Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Yaaap ,nashukuru mleta mada maana amenigusa sana Nina mpango wa kufuga samaki hapa mwanza!

Na nimepewa somo hilo hivi karibuni, na kwa Bahati tena nimelipata hapa asanteni sana
 
Sasa huwezi changanua humu gharama zake.namna ya kupata hao Samaki wadogo kwa faida ya wengi

Bei ya rejareja kwa kifaranga kimoja ni sh 300 kwa sato na 500 kwa kambale.Tanzania wanapatikana TAFIRI mwanza,dar wapo wanaitwa Big Fish(bigfishtz.com) na Kenya wapo wanaitwa Jambo Fish Farm(jambofish.co.ke) hawa ndio wana mbegu nzuri zinazokua haraka.Sijui maelezo yamejitosheleza?
 
Bado jayajajitosheleza mkuu, mchanganuo wa gharama haupo umeeleza tu bei ya vifaranga.
 
Kwenye thread mwanzoni nimeelezea rasilimali zinazohitajika
1.Ardhi
2.Nguvu kazi
3.Maji
4.Fedha

Sasa nashindwa kuweka monetary value ya hizo rasilimali sababu zinabadilika badilika kulingana na eneo husika.kwa mfano maeneo ya arusha ardhi iko juu kwa ekari moja unaweza gharamia 14m na hapo ni kijijini.

Uchimbaji nao pia inategemea unachimba na mashine au watu,ila uchimbaji na mashine ndio mzuri lakini gharama zake ziko juu kidogo kama nilivosema nimekodisha mashine kuchimba 43m*15m kwa 700,000 kina cha meter 3.

Maji nayo nategemea maji ya mferejeni nimejiunga na wana kijiji,ila haya maji sio reliable nikipata hela ntachimba kisima changu mwenyewe.

Vibarua wa kufanya kazi hawa ndio hawana gharama ni maelewano tu.
 
Mkuu embu nijuze jambo moja hapa hapo kwenye maji hivi naweza fugia maji ya kisima namaanisha hapo shambani kwangu nimechimba kisima na maji yanachumvi kwa mbali sana
 
Ndio yanafaa hayo hayana shida mkuu.
 
Kwenye thread mwanzoni nimeelezea rasilimali zinazohitajika
1.Ardhi
2.Nguvu kazi
3.Maji
4.Fedha

Sasa nashindwa kuweka monetary value ya hizo rasilimali sababu zinabadilika badilika kulingana na eneo husika.kwa mfano maeneo ya arusha ardhi iko juu kwa ekari moja unaweza gharamia 14m na hapo ni kijijini.

Uchimbaji nao pia inategemea unachimba na mashine au watu,ila uchimbaji na mashine ndio mzuri lakini gharama zake ziko juu kidogo kama nilivosema nimekodisha mashine kuchimba 43m*15m kwa 700,000 kina cha meter 3.

Maji nayo nategemea maji ya mferejeni nimejiunga na wana kijiji,ila haya maji sio reliable nikipata hela ntachimba kisima changu mwenyewe.

Vibarua wa kufanya kazi hawa ndio hawana gharama ni maelewano tu.

Uelewa sasa unaanza kuja.maji unabadilisha mala ngapi.? Au hayo hayo mpaka wakue
 
Swali zuri.kuna kipimo traditional cha usafi wa maji; Ingiza mkono wako bwawani mpaka kwenye kiwiko(kipepsi) then angalia visibility ya kiganja chako ikoje. Kama kiganja kinaonekana maji bado mi masafi kama hakionekani unahitaji kubadilisha.

Na kumbuka sio lazima ifikishe kwenye kiwiko unaweza ingiza mpaka nusu then inaangalia kama unakiona kiganja chako.
 
je unahitaj samaki Sato wabichi fresh from pond.. ya fish farming. contact me 0717451771. kwa wanunuzi wa jumla tuu
 
je unahitaj samaki Sato wabichi fresh from pond. contact me 0717451771. kwa wanunuzi wa jumla
 
ImageUploadedByJamiiForums1449417132.496946.jpg
 
Back
Top Bottom