Ufugaji wa Bata Mzinga, Bata Bukini na Kanga: Maoni, Ushauri, Utaalamu na Masoko

G-son

Member
Sep 5, 2008
68
17
Wana JF Habari za mapumziko ya sikukuu ya X-mas.

Leo nina jambo nataka uliza. Nimepata fununu kuwa katika kipindi cha hivi karibuni biashara ya mayai ya Kanga imekuwa nzuri sana kwani yai linafika hadi Tsh 1000 hasa kwa Jijiji Dsm.

Mimi huwa najishughulisha sana na ufugaji wa kuku wa kienyeji na niliposikia hii biashara mpya inayolandana na nifanyayo nikavuitwa, ila sina taarifa za kutosha kuanza kulifanyia kazi. Hivyo nimeona nililete hapa jukwaani ambapo kuna utaalam wa kila aina ili kunifungua macho.

Kwa kuanzia tu,
(1) Je ufungaji wa Kanga unakuwaje ukiliganisha na wa Kuku?
(2) Kuna sehemu maalum ambapo naweza pata hawa Kanga (vifaranga) wa kuanzia?
(3) Hivi Kanga sio maliasili ya Taifa? nikimaanisha sitasumbuliwa na Afisa wanyama pori pindi wakigundua nafuga Kanga?

Ni hayo tu kwa leo na asanteni

Ili kuzaliana na kumpatia mfugaji faida, bata mzinga wanahitaji matunzo ya hali ya juu. Kwa kawaida bata mzinga hula chakula kingi kuliko kuku. Bei yake ni ghali zaidi. Kabla ya kuanza ufugaji wa bata mzinga ni lazima kuhakikisha una chakula cha kutosha kwa sababu ulishaji wa ndege hawa kadri wanavyokua huwa na gharama kubwa zaidi. Ni muhimu pia kujifunza kwa undani na kufahamu namna ya kutunza vifaranga wa bata mzinga kwa kuwa hufa kwa urahisi sana. Pia, unapaswa kujikita kutafuta soko kwa sababu wanapokuwa ni vigumu kuwatunza kwa muda mrefu kutokana na ukubwa wa gharama ya chakula.
Wafugaji wachache kati ya wengi waliojaribu kuwafuga ndege hawa na kufanikiwa hata kufikia malengo yao ni kutokana na kuzingatia lishe kamili. Pamoja na hayo, wapo wafugaji ambao walishindwa kutokana na magonjwa pamoja na gharama ya utunzaji.
Chakula
Chakula cha bata mzinga hakina tofauti na cha kuku. Vifaranga wanahitaji kupata lishe kamili yenye protini kwa wingi ili waweze kukua vizuri. Vifaranga kwa siku za awali wanahitaji kiasi cha asilimia 27 ya protini mpaka wanapofikia umri wa wiki sita. Baada ya hapo mfugaji anaweza kupunguza hadi kufikia asilimia 18, na kuendelea hivyo hadi wanapokomaa. Kutokana na gharama ya kununua chakula kuwa kubwa, unaweza kutumia reseheni ifuatayo kwa ajili ya kutengeneza chakula cha bata mzinga wewe mwenyewe.

Mahitaji
• Mahindi 5kg (yasiyokuwa na dawa)
• Karanga 5kg
• Dagaa 5kg
• Mashudu 10kg
• Chokaa 5kg (chokaa inayotumika kwa lishe ya mifugo)
Namna ya kutengeneza chakula
Twanga au saga pamoja kiasi cha kulainika kisha walishe vifaranga. Mchanganyiko huu hutegemeana na wingi wa bata mzinga unaowafuga. Hakikisha kila bata anapata chakula cha kutosha na chenye uwiano ulioelekezwa. Pia waangalie mara kwa mara kuhakikisha wana chakula cha kutosha.
Uhifadhi: Hifadhi chakula cha ziada kwenye mifuko au debe kisha weka sehemu isiyo na unyevu.
Kutaga
Bata mzinga huanza kutaga anapofikisha umri wa mwaka mmoja. Ndege hawa wana uwezo wa kutaga kati ya mayai 15 hadi 20 kwa mara ya kwanza na kisha kuhatamia. Anapoendelea kukua huweza kutaga hadi mayai 30. Hii ni kulingana na lishe nzuri atakayopatiwa.
Kuhatamia
Bata mzinga anaweza kuhatamia mayai 17 hadi 20. Mayai hayo huhatamiwa kwa siku 28 na huanza kuanguliwa vifaranga kwa muda wa siku 3, kuanzia siku ya 28 hadi 31. Baada ya hapo mayai yaliyosalia bila kuanguliwa hutakiwa kutupwa kwa kuwa hayatoanguliwa tena na hayafai kwa matumizi mengine.
Utunzaji wa vifaranga
Baada ya vifaranga kuanguliwa, watenge na mama yao kwa kuwaweka kwenye banda safi lisilopitisha baridi. Unaweza kuwawekea taa ya kandili au ya umeme endapo upo kwenye sehemu unakopatikana.
Banda
Ni vyema banda liwe limesakafiwa au banda la asili la udongo usiotuhamisha maji. Pia, unaweza kutumia banda lenye mbao au mabanzi kwa chini. Unaweza pia kutandaza maranda kwenye mabanda. Hakikisha kuta za banda zimefunikwa vizuri ili kuwakinga dhidi ya baridi.
Maji
Kama ilivyo ndege wengine, bata mzinga pia wanahitaji kupatiwa maji masafi na ya kutosha wakati wote. Wawekee maji katika chombo ambacho hawatamwaga na wanakifikia vizuri. Hakikisha maji hayamwagiki bandani kwani kwa kufanya hivyo banda litachafuka na kukaribisha magonjwa kwa urahisi. Ni vizuri kuwalisha bata mzinga vyakula vingine kama majani. Majani husaidia kuwapatia protini: mfano; kunde, fiwi na aina nyingine za majani jamii ya mikunde huhitajika zaidi kwa kiasi cha 25% hadi 30%.
Magonjwa
Bata mzinga hushambuliwa na magonjwa kama taifodi, mafua na kuharisha damu. Wanapougua ni rahisi kuambukiza kuku, bata na ndege wengine wanaofugwa kwa haraka sana. Pia, ndege hawa husumbuliwa na viroboto wanaosababishwa na uchafu wa banda hasa linapokuwa na vumbi.
Chanjo
Bata mzinga wanatakiwa kupatiwa chanjo ya ndui (mara moja kila mwaka), kideri (kila baada ya miezi mitatu), gumboro (kwa muda wa wiki tano - ukiwapa jumatatu, basi unawapatia kila jumatatu ya wiki), na vitamini A mara baada ya kuanguliwa.
 
Mkuu bluetooth hakika umenisoma, Kumradhi ni Kware wanaJF

Asante bluetooth

Kawaone JB farms pale kwa Mathias Kibaha, au nenda pale Ubungo mataa karibu na YENU BAR wana ofisi pale. Kingine ni kwamba, wewe fuga kware, hao maliasili mpaka waje utakuwa umeshapata ujuzi tosha wa kufuga, naamini wakikufikia, mtaelewana. Vibali utapata mwaka 2019, upoooo
 
Nimekua mpenzi wa ufugaji, hasa jamii ya ndege, nimeanza mwaka jana kufuga kanga nilinunua mayai na kutotolesha kupitia kuku, kiukweli nilifanikiwa na kutotolesha vizuri.

Msaada naomba kwamwenye uelewa kuhusu mayai ya kanga huchukua muda gani kutotolewa/kuanguliwa kupitia kuku? na ili kutotolesha mayai ya kanga na kuku kwa pamoja unafanyeje? Msaada tafadhari.
 
Nimekua mpenzi wa ufugaji, hasa jamii ya ndege, nimeanza mwaka jana kufuga kanga nilinunua mayai na kutotolesha kupitia kuku, kiukweli nilifanikiwa na kutotolesha vizuri. Msaada naomba kwamwenye uelewa kuhusu mayai ya kanga huchukua muda gani kutotolewa/kuanguliwa kupitia kuku? na ili kutotolesha mayai ya kanga na kuku kwa pamoja unafanyeje? Msaada tafadhari.

Ndg yang KUHUSU kanga Mayai yake yanatotolewa baada ya siku 28, iwe kwenye mashine au kwa kuku. Mayai ya kuku huchukua siku 21. Hii Ina maana unaweka mayai ya kanga kwa siku saba Kisha siku ya nane unaweka ya kuku ili yaje yatotolewe pamoja.
swaw?
 
Ndg yang KUHUSU kanga Mayai yake yanatotolewa baada ya siku 28, iwe kwenye mashine au kwa kuku. Mayai ya kuku huchukua siku 21. Hii Ina maana unaweka mayai ya kanga kwa siku saba Kisha siku ya nane unaweka ya kuku ili yaje yatotolewe pamoja.swaw?
hapa ndo huwa napenda yaani kama hujuikitu we uliza kisha utapata majibu yanayo stahili bila taabu na kuwaelewesha wengine maana hatamimi nilikuwa naitaji sana nshu hii
 
Ndg yang KUHUSU kanga Mayai yake yanatotolewa baada ya siku 28, iwe kwenye mashine au kwa kuku. Mayai ya kuku huchukua siku 21. Hii Ina maana unaweka mayai ya kanga kwa siku saba Kisha siku ya nane unaweka ya kuku ili yaje yatotolewe pamoja.
swaw?

Nimekusoma ndugu nashukuru sana heri na amani juuyako
 
hapa ndo huwa napenda yaani kama hujuikitu we uliza kisha utapata majibu yanayo stahili bila taabu na kuwaelewesha wengine maana hatamimi nilikuwa naitaji sana nshu hii

Umeona unatatizo ingia hm toa/uliza irimladi usitukane wala kumlenga mtu vibaya karibu nawe
 
Usisahau kuwapa chanjo ya Newcastle siku ya 7 na gumboro siku ya 14 na hakikisha siku ya 19 hadi 23 unawapa dawa ya mafua, wawe na mafua au hawana mafua (kipindi hiki kanga hushambuliwa sana na mafua), wakifika siku ya 25 salama basi umekula bingo.

Nashukur kwa taarifayako samahani, hebu nipena elim nzuri upande wa kuku dawaipi nzuri ? pia nikuulize kaswari kimasihara, hivi kanga unawatofautishaje huyu dume au jike?
 
Kwa mjini hasa dar kang mkubwa ananzia ela ngap coz huk kwet kanga mkubwa kabisa ni tsh 6,000-7,000
mtena kanga dar ni elfu 35 mpaka 40. Hii ni bei ya sehemu moja makumbusho karibu na millenium tower. Ilikua inapigwa bendi zamani. Mimi nilinunua kanga mdogo wa wiki 4 elfu 15 kwa kubembeleza sana. Kwenu wewe wapi?
 
mtena kanga dar ni elfu 35 mpaka 40. Hii ni bei ya sehemu moja makumbusho karibu na millenium tower. Ilikua inapigwa bendi zamani. Mimi nilinunua kanga mdogo wa wiki 4 elfu 15 kwa kubembeleza sana. Kwenu wewe wapi?
Ee wewe kumbe ndoivyo da jamani kumbe tujitume vijana fulsa tunazo
 
Usisahau kuwapa chanjo ya Newcastle siku ya 7 na gumboro siku ya 14 na hakikisha siku ya 19 hadi 23 unawapa dawa ya mafua, wawe na mafua au hawana mafua (kipindi hiki kanga hushambuliwa sana na mafua), wakifika siku ya 25 salama basi umekula bingo.
Naanza kufuga kwa kupitia wafugaji wa jf naona humu naweza pata japo fikra ya kunirejesha nam ktk ulimwengu
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom