Ufugaji wa Bata: Aina za bata, ujuzi, gharama, changamoto, faida na masoko

jipatie mallard, Rouen na jumbo perkin
Wana mwezi mmoja
Bei 20000
Wapo chanika kwa singa
Call 0783291107

712D9E57-0A0E-43C5-A2FC-99C3E1B4F5DA.jpeg


8DFF4677-DE71-4C81-AE0B-C83CCDD92EAA.jpeg
 

Attachments

  • IMG_7026.MOV
    12.2 MB
M
Naomba nijibu kwa kadiri ya ujuzi wangu, Bata wote wanapenda maji, Bata wakikosa maji na wakaweza kujua yanapo patikana watakuwa ukiwafungulia wanaruka kuyafwata kwahiyo unajiweka ktk hatari ya kupoteza mifugo kila mara.
Kushu migomba Bata huaharibu migomba, kwanza ile michanga huwa wanaiwahi kiharibu kwakuwa ni michanga, pili ile mikubwa huwa wanaiharibu kwa kuchimba kwenye shina pale panaunyevu unyevu na baadhi ya wadudu.
Bata furaha yake kubwa ipo kwenye kucheza na maji kwamfano Bukini wakishamaliza kula huwa wanapenda kuogelea na maji yakichafuka watapiga kelele wakiwa pembeni ya bwawa mpaka uya badili, Pekini,indian runer,sweedih, na hawa wakawaida pindi tu wanapo kuwa wameshiba vyema hupenda kuoga hasa kipindi cha mchana na ni njia ya kujipooza na joto.
Kuhusu utagaji kwakweli Bukuni nichangamoto sana maana utagaji wao ni apole pole sana na nikwamsimu, pekini waohutaga vyema lakini ni aghalabu kulalia. Nimezungumzia uzoefu wangu nakubali kukosolewa pale nilipo kosea.
Mimi nahitaji hao Pekin. Napata je?
 
Naomba kufahamishwa kwa ufupi kuhusu bata aina ya jumbo pekin , nimesikia ni broiler ya bata , Vipi upatikanaji wa mbegu hapa tz na ufugaji wake ni kama wa bata wa kawaida?
Mbegu zipo , wanasema ni broiler kwa sababu ukiwalisha sana wanana wana nenepa kupita kias
 
UTANGULIZI

Habari zenu wanajamvi, kwanza napenda kudeclare interest mimi ni mfugaji mchanga wa Bata, na nilifikia uamuzi wa kufuga bata baada ya maradhi kuwapiga kuku wangu na wakafa wote. Nimepitia threads nyingi sana za humu na sijaona special thread inayoongelea bata na bila hiyana nimemua kuileta ili wafugaji bata na wataalam tukutane hapa kupeana ujuzi. Bata ni ndege mtamu nadhani kushinda hata kuku, watu wengi wanapenda kumla bata ila hawataki kabisa kumfuga kutokana na mazingira yake. Ufugaji wa bata una faida na unaweza kukufanya ukawa Tajiri ndani ya kipindi kifupi.

MAGONJWA YA BATA
Lazima tuelewe magonjwa anayopata kuku na jamii ingine ya ndege bata pia hupata, tofauti ya bata na ndege wengine wana uwezo wa kuhimili magonjwa, yafuatayo ni baadhi ya magonjwa ya bata;

1. Duck Viral hepatitis.
Ugonjwa huu unawashambulia vifaranga vya bata ambavyo vipo chini ya wiki 6, utakuta vifaranga wanakosa nguvu ya kusimama, kutembea na hatimaye vifo.

2. Aflatoxins Poisoning
Ugonjwa huu ni pale unapompa kifaranga pumba yenye madonge madonge ambayo ukiichunguza utakuta tayari imeanza kuweka kijani, hii ni sumu kabisa na haichelewi kumuondoa bata.

3. Cholera
Ugonjwa huu ni hatari kwa bata wadogo, utakuta bata wanajinyonga shingo na kuanguka.

4.Bata pia hushambuliwa na wadudu (parasites) mbalimbali ambao hupatikana ndani na nje ya mwili wake mfano viroboto, utitiri, chawa, ukurutu n.k ndani ya mwili anaweza kupata minyoo ya kwenye utumbo na maini.

5.Yapo magonjwa mengine hatari ya bata kama Duck viral enteritis, Aspergillosis, Collibasillosis n.k. kwa wale tunaofuga unaeza ambiwa bata ana matatizo ya mifupa, mafua, Typhoid au hata Pneomonia.

Magonjwa mengi ya bata husababishwa na ukosefu wa Vitamins, Madini na bila kusahau uchafu.

DAWA ZA KUWATIBU

Zipo dawa nyingi sana ambazo zinaweza kusaidia/kuokoa au kuimarisha hasa maisha ya vifaranga vya bata.

1. DCP
Dawa hii imeonyesha uwezo mkubwa sana wa kuwakinga na kuwaimarisha bata katika miili yao hasa mifupa yao maana ina Calcium+Phosphorous. Matumizi yake unachanganya tu kwenye pumba.

2. Amin'total
Ni dawa moja nzuri sana inayosaidia absorption ya DCP ktk utumbo wa bata kwakuwa ina kiwango kikubwa cha D3. Dawa hii ni expensive kama una bata wachache si vema kuinunua kama unajiweza unaweza kuinunua.

3. Fluban (enrofloxaxin)
Imethibitika ni dawa nzuri sana hasa pale bata wanapopata typhoid. Ni dawa yenye nguvu na inatibu haraka.

4. Ivermectin
Ni dawa iliyoonyesha uwezo wa kuua wadudu wote wanaomdhuru bata ndani na nje kwa mkupuo.

5. Neoxychick
Ni dawa inayofanya vizuri hasa kukuzia bata wadogo, dawa hii ni antibiotics na ina Vitamins, na Minerals. Pia unaweza kutumia kitunguu swaumu kama mbadala wa dawa hii ikiwa tu uchumi wako hauko vizuri, unamenya kitunguu swaumu, kitwange kisha changanya na maji, wape vifaranga siku3 za kwanza baada ya kuzaliwa.

6.Piperazine
Hapa wafugaji wa sungura watakuwa wamenielewa, hii ni dawa moja nzuri na inayoonyesha matokeo ya haraka. Ni dawa inayoua minyoo ya aina zote. Mimi binafsi napendelea kuitumia hii kwa bata wangu.

7. ESB3
Dawa moja makini sana pale bata anapoanza kuharisha, ukiona magonjwa ya tumbo yanamsumbua bata hasa kuharisha choo cheupe mpe hii dawa.

DAWA ZINGINE MUHIMU PALE UNAPOONA MABADILIKO YA BATA WAKO NI OTC, TYLOSIN, LIMOXIN, NA DOXCOL. Hizi zinatibu magonjwa mengi.

NADHARIA/IMANI/MISEMO
Kuna maneno mengi sana husemwa huko mitaani hasa kuhusiana na bata na kuna Imani zipo ktk jamii kwamba unapotaka kumchinja bata usimuonyeshe kisu kwani nyama yake itakuwa chungu sana, Wengine husema bata akitaga mayai yake anayahesabu na ukichukua mayai yake kila siku basi itafika kipindi atasusa kutaga na atapata stress ambazo zinaweza mfanya Asitage kwa muda mrefu, Wengine husema wakati wa kumnyonyoa bata haitakiwi kuongea maana mkiongea basi ataota tena manyoya mengine, Pia kuna wengine husema bata wa ukoo mmoja wakipandana inaweza kuwa chanzo hasa cha vifo vya bata wadogo, Yote kwa yote misemo ipo mingi tu inayoongelea bata japo mimi binafsi sitaki kusema lolote kuhusu hiyo misemo.

MUHIMU UNAPOFUGA BATA

1. Hakikisha maji wanayokunywa ni safi pia jitahidi kuwabadilishia maji mara kwa mara.
2. Hakikisha vyombo vya maji na chakula viwe safi muda wote.
3.Wape chakula safi na cha kutosha ili kuboresha ukuaji wao
4.Pia muhimu sana hasa kwa bata wadogo na wakubwa kuwachanganyia damu iliyokaushwa, chokaa, mifupa na mashudu ya alizeti ikiwezekana ili waweze kupata madini ya Calcium + phosphrus na trace Minerals. Pia itafanya bata wasiwe na hamu ya kula mayai. Na vilevile mchanganyiko huu unasaidia kupevusha mayai ya bata hivyo bata huwai kutaga mayai.
5.Vifaranga vikizaliwa unaweza kuvipa antibiotics kuzuia magonjwa na bacteria pia usiache kuwapa Vitamins ili kuwaongezea hamu ya kula na kinga ya magonjwa.
6. Unga wa sulphur umeonyesha matokeo mazuri hasa katika kuwalinda na bacteria.
7. Intensive System.. inashauriwa kama unajiweza ufanye ufugaji wa ndani wa bata hii itakupa matokeo mazuri na ya haraka.
8.Vifaranga vya bata havitakiwi kuoga au kunyeshewa na mvua kwa muda angalau wiki 10 za kwanza baada ya kuzaliwa.
9. Kipindi cha wiki 2 za kwanza vifaranga vya bata havitakiwi kupata baridi kama banda lako halina joto la kutosha unaweza kuwawekea majiko ya Mkaa ili kuwaongeza joto.
10.Hakikisha banda lako halina matundu yanayowawezesha panya kupita, Panya huwa wanawadhuru vifaranga wadogo hasa walio chini ya wiki mbili.
11. Changamoto kubwa ya bata ni chakula kwanza wanazaana kwa kasi, inabidi angalau uandae gunia la pumba pamoja na virutubisho vya kutosha. Pia bata wanakula sana majani hata kama unafugia ndani jitahidi siku moja moja uwe unawakatia majani hawa bata wa kienyeji ni sawa na kuku huwaga wanapenda kula majani.
12.Vifaranga wa bata hawatakiwi kula pumba iliyochanganywa na maji, kwa kufanya hivyo unawahatarishia maisha.

NB; MAGONJWA YOTE YA BATA YANAWEZA KUZUILIKA KWA USAFI TU. NA LAZIMA TUKUMBUKE BATA SIO MCHAFU ILA WEWE MFUGAJI NDIO MCHAFU.

AINA ZA BATA
Wapo bata wa aina mbalimbali ila hapa nitataja chache tu. Tukianza na bata wa kienyeji (Muscovy Duck) ambao kila mtu anawajua. Bata wengi wa kienyeji wanataga mayai 10 hadi 12 na mara nyingi wanataga alfajiri, bata hawa hutotoa watoto kuanzia 8+, wafugaji wengine wamebahatika kupata mbegu tofauti za hawa bata hivyo wanasema bata hawa wana uwezo wa kutaga mayai hadi 30.
Pia kuna bata wanaitwa Pekin, hawa asili yao ni china hapa Tanzania wapo ila sio wengi sana.
Aina ingine ya bata ni Bukini hawa sasa watu wengi wanawafuga kibiashara, na pia wana gharama hata kuwanunua kwake. Chakula Chao kikubwa majani.
Aina ingine ya Bata ni bata mzinga hawa ni gharama sana kuwafuga, tena wakiwa wanakua ndio balaa inatakiwa uwe na chakula cha kutosha ndani kwani wanakula mno, asilimia kubwa ya waliojaribu kuwafuga hawakufikia malengo yao kutokana na gharama ya chakula na magonjwa, bata mzinga hutaga mayai 15 hadi 20 kwa mara ya kwanza, akitaga kwa mara ya pili hutaga mayai 25 hadi 30, na analalia kwa siku 28, siku ya 29 hadi 31 ni siku ambazo mayai hutotolewa, ikifika siku ya 32 kama mayai yamebaki basi hayo ni ya kutupa.
Aina ingine ya bata ni mchovya hawa wana midomo ya njano, Tabia zao hazitofautiani sana na bata wengine.

MASOKO NA BEI
Maneno mengi husemwa kwamba bata mchafu wengine husema sio mtamu, basi tu ili mradi kila mtu anasema yake, bata wana masoko sana hasa wageni wanapenda sana bata, shida ya upatikanaji wake ndio imesababisha bata waonekane wana bei sana na kama chakula cha anasa, tufuge bata kwa wingi ili upatikanaji wake usiwe wa kusua sua. Na pia bata wakiwa wengi na bei ikiwa ya kawaida itafanya watu wale bata kwa wingi.

CHANJO ZA BATA
Bata wakiwa ni ndege kama kuku nao wanastahili kupewa kinga. Bata unaweza kuwakinga na maradhi kwa kuwaweka sehemu safi. Ila kama unataka uhakika wa asilimia 200 bata wako wasife wape chanjo kwa mtiririko ufuatao.
* Bata wako wakifika siku saba yani wiki ya kwanza (baada ya kumaliza kutumia Neoxychick) wape chanjo ya Newcastle
*Bata wako wakifika siku Kumi na nne yaani wiki ya pili wape chanjo ya Kideri
*Bata wako wakifika siku ya Ishirini ya moja yani wiki ya tatu wape chanjo ya Newcastle tena.
*Bata wako wakifika siku ya Ishirini na nne yaani wiki ya 4, wape chanjo ya Gumboro. Hapo utakuwa umekata mzizi wa fitina, ila usafi lazima pamoja na lishe bora. Na inashauriwa kila unapowapa chanjo wape Vitamin kabla hujawapa chanjo ingine, na Vitamin nzuri inaitwa IntroVit A ina vitamin nyingi nyingi sana. Baada ya hapo unaweza kuwapa vifaranga wapo Growers Mash bila chanjo tena na watakuwa vizuri bila tatizo.

HITIMISHO
Kupitia thread hii wale wote wanaofuga au wanaotarajia kufuga bata tukutane kushea mambo mbalimbali yahusuyo bata. Pia natoa wito Kwa moderators wa JF waweke PIN hii posti iwe juu kwa ajili ya sisi wapenzi wa kula na kufuga bata. Wataalam wa mifugo wanakaribishwa kutoa mawazo yao mbali mbali yahusuyo mfugo huu adhimu.

NYONGEZA
Bata wamekuwa wakifugwa miaka mingi katika ardhi ya Tanzania, na njia za ufugaji ni tofauti. Bata hasa wakiwa wadogo inashauriwa wale starter kwa angalau mwezi na wawekewe Glucose ile ya kuku kwenye Maji pamoja na Vitamin, ila kuna ambao hawafuati haya masharti. Kùna ambao wanawanyoosha shingo bata wakiwa wadogo na bata hukua bila tatizo lolote. Pia kuna ambao hawawapi bata dawa yoyote zaidi ya muarobaini, alovera na majani ya Mpapai. Well kila mtu ana njia yake ya ufugaji ili mradi malengo yafikiwe.

NAWASILISHA.
Asante sana.

Naomba msaada wako.
Naomba kujua muda wa kumwachisha bata watoto ili aweze kutaga tena. Nina bata katotoa, sasa ni siku ya 23. nataka nimtoe mama yao nimpeleke shamba maana naona kama watoto wamekuwa wakubwa wa kujitegemea. Je inahauriwa watoto wawe peke yao baada ya siku ngapi? Naweza kuwatoa kwa mama yao sasa?
 
Mkuu Raia Mtata bata wangu katotoa Jana ,ila kuna baadhi ya vifaranga nawakuta wamelala Chali ,kila nikiwarudisha kwa mama yao baada ya muda nawakuta tena wametoka kwa mama na kulala Chali kwenye vimchanga maana nimeweka mchanga kiasi sehemu alipokua anatagia,je hii ikoje ikoje maana mi ndo nimeanza hivi ufugaji na Nina Nia ya kuwa na bata wengi sana.
 
mkuu unaweza kutoa elimu jinsi ya kutengeneza mabanda ya bata ya kisasa?kwasabu umezungumzia usafi kwenye ufugaji wake naamini hata banda lafaa kujengwa kisasa sio kama tulivyozoea kuejnga banda la bata uwani karibu na choo
 
haba
Asante sana.

Naomba msaada wako.
Naomba kujua muda wa kumwachisha bata watoto ili aweze kutaga tena. Nina bata katotoa, sasa ni siku ya 23. nataka nimtoe mama yao nimpeleke shamba maana naona kama watoto wamekuwa wakubwa wa kujitegemea. Je inahauriwa watoto wawe peke yao baada ya siku ngapi? Naweza kuwatoa kwa mama yao sasa?
Habari,tafadhali naomba jibu la hilo swali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom