Ufugaji wa kisasa wa samaki: Utaalamu na Masoko | Page 14 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufugaji wa kisasa wa samaki: Utaalamu na Masoko

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by bukoba boy, Nov 23, 2015.

 1. bukoba boy

  bukoba boy JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2015
  Joined: Jan 15, 2015
  Messages: 5,133
  Likes Received: 2,702
  Trophy Points: 280
  Tujifunze kuhusu ufugaji wa samaki wa kisasa ambao hufanyika kwenye mabwawa ya kuchimbwa au visima na vitu vingine vinavofanana na hivyo.

  Kuna aina nyingi za samaki wa maji baridi ambao wanaweza kufugika kwa urahisi au ugumu kidogo tu na aina hizo wapo wale ambao sio wa kuzaliana(monosexual) na wale wa kuzaliana(heterosexual)

  Urahisi hapa uko zaidi kwenye kuwafuga wasiozaliana sababu hawaongezeki wakati wale wanaozaliana utakuwa na utaratibu wa kuhamisha fishling(vifaranga) sehemu nyingine.

  Rasilimali muhimu za kuwa nazo ili kufanikisha shughuli hii ni eneo la ardhi,maji, rasilimali watu na rasilimali fedha.Eneo la ardhi ndio litakaloonyesha ni kwa namna gani bwawa lako liwe,aidha la kujengea na cement,kutandika plastic au kuchimba na kulitumia hivyohivyo.Bwawa huchimbwa/kujengwa kwa kuwa na sakafu yenye ulalo kiasi(gentle slope/gradient)

  Wapo samaki aina ya Sato(Tilapia),Kambale(African catfish) na wengine aina ya pangasius ambao hufugwa kwa wingi sana.
  Unahitaji samaki 7-8 katika meter moja ya mraba(1m^2) ,kwa maana hiyo kama una meter za mraba 600 nasi unaweza kufuga samaki 4500.Haishauriwi kulundika samaki kwenye eneo dogo kwani itawasababishia ukosefu wa hewa(oxygen).Ingawa zipo njia za kuweza kuongeza upatikanaji wa hewa kwenye mabwawa.

  Ukishachimba bwawa lako(aidha na kulijengea) unaingiza maji kwenye bwawa hakikisha yamekaribia futi 2.5 mpaka kujaa full.Itakubidi kufanya liming(kumwagia chokaa bwawa kabla ya kuweka maji ili kuua bacteria hatarishi kwa maisha na afya ya samaki wako) pia unahitajika kuyarutubisha hayo maji kwa kuchanganya na mbolea(kama ya ng'ombe na za viwandani pia ingawa haishauriwi sana) na kusubiria kwa muda usiopungua siku 21 au zaidi.Unafanya hivi ili kuweka mazingira ya chakula asili(natural foood) kwa ajili ya samaki kujitengeneza,vyakula hivo hua katika hali ya mimea na viumbe wadogo(microorganisms)

  Upatikanaji wa vifaranga vya samaki,hapa inakubidi uwe makini sana kama umeamua kuzalisha sato,changamoto kubwa ya sato ni kupata mbegu ambayo under right conditions vifaranga vitaweza kua samaki wenye uzito wa kutosha(miezi 6 awe at least 500grams au zaidi).Mbegu ya sato hupatikana kwa bei rejareja ya sh 300 na kambale sh 500 kwa kifaranga kimoja.Wapo wazalishaji wengi wa mbegu za vifaranga wa ndani na nje ya nchi ila kwa Tanzania nimewakubali Tanzania Fisheries Research Institute(TAFIRI) Nyegezi,Mwanza(Nimefwatilia performance yao shambani).



  Ulishaji wa vifaranga vyako ,chakula chao kinategemea na uzito wao mfano samaki hula 5% ya uzito wake wa mwili akiwa mdogo na 3% akiwa mkubwa.Hapa tunaongelea ulishaji wa chakula cha ziada(supplement food),sababu cha asili amekipata kwenye ile mbolea ulioweka.Kama una vifaranga 100 vyenye gram 10 kila kimoja basi utahitaji gram 50 kuwalisha.

  Itakuchukua Miezi 6-9 kuanza kuvuna samaki wako ambao unaweza kuwauza kulingana na uzito au au njia utayoona inakufaa.Samaki wengi wa kwenye mabwawa wanavunwa kwa kutumia nyavu au kumwaga maji yote nje ya bwawa.Masoko yake haya samaki ni pamoja na supermarkets, wafanyabiashara sokoni na mitaani pamoja na watu binafsi.

  N:B
  Wataalam wapo wengi humu naomba muongeze na mambo mengine niliyoyasahau au kuyakosea.
   

  Attached Files:

 2. Ze Heby

  Ze Heby JF-Expert Member

  #261
  Jan 14, 2018
  Joined: May 20, 2012
  Messages: 4,104
  Likes Received: 2,295
  Trophy Points: 280
  Hebu weka mliotengeneza so far sio hizo za mitandaoni
   
 3. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #262
  Jan 14, 2018
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 2,089
  Likes Received: 633
  Trophy Points: 280
 4. Southern Highland

  Southern Highland JF-Expert Member

  #263
  Jan 14, 2018
  Joined: Mar 22, 2017
  Messages: 2,685
  Likes Received: 3,777
  Trophy Points: 280
  Weka kazi mlizofanya nyie. Then utupe muongozo ni kwa jinsi gan inafanya kazi na maelezo kidogo.
  Shukrani
   
 5. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #264
  Jan 14, 2018
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 7,953
  Likes Received: 4,090
  Trophy Points: 280
 6. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #265
  Jan 14, 2018
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 7,953
  Likes Received: 4,090
  Trophy Points: 280
  Tembelea Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) hapo Morogoro hakika utapata shule ya uhakika, hasa ukimpata Dr. Mnembuka hakika utapapenda!
   
 7. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #266
  Jan 15, 2018
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 7,953
  Likes Received: 4,090
  Trophy Points: 280
  Mbona sasa unatapatapa,, povu jiiingi utafikri umefungiwa omo mdomoni? Haya mambo ya picha za Ulaya ndizo zinaingiza watu mkenge. Watu waliaminishwa kwa picha kuhusu green house lakini ukija kwenye uhalisia inakuwa tofauti na walivyokuwa wanaona. Sasa na wewe unatuwekea hydroponic za kwenye mitandao tukueleweje sasa? SUA kwenyewe hizo hazipo na wewe unakuja kutupigisha story hapa!! Labda hii kitu aje aitetee mwalimu wako Mnembuka au Lamtane ndo kidogo tutawasikiliza, wewe bado mchanga sana nenda kwanza field ukapige kazi upate uzoefu siyo utaalam wa kutumia rejea za kwenye mtandao!!
   
 8. m

  masagati JF-Expert Member

  #267
  Jan 18, 2018
  Joined: Oct 16, 2012
  Messages: 409
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Nitawacheki
   
 9. shin gun wook

  shin gun wook JF-Expert Member

  #268
  Jan 18, 2018
  Joined: Sep 26, 2017
  Messages: 920
  Likes Received: 1,296
  Trophy Points: 180
  wafundishe yote ila kwa kua hauwauzii Vifaranga .ntawauzia Mimi.Kambale na sato
   
 10. knowledge quench

  knowledge quench JF-Expert Member

  #269
  Jan 20, 2018
  Joined: Nov 4, 2017
  Messages: 228
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Umefanyikiwa?
   
 11. Nyamtukila

  Nyamtukila Member

  #270
  Jan 23, 2018
  Joined: Dec 9, 2017
  Messages: 26
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Wadau hebu tujuzane kwa mjadala, ni maeneo gani bei ya samaki iko juu zaidi hapa tanzania?
  Hasa kwa samaki aina ya sato na sangara?
   
 12. mjr95

  mjr95 JF-Expert Member

  #271
  Jan 23, 2018
  Joined: Oct 10, 2016
  Messages: 5,326
  Likes Received: 6,611
  Trophy Points: 280
  Iko juu kwa kuuza ama kununua??
   
 13. MBITIYAZA

  MBITIYAZA JF-Expert Member

  #272
  Jan 23, 2018
  Joined: Jan 22, 2017
  Messages: 15,308
  Likes Received: 25,061
  Trophy Points: 280
  SATO IKO JUU
   
 14. g

  gasgas JF-Expert Member

  #273
  Jan 28, 2018
  Joined: Jan 25, 2015
  Messages: 639
  Likes Received: 177
  Trophy Points: 60
  Naomba kujua namna ya kuonganisha hizi plastic liner katika bwawa iwapo unahitaji mbili ili ziweze kutosha bwawa.

  Cellotape haishiki
   
 15. g

  gasgas JF-Expert Member

  #274
  Jan 28, 2018
  Joined: Jan 25, 2015
  Messages: 639
  Likes Received: 177
  Trophy Points: 60
  Vp ulifanikiwa?
   
 16. g

  gasgas JF-Expert Member

  #275
  Jan 28, 2018
  Joined: Jan 25, 2015
  Messages: 639
  Likes Received: 177
  Trophy Points: 60
  Ulifanikiwa mkuu?
   
 17. g

  gasgas JF-Expert Member

  #276
  Jan 28, 2018
  Joined: Jan 25, 2015
  Messages: 639
  Likes Received: 177
  Trophy Points: 60
  Zinaunganishwa vipi?
   
 18. politburo

  politburo Member

  #277
  Feb 2, 2018
  Joined: Feb 1, 2018
  Messages: 96
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 25
  Ungeandika makala hapa ingesaidia wengi zaidi
   
 19. T

  Turnkey JF-Expert Member

  #278
  Feb 2, 2018
  Joined: Jul 9, 2013
  Messages: 2,626
  Likes Received: 1,402
  Trophy Points: 280
  Gharama ya bwawa Square metres 600
   
 20. m

  msemakweliznz New Member

  #279
  Feb 4, 2018
  Joined: Oct 18, 2015
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mimi nahitaji vifaranga sato, lakini vifike Zanzibar, je munasafirisha?
   
 21. M

  Mavipakos Member

  #280
  Feb 11, 2018
  Joined: Aug 15, 2016
  Messages: 16
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 5
  Mhhhhh!!!!! Tangazo halivutiiiiiiii hata kidogo....
  Weka kazi uliyoifanya tuione then tukutafute
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...