Aman Ng'oma
JF-Expert Member
- Nov 8, 2011
- 954
- 510
TUANGAZIE UFUGAJI WA MBUZI KATIKA BIASHARA
Kwa ujumla ufugaji wa mbuzi ni biashara kubwa. Kama mfugaji atafuata na kuzingatia kanuni bora za ufugaji wa mbuzi hataweza kupata hasara.
Mara nyingi mbuzi husumbuliwa zaidi na magonjwa ya mapafu. Ugonjwa huu ikiwa mbuzi watacheleweshwa kutibiwa utawafanya wafe kwa wingi na kwa haraka. Dalili ya ugonjwa wa mapafu ni pamoja na kwamba mbuzi wanakuwa na homa kali, kukohoa, na vifo hutokea baada ya siku 1-2 tu. Ni muhimu kutambua mapema dalili za ugonjwa huo ili mbuzi wawahi kutibiwa kwa haraka.
Mbuzi ni tofauti na ng'ombe ni wastahimilivu sana dhidi ya ukame. Wanakula nyasi pia wanakula majani ya miti. Ikitokea nyesi zimekwisha au kukauka watandelea kuishi na kuzaliana kwa kula majani ya miti.Wakati wa kiangazi mmiliki wa mradi wa ufugaji wa mbuzi huwi na presha juu ya chakula cha kuwalisha mbuzi.
Thamani ya mbuzi imekuwa kubwa hasa mjini kutoka na watu wengi kuhitaji nyama choma ya mbuzi hivyo hutoa hakikisho la faida kwa mwenye mradi .Isiteshe mbuzi huzaliana haraka sana ndani ya muda mfupi na kufanya kundi lao liongezeka kwa kasi. Kwa wastani toka mbuzi ashike mimba hadi kuzaa(Gestation period) huwa inamchukua siku 150 sawa na miezi 5,ndani ya mwaka mmoja mbuzi anazaa mara 2.
Ukiwa na mbuzi 50 majike na madume 2 katika uwiano wa 1:25, ndani ya miaka 3 utakuwa na mbuzi majike jumla 200+madume 152 hawa ni wazazi na watoto wao +118 majike na 118 madume hawa ni watoto wa watoto. Kwahiyo jumla kuu utakuwa na mbuzi 588 hii idadi na ndani ya miaka 3 kati ya hao madume yatakuwa 270 na majike yatakuwa 318. Hii hesabu niliyofanya kupata hii idadi ya mbuzi jumla kwa miaka 3 ni hesabu kali sana. Unaanza na mbuzi hamsini unamaliza na mbuzi 588 ndani ya miaka 3.