Ufugaji wa kisasa wa Nyuki: Faida, Utaalam na Masoko

Mkuu Malila ,kijiji cha Chogo kipo wapi?Je wanaweza kuituma Dar mizinga kwa bei nafuu.
Mkiunganisha nguvu mtafanikiwa haraka, kwa mfano,mwezi jana nilipokuwa kijiji kimoja kinaitwa Chogo huko Iringa,niliona mzinga mmoja unafikia Tsh 8000/ kuutengeneza kisasa pale pale kijijini na wenyewe wanasema una ujazo wa debe moja na nusu. Mavuno ni mara mbili kwa mwaka.
 
Mkuu Malila ,kijiji cha Chogo kipo wapi?Je wanaweza kuituma Dar mizinga kwa bei nafuu.

Kipo Iringa wilayani Mfindi. Kama ni mizinga ya nyuki nenda Kibaha pale karibu na kituo cha polisi,lipo shamba pale la mfano,unachukua mzinga mmoja unampa fundi anakutengenezea,japokuwa bei itakuwa juu kidogo kwa sababu ya vifaa hasa mbao. Mizinga inaweza kusafirishwa bila taabu kutokea Uyole Mbeya. Unaweza kupata yenye nyuki tayari,hasa nyuki wadogo. Ukiwa tayari,bora ufuge nyuki wadogo kwa sababu hawaumi na unaweza kukaa nao ndani kwako bila taabu.

Jamaa yangu wa Mbeya huwa anawaletea mizinga hiyo yenye nyuki wadogo. Na ukiwa na bustani yenye miti michache na ukaitundika hapo inapendeza sana. Kuna jamaa pale Kimara ana mizinga miwili upenuni mwa nyumba yake ktk dirisha la sebuleni hadi raha.
 
jamani yeyote anayejua kuhusu ufugaji wa nyuki, mizinga na jinsi ya kulina anieleweshe. natamani kufanya biashara hii nkimaliza chuo.

Ufugaji wa Nyuki ni Ajira nzuri kwa mtu makini. Na wala usihofu kuhusu soko, weka mkazo katika kuhakikisha unazalisha asali ya kutosha. Na hili utalifanikisha pale tu ukiweza kutumia pembejeo (m.f mizinga, n.k) zilizoboreshwa.

Mizinga inayopendekezwa ni ile ya Tanzania Top Bar Hives. Natofautiana na Malila, mizinga hii inauzwa kati ya TShs. 35,000-50,000 mmoja. Na hata ukitengeneza mwemyewe, gharama ya mbao na vifaa vingine haiwezi kuwa chini ya TShs. 20,000! Mizinga hii ndo imethibitisha uwezo wa kuzalisha makundi makubwa ya nyuki na hivyo kufanya uzalishaji wake wa mazao ya nyuki (asali, royal jery, propolis, nta) nao pia kuwa mzuri. Ni rahisi kupandisha mzinga huu na pia ni rahisi kupakua/kulina asali kwa kutumia mzinga huu.

Unaweza kupata ushauri na maelezo zaidi juu ya Ufugaji na maelekezo ya wapi utapata pembejeo kupitia watu wafuatao:

Dr. Mushtaq Osman-UDSM
Dr. Danstan Kabialo-Afri Honey/Tanzania Honey Council
Mr. Sosthenes Sambua-TPSF
Mr. David Kamala-Tanzania National Beekeeping Supply Ltd
Mr. Jumanne Msuya-MNRT Beekeeping Division

Hawa niliowataja watakushauri haraka na kwa wepesi. Wamebobea na kuzama vilivyo katika sekta hiyo. Iwapo utasoma hapa na kama una dhamira thabiti juu ya ombi lako, nitakuwa tayari kukuunganisha na yoyote kati ya hao watu niliowataja. Japo mara nyingine wao hutoza ghalama kidogo ya thamani ya muda, taarifa na maarifa.

Dah afadhali umeamua kuanza harakati za kijiajiri mapema. Na mimi nataka kujiajiri nitafurahi kupata maelekezo juu ya ufugaji nyuki

Hata mimi niko tayari kwa kujiajiri, ila tatizo na kupata watu ambao mna lengo moja. Mimi binafsi nimependa idea ya kufuga nyuki lakini mnaonaje tukiunganisha nguvu na kufanya kitu in large scale?
 
Nadhani the best way to tackle hii issue ni kuangalia from selling point of view, market.... Je unaweza kununua asali lets say from Tabora ukaipackage vizuri na kuiza nchi za nje au sehemu nyingine. From my research other people make more money from bees than the bee keepers just like the middle men wanavyotengeneza pesa zaidi kuliko wakulima wenyewe. Kwahiyo soma hiyo link niliyokupa hapo juu kuhusu kufuga nyuki ila kama unataka kama biashara pekee utatengeneza more money kuinunua kwa jumla from tabora (including nta) package vizuri na kuresale kwenye supermarkets, au nchi nyingine My point being to make profit from eggs you dont need kufuga kuku unless you love and you are ready kufuga kuku na kuna forum ya wafuga nyuki Can you make a living with Bees - Beesource Beekeeping Forums

Nimpenda mchango wako kuhusu swala zima la kufuga nyuki. Ninachouliza, hivi hatuwezi kuunganisha nguvu na kuanzisha project ya producing, processing and packaging? Siyo lazima tuanze vyote kwa pamoja ila inaeweza ikawa ndiyo mid or long-term objectives.
Nawasilisha. Thanks.
 
Nadhani the best way to tackle hii issue ni kuangalia from selling point of view, market.... .. From my research other people make more money from bees than the bee keepers just like the middle men wanavyotengeneza pesa zaidi kuliko wakulima wenyewe. [/url]

Huu ni UKWELI usiopingika. Na hii si katika mazao ya nyuki (asali, nta, maziwa ya nyuki, propolis, venom) tu, balii suala hili liko katika mazao yote ya kilimo ambayo hayana Bodi au Watetezi.

Kwa kutambua huu unyonyaji wa middle-men, SIDO imeanzisha mradi unaitwa Muunganisho wa Ujasiriamali Vijijini (MUVI). Moja ya eneo kuu linaloshughulikiwa na MUVI ni kuhakikisha, pamoja na mkulima kulifikia soko kupitia madalali lakini naye apate tija (Farm gate price) ya suluba anapata kuzalisha
 
Ufugaji wa Nyuki ni Ajira nzuri kwa mtu makini. Na wala usihofu kuhusu soko, weka mkazo katika kuhakikisha unazalisha asali ya kutosha. Na hili utalifanikisha pale tu ukiweza kutumia pembejeo (m.f mizinga, n.k) zilizoboreshwa.

Mizinga inayopendekezwa ni ile ya Tanzania Top Bar Hives. Natofautiana na Malila, mizinga hii inauzwa kati ya TShs. 35,000-50,000 mmoja. Na hata ukitengeneza mwemyewe, gharama ya mbao na vifaa vingine haiwezi kuwa chini ya TShs. 20,000! Mizinga hii ndo imethibitisha uwezo wa kuzalisha makundi makubwa ya nyuki na hivyo kufanya uzalishaji wake wa mazao ya nyuki (asali, royal jery, propolis, nta) nao pia kuwa mzuri. Ni rahisi kupandisha mzinga huu na pia ni rahisi kupakua/kulina asali kwa kutumia mzinga huu.

Unaweza kupata ushauri na maelezo zaidi juu ya Ufugaji na maelekezo ya wapi utapata pembejeo kupitia watu wafuatao:

Dr. Mushtaq Osman-UDSM
Dr. Danstan Kabialo-Afri Honey/Tanzania Honey Council
Mr. Sosthenes Sambua-TPSF
Mr. David Kamala-Tanzania National Beekeeping Supply Ltd
Mr. Jumanne Msuya-MNRT Beekeeping Division

Hawa niliowataja watakushauri haraka na kwa wepesi. Wamebobea na kuzama vilivyo katika sekta hiyo. Iwapo utasoma hapa na kama una dhamira thabiti juu ya ombi lako, nitakuwa tayari kukuunganisha na yoyote kati ya hao watu niliowataja. Japo mara nyingine wao hutoza ghalama kidogo ya thamani ya muda, taarifa na maarifa.

Ericus Kimasha,
+255-71-3-177-372
E-mail: ekimasha@gmail.com

Uko sahihi kabisa, kwa sababu niliagiza mzinga mmoja wa aina hii ya Top bar pale Uyole na bei yake ilikuwa ina-range kati ya Tsh 30,000/ mpaka 35,000/. Tatizo mizinga inayotengenezwa vijijini hawafuati utalaam wo wote, na bado nilipofika Image jamaa alikuwa tayari kunitengenezea mzinga kwa miti asili kwa Tsh 5000/ tu. Suala linakuja wakati wa kuvuna asali.

Asante kwa contacts hizo, zitatumika tu soon.
 
Ndugu wanaJamii,

Natanguliza shukruni zangu kwa Elimu ya michango yenu mingi juu ya kilimo, ufugaji wa kuku, na mambo mbalimbali yahusuyo ustawi wa taifa letu.

Niwapongezeni pia wale wanaosukuma gurudumu la maendeleo ya nchi za nje, kwani wanalipa kodi ambayo inakuja kama mkopo au msaada hapa Tanzania!

Wakuu popote mlipo nimeamua kujichukulia pori la kutosha, plan yangu ni kufuga nyuki na kuzalisha asali ya kutoka na kuiuza ndani na nje ya nchi.

Wanajamii haswa wale wa Bee Keeping SUA, nisaidieni utalaamu!
 
Mkuu nenda Mkambalani Moro pale, kuna kikundi kinahudumiwa na watalaamu wa SUA, utapata vyote pamoja, simu yao ni 0754878626.
 
Vilevile Tabora kuna chuo cha Nyuki itakuwa vizuri kwenda kupata utaalamu zaidi.
 
Ninataka kujikita rasmi kwenye ujasirimali ambao hautakua na risk kubwa. Nimefikiri Ufugaji wa Nyuki unaweza kuwa na tija kwa sababu hawahitaji chanjo, maji, umeme, ni kuweka mzinga na kwenda tu kuvuna kila inapojaa.

Ni nani mwenye taarifa kuhusu mradi kama huu?

- Ni wapi hasa kunafaa kwa ufugaji? nawezafuga vizuri mikoa ya pwani?
- risk zake ni zipi?
- soko lake likoje?
 
Kuna uzi kama huu ktk jukwaa hili,utafute ili upate kila kitu. Mikoa ya pwani sio mizuri sana kwa nyuki kwa sababu ya uhaba wa chakula cha nyuki kwa sehemu kubwa sana ya mwaka. Nimeona mizinga michache ktk pori la muhoro mpaka Somanga. Tabora/Chunya/Singida ni kuzuri kwa sababu manpower yenye kuelewa ufugaji wa nyuki ipo.

Ili ufuge na kupata asali bora, epuka maeneo yenye mashamba makubwa yanayotumia madawa ya kuulia wadudu. Jitahidi upate asali safi kwa maana kwamba isiwe na traces za madawa. Nyuki huruka umbali wa kilomita 4 toka ulipo mzinga wake.

Ukienda SUA kuwapata watalaam itakuwa bora,wao wanajua mapori mazuri kwa nchi nzima.
 
kama unaweza fika Arusha wasiliana kwa namba hii 0754978750 .Anaitwa Mwl Makawa,atakusaidia sana maana ni mtaalamu wa ufugaji nyuki.
 
Wadau naomba msaada ni wapi jijini Dar-es-salaam naweza kupata ushauri kuhusu Ufugaji wa nyuki kwa kutumia njia za kisasa. nina shamba nje ya jiji ambalo nataka nifanye shughuli hiyo. Asante!
 
Mkuu ungekuwa unaishi Arusha ningekushauri upitie TAWIRI maeneo ya Njiro mkabala na IAA kama una jamaa yako Arusha mwambie apitie TAWIRI achote elimu ya uhakika.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom