Ufugaji wa kisasa wa Nyuki: Faida, Utaalam na Masoko

nimeku PM namba yangu tuwasiliane,majibu ya maswali yako yote nnayo tuwasiliane mkuu
 
nimevutiwa na ufugaji wa nyuki yaani uvunaji wa asali, nimesikia ni ujasiriamali mzuri ambao unaweza kumtoa mtu kimaisha. Anayefahamu ufugaji wa nyuki naomba anisaidie nipate kufahamu huu ufugaji kiundani, ikiwezekana gharama na mchanganuo wa ufugaji wake.

1. Naomba ufafanuzi nasikia kuna asali nzito na nyepesi, pia asali ya nyuki wadogo na asali ya nyuki wakubwa. Kuna asali ya aina gani na ipi?

2. Je, ufugaji wa nyuki una msimu? Miezi ipi basi ni mizuri kwa ufugaji wa nyuki?

3. Asali nzuri inayopendwa sana ni ya mkoa gani?

4. Utengenezaji wa mizinga unakuwaje, ukubwa wa mizinga au dimensions ipi ni kikomo au ipi ni safi? Gharama za kutengeneza mzinga ni ipi?

5. Utoaji wa asali unakuwaje lita ngapi kwa dimension ipi ya mzinga?

6. Mahitaji muhimu kwa ufugaji wa nyuki / kinachovuta nyuki ni kipi?

7. Asali inaiva inakomaa baada ya muda gani?

8. Soko la asali kwa bei ya jumla lipo wapi hapa dar?

9. Je soko la nje la asali lipo wapi sana? Usafirishaji wa asali nje ya nchi unakuwaje?

10. Changamoto na mengineyo ni yapi?

Asanteni

wasiliana na liwalo naliwe
 
..1. Naomba ufafanuzi nasikia kuna asali nzito na nyepesi, pia asali ya nyuki wadogo na asali ya nyuki wakubwa. Kuna Asali ya aina gani na ipi?
Ni kweli ziko asali nzito na nyepesi, amber, nyeupe na nyeusi. Uzito au rangi za asali kwa kiwango kikubwa huchangiwa na aina ya maua ambayo nyuki huchukua mchozo wa kutengenezea asali. Mfano asali ya maeneo mengi ya Tabora ni nyeusi wakati ile ya Singida maeneo ya Sanjaranda na Itigi ni amber ilhali ile ya Dodoma ni nyeupe na ina machicha kama barafu.

Aina ya nyuki wanaofungwa zaidi katika maeneo ya Kitropiki na Tanzania ikiwemo ni Apis Mellifera mbao tuliowengi tunawafahamu kama nyuki wakubwa. Hawa nyuki ni wakali na wana mwiba unaotumika kujihami. Tofauti na nyuki wadogo ambao ni wapole na asali yake inatumika zaidi kama dawa
..2. Je, ufugaji wa nyuki una msimu? Miezi ipi basi ni mizuri kwa Ufugaji wa Nyuki?
Ufugaji wa Nyuki ni kazi ya kudumu lakini uvunaji wa mazao ya nyuki hufanyika kwa misimu. Iko mikoa nchini mwetu ambayo huwa na misimu miwili kwa mwaka; Msimu mdogo na msimu mkubwa. Maranyingi asali inayopatikana katika msimu mdogo huwa ni ya masega ambayo hayajakomaa. Ninaweza kukushauri kwenye hili pale utakapo kuwa umeisha amua wapi utaweka mizinga. La muhimu ni kujua msimu wa maua unaanza lini. Hii itakusaidia kupata nyuki-wakaaji hii itakuhakikishia masega kujenjwa katika muda mfupi.
..3. Asali nzuri inayopendwa sana ni ya mkoa gani?
Watanzania wengi wanapenda asali ya amber. Ili kisayansi asali ya Dark-Blue ina virutubisho vingi zaidi. Mkoa wa Kigoma unaibuka kama chanzo cha asali nzuri na bora. Ninaposema bora namaanisha ulinaji unaozingatia kanuni bora, ukamuaji unaojali usafi na upakiaji katika vifaa safi na bila kuongeza kitu chochote (adulteration)
..4. Utengenezaji wa mizinga unakuwaje, ukubwa wa mizinga au dimensions ipi ni kikomo au ipi ni safi? gharama za kutengeneza mzinga ni ipi?
Iko mizinga ya aina mbalimbali na hivyo bei tofauti tofauti. Kwa maelezo ya kina nitumie email ekimasha@jamiiforums.com
..5. Utoaji wa asali unakuwaje lita ngapi kwa dimension ipi ya mzinga?
Aina ya mzinga inaushawishi katika ubora na kiwango cha asali inayopatikana. Majibu zaidi ya swali hili nitayaandaa au nitakupatia vitabu vyenye vipimo ambavyo vitakupanua uelewa kwenye suala hili.
..6. Mahitaji muhimu kwa ufugaji wa nyuki / kinachovuta nyuki ni kipi?
Miti na maua yanayotoa mchozo ni muhimu sana. Lakini pia chanzo cha maji lazima kipatikane katika eneo la mzingo usiozidi ekari tano
..7. Asali inaiva inakomaa baada ya muda gani?
Sikumbuki vizuri. Nitauliza
..8. Soko la Asali kwa bei ya jumla lipo wapi hapa dar?
Soko la Jumla litakulipa lakini si vizuri sana kama kupaki kwenye chupa na kusambaza katika Min and Supermarkets. Pia unaweza kufanya direct home delivery. Soko la Jumla liko kwa wapakiaji wa Dar (Honey Packers) ambao wengine hufuata moja kwa moja kutoka huko mikoani.
..9. Je soko la nje la asali lipo wapi sana? Usafirishaji wa Asali nje ya nchi unakuwaje?
Mimi ni muumini wa soko la ndani. Hii inatokana na ugumu na vikwazo vingi vilivyoko katika soko la nje na mwisho wa siku profit-margin ni ndogo sana. Soko la ndani ni kubwa mno ndo maana bado supermarkets zetu zimejazwa na asali kutoka Brazil, india na China.
 
Mkuu Kimasha kaeleza vizuri, nyongeza zitafuata baada ya mwenye uzi kuzitaka. Mfano, wapi nyuki wadogo wanapatikana kirahisi,nk
 
Wadau Wa Ufugaji Nyuki. Naombeni Ushauri Wa Kitalaamu Juu Ya Ufugaji Nyuki Na Uvunaji Wake Kwa Njia Za Kisasa. Pia Mnijuze Bei Ya Mzinga Mmoja Wa Kisasa Kwa Ajili Ya Kufugia Nyuki Ni TSh. Ngapi?
 
Ndugu,

Ufugaji nyuki kisasa una mambo mengi ya kuzingatia, kwa uchache mambo hayo ni:
  • Uchaguzi bora wa eneo la kufugia nyuki - liwe na chakula kwa ajili ya nyuki (ingawaje nyuki hujitafutia wenyewe chakula hata maeneo ya jirani), kuwe na maji (ya asili au ya kuwekwa), liwe na utulivu, liwe mbali na makazi ya watu na liwe linafikika.
  • Aina ya mizinga ya kutumia - Ili uwe ufugaji wa kisasa, mizinga ya kutumia pia iwe ya kisasa. Kuna aina nyingi ya mzinga kama traditional hives, modern top bar hives na commercial hives. Bei hutofautiana kulingana na eneo ulilopo na ubora. Kwa eneo nilipo mzinga wa modern top bar ni kati ya Tshs 60k na 70k, commercial beehive ni kati ya Tshs 120k na 150k. Ushauri wangu kwako kama uwezo unaruhusu nunua commercial beehives kwani inakuhakikishia kumantain makundi ya nyuki na mavuno ni mara nyingi kwa mwaka (utapata asali nyingi) na hutoa asali bora.
  • Vitendea kazi vya kisasa - hapa nazungumzia vifaa vya ukaguzi, mashine ya uvunaji pamoja na vifaa vya kuhifadhia asali. Mfano mavazi ya kujikinga na nyuki, smoker, mashine ya kurina asali n.k. Cha kuzingatia hapa ni kuwa na vifaa vya kutosha na bora.
  • Usimamizi wa shamba na nyuki wenyewe - hapa ndio wafugaji wengi wanakwama. Wengi hudhani nyuki hawahitaji ukaguzi. Ukweli ni kwamba usimamizi bora wa shamba na ukaguzi wa angalau mara 1 - 2 kwa mwezi husaidia kujua hali ya mzinga, maendeleo ya kundi, lini utarajie kuvuna n.k. Pia husaidia kuondoa wadudu waharibifu wa nyuki na vihatarishi vingine.
Nafikiri nimekusaidia kidogo mahali pa kuanzia ufugaji wako wa kisasa wa nyuki. Mimi pia ni mfugaji, kwa msaada zaidi tuwasiliane.
 
Mkuu nina mswali mawili matatu mkuu...

Mzinga huo wa commercial unaweza kutoa lita ngapi kwa mwaka?? hasa ukizingatia kuwa uvunaji hufanyika mara mbili..

Je kama utapata eneo na ukaandaa kabisa bustani ya maua na maji ya kutosha je itaongeza uzalishaji wa asali???
 
Ndugu,

Ufugaji nyuki kisasa una mambo mengi ya kuzingatia, kwa uchache mambo hayo ni:
  • Uchaguzi bora wa eneo la kufugia nyuki - liwe na chakula kwa ajili ya nyuki (ingawaje nyuki hujitafutia wenyewe chakula hata maeneo ya jirani), kuwe na maji (ya asili au ya kuwekwa), liwe na utulivu, liwe mbali na makazi ya watu na liwe linafikika.

  • Aina ya mizinga ya kutumia - Ili uwe ufugaji wa kisasa, mizinga ya kutumia pia iwe ya kisasa. Kuna aina nyingi ya mzinga kama traditional hives, modern top bar hives na commercial hives. Bei hutofautiana kulingana na eneo ulilopo na ubora. Kwa eneo nilipo mzinga wa modern top bar ni kati ya Tshs 60k na 70k, commercial beehive ni kati ya Tshs 120k na 150k. Ushauri wangu kwako kama uwezo unaruhusu nunua commercial beehives kwani inakuhakikishia kumantain makundi ya nyuki na mavuno ni mara nyingi kwa mwaka (utapata asali nyingi) na hutoa asali bora.

  • Vitendea kazi vya kisasa - hapa nazungumzia vifaa vya ukaguzi, mashine ya uvunaji pamoja na vifaa vya kuhifadhia asali. Mfano mavazi ya kujikinga na nyuki, smoker, mashine ya kurina asali n.k. Cha kuzingatia hapa ni kuwa na vifaa vya kutosha na bora.

  • Usimamizi wa shamba na nyuki wenyewe - hapa ndio wafugaji wengi wanakwama. Wengi hudhani nyuki hawahitaji ukaguzi. Ukweli ni kwamba usimamizi bora wa shamba na ukaguzi wa angalau mara 1 - 2 kwa mwezi husaidia kujua hali ya mzinga, maendeleo ya kundi, lini utarajie kuvuna n.k. Pia husaidia kuondoa wadudu waharibifu wa nyuki na vihatarishi vingine.
Nafikiri nimekusaidia kidogo mahali pa kuanzia ufugaji wako wa kisasa wa nyuki. Mimi pia ni mfugaji, kwa msaada zaidi tuwasiliane.

Mkuu ni muda gani muafaka wa kulina asali? au miezi ipi? au kipi kiashiria sasa ni muda muafaka wa kulina asali?
 
kwa kweli namimi napenda kufuga nyuki lakini eneo lenyewe ni pwani. halafu maeneo ya karibu watu
wanalima matikiti ambayo hupuliziwa dawa. napata kigugumizi kidogo
 
1.Pata ufahamu wa uhusiano baina ya nyuki na mwanadamu katika eneo lako
2.Jifunze namna ya kufuga nyuki
3.
Pitia visa kadhaa vya kung’atwa kabla ya kujitolea kufuga nyuki
4.Unda utaratibu mzuri na ulioboreshwa wa ufugaji wa nyuki
KUMBUKA KUJUA
1.Ni nani wa kufanya kazi naye?
2.Vifaa gani vinafaa kutumiwa?
3.Ni wapi pa kuuza bidhaa za mzinga?
Karibu tuweze kukusaidia namna ya kuandaa mchanganuo wa mradi wa nyuki
Ni mchanganuo ambao ni wa kiushindani na unaweza kuupeleka benki na ukapewa mkopo bila shida AU tunaandika mchanganuo ambao utatumia ukiwa na mtaji wako mwenyewe

0713659828 au 0763487330

Ahsante sana.

Swali, Je nyuki wanaweza kupatikana mahali popote as long as kuna mapori naweza kutundika mzinga wangu?
 
Salaam,
miaka mingi iliyopita, nilimsikia mtaalam mmoja akielezea vitu kuhusu ufugaji wa nyuki ambavyo sikubaini undani wake, kimoja wapo ni kuhitajika pembe tatu kati ya chanzo cha chakula, maji, na mzinga kama, sijasahau. Unaweza nipa dokezo maana nafikiria usoni kufuga na nyuki.
 
Habari ndugu yangu,
Siyo kweli kwamba kila msitu unaweza kuwa mahali sahihi kwa maisha ya nyuki. Nyuki hupendelea sana sehemu yenye maua, hivyo msitu wenye miti yenye maua inaweza kuvutia nyuki LAKINI nyuki huwa wananunuliwa katika makundi,kwa maana hiyo hata kama msitu hauna maua,unaweza kupanda miti inayotoa maua mara baada ya kununua hao nyuki.
Kuhusu pembe tatu ni kwamba, Sehemu yeyote yenye mzinga lazima iwe na chakula cha nyuki na mara nyuki wakishakula lazima wapate maji ya kunywa. MZINGA+CHAKULA+MAJI=ASALI
 
Sikufahamu kwamba naweza kuwapanda nyuki shambani!!

Sasa hao nyuki wanauzwa wapi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom