Ufugaji kuku sio mwanzo wa utajiri pekee, unaweza ukawa mwanzo wa umasikini wa uhakika. Zingatia yafuatayo ili upate mema kupitia kuku

Tangantika

JF-Expert Member
Aug 12, 2018
1,583
2,000
Hivi kwa hizi akili zako hata kama utapewa formula ambayo ni bora kuliko silva land utaamini?Kwani hawa jamaa wametoa mbinguni?Wandugu tuache fikra mbovu kama hizi tunajichelewesha.
Ulevi wa brand name ni mbaya sana,kwa wewe kama mtu akichukua kiroba cha silver land akaweka humo chakula cha falcon utaendelea tu kusifia silver land kumbe kilichomondani sicho.
Jifunze kwa kuuliza wengine itakusaidia sana kwenye ufugaji kuliko kuendelea kukariri.
Kizuri kinajiuza.Hakuna muuzaji wa chakula aliweza kusindika kumzidi silver land.Wengine huuza vumbi ukalishe kuku.Kama we we ni mfugaji na hukipendi chakula cha sulverland basi namashaka na wewe. That food is one of the best invention in poultry industry.Kama unacho mbadala nijuze, mi napenda vitu bora has a ktk mifugo. Hizo formula za sua na mitandaoni ninazo nyingi sana.

Mkuu watu wapo maabara kuja na vitu bora sio bla bla za wabongo.
Kama una formula bora tengeza chakula uza watu watapima ubora sio maneno.
 
MTOCHORO

JF-Expert Member
Dec 18, 2016
3,470
2,000
chakula cha kuku kivipi ? au mnamaanisha makuku ya kizungu.mbona kuku wa kienyeji alfajiri tu wanafunguliwa wanaingia mitaani jioni wanarudi wenyewe wakiwa wameshiba au mimi ndio sielewi
Wanakomaa baada ya miaka miwili
 
morganmasha

Member
Jul 6, 2016
60
125
Kizuri kinajiuza.Hakuna muuzaji wa chakula aliweza kusindika kumzidi silver land.Wengine huuza vumbi ukalishe kuku.Kama we we ni mfugaji na hukipendi chakula cha sulverland basi namashaka na wewe. That food is one of the best invention in poultry industry.Kama unacho mbadala nijuze, mi napenda vitu bora has a ktk mifugo. Hizo formula za sua na mitandaoni ninazo nyingi sana.
Mkuu watu wapo maabara kuja na vitu bora sio bla bla za wabongo.
Kama una formula bora tengeza chakula uza watu watapima ubora sio maneno.
Sio kweli, uliza mfugapi yeyote wa Dar, pwani, morogoro, zanzibar, tanga. Utapata majibu. Kampuni zinazofanya vizuri kwa sasa katika hiyo mikoa kwa mpangilio
1. Backbone
2. Hill feed
3. Falcon.
4. Irvine’s (amadori ya zamani)

Silverland ni kuwa alijitanua sana mikoani lakini chakula chake sasa hivi kimekutana na ushindani mkubwa, hii mikoa hauzi kitu. Silverland nawafaham hadi sales Manager wao ni kijana huwa tunapeana changamoto za haya mambo
 
Inawezekana mkuu, Nina miaka 2 nje ya industry ntaporudi mwakani ntajaribu hicho chakula.Ila kama kweli hivyo vyakula ni bora basi vingesambaa na mikoani.
 
morganmasha

Member
Jul 6, 2016
60
125
Inawezekana mkuu, Nina miaka 2 nje ya industry ntaporudi mwakani ntajaribu hicho chakula.Ila kama kweli hivyo vyakula ni bora basi vingesambaa na mikoani.
Wafugaji wengi wako mjini hivo ukishashika hiyo mini nliyokutajia ndo ina market kubwa kwa broiler feeds kwa sababu walaji ni wengi, transportation cost ni ndogo utauza kwa profitable price
 
morganmasha

Member
Jul 6, 2016
60
125
Exactly kwa njombe huna option nyingine. Silverland ye yupo iringa. Kuleta hapo kwa bei rahisi inampa faida. Kuliko hizi kampuni nyingine za dar ambazo mara zote bei ya chakula ipo juu kwa silverland, ilete hadi njombe bei itaingezeka soko ni dogo na bei pia kubwa haiwezi kuuza
 
kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
6,179
2,000
Hivi unaweza jitengenezea chakula bora kama cha silverland.Hats ufanyeje ile formula ni noma.Labda uende SUA ukafanyie PhD. Aisee ilw formula sijaona mbongo alieiweza.Piga UA chakula cha silver land hukikwepi kama kweli wewe in mfugaji.
Mm.nimeweza...kuku wangu nawapa.chakula.cha silverland mwezi 1 tuu then natengeneza changu na wanakua vuzuri sana
 
Lihove2

JF-Expert Member
Mar 23, 2018
985
1,000
Kwa miaka ya hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa sana la watu kuweka ndoto za mafanikio kwenye swala zima la ufugaji kuku, swala ambalo watu wengi wanakosea kuingia kwenye ufugaji bila tathmini za kina HASA juu ya gharama na changamoto za ufugaji huo. Mara nyingi huwa tunaingia na mawazo chanya ya kufanikiwa haraka sana mara tu tunapoanza kufuga.

Ukweli ni kwamba hakuna kitu chenye faida kisichopitia hasara wala changamoto.

Changamoto kubwa ambayo wengi tunaisahau ni gharama za kuwatunza hao viumbe na kama tunazifahamu basi hatuzitafakari kwa kina na mwisho wa siku tunapoanza kufuga tunajikuta tunaanza kutumbukia kwenye utumwa wa kutoa pesa za chakula na madawa ya kuku bila kupenda ama kutarajia. Kuku ni viumbe na wanahitaji chakula bora pamoja na afya njema.

Changamoto kubwa mbili ni:
1) Gharama ya chakula ambayo huwa ni asilimia 75 ya gharama ya ufugaji kuku.

2) Gharama ya matibabu na kinga ambayo hufikia karibu asilimia 5 ya ufugaji wako.

Gharama hizo ni za matunzo ukitoa gharama za ujenzi wa banda pamoja na miundo mbinu.

Naomba nikupe mbinu za kupambana na changamoto hizo nilizo zitaja:

Kwa changamoto ya chakula; Unaweza ukatengeneza chakula cha aina yoyote ya kuku unayefuga kwa kutumia malighafi zilezile zinazotumika kutengenezea chakula kiwandani, kwa kufanya hivi utaokoa gharama karibu asilimia 60, yaani kama ulitakiwa ulishe kuku wako chakula cha sh 1,000,000 basi utajikuta kwa kutengeneza mwenyewe utatumia sh 400,000 kutengeneza chakula chenye ubora uleule wa chakula cha milioni 1.

Kwa changamoto ya maradhi pamoja na kinga unashauriwa uzingatie sana usafi wa jumla kwenye ufugaji wako, usafi huo ni kuanzia wewe mwenyewe, mazingira ya ndani na nje ya banda hasa uhakikishe banda liwe kavu, chakula pamoja na maji safi. Hii ni pamoja na vyombo vya chakula na maji kuwa safi muda wote, cha mwisho ni kuzingatia chanjo kwa wakati.

Kumbuka: Kutozingatia chakula bora cha kuku ni kujihakikishia ukosefu wa kuku bora wasiofaa sokoni na kuwa mzembe dhidi ya afya za kuku ni kujihakikishia msiba wa kuku wako wote.

UKIZINGATIA HAYO UTAJIKUTA UNAIFIKIA ILE HAZINA KUBWA SANA YA UTAJIRI ILIYOJIFICHA KWENYE UFUGAJI AMBAYO WENGI WAMEINGIA HUKO BILA UTASHI na KUIKOSA NA KUJIKUTA WANATAJIRISHA WENGINE NA WAO WAKIISHIA KUWA WATUMWA.

Kwa ushauri na pia malighafi za kutengeneza chakula cha kuku aina yoyote basi tuwasiliane.

Hapo mwisho pameonyesha wewe unatafita fursa ya kuuza vyakula vya mifugo,.ungetoa tuu majina ya hizo materials za kuchanga ili mtu akatafute mwenyewe popote alipo hapa Tanzania.Kuanza kuwasiliana tena na wewe labda kama ulimaanisha hapa hapa Jf
 
gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
2,605
2,000
Kizuri kinajiuza.Hakuna muuzaji wa chakula aliweza kusindika kumzidi silver land.Wengine huuza vumbi ukalishe kuku.Kama we we ni mfugaji na hukipendi chakula cha sulverland basi namashaka na wewe. That food is one of the best invention in poultry industry.Kama unacho mbadala nijuze, mi napenda vitu bora has a ktk mifugo. Hizo formula za sua na mitandaoni ninazo nyingi sana.
Mkuu watu wapo maabara kuja na vitu bora sio bla bla za wabongo.
Kama una formula bora tengeza chakula uza watu watapima ubora sio maneno.
Narudia tena ulevi wa brand name ni ulevi mbaya sana.Nasisitiza mwisho wa siku kinachohitajika ni jinsi gani utapata faida maradufu.
 
ij rafael

Member
Sep 6, 2018
23
45
nilich
Hapo mwisho pameonyesha wewe unatafita fursa ya kuuza vyakula vya mifugo,.ungetoa tuu majina ya hizo materials za kuchanga ili mtu akatafute mwenyewe popote alipo hapa Tanzania.Kuanza kuwasiliana tena na wewe labda kama ulimaanisha hapa hapa Jf
okifanya ni kutengeneza awareness kwa public na matokeo ni watu kuwa na interest, lakini kumbuka sio kila mtu atakuwa na hiyo interest, hivyo atakaye kuwa na interest basi sijamkataza kunitafuta ili nimpe hayo mengine atakayohitaji kama ulivyotaka nitaje, hata mwalimu hafundishagi vyote lakini, tunajengeana njia tu ya kutambua uhalisia wa jambo
 
kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
6,179
2,000
Kwa nini unawapa huo mwezi mmoja,si uwalishe chakwako usevu money.
Ufugaji ni mbinu mkuu kwa wafugaji wazoefu wana mbinu za kufuga ambazo huwasaidia kupunguza garama na kuongeza faida...silverland chakula chao ni kizuri ila ukiwalisha kuku wa kienyeji sana faida itakua ndogo sana....hivyo nawalisha mwezi 1 baada ya hapo natengezeza changu..
Mwisho wa siku natumia garama kidogo kwa malengo yale yale na yule aliyetumia chakula cha silverland
 
Appollo 11

Member
Apr 15, 2016
98
150
tupeni ujuzi
Ufugaji ni mbinu mkuu kwa wafugaji wazoefu wana mbinu za kufuga ambazo huwasaidia kupunguza garama na kuongeza faida...silverland chakula chao ni kizuri ila ukiwalisha kuku wa kienyeji sana faida itakua ndogo sana....hivyo nawalisha mwezi 1 baada ya hapo natengezeza changu..
Mwisho wa siku natumia garama kidogo kwa malengo yale yale na yule aliyetumia chakula cha silverland
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom