Ufugaji wa kisasa wa samaki: Utaalamu na Masoko


bukoba boy

bukoba boy

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2015
Messages
5,266
Likes
2,938
Points
280
Age
33
bukoba boy

bukoba boy

JF-Expert Member
Joined Jan 15, 2015
5,266 2,938 280
Tujifunze kuhusu ufugaji wa samaki wa kisasa ambao hufanyika kwenye mabwawa ya kuchimbwa au visima na vitu vingine vinavofanana na hivyo.

Kuna aina nyingi za samaki wa maji baridi ambao wanaweza kufugika kwa urahisi au ugumu kidogo tu na aina hizo wapo wale ambao sio wa kuzaliana(monosexual) na wale wa kuzaliana(heterosexual)

Urahisi hapa uko zaidi kwenye kuwafuga wasiozaliana sababu hawaongezeki wakati wale wanaozaliana utakuwa na utaratibu wa kuhamisha fishling(vifaranga) sehemu nyingine.

Rasilimali muhimu za kuwa nazo ili kufanikisha shughuli hii ni eneo la ardhi,maji, rasilimali watu na rasilimali fedha.Eneo la ardhi ndio litakaloonyesha ni kwa namna gani bwawa lako liwe,aidha la kujengea na cement,kutandika plastic au kuchimba na kulitumia hivyohivyo.Bwawa huchimbwa/kujengwa kwa kuwa na sakafu yenye ulalo kiasi(gentle slope/gradient)

Wapo samaki aina ya Sato(Tilapia),Kambale(African catfish) na wengine aina ya pangasius ambao hufugwa kwa wingi sana.
Unahitaji samaki 7-8 katika meter moja ya mraba(1m^2) ,kwa maana hiyo kama una meter za mraba 600 nasi unaweza kufuga samaki 4500.Haishauriwi kulundika samaki kwenye eneo dogo kwani itawasababishia ukosefu wa hewa(oxygen).Ingawa zipo njia za kuweza kuongeza upatikanaji wa hewa kwenye mabwawa.

Ukishachimba bwawa lako(aidha na kulijengea) unaingiza maji kwenye bwawa hakikisha yamekaribia futi 2.5 mpaka kujaa full.Itakubidi kufanya liming(kumwagia chokaa bwawa kabla ya kuweka maji ili kuua bacteria hatarishi kwa maisha na afya ya samaki wako) pia unahitajika kuyarutubisha hayo maji kwa kuchanganya na mbolea(kama ya ng'ombe na za viwandani pia ingawa haishauriwi sana) na kusubiria kwa muda usiopungua siku 21 au zaidi.Unafanya hivi ili kuweka mazingira ya chakula asili(natural foood) kwa ajili ya samaki kujitengeneza,vyakula hivo hua katika hali ya mimea na viumbe wadogo(microorganisms)

Upatikanaji wa vifaranga vya samaki,hapa inakubidi uwe makini sana kama umeamua kuzalisha sato,changamoto kubwa ya sato ni kupata mbegu ambayo under right conditions vifaranga vitaweza kua samaki wenye uzito wa kutosha(miezi 6 awe at least 500grams au zaidi).Mbegu ya sato hupatikana kwa bei rejareja ya sh 300 na kambale sh 500 kwa kifaranga kimoja.Wapo wazalishaji wengi wa mbegu za vifaranga wa ndani na nje ya nchi ila kwa Tanzania nimewakubali Tanzania Fisheries Research Institute(TAFIRI) Nyegezi,Mwanza(Nimefwatilia performance yao shambani).Ulishaji wa vifaranga vyako ,chakula chao kinategemea na uzito wao mfano samaki hula 5% ya uzito wake wa mwili akiwa mdogo na 3% akiwa mkubwa.Hapa tunaongelea ulishaji wa chakula cha ziada(supplement food),sababu cha asili amekipata kwenye ile mbolea ulioweka.Kama una vifaranga 100 vyenye gram 10 kila kimoja basi utahitaji gram 50 kuwalisha.

Itakuchukua Miezi 6-9 kuanza kuvuna samaki wako ambao unaweza kuwauza kulingana na uzito au au njia utayoona inakufaa.Samaki wengi wa kwenye mabwawa wanavunwa kwa kutumia nyavu au kumwaga maji yote nje ya bwawa.Masoko yake haya samaki ni pamoja na supermarkets, wafanyabiashara sokoni na mitaani pamoja na watu binafsi.

N:B
Wataalam wapo wengi humu naomba muongeze na mambo mengine niliyoyasahau au kuyakosea.
 

Attachments:

Zanzibar Spices

Zanzibar Spices

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2013
Messages
7,511
Likes
2,070
Points
280
Zanzibar Spices

Zanzibar Spices

JF-Expert Member
Joined Jul 14, 2013
7,511 2,070 280
Uzi kama huu upo stick kwenye page ya mwanzo.ungejazia pale
Hope moderator watafanya hivyo
 
bukoba boy

bukoba boy

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2015
Messages
5,266
Likes
2,938
Points
280
Age
33
bukoba boy

bukoba boy

JF-Expert Member
Joined Jan 15, 2015
5,266 2,938 280
Uzi kama huu upo stick kwenye page ya mwanzo.ungejazia pale
Hope moderator watafanya hivyo
Wangafanyia update pale juu,nimemaliza kuandika ndio nikauona! Invisible
 
Last edited by a moderator:
S

shela

Member
Joined
Jun 3, 2015
Messages
5
Likes
0
Points
0
S

shela

Member
Joined Jun 3, 2015
5 0 0
Au anaejua wachimba hayo mabwawa wazuri naomba aniambie maan nataka nianze mradi wa ufugaji samaki
 
bukoba boy

bukoba boy

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2015
Messages
5,266
Likes
2,938
Points
280
Age
33
bukoba boy

bukoba boy

JF-Expert Member
Joined Jan 15, 2015
5,266 2,938 280
Nimepnda je wajua gharama za kuchimba hyo mabwawa
Uchimbaji wa bwana unategemea na ukubwa wa bwawa,ukitaka kazi na bwawa likae vizuri inakuhitaji uwe na excavators ila pia wapo watu wanachimba ila wanachukua mda mrefu sana. Kwa mfano nimechimba na excavator size ya 43mx15m kwa shilling 700,000 arusha.
 
Mathenge

Mathenge

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2013
Messages
744
Likes
289
Points
80
Age
46
Mathenge

Mathenge

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2013
744 289 80
Yaaap ,nashukuru mleta mada maana amenigusa sana Nina mpango wa kufuga samaki hapa mwanza ! Na nimepewa somo hilo hivi karibuni,na kwa Bahati tena nimelipata hapa asanteni sana
 
bukoba boy

bukoba boy

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2015
Messages
5,266
Likes
2,938
Points
280
Age
33
bukoba boy

bukoba boy

JF-Expert Member
Joined Jan 15, 2015
5,266 2,938 280
Sasa huwezi changanua humu gharama zake.namna ya kupata hao Samaki wadogo kwa faida ya wengi
Bei ya rejareja kwa kifaranga kimoja ni sh 300 kwa sato na 500 kwa kambale.Tanzania wanapatikana TAFIRI mwanza,dar wapo wanaitwa Big Fish(bigfishtz.com) na Kenya wapo wanaitwa Jambo Fish Farm(jambofish.co.ke) hawa ndio wana mbegu nzuri zinazokua haraka.Sijui maelezo yamejitosheleza?
 
L

Lacute

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2015
Messages
310
Likes
28
Points
45
L

Lacute

JF-Expert Member
Joined Apr 28, 2015
310 28 45
Bei ya rejareja kwa kifaranga kimoja ni sh 300 kwa sato na 500 kwa kambale.Tanzania wanapatikana TAFIRI mwanza,dar wapo wanaitwa Big Fish(bigfishtz.com) na Kenya wapo wanaitwa Jambo Fish Farm(jambofish.co.ke) hawa ndio wana mbegu nzuri zinazokua haraka.Sijui maelezo yamejitosheleza?
Bado jayajajitosheleza mkuu, mchanganuo wa gharama haupo umeeleza tu bei ya vifaranga.
 
bukoba boy

bukoba boy

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2015
Messages
5,266
Likes
2,938
Points
280
Age
33
bukoba boy

bukoba boy

JF-Expert Member
Joined Jan 15, 2015
5,266 2,938 280
Yaaap ,nashukuru mleta mada maana amenigusa sana Nina mpango wa kufuga samaki hapa mwanza ! Na nimepewa somo hilo hivi karibuni,na kwa Bahati tena nimelipata hapa asanteni sana
Karibu sana kiongozi.
 

Forum statistics

Threads 1,238,798
Members 476,185
Posts 29,330,975