Pata ushauri, michango na mawazo ya ufugaji wa bata wa kienyeji kibiashara

Rinsa

Member
Dec 13, 2007
8
3
Wanajamii,

Kama kuna mtu ana utaalam wowote wa ufugaji wa bata naomba tupeane elimu ili tuweze kufuga kisasa kwa ajili ya kutengeneza kipato.

Naombwa kujuzwa wana jamvi na kupewa darasa kuhusu elimu ya ufugaji bata

1. Wapo aina ngapi?
2. Wanaatamia mayai kwa mwaka mara ngapi?
3. Soko halisi likoje kwa mfano kama naishi DSM
4. Vyakula wanavyokula kama nikitaka kuwafuga kibiashara
5. Je, naweza kutotoleshea mayai yao kwa kutumia incubator?

Kama kuna mtu anawafuga naomba anipe mawasiliano yake niweze kupata ujuzi kwa vitendo kwake. Nashukuruni na nawatakia mwisho mwema wa mwaka.

Wenu katika ujenzi wa taifa.
Kifuniko

distance_week_four_1.jpg


===============
Bata ni kama walivyo jamii nyingine ya ndege yaani poultry mfano kuku,kanga,Bata mzinga,njiwa,kwereakwerea, nk,.Mahihitaji yao yanafanana kabisa na yale ya jamii nyingine ya ndege.Chakula ambacho kuku anakula hata bata anakula. Bata wakilishwa vyakula vya kuku wa kisasa wanakua haraka na uzito wao huu mkubwa kwa muda mfupi .

Utagaji wa bata utakuwa mzuri kama utakuwa aidha na bwawa au mto uliopitishwa shambani kwani Bata anahitaji maji kwa asilimia 90.

Magonjwa yote anayopata kuku au jamii nyingine ya ndege pia bata hupata. Lakini ugonjwa unaowasumbua zaidi ni Mafua na kipindupindu.B ata ni wastahimilivu wa kupata magonjwa lakini wakipata ugonjwa uwezo wa kustahimili kwao huwa ni mdogo sana, mara nyingi huwa wanakufa hovyo hivyo umakini unahitajika.

Masoko ya Bata yako ya kutosha hasa kwenye mahoteli makubwa ya mijini. Wageni wengi sana wanahitaji nyama ya bata na kutokana uzalishaji wake kuwa mdogo ndio maana unakuta bei ya bata haikamatiki.

Ukijuhusisha na ufugaji wa bata, ndani ya muda mfupi, uwezekano wa kuwa tajiri ni mkubwa sana. Hebu tazama Tanzania sijasikia kampuni yoyote inayojihusisha na utotoreshaji na uuzaji wa vifaranga wa bata.

Asikudanganye mtu nyama ya bata ni tamu sana. Tatizo letu watanzania ni mazoea mazoea. Tumezoea zaidi nyama ya Ng'ombe, mbuzi na kuku. Lakini nyama ya Kondoo, bata na kanga si maarufu sana.

Kama mtu ukaaanzisha miradi ya ufugaji wa wanyama kama kondoo, bata na kanga wakapewa promo nadhani biashara itafanyika. Ebu fikiria hoteli zinaagiza bata kutoka magereza bwawani na unakuta mahitaji yanakuwa makubwa kuliko uzalishaji.
 
Rinsa,

Binafsi sina utaalamu sana katika kufuga bata, bali naweza kuzungumzia juu ya uzoefu. Sijafahamu unahitaji kufuga bata wa aina gani, lakini mimi nimeshawahi kufuga bata maji (kawaida) na bata mzinga, hawa bata maji nilinunua watano tu na hatimae baada ya muda mfupi nilikuwa na bata wengi sana hadi nikaaza kuona kero hapo nyumbani kwani nilikuwa nawaachia tu, niliamua kuwavuna wote kwani nilishauriwa na daktari kwamba siyo vyema kuweka bata hawa endapo ninafuga kuku wa kisasa (broiler); lakini bata mzinga bado ninaendelea nao.

Sijaona shida sana katika ufugaji wa bata, hivyo naweza kukushauri kufuga tu. Kuhusu soko nasikia wachina wanawanunua sana, hivyo kama kuna Chinese restaurant karibu unaweza kuulizia soko lake.
 
Last edited by a moderator:
Hata mimi niko na interest na hili, reason being, bata sio wasumbufu kwenye ufugaji wake, ishu ni namna gani unaweza kuwafuga wengi kibiashara?
 
Ni mapishi tu!
Hata nyama unazofikiri ni tamu, zisipopikwa/andaliwa vizuri zinakuwa sio tamu.
Wabongo wengi hawana ubunifu katika mapishi, na wanaanda bata kama wanavyoaandaa kuku, ndio maana anakuwa si mtamu.

mkuu...asante sana...nyama ya bata ni tamu sana especially ikitengenezwa in dry form... i love this stuff ...ukitengeneza mamichuzi imekula kwako
 
Wanajamii ,
Kama kuna mtu anautaalamu wowote wa ufugaji wa bata kibiashara naomba anijuze.Hii ikiwa ni pamoja na soko lake na management yake kwa ujumla.Mimi ni mwajiriwa na nipo hapa Dare salaaam nipo interested sana na ufugaji.Nawasilisha.

Watu wa Sua Morogoro nadhani watakuwa msaada ktk hili
 
Mkuu utapata hasara tuu kwani hakuna mtu anapenda bata siku hizi labda wachina tu. Nyama ya bata si tamu

Mkuu hapo kwenye red! We we we weeeeeeee! Nani alikwambia? Mkuu naona mama yoyo wako alichemsha kumtengeneza huyo bata! Asikwambie mtu Nyama ya bata haina mfano kama utakuta imepikwa na mtaalam wa mapishi hasa hasa mama kwa Kisukuma.

Hawa wadudu nilikuwa nawafuga enzi zile nikiwa shule ya msingi miaka ya late 70's na mapema 80's. Ilifikia hatua nikawa nao zaidi ya 100 kijiji kizima nilifahamika kwa ufugaji wa bata na nilikuwa natengeneza pesa siyo kawaida. Kwa ufupi hawana usumbufu kama wa kuku (mfano hawana magonjwa ya ajabu ajabu). Kwa muda wote niliokaa nao sikuwahi kuwapa dawa yoyote.

Kwa hiyo mkuu nakuomba ujaribu tena na uhakikishe mama yoyo amempika vizuri kabisa naamini utatuletea ushahidi hapa hapa jamvini!
 
Kuna mwanaJF mmoja aliuliza hivi karibuni kwenye uzi wake kwanini askari magereza wanapenda sana kufuga bata. Kama upo karibu na askari hao, jaribu kuwauliza taratibu za ufugaji wa bata!
 
Sijawahi ona chipsi bata, wala kwenye sherehe watu wanakula wali au pilau bata, wala sijawahi ona chips mayai ya bata.

Kwa mtazamo wangu hii inaashiria soko la bata ni finyu. Labda kama unafuga kwa chakula nyumbani na familia yako
 
Yai la bata bukini moja ni sh elfu kumi,bata bukini hapo makumbusho anauzwa laki mbili sabini bila kupungua,bata mzinga laki sabini bata maji elfu 30
 
Nimeanza na bata 40 me(10) na ke(30) ..je kuna mtu ana utaalamu ktk ufugaji wa bata wa kienyeji anisaidie.
 
Safi sana ndugu, hvi kuna bata wa kisasa na kienyeji?sina ujuzi ila ulizia ofisi za mifugo watasaidia sana na tafuta vitabu vya ufugaji pia. Mie nilifuga bata mzinga sema nilipohama ikasumbua nikawauza now nawaza tena.
 
Uzuri wa bata hawana shida ya magonjwa sana. Weka na kibwawa chao kidogo cha kuogelea!
 
MORIA... upo wapi. I have the same idea ya kufuga in large scale kwa matunzo ya kisasa zaidi .... nimejaribu kuwatunza watoto 11 wa bata walioanguliwa mwezi wa 7 kwa kuwapa broiler starter in first three weeks na baade kuwapa growers mash ikichanganywa na portion ya pumba za mahindi na matokeo ni mazuri sana ... watoto hawa sasa ni wakubwa sana with a high yield in growth

ninachotaka kufanya sasa hivi ni kununua mayai ya bata kwa wafugaji mbalimbali na kuyapeleka kuanguliwa kwa incubator machine, naanza na mayai 50 ... then from there I can propel the project well.

kumbuka bata wanakuwa vizuri kwa malisho ya majani (grazing) na maji kwa ajili ya spreening
 
Naomba msaada kama kuna mtu ana idea ya ufugaji bata kibiashara. Ninashukuru kwa mawazo chanya
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom