Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Wataalamu wa mambo ya kiuchumi Duniani wanasema kwamba watu ambao wako busy na maswala ya siasa ni watu wasiokuwa na kazi na ambao kwa nchi zilizoendelea wanaishi kwa kutegema msaada wa serikali, kwani watu ambao wana kazi huwa hawana muda wa kufwatilia mambo ya siasa kwa sana!
Hili jambo ni la kweli kabisa ukilileta hapa TZ, utaona watu wengi hawana kazi au niseme uzalishaji wao kazini ni mdogo sana na ndiyo maana ili kufidia huwo muda hutafuta jambo la kufanya na hivyo basi huwekeza kwenye siasa!
Sijawahi kuona wala kusikia popote pale Dunia hii kwamba nchi inatawaliwa na majadiliano ya kuangalia Bunge live, au watu asubuhi tu na kutwa nzima wanajadili kuhusu Bunge na siasa zake, hii ni ishara tosha kwamba TZ uzalishaji (productivity) ni 0, kwani mtu ambaye ana high productivity kazini hutumia muda mwingi kujiandaa na kazi zake, kama ni Mwalimu basi hutayarisha cha kufundisha, kama ni Mtafiti (maprofesa kama Baregu) wanapaswa wawe busy kufanya utafiti na kuchapisha tafiti zake lkn kutwa nzima yuko JM na kujadili Bunge!
Hivyo maendeleo nchi yetu bado sana, na naipongeza Serikali kwa uamuzi wake wa kusitisha Bunge kuonyeshwa muda wa kazi, ilifikia mahali watu walikuwa wanakaa wanasubiria Bunge lifike waanze kuangalia mipasho!
Nawasishi wekezeni muda wenu mwingi kwenye uzalishaji na acheni blah blah, tembeeni hii Dunia muone kama kuna watu makini ambao wanakaa kutwa nzima kujadili Bunge la nchi yao, wako kazini wanapiga mzigo ili kujiongezea kipato hakuna huwo muda wa kuangalia Bunge!
Wazungu wanasema Time is Money, sasa ninyi mnataka mkae kuanzia asubuhi mpaka jioni mkiangalia Bunge unawezaje kupata fedha kama siyo wizi???