Ben255
New Member
- Dec 6, 2017
- 2
- 3
karibu mkuu kwenye fursa ya ufugaji wa bata mzinga. bata mzinga wanafugika kirahisi kuliko kuku kwa maana kwamba hawana changamoto nyingi kama kuku, ninawafuga bata mzinga pia nafuga kuku nimeona nakuthibitisha mwenyewe kauli hii niliyotoa. uzuri wao wana uwezo mkubwa wakustahimili magonjwa labda tuseme baadhi tu ya magonjwa ya kuku kama ndui ndio inaweza kuwasumbua ila si kwamba yaweza kuwaua kirahisi. ukiwa makini kuwapa chanjo na kua makini kufanya usafi bandani kwao. nikiwa na maana ya mazingira ya banda na vyombo vyakuwalishia chakula na maji, hutaona batamzinga akifa ovyo. jambo jingine ni umakini wa mazingira unapowafugia kwani hua wanapenda kudonoadonoa vitu mbalimbali na kumeza wakati mwingine vitu vikubwa ambavyo vyaweza kuwashinda kumeza jambo linaloweza kuwasababishia kifo endapo kitawakaba na kukosa mtu wakuwasaidia kutoa vilivyowakaba kooni. kuepuka changamoto hii ni kuhakikisha unawafugia bandani kwani humo bandandi utakua na uhakika na wanachokula hivyo kuepuka hasara inayoweza kutokana na changamoto hiyo. kwa anaehitaji vifaranga waweza kunitafuta kwa namba 0714756625 :::: 0623460298: napatikana dar es salaamNataka kufuga bata mzinga ila naomba mnifahamishe changamoto zao pia naomba kujua upatkanaji Wa masoko ya kuwauza pia ni wap nitapata vifaranga vya bata mzinga?
Naomba msaada wenu wakuu
Sent using Jamii Forums mobile app