Ufugaji samaki kwa Vizimba (Cage Fish Farming)

Serikali ya kipuuzi sana hii, gharama zote hizo kwenye vibali za nini? Vijana watajikomboaje kwa mfumo huu?
Iko haja ya wadau kukaa kwa pamoja na kuja na mapendekezo ya namna gani vibali viweze kuoatikana kwa gharama nafuu na kwa urahisi.
 
Ahsante kwa andiko zuri, hicho chakula ulichoandika ni kwa muda gani yaani kwa siku, mwezi au miezi kadhaa?
 
Ufugaji wa samaki kwa vizimba ni njia rahisi na yenye tija kwa wafugaji samaki kibiashara. Nitakuelezea hapa hatua na gharama zake na mambo mengine ya kuzingatia.

1.Vibali vya uendashaji wa shuguli za ukuzaji viumbe hai majini

I)Mhutasari wa kikao cha serikali ya kijiji au mtaa ambapo mradi utafanyika.

II)TAFIRI- Kufanya survey kwenye eneo ambapo vizimba vitawekwa, kupima kina cha maji, ubora wa maji, mkondo wa maji, ukubwa mawimbi n.k. galama ni Tsh. 2,700,000/=

III)NEMC-Kufanya Environmental Impact Assessment, galama yao n 4,200,000/=

IV)Bonde la Ziwa Victoria- Kutoa kibali cha matumizi ya maji

V)Barua ya Afsa uvuvi wa eneo husika

VI) Kibari kutoka Wizara ya mifugo na uvuvi idara ya ukuzaji viumbe hai majini.

2.Kutengeneza kizimba na Kupanda vifaranga.
-Kizimba chenye urefu wa mita6, upana mita6 na kina cha mita6, kinaweza kubeba vifaranga 10,000.
-Galama za kutengeneza kizimba ni 3,500,000/= na vifaranga tsh.2,000,000 kwa vifaranga 10,000.

3.Galama za vyakula.
Kilo1 ya samaki ni sawa na kilo1.3 za chakula. Hivyo matalajio ya mavuno yatategemea pia kiasi cha chakula.
Mfano; samaki 10,000 wanaweza kufika wastani wa kilo 2500 mpaka 3000.
Hivyo watakula kilo 3250 mpaka 3900.
Vyakula vimegawanyika katika makundi 3
  • Starter
  • Glower
  • Finisher

(Galama ni kati tsh2500/kg mpaka 3000/kg)

4.Galama ya usimamizi na ulinzi wa mradi (Ni makubaliano)

5.Mavuno; Kwenye kizimba cha ukubwa wa mita za eneo 36 kinaweza kubeba vifaranga mpaka 10,000 vya sato, Matarajio ya kuvuna ni samaki 8500 mpaka 9000 ambao wanakadiliwa kuwa na uzito wa gram 400 mpaka 600
Wastani wa mavuno ni tani 2.5 kwa miezi 6.
Cc.Babilas 25
NICHEKI WATSUP 0762212623 NIKUUNGANISHE NA WATEJA
 
Nilikuwa natamani kufuga ila nikiwaza hizo gharama tamaa ime nikifu yaani Tafiti 2,700,000 NEMC 4,200,000. Kizimba kimoja cha 36 eneo la mraba 3,500,000 vifaranga 10,000 ni 2,000,000. Hapo huja weka Chakula tayar 11,400,000/- maana chakula pekee 11,700,000.

Hapa jumla kuu ni 23,100,000/- kwa tani 2.5 ambapo bei ya Jumla ni 5500 ambapo mavuno ni 13,750,000/+ hapo Hasara ya −9,350,000 kwa Cage
 
Duuuuu kwa. Gharama hizi si bora uwe. Mvuvi au broker wa samaki
 
Nilikuwa natamani kufuga ila nikiwaza hizo gharama tamaa ime nikifu yaani Tafiti 2,700,000 NEMC 4,200,000. Kizimba kimoja cha 36 eneo la mraba 3,500,000 vifaranga 10,000 ni 2,000,000. Hapo huja weka Chakula tayar 11,400,000/- maana chakula pekee 11,700,000.

Hapa jumla kuu ni 23,100,000/- kwa tani 2.5 ambapo bei ya Jumla ni 5500 ambapo mavuno ni 13,750,000/+ hapo Hasara ya −9,350,000 kwa Cage
Dah
 
Mkuu hesabu za uwekezaji Huwa haziko hivyo, Kuna gharama nyingi Huwa hazijirudii
 
Vibali kama nasafirisha silaha vile. Nilipie milioni 4 ya kibali huo si ni mtaji wa kujenga bwawa dogo kwa simenti kwenye kiwanja changu
Serikali ya kipuuzi sana hii, gharama zote hizo kwenye vibali za nini? Vijana watajikomboaje kwa mfumo huu?
Shida ipo kwa watunga sera wetu, watu wanashindwa kuweza kujiajiri sababu kubwa ikiwa ni pamoja na hii
Yaani hapo Kuna vibali Kama 6 na gharama Yake ni milioni 7, na hapo una assume Kama hujaletewa longolongo za rushwa, nchi Ngumu Sana hii
 
Back
Top Bottom