Ufugaji wa Bata Mzinga, Bata Bukini na Kanga: Maoni, Ushauri, Utaalamu na Masoko

Usisahau kuwapa chanjo ya Newcastle siku ya 7 na gumboro siku ya 14 na hakikisha siku ya 19 hadi 23 unawapa dawa ya mafua, wawe na mafua au hawana mafua (kipindi hiki kanga hushambuliwa sana na mafua), wakifika siku ya 25 salama basi umekula bingo.

Mkuu wangu kidogo wameanza kudhoofika baada ya kuku kuanza kuumwa je naweza kuwapa chanjo au bado kwanza??
 
upload_2017-10-5_10-31-13.jpeg
Ili kuzaliana na kumpatia mfugaji faida, bata mzinga wanahitaji matunzo ya hali ya juu. Kwa kawaida bata mzinga hula chakula kingi kuliko kuku. Bei yake ni ghali zaidi. Kabla ya kuanza ufugaji wa bata mzinga ni lazima kuhakikisha una chakula cha kutosha kwa sababu ulishaji wa ndege hawa kadri wanavyokua huwa na gharama kubwa zaidi. Ni muhimu pia kujifunza kwa undani na kufahamu namna ya kutunza vifaranga wa bata mzinga kwa kuwa hufa kwa urahisi sana. Pia, unapaswa kujikita kutafuta soko kwa sababu wanapokuwa ni vigumu kuwatunza kwa muda mrefu kutokana na ukubwa wa gharama ya chakula.
Wafugaji wachache kati ya wengi waliojaribu kuwafuga ndege hawa na kufanikiwa hata kufikia malengo yao ni kutokana na kuzingatia lishe kamili. Pamoja na hayo, wapo wafugaji ambao walishindwa kutokana na magonjwa pamoja na gharama ya utunzaji.
Chakula
Chakula cha bata mzinga hakina tofauti na cha kuku. Vifaranga wanahitaji kupata lishe kamili yenye protini kwa wingi ili waweze kukua vizuri. Vifaranga kwa siku za awali wanahitaji kiasi cha asilimia 27 ya protini mpaka wanapofikia umri wa wiki sita. Baada ya hapo mfugaji anaweza kupunguza hadi kufikia asilimia 18, na kuendelea hivyo hadi wanapokomaa. Kutokana na gharama ya kununua chakula kuwa kubwa, unaweza kutumia reseheni ifuatayo kwa ajili ya kutengeneza chakula cha bata mzinga wewe mwenyewe.

Mahitaji
• Mahindi 5kg (yasiyokuwa na dawa)
• Karanga 5kg
• Dagaa 5kg
• Mashudu 10kg
• Chokaa 5kg (chokaa inayotumika kwa lishe ya mifugo)
Namna ya kutengeneza chakula
Twanga au saga pamoja kiasi cha kulainika kisha walishe vifaranga. Mchanganyiko huu hutegemeana na wingi wa bata mzinga unaowafuga. Hakikisha kila bata anapata chakula cha kutosha na chenye uwiano ulioelekezwa. Pia waangalie mara kwa mara kuhakikisha wana chakula cha kutosha.
Uhifadhi: Hifadhi chakula cha ziada kwenye mifuko au debe kisha weka sehemu isiyo na unyevu.
Kutaga
Bata mzinga huanza kutaga anapofikisha umri wa mwaka mmoja. Ndege hawa wana uwezo wa kutaga kati ya mayai 15 hadi 20 kwa mara ya kwanza na kisha kuhatamia. Anapoendelea kukua huweza kutaga hadi mayai 30. Hii ni kulingana na lishe nzuri atakayopatiwa.
Kuhatamia
Bata mzinga anaweza kuhatamia mayai 17 hadi 20. Mayai hayo huhatamiwa kwa siku 28 na huanza kuanguliwa vifaranga kwa muda wa siku 3, kuanzia siku ya 28 hadi 31. Baada ya hapo mayai yaliyosalia bila kuanguliwa hutakiwa kutupwa kwa kuwa hayatoanguliwa tena na hayafai kwa matumizi mengine.
Utunzaji wa vifaranga
Baada ya vifaranga kuanguliwa, watenge na mama yao kwa kuwaweka kwenye banda safi lisilopitisha baridi. Unaweza kuwawekea taa ya kandili au ya umeme endapo upo kwenye sehemu unakopatikana.
Banda
Ni vyema banda liwe limesakafiwa au banda la asili la udongo usiotuhamisha maji. Pia, unaweza kutumia banda lenye mbao au mabanzi kwa chini. Unaweza pia kutandaza maranda kwenye mabanda. Hakikisha kuta za banda zimefunikwa vizuri ili kuwakinga dhidi ya baridi.
Maji
Kama ilivyo ndege wengine, bata mzinga pia wanahitaji kupatiwa maji masafi na ya kutosha wakati wote. Wawekee maji katika chombo ambacho hawatamwaga na wanakifikia vizuri. Hakikisha maji hayamwagiki bandani kwani kwa kufanya hivyo banda litachafuka na kukaribisha magonjwa kwa urahisi. Ni vizuri kuwalisha bata mzinga vyakula vingine kama majani. Majani husaidia kuwapatia protini: mfano; kunde, fiwi na aina nyingine za majani jamii ya mikunde huhitajika zaidi kwa kiasi cha 25% hadi 30%.
Magonjwa
Bata mzinga hushambuliwa na magonjwa kama taifodi, mafua na kuharisha damu. Wanapougua ni rahisi kuambukiza kuku, bata na ndege wengine wanaofugwa kwa haraka sana. Pia, ndege hawa husumbuliwa na viroboto wanaosababishwa na uchafu wa banda hasa linapokuwa na vumbi.
Chanjo
Bata mzinga wanatakiwa kupatiwa chanjo ya ndui (mara moja kila mwaka), kideri (kila baada ya miezi mitatu), gumboro (kwa muda wa wiki tano - ukiwapa jumatatu, basi unawapatia kila jumatatu ya wiki), na vitamini A mara baada ya kuanguliwa.

Kwa mafunzo zaid tembelea www.lengisho.blogspot.com
 
View attachment 602460Ili kuzaliana na kumpatia mfugaji faida, bata mzinga wanahitaji matunzo ya hali ya juu. Kwa kawaida bata mzinga hula chakula kingi kuliko kuku. Bei yake ni ghali zaidi. Kabla ya kuanza ufugaji wa bata mzinga ni lazima kuhakikisha una chakula cha kutosha kwa sababu ulishaji wa ndege hawa kadri wanavyokua huwa na gharama kubwa zaidi. Ni muhimu pia kujifunza kwa undani na kufahamu namna ya kutunza vifaranga wa bata mzinga kwa kuwa hufa kwa urahisi sana. Pia, unapaswa kujikita kutafuta soko kwa sababu wanapokuwa ni vigumu kuwatunza kwa muda mrefu kutokana na ukubwa wa gharama ya chakula.
Wafugaji wachache kati ya wengi waliojaribu kuwafuga ndege hawa na kufanikiwa hata kufikia malengo yao ni kutokana na kuzingatia lishe kamili. Pamoja na hayo, wapo wafugaji ambao walishindwa kutokana na magonjwa pamoja na gharama ya utunzaji.
Chakula
Chakula cha bata mzinga hakina tofauti na cha kuku. Vifaranga wanahitaji kupata lishe kamili yenye protini kwa wingi ili waweze kukua vizuri. Vifaranga kwa siku za awali wanahitaji kiasi cha asilimia 27 ya protini mpaka wanapofikia umri wa wiki sita. Baada ya hapo mfugaji anaweza kupunguza hadi kufikia asilimia 18, na kuendelea hivyo hadi wanapokomaa. Kutokana na gharama ya kununua chakula kuwa kubwa, unaweza kutumia reseheni ifuatayo kwa ajili ya kutengeneza chakula cha bata mzinga wewe mwenyewe.

Mahitaji
• Mahindi 5kg (yasiyokuwa na dawa)
• Karanga 5kg
• Dagaa 5kg
• Mashudu 10kg
• Chokaa 5kg (chokaa inayotumika kwa lishe ya mifugo)
Namna ya kutengeneza chakula
Twanga au saga pamoja kiasi cha kulainika kisha walishe vifaranga. Mchanganyiko huu hutegemeana na wingi wa bata mzinga unaowafuga. Hakikisha kila bata anapata chakula cha kutosha na chenye uwiano ulioelekezwa. Pia waangalie mara kwa mara kuhakikisha wana chakula cha kutosha.
Uhifadhi: Hifadhi chakula cha ziada kwenye mifuko au debe kisha weka sehemu isiyo na unyevu.
Kutaga
Bata mzinga huanza kutaga anapofikisha umri wa mwaka mmoja. Ndege hawa wana uwezo wa kutaga kati ya mayai 15 hadi 20 kwa mara ya kwanza na kisha kuhatamia. Anapoendelea kukua huweza kutaga hadi mayai 30. Hii ni kulingana na lishe nzuri atakayopatiwa.
Kuhatamia
Bata mzinga anaweza kuhatamia mayai 17 hadi 20. Mayai hayo huhatamiwa kwa siku 28 na huanza kuanguliwa vifaranga kwa muda wa siku 3, kuanzia siku ya 28 hadi 31. Baada ya hapo mayai yaliyosalia bila kuanguliwa hutakiwa kutupwa kwa kuwa hayatoanguliwa tena na hayafai kwa matumizi mengine.
Utunzaji wa vifaranga
Baada ya vifaranga kuanguliwa, watenge na mama yao kwa kuwaweka kwenye banda safi lisilopitisha baridi. Unaweza kuwawekea taa ya kandili au ya umeme endapo upo kwenye sehemu unakopatikana.
Banda
Ni vyema banda liwe limesakafiwa au banda la asili la udongo usiotuhamisha maji. Pia, unaweza kutumia banda lenye mbao au mabanzi kwa chini. Unaweza pia kutandaza maranda kwenye mabanda. Hakikisha kuta za banda zimefunikwa vizuri ili kuwakinga dhidi ya baridi.
Maji
Kama ilivyo ndege wengine, bata mzinga pia wanahitaji kupatiwa maji masafi na ya kutosha wakati wote. Wawekee maji katika chombo ambacho hawatamwaga na wanakifikia vizuri. Hakikisha maji hayamwagiki bandani kwani kwa kufanya hivyo banda litachafuka na kukaribisha magonjwa kwa urahisi. Ni vizuri kuwalisha bata mzinga vyakula vingine kama majani. Majani husaidia kuwapatia protini: mfano; kunde, fiwi na aina nyingine za majani jamii ya mikunde huhitajika zaidi kwa kiasi cha 25% hadi 30%.
Magonjwa
Bata mzinga hushambuliwa na magonjwa kama taifodi, mafua na kuharisha damu. Wanapougua ni rahisi kuambukiza kuku, bata na ndege wengine wanaofugwa kwa haraka sana. Pia, ndege hawa husumbuliwa na viroboto wanaosababishwa na uchafu wa banda hasa linapokuwa na vumbi.
Chanjo
Bata mzinga wanatakiwa kupatiwa chanjo ya ndui (mara moja kila mwaka), kideri (kila baada ya miezi mitatu), gumboro (kwa muda wa wiki tano - ukiwapa jumatatu, basi unawapatia kila jumatatu ya wiki), na vitamini A mara baada ya kuanguliwa.

Kwa mafunzo zaid tembelea www.lengisho.blogspot.com
 
Asnte kwa maelezo murua..nakuomba uje na mtiririko kama huu..kwa kanga wakufuga..be blessed
 
Mkuu jovin607 angalia hizo picha 3 ya kwanza ni bata mzinga ya pili ni bata bikini ya tatu ni kanga ,bata mzinga anaitwa turkey bata bikini anaitwa goose kanga anaitwa Guinea fowl.Bata bikini ana tabia akitembea anaangalia juu.Sasa uzuri wa bata bikini ni mlinzi wa nyumbani mchana kama mbwa wawapo bandani au nje akiingia mtu mgeni hawajui wanapiga makelele sana na kama wako nje wanamfukuza

Sent using Jamii Forums mobile app
Nasikia bata bukini wanampigia kelele zaidi mtu mwenye nia mbaya kama mchawi/mwizi ni kweli?
 
Wakuu mimi naomba nishare some information.Mimi nafuga bata bukini now ni mwaka wangu wa kumi na moja+ nikiwa na akili zangu timamu hawa bata ni wazuri na hawana complication na siyo gharama kuwafuga. life span ya bata mmoja ni miaka 25 na hawana magonjwa wala nini wewe ni kuwapa chakula tu.karibuni wako pia naowauza kwa mmoja ni 150,000 na utapata maelezo mazuri zaidi
Una bukini weupe au wa rangi mchanganyiko?
 
Wana forum naombeni msaada wa maelekezo ya kufuga Kanga. Nataka kufuga nyumbani ambapo nina uwanja wa kutosha na nyumba ina fence ya ukuta.
Pamoja na faida nyingine, lengo kubwa ni kufuga Kanga kama mapambo ya nyumba, sababu nawapenda kimwonekano.
Kwa sababu hiyo ninalenga kufuga wachache, kama 6 nafikiri wanatosha.
Naomba maelezo kama yupo mwenye uzoefu au ujuzi wa ufugaji wa Kanga, kuanzia ujenzi wa banda, vyakula na ulishaji, magonjwa na matibabu yake, uzalishaji na utunzaji wa vifaranga na mambo mengine muhimu.
Tafadharini, mwenye maelezo anaombwakuyatoa hapa.
Nafikiri ni muhimu sehemu ya kufugia ikawa imezibwa juu maana wanapenda kururuka kwa mbawa na wanaweza kuruka umbali mrefu kiasi.
 
Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom