Ufugaji wa kisasa wa samaki: Utaalamu na Masoko | Page 13 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufugaji wa kisasa wa samaki: Utaalamu na Masoko

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by bukoba boy, Nov 23, 2015.

 1. bukoba boy

  bukoba boy JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2015
  Joined: Jan 15, 2015
  Messages: 5,133
  Likes Received: 2,698
  Trophy Points: 280
  Tujifunze kuhusu ufugaji wa samaki wa kisasa ambao hufanyika kwenye mabwawa ya kuchimbwa au visima na vitu vingine vinavofanana na hivyo.

  Kuna aina nyingi za samaki wa maji baridi ambao wanaweza kufugika kwa urahisi au ugumu kidogo tu na aina hizo wapo wale ambao sio wa kuzaliana(monosexual) na wale wa kuzaliana(heterosexual)

  Urahisi hapa uko zaidi kwenye kuwafuga wasiozaliana sababu hawaongezeki wakati wale wanaozaliana utakuwa na utaratibu wa kuhamisha fishling(vifaranga) sehemu nyingine.

  Rasilimali muhimu za kuwa nazo ili kufanikisha shughuli hii ni eneo la ardhi,maji, rasilimali watu na rasilimali fedha.Eneo la ardhi ndio litakaloonyesha ni kwa namna gani bwawa lako liwe,aidha la kujengea na cement,kutandika plastic au kuchimba na kulitumia hivyohivyo.Bwawa huchimbwa/kujengwa kwa kuwa na sakafu yenye ulalo kiasi(gentle slope/gradient)

  Wapo samaki aina ya Sato(Tilapia),Kambale(African catfish) na wengine aina ya pangasius ambao hufugwa kwa wingi sana.
  Unahitaji samaki 7-8 katika meter moja ya mraba(1m^2) ,kwa maana hiyo kama una meter za mraba 600 nasi unaweza kufuga samaki 4500.Haishauriwi kulundika samaki kwenye eneo dogo kwani itawasababishia ukosefu wa hewa(oxygen).Ingawa zipo njia za kuweza kuongeza upatikanaji wa hewa kwenye mabwawa.

  Ukishachimba bwawa lako(aidha na kulijengea) unaingiza maji kwenye bwawa hakikisha yamekaribia futi 2.5 mpaka kujaa full.Itakubidi kufanya liming(kumwagia chokaa bwawa kabla ya kuweka maji ili kuua bacteria hatarishi kwa maisha na afya ya samaki wako) pia unahitajika kuyarutubisha hayo maji kwa kuchanganya na mbolea(kama ya ng'ombe na za viwandani pia ingawa haishauriwi sana) na kusubiria kwa muda usiopungua siku 21 au zaidi.Unafanya hivi ili kuweka mazingira ya chakula asili(natural foood) kwa ajili ya samaki kujitengeneza,vyakula hivo hua katika hali ya mimea na viumbe wadogo(microorganisms)

  Upatikanaji wa vifaranga vya samaki,hapa inakubidi uwe makini sana kama umeamua kuzalisha sato,changamoto kubwa ya sato ni kupata mbegu ambayo under right conditions vifaranga vitaweza kua samaki wenye uzito wa kutosha(miezi 6 awe at least 500grams au zaidi).Mbegu ya sato hupatikana kwa bei rejareja ya sh 300 na kambale sh 500 kwa kifaranga kimoja.Wapo wazalishaji wengi wa mbegu za vifaranga wa ndani na nje ya nchi ila kwa Tanzania nimewakubali Tanzania Fisheries Research Institute(TAFIRI) Nyegezi,Mwanza(Nimefwatilia performance yao shambani).  Ulishaji wa vifaranga vyako ,chakula chao kinategemea na uzito wao mfano samaki hula 5% ya uzito wake wa mwili akiwa mdogo na 3% akiwa mkubwa.Hapa tunaongelea ulishaji wa chakula cha ziada(supplement food),sababu cha asili amekipata kwenye ile mbolea ulioweka.Kama una vifaranga 100 vyenye gram 10 kila kimoja basi utahitaji gram 50 kuwalisha.

  Itakuchukua Miezi 6-9 kuanza kuvuna samaki wako ambao unaweza kuwauza kulingana na uzito au au njia utayoona inakufaa.Samaki wengi wa kwenye mabwawa wanavunwa kwa kutumia nyavu au kumwaga maji yote nje ya bwawa.Masoko yake haya samaki ni pamoja na supermarkets, wafanyabiashara sokoni na mitaani pamoja na watu binafsi.

  N:B
  Wataalam wapo wengi humu naomba muongeze na mambo mengine niliyoyasahau au kuyakosea.
   

  Attached Files:

 2. J

  JFK wabongo JF-Expert Member

  #241
  Sep 13, 2017
  Joined: Aug 11, 2015
  Messages: 3,427
  Likes Received: 2,253
  Trophy Points: 280
  Inategemea na aina ya samaki na uzito kwa kunaotarajia kuvuna kwa kila mmoja. Kama unataka kufuga sato na unatarajia kuvuna akiwa na uzito wa kati ya gramu 150-250 basi unatakiwa uweke vifaranga takribani 1,200 mpaka 2400 tu.
   
 3. cuthbert sezari

  cuthbert sezari Member

  #242
  Sep 18, 2017
  Joined: Sep 5, 2014
  Messages: 29
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 25
  Nauza kambale kg 6000 nina pic elifu 10 napatikana mwanza kwa Mawasiliano 0769752665
   
 4. cuthbert sezari

  cuthbert sezari Member

  #243
  Sep 18, 2017
  Joined: Sep 5, 2014
  Messages: 29
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 25
  [​IMG]
   
 5. cuthbert sezari

  cuthbert sezari Member

  #244
  Sep 18, 2017
  Joined: Sep 5, 2014
  Messages: 29
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 25
  Kwa wale wanahitaji mafunzo ya ufugaji samaki na kutenezewa mabwawa ya samaki na kufuga kwa huhakika tunaweza Wasiliana bei zangu ni nafuu sana kwa Mawasiliano 0769752665 email address sezarialfred@gmail.com [​IMG]
   
 6. Raykidd

  Raykidd Member

  #245
  Sep 18, 2017
  Joined: Sep 28, 2016
  Messages: 32
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 15
  pamoja kaka tutakutafuta maana mepitia published books na kutembelea maeneo baadhi kikubwa si vibaya ukatoe elimu kidogo ili kila mtu awe na mwanga ni hayo tu mkuu
   
 7. J

  JFK wabongo JF-Expert Member

  #246
  Sep 18, 2017
  Joined: Aug 11, 2015
  Messages: 3,427
  Likes Received: 2,253
  Trophy Points: 280
  Natafuta vifaranga vya sato. Ni wapi naweza kupata kwa mwanza?
   
 8. lawyerrr

  lawyerrr Member

  #247
  Nov 25, 2017
  Joined: Jun 20, 2017
  Messages: 68
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 25
  Ukijibiwa niambie.namimi nahitaji
   
 9. Nurdyn rasheed

  Nurdyn rasheed New Member

  #248
  Nov 25, 2017
  Joined: Nov 20, 2016
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Niliwahi kufuga samaki enzi za utoton, samaki kama tambala wenye mikia mirefu,kisoda,mkasi,kimwezi n.k
  Navutiwa sana na ufugaji samaki huu wa sasa ivi. Ni wa kisasa na wenye faida kubwa nadhani vijana turudie zile enzi zetu za kufuga samaki,njiwa ( kuku) n.k mana tulishawahi kufuga enzi za utotoni mana unafaida sana kwa miaka hii tunayoishi
  NB:
  Bado sijawa mfugaji ila natarajia kuanza hiyo kazi Allah aniongoze
   
 10. Ronzobe B29

  Ronzobe B29 Senior Member

  #249
  Dec 1, 2017
  Joined: Jul 8, 2017
  Messages: 134
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Kuchimba sawa lakin gharama ni msosi wa kuwalisha hao samaki
   
 11. S

  Shaban Rajab Member

  #250
  Dec 2, 2017
  Joined: Nov 1, 2017
  Messages: 79
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 25
  Ofa!!!ofa!!!ofa!!!Ofa!!!ofa!!!ofa!!!Ofa!!!ofa!!!ofa!!!Ofa!!!ofa!!!ofa!!!Ofa!!!ofa!!!ofa!!!Ofa!!!ofa!!!ofa!!!
  Ninauza mayai ya kuku wa kienyeji(Malawi) kwa ajili ya kula na pia ukitaka kwa ajili ya kutotolesha yanapatikana kwa order.

  Bei ya tray moja ni elfu kumi tu(10,000tsh) ninapatikana Dar es salaam Tegeta-Madale na ukitaka tray kuanzia kumi unaletewa popote ulipo bure ila ukihitaji pungufu ya hapo utatoa nauli nusu na sisi tutakuchangia nusu..kwa mawasiliano zaidi 0769345032 au 0654250816 karibuni sana.
   
 12. lawyerrr

  lawyerrr Member

  #251
  Dec 3, 2017
  Joined: Jun 20, 2017
  Messages: 68
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 25
  Mkuu naomba mawasiliano ya wauzaji wa liner zile nylon za bwawani
   
 13. lawyerrr

  lawyerrr Member

  #252
  Dec 3, 2017
  Joined: Jun 20, 2017
  Messages: 68
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 25
  Habari naomba mawasuliano ya wanapouza liner zile nylon za bwawani
   
 14. theriogenology

  theriogenology JF-Expert Member

  #253
  Dec 12, 2017
  Joined: Oct 7, 2016
  Messages: 5,294
  Likes Received: 8,128
  Trophy Points: 280
 15. Raphael wa Ureno

  Raphael wa Ureno JF-Expert Member

  #254
  Dec 20, 2017
  Joined: Jul 12, 2016
  Messages: 6,359
  Likes Received: 10,360
  Trophy Points: 280
  Wana Yanga Fursa hiyo pale Kwenye mtaa wenu mnaweza kuweka huo mradi wa Kufuga samaki.
   
 16. mavado

  mavado JF-Expert Member

  #255
  Jan 12, 2018
  Joined: Jun 25, 2014
  Messages: 840
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 60
  Weka mifano ya picha hapa
   
 17. mavado

  mavado JF-Expert Member

  #256
  Jan 12, 2018
  Joined: Jun 25, 2014
  Messages: 840
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 60
  -kwanza kabisa soko la samaki lipo vip kwa mkoa wa Kilimanjaro na Arusha maana Kilimanjaro ndipo project yangu itakuwepo!??
  -Then members kama kichwa kinavohusika hapo, soon nahitaji kuanza ufugaji wa samaki, aina ya sato na sangara na jamii ingine.
  -Hivo naomba mtaalamu yoyote ambaye anajua kuhusu mambo hizi za ufugaji wa samaki ambaye ataweza kuniandikia proposal kuhusu ufugaji wa samaki ambayo itanisaidia kupata mkopo.
  Please Inbox Ikiwa wewe ni mtaalamu katika hivi
   
 18. MASAMILA

  MASAMILA JF-Expert Member

  #257
  Jan 13, 2018
  Joined: Jun 22, 2014
  Messages: 1,240
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Sangara (Nile perch) ni mgumu kufuga sababu ni obligate carnivore.

  Isitoshe na genetics,breeding and seed production kwa Tanzania na East Africa kiujumla ya huyu samaki Haipo.
   
 19. knowledge quench

  knowledge quench JF-Expert Member

  #258
  Jan 13, 2018
  Joined: Nov 4, 2017
  Messages: 228
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Nenda Wizara ya uvuvi na livestock utapata watalam na information hitajika kwa ufanisi. Hongera sana. Kazi nzuri sana.
   
 20. mavado

  mavado JF-Expert Member

  #259
  Jan 13, 2018
  Joined: Jun 25, 2014
  Messages: 840
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 60
  shukrani kwa kunipa info
   
 21. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #260
  Jan 13, 2018
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 2,089
  Likes Received: 630
  Trophy Points: 280
  Tembelea chuo cha maswala ya uvuvi mbegani.Bagamoyo.utapata shule na vifaranga vya samaki
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...