Mwongozo wa ufugaji wa kisasa wa Mbuzi wa nyama na maziwa

Samadi tu inatosha na matokeo yanakua mazuri hizo za kiwandani achana nazo zisikuumize kichwa...
Ahsante Mkuu!

Sasa je mavuno yatakua mengi na Mara kwa Mara kama ambao wanatumia ya kiwandani?

Nimesoma mahali nikaone wanasema mbolea inayohitajika Ni Single/Triple super phosphate(TSP) ya maji!
je nikitumia TSP ya punje nitakua nimekosea?

Nisaidie hayo maswali kama unauelewa nayo mkuu
 
Habar zenu, jaman naomben mnisaidie nahitaji kuanza kufuga mbuzi wa kienyej na baadae kuwauza nipen idea , naweza kupata wa sh ngap ngap?
 
Huu uzi wako utakuwa msaada kwangu. Maana nilikuwa na wazo hili.

Wafugaji mje mtupe maujanja
 
Inategemea upo wapi mfano huku Arumeru mnadani ijumaa unaweza pata kuanzia 55 hadi 80 itategemea na mbuzi ukubwa na hali ya mnada ilivyo.

Wazo lako zuri sana ila inabidi ucheze sana na muda.
 
Asante mkuu mi nipo Dsm
Dsm hautafaidi, maana naona kama dsm pamebanana sana na risk ni nyingi.

Huo mradi ufanyie mikoani ambapo kuna nafasi pamoja na chakula cha kutosha.

Maeneo ya Tabora wilaya za Uyui, Nzega na Igunga inafaa sana kufuga hao small ruminant goat inclusive.

Maeneo yote ya Singida na Dodoma yanafaa pia.
 
cha mideko huyu anataka kufuga ama mwingine? anyway unaweza sogea hapo vigwaza mnadani ama ukaingia kule kwa mang'ati kule vigwaza ukasaula saula na kuvuruga vuruga huko utatoka na mbuzi wengi na kwa bei nafuu, mfano nbuzi wa wastani yani mwaka mmoja unaweza kumpata kwa 30-50 elfu, niiishie hapo maana ndo ulihitaj hapo, Mafanikio mema mkuu
 
Mkuu hizo mbegu mara nyingi ni genetically modified kama vitu vingine ili tu kukidhi mahitaji ya binadamu. So, sijui unafki wangu unahusika na nini hapa.

Hilo nakukatalia. Nimekwishaona local breeds kabisa anazaa wa4 kule Kasulu Kigoma. GMO imetoka wapi kwa mbuzi wa kijijini namna hiyo?
 
mimi natafuta ranch kubwa hizo za selikali, nataka kufuga ng'ombe wa maziwa na nyama si chini ya mia tano kwa kuanzia. kama kuna mtu anayeweza kunisaidia namna ya kuzipata anipigie pande hapa. kwahabari ya pesa, si zaidi ya $1 million. asanteni.

Mkuu shambaboy nipo
 
Back
Top Bottom