoa chakula bora kwa ajili ya kuwalisha samaki wako

Jinsi ya kuwalisha samaki

Baada ya kutengeneza chakula chako kwa ajili ya samaki, hakikisha unasimama katika pembe moja yapo ya bwawa la samaki na fanya kurusha chakula kwa kutumia mkono wako katika muda maalumu ambao huo muda ndio utakuwa muda maalamu kwa samaki kula chakula chao.

Baada ya kurusha chakula anza kutazama kama samaki watakikubali chakula ulichowapa hii itajidhirisha kwa samaki kula chakula na wao watajenga mazoea kuibuka muda huo kuja kula chakula na katika pembe husika uliyowarushia samaki…. Na kwa kawaida samaki huchukua takrabi dakika kumi na tano kula chakula.

Muda wa kuwalisha samaki

Kwa kawaida tilapia (sato) hutumia muda mwingi kunywa maji na hula chakula kidogo sana kwa kuwa huwa na matumbo madogo. Na kwa kawaida unatakiwa kuwalisha sato katika muda wa saa4 asubuhi na saa10 jioni hii ni kwa sababu joto la maji pamoja na kiwango cha oxygen (dissolved oxygen) huwa juu sana.

Na hakikisha unazingatia muda ambao unautu ia kuwalisha samaki na sehemu husika ambayo uitumia kuwalisha samaki na mtu ambaye hutumika kuwalisha samaki anatakiwa kuwepo muda wote na aipende kazi yake.

Faida za kuwalisha samaki kwa kutumia mkono

Kuna njia mbalimabli ambazo mfugaji anaweza kuzitumia kwa ajili ya kuwalisha samaki lakni mkulima anashauriwa kuwalisha samaki kwa kutumia mkono ili kuweza kuwaangalia kama samaki wako katika hali nzuri(afya) kwa kuwaangalia jinsi wanavyokula kwa kawaida samaki wanapoona chakula hufurahia na huwa katika staili fualni hivi ya kupigania chakula nje ya hapo ukiona samaki hayuko katika hali hiyo jua kuwa kuna tatizo…

Vifuatavyo huweza sababisha samaki wasiweze kula chakula kama hapo mwanzo:

  • Maji ya bwawa yaweza kuwa baridi
  • Kiwango cha oxygen (dissolve oxygen) kipo chini
  • Samaki wanaweza kuwa wagonjwa
  • Samaki baadhi wanaweza kuwa wamekufa
  • Chakula kinaweza kuwa kizito ambavyo yaweza pelekea kuzama chini

Kiwango cha chakula anachokula samaki

Wewe kama mfugaji unashauriwa kuwa na record ni samaki wangapi ambao wapo kwenye bwawa lako kwa kawaida pale unapoweka fingerling katika bwawa lako ni vyema kuwa na record sahihi umeingiza vifaranga wangapi wa samaki katika bwawa lako hii itakupelekea wewe mfugaji kujua ni kiwango gani cha chakula kinahitajika kuwalisha samaki katika bwawa lako:

Hapa chini nimeambatanisha jedwali ambalo litakupa mwanga ni kiwango gani cha chakula kinahitajika katika kila umri..

View attachment 621374

Imeandaliwa na

theriogenology

Doctor of Veterinary Medicine

Karibuni kwa maswali na Huduma
heb nisaidie, cjaanza kufuga samaki lakin natak kufaham kitaalam samaki hula kias gani cha chakula kwa siku nzima?
 
heb nisaidie, cjaanza kufuga samaki lakin natak kufaham kitaalam samaki hula kias gani cha chakula kwa siku nzima?
8a2e640fc61dbab06248f206ab8d6bb7.jpg

Ukiangalia jedwali hapo juu inategemea na ukubwa wa samaki mkuu.....

Na mara nyingi unapowapa chakula samaki mara nyingi huwa wanakuja usawa ma maji kula chakula na ukitaka kujua kuwa wameridhika na chakula unapokuwa unarusha tena chakula kwenye maji hutowaona wakija juu kula chakula hapo ndipo utajua ya kuwa wametosheka na chakula mkuu....

Na ukiona kwenye jedwali hapo juu kwenye picha utaona kabisa samaki wa mwezi mmoja anakula kiasi cha gram 1 mpaka 2 na yule wa kuanzia miezi mitano anakula gram 4 za chakula...

Nadhani nitakuwa nimejaribu kukuelewesha mkuu....
 
Ahsant san mkuu, nafikir sikuweka sawa swali, nilikuwa nalenga zaid ufugaji wa samaki katika matenki, maana katika mabwawa samaki hupata pia chakula cha asili, sasa je kwa hawa wa kwenye matenki (intensive aquaculture) wanalishwa kias gani?
 
-kwanza kabisa soko la samaki lipo vip kwa mkoa wa Kilimanjaro na Arusha maana Kilimanjaro ndipo project yangu itakuwepo?

-Then members kama kichwa kinavohusika hapo, soon nahitaji kuanza ufugaji wa samaki, aina ya sato na sangara na jamii ingine.

-Hivo naomba mtaalamu yoyote ambaye anajua kuhusu mambo hizi za ufugaji wa samaki ambaye ataweza kuniandikia proposal kuhusu ufugaji wa samaki ambayo itanisaidia kupata mkopo.

Please Inbox Ikiwa wewe ni mtaalamu katika hivi
 
-kwanza kabisa soko la samaki lipo vip kwa mkoa wa Kilimanjaro na Arusha maana Kilimanjaro ndipo project yangu itakuwepo!??
-Then members kama kichwa kinavohusika hapo, soon nahitaji kuanza ufugaji wa samaki, aina ya sato na sangara na jamii ingine.
-Hivo naomba mtaalamu yoyote ambaye anajua kuhusu mambo hizi za ufugaji wa samaki ambaye ataweza kuniandikia proposal kuhusu ufugaji wa samaki ambayo itanisaidia kupata mkopo.
Please Inbox Ikiwa wewe ni mtaalamu katika hivi
Nenda Wizara ya uvuvi na livestock utapata watalam na information hitajika kwa ufanisi. Hongera sana. Kazi nzuri sana.
 
Sangara (Nile perch) ni mgumu kufuga sababu ni obligate carnivore.

Isitoshe na genetics,breeding and seed production kwa Tanzania na East Africa kiujumla ya huyu samaki Haipo.
shukrani kwa kunipa info
 
34 Reactions
Reply
Back
Top Bottom