Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

blakafro, Inategemea na aina ya samaki na uzito kwa kunaotarajia kuvuna kwa kila mmoja. Kama unataka kufuga sato na unatarajia kuvuna akiwa na uzito wa kati ya gramu 150-250 basi unatakiwa uweke vifaranga takribani 1,200 mpaka 2400 tu.
 
3369ab8d6c1a1c238f4ec99fe0fc0a25.jpg
 
pamoja kaka tutakutafuta maana mepitia published books na kutembelea maeneo baadhi kikubwa si vibaya ukatoe elimu kidogo ili kila mtu awe na mwanga ni hayo tu mkuu
 
Utangulizi

Kitu muhimu cha kuzingatia wakati wa ufugaji wa samaki ili kuongeza uzalishaji ni kuwalisha samaki chakula ambacho kipo kamili (balanced diet). Mfugaji hapo nyumbani unaweza kutengeneza chakula chako hapo nyumbani kama upon a malighafi zifuatazo pumba za mahindi pamoja , mashudu , dagaa,pumba za mchele katika mchanganyiko maalamu ambao utatoa chakula bora kwa ajili ya kuwalisha samaki wako


Jinsi ya kuwalisha samaki

Baada ya kutengeneza chakula chako kwa ajili ya samaki, hakikisha unasimama katika pembe moja yapo ya bwawa la samaki na fanya kurusha chakula kwa kutumia mkono wako katika muda maalumu ambao huo muda ndio utakuwa muda maalamu kwa samaki kula chakula chao.

Baada ya kurusha chakula anza kutazama kama samaki watakikubali chakula ulichowapa hii itajidhirisha kwa samaki kula chakula na wao watajenga mazoea kuibuka muda huo kuja kula chakula na katika pembe husika uliyowarushia samaki…. Na kwa kawaida samaki huchukua takrabi dakika kumi na tano kula chakula.

Muda wa kuwalisha samaki

Kwa kawaida tilapia (sato) hutumia muda mwingi kunywa maji na hula chakula kidogo sana kwa kuwa huwa na matumbo madogo. Na kwa kawaida unatakiwa kuwalisha sato katika muda wa saa4 asubuhi na saa10 jioni hii ni kwa sababu joto la maji pamoja na kiwango cha oxygen (dissolved oxygen) huwa juu sana.

Na hakikisha unazingatia muda ambao unautu ia kuwalisha samaki na sehemu husika ambayo uitumia kuwalisha samaki na mtu ambaye hutumika kuwalisha samaki anatakiwa kuwepo muda wote na aipende kazi yake.

Faida za kuwalisha samaki kwa kutumia mkono

Kuna njia mbalimabli ambazo mfugaji anaweza kuzitumia kwa ajili ya kuwalisha samaki lakni mkulima anashauriwa kuwalisha samaki kwa kutumia mkono ili kuweza kuwaangalia kama samaki wako katika hali nzuri(afya) kwa kuwaangalia jinsi wanavyokula kwa kawaida samaki wanapoona chakula hufurahia na huwa katika staili fualni hivi ya kupigania chakula nje ya hapo ukiona samaki hayuko katika hali hiyo jua kuwa kuna tatizo…

Vifuatavyo huweza sababisha samaki wasiweze kula chakula kama hapo mwanzo:

  • Maji ya bwawa yaweza kuwa baridi
  • Kiwango cha oxygen (dissolve oxygen) kipo chini
  • Samaki wanaweza kuwa wagonjwa
  • Samaki baadhi wanaweza kuwa wamekufa
  • Chakula kinaweza kuwa kizito ambavyo yaweza pelekea kuzama chini

Kiwango cha chakula anachokula samaki

Wewe kama mfugaji unashauriwa kuwa na record ni samaki wangapi ambao wapo kwenye bwawa lako kwa kawaida pale unapoweka fingerling katika bwawa lako ni vyema kuwa na record sahihi umeingiza vifaranga wangapi wa samaki katika bwawa lako hii itakupelekea wewe mfugaji kujua ni kiwango gani cha chakula kinahitajika kuwalisha samaki katika bwawa lako:

Hapa chini nimeambatanisha jedwali ambalo litakupa mwanga ni kiwango gani cha chakula kinahitajika katika kila umri..


upload_2017-10-31_7-36-0.png


Imeandaliwa na

theriogenology


Doctor of Veterinary Medicine


Karibuni kwa maswali na Huduma
 
Wakuu nina mtaji wa milioni 1.5, je naweza anzisha hii project ya ufugaji wa samaki? Nakaa Arusha na kuhusu bwawa tayari lipo kwa taasisi nataka tu kuingia nao makubaliano wanipe nilitumie.

Nataka kujua Kama huo mtaji wangu utatosha kununulia vifaranga wa samaki idadi ya 1000 na kuhudumia chakula hadi kufikia muda wa kuwauza ili nipate faida na kujipanua kwenye mtaji zaidi.
 
Niliwahi kufuga samaki enzi za utoton, samaki kama tambala wenye mikia mirefu, kisoda, mkasi, kimwezi n.k

Navutiwa sana na ufugaji samaki huu wa sasa ivi. Ni wa kisasa na wenye faida kubwa nadhani vijana turudie zile enzi zetu za kufuga samaki, njiwa ( kuku) n.k mana tulishawahi kufuga enzi za utotoni mana unafaida sana kwa miaka hii tunayoishi

NB:
Bado sijawa mfugaji ila natarajia kuanza hiyo kazi Allah aniongoze
 
Ofa!!!ofa!!!ofa!!!Ofa!!!ofa!!!ofa!!!Ofa!!!ofa!!!ofa!!!Ofa!!!ofa!!!ofa!!!Ofa!!!ofa!!!ofa!!!Ofa!!!ofa!!!ofa!!!
Ninauza mayai ya kuku wa kienyeji(Malawi) kwa ajili ya kula na pia ukitaka kwa ajili ya kutotolesha yanapatikana kwa order.

Bei ya tray moja ni elfu kumi tu(10,000tsh) ninapatikana Dar es salaam Tegeta-Madale na ukitaka tray kuanzia kumi unaletewa popote ulipo bure ila ukihitaji pungufu ya hapo utatoa nauli nusu na sisi tutakuchangia nusu..kwa mawasiliano zaidi 0769345032 au 0654250816 karibuni sana.
 
Kwanza kwa wadau wote wa huu uzi waliotamani field tour wanisamehe kwa sasa nimekwama kidogo ,nimekutana na changamoto ya upatikanaji wa maji na ardhi inanyonya maji sana.

Tumetumia pesa nyingi sana(karibia 30m)so far na bado project iko utotoni kabisa.Na mara ya kwanza i never thought this project was huge(mabwawa 6 ya square meter 400 kila moja).

So im looking for partners now wa kusonga nao mbele zaidi sababu hapo nahitaji either liner au kujengea kwa cement which are both equally expensive.Na pia kuchimba maji(sio changamoto sana)

Lakini unaweza kutumia nylon za kawaida(Sisi wa Itabagumba Sengerema tunaita kavelo)ila uwe makini na zile pindo inapopita uzi na overlap za hizo nylon zisipitishe maji na zinakaa for at least 2 years, wakati zile zenyewe special zinakaa kama miaka 10 hivi ila zina bei balaa,Balton Tanzania wanazo.
Mkuu naomba mawasiliano ya wauzaji wa liner zile nylon za bwawani
 
asante sana miaka 2 ni tosha kwa kuanzia project ikikua nitatumia hizo za balton. Kkoo nilikuta 12x4m ni 150,000 nitajitaidi kuleta feedback nikifanikiwa
Habari naomba mawasuliano ya wanapouza liner zile nylon za bwawani
 
  • Fahamu aina za mbolea za kurutubisha mabwawa na jinsi ya uwekaji mbolea
  • Na kwa wale wanaotaka kufuga samaki na kuku kwa wakati mmoja pia tunatoa huduma hiyo kama vile kujua idadi ya kuku .
  • Fahamu namna ya uchimbaji wa mabwawa katika maeneo mbalimbali.
  • Vile vile tunandika mpango kazi (business plan ) ya kukuwezesha kufahamu faida ya ufugaji samaki utaipata vpi
Tupigie cmu no 0759678821 au 0625939789

mkuu hebu niambie nataka kufuga samaki, niambie ni chakula gani napaswa kuwapa, kujua magonjwa nk?
 
Back
Top Bottom