Ufugaji wa kisasa wa samaki: Utaalamu na Masoko | Page 15 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufugaji wa kisasa wa samaki: Utaalamu na Masoko

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by bukoba boy, Nov 23, 2015.

 1. bukoba boy

  bukoba boy JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2015
  Joined: Jan 15, 2015
  Messages: 5,133
  Likes Received: 2,702
  Trophy Points: 280
  Tujifunze kuhusu ufugaji wa samaki wa kisasa ambao hufanyika kwenye mabwawa ya kuchimbwa au visima na vitu vingine vinavofanana na hivyo.

  Kuna aina nyingi za samaki wa maji baridi ambao wanaweza kufugika kwa urahisi au ugumu kidogo tu na aina hizo wapo wale ambao sio wa kuzaliana(monosexual) na wale wa kuzaliana(heterosexual)

  Urahisi hapa uko zaidi kwenye kuwafuga wasiozaliana sababu hawaongezeki wakati wale wanaozaliana utakuwa na utaratibu wa kuhamisha fishling(vifaranga) sehemu nyingine.

  Rasilimali muhimu za kuwa nazo ili kufanikisha shughuli hii ni eneo la ardhi,maji, rasilimali watu na rasilimali fedha.Eneo la ardhi ndio litakaloonyesha ni kwa namna gani bwawa lako liwe,aidha la kujengea na cement,kutandika plastic au kuchimba na kulitumia hivyohivyo.Bwawa huchimbwa/kujengwa kwa kuwa na sakafu yenye ulalo kiasi(gentle slope/gradient)

  Wapo samaki aina ya Sato(Tilapia),Kambale(African catfish) na wengine aina ya pangasius ambao hufugwa kwa wingi sana.
  Unahitaji samaki 7-8 katika meter moja ya mraba(1m^2) ,kwa maana hiyo kama una meter za mraba 600 nasi unaweza kufuga samaki 4500.Haishauriwi kulundika samaki kwenye eneo dogo kwani itawasababishia ukosefu wa hewa(oxygen).Ingawa zipo njia za kuweza kuongeza upatikanaji wa hewa kwenye mabwawa.

  Ukishachimba bwawa lako(aidha na kulijengea) unaingiza maji kwenye bwawa hakikisha yamekaribia futi 2.5 mpaka kujaa full.Itakubidi kufanya liming(kumwagia chokaa bwawa kabla ya kuweka maji ili kuua bacteria hatarishi kwa maisha na afya ya samaki wako) pia unahitajika kuyarutubisha hayo maji kwa kuchanganya na mbolea(kama ya ng'ombe na za viwandani pia ingawa haishauriwi sana) na kusubiria kwa muda usiopungua siku 21 au zaidi.Unafanya hivi ili kuweka mazingira ya chakula asili(natural foood) kwa ajili ya samaki kujitengeneza,vyakula hivo hua katika hali ya mimea na viumbe wadogo(microorganisms)

  Upatikanaji wa vifaranga vya samaki,hapa inakubidi uwe makini sana kama umeamua kuzalisha sato,changamoto kubwa ya sato ni kupata mbegu ambayo under right conditions vifaranga vitaweza kua samaki wenye uzito wa kutosha(miezi 6 awe at least 500grams au zaidi).Mbegu ya sato hupatikana kwa bei rejareja ya sh 300 na kambale sh 500 kwa kifaranga kimoja.Wapo wazalishaji wengi wa mbegu za vifaranga wa ndani na nje ya nchi ila kwa Tanzania nimewakubali Tanzania Fisheries Research Institute(TAFIRI) Nyegezi,Mwanza(Nimefwatilia performance yao shambani).  Ulishaji wa vifaranga vyako ,chakula chao kinategemea na uzito wao mfano samaki hula 5% ya uzito wake wa mwili akiwa mdogo na 3% akiwa mkubwa.Hapa tunaongelea ulishaji wa chakula cha ziada(supplement food),sababu cha asili amekipata kwenye ile mbolea ulioweka.Kama una vifaranga 100 vyenye gram 10 kila kimoja basi utahitaji gram 50 kuwalisha.

  Itakuchukua Miezi 6-9 kuanza kuvuna samaki wako ambao unaweza kuwauza kulingana na uzito au au njia utayoona inakufaa.Samaki wengi wa kwenye mabwawa wanavunwa kwa kutumia nyavu au kumwaga maji yote nje ya bwawa.Masoko yake haya samaki ni pamoja na supermarkets, wafanyabiashara sokoni na mitaani pamoja na watu binafsi.

  N:B
  Wataalam wapo wengi humu naomba muongeze na mambo mengine niliyoyasahau au kuyakosea.
   

  Attached Files:

 2. Akilidebe

  Akilidebe JF-Expert Member

  #281
  Feb 20, 2018
  Joined: Feb 18, 2018
  Messages: 206
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 60
  Usifunze kwa maandishi jifunze kwa vitendo
   
 3. bachelor sugu

  bachelor sugu JF-Expert Member

  #282
  Mar 9, 2018
  Joined: Jan 30, 2018
  Messages: 926
  Likes Received: 932
  Trophy Points: 180
  Anzisha uzi wako acha fujo ,we unazungumzia Eicher na watu tumeona Scania Marcopolo,Nissan Diesel,Volvo na ss hv Mchina kashika kamba lakini watu walifilisika na wengine kufa kwa presha unataka kutudanganya nn.
   
 4. Mlaleo

  Mlaleo JF-Expert Member

  #283
  Mar 9, 2018
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 10,259
  Likes Received: 3,702
  Trophy Points: 280
  Acha umaku kuquote post za kale unataka kubanduliwa stamp?
   
 5. Deus oden

  Deus oden New Member

  #284
  Mar 11, 2018
  Joined: Jul 10, 2017
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Hbr,natamani nifuge japo kwa kiasi kidogo samaki kwa ajili ya familia.Kitaaramu naweza kuanda bwawa la ukubwa wa mita 4 kwa mita4.
   
 6. agadinho

  agadinho JF-Expert Member

  #285
  Mar 11, 2018
  Joined: Dec 28, 2012
  Messages: 564
  Likes Received: 294
  Trophy Points: 80
  Floating Cages mtu yeyote ajuaye huu ufugaji tafadhali
   
 7. Deus oden

  Deus oden New Member

  #286
  Mar 13, 2018
  Joined: Jul 10, 2017
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ok
   
 8. IHOLOMELA

  IHOLOMELA JF-Expert Member

  #287
  Mar 24, 2018
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,237
  Likes Received: 823
  Trophy Points: 280
  Nipo Igunga Tabora nataka kufuga samaki. Naomba mtaalamu aje kunishauri. Ntamjali pindi mradi ukianza
   
 9. Luo

  Luo Member

  #288
  Mar 24, 2018
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 82
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 25
  Umeishapata mtaalam kama bado nicheki PM tuongee.
   
 10. cuthbert sezari

  cuthbert sezari Member

  #289
  Apr 11, 2018
  Joined: Sep 5, 2014
  Messages: 29
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 25
  Mie ni mtaalamu wa Samaki utengenezaji wa cage,mabwawa,samaki wa mapambo nk ukinitaka 0769752665 mwanza ndio kwangu pia tunazalisha Vifaranga bora karibuni
   
 11. cuthbert sezari

  cuthbert sezari Member

  #290
  Apr 11, 2018
  Joined: Sep 5, 2014
  Messages: 29
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 25
  Niko hapa kaka floating cages
   
 12. cuthbert sezari

  cuthbert sezari Member

  #291
  Apr 11, 2018
  Joined: Sep 5, 2014
  Messages: 29
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 25
  Niwewe tu IMG-20180302-WA0003.jpg
   
 13. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #292
  Jul 6, 2018
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,606
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mi nataka kuanzisha samaki kwa ajili ya kitoweo / yaani kutumia nyumbani hapa Dar. mwaka jana nilitembelea sabasaba nikakuta JKT wanatumia matenk ya maji ktk ufugaji. Changamoto niliyo ona ni kumwaga maji kila siku nikaona kutakuwa na usumbufu au kupoteza maji mengi kwa bill ya dawasco itakuwa kubwa.
  Je kuna njia ya water re circling ili nisitumie kiasi kikubwa cha maji?
   
 14. candygrapez

  candygrapez Member

  #293
  Jul 9, 2018
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 12
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Mdau sijui ya mwaka jana ila mwaka huu wako na system ambayo sijui ndo hiyo aquaponic ambayo wana pump, mabwawa na vitank viwili pemben vya kuchuja taka ngumu na ammonia na wana system ya kuingiza oxygen moja kwa moja kwenye maji na wanasema maji ni hayo hayo kuanzia unaanza kufuga mpaka unavuna. JKT mbweni.
   
 15. kalamu ya chuma

  kalamu ya chuma JF-Expert Member

  #294
  Jul 18, 2018 at 4:44 PM
  Joined: Jan 22, 2014
  Messages: 201
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  safi sana
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...