Ufoo Saro wa ITV ajeruhiwa kwa risasi, mamake auawa!

Status
Not open for further replies.
Maskini ! Haya mapenzi haya!! Sasa mana yake anahusika vipi kwenye hili saga?
mkuu akina mama wengine hucheza deal bega kwa bega na mabinti zao si ajabu jamaa alishakuwa na data za kutosha kuhusu nyendo za Ufoo labda na bi mkubwa nae akafumbia macho si unajua tena mambo ya mjini kama mama nae anatembezewa mafao na kidumu cha mwanae anakausha tu si bure kuna jambo hapo maamuzi mazito sana jamaa kafanya. Yaweza kuwa fundisho kwa mama wengine tutajua tu.
 
Mwandishi wa ITV Ufoo Saro amejeruhiwa na Mama yake kuuawa kwa risasi

Mkuu hebu tuliza akili kidogo utupe taarifa iliyokamilika. Imetokea lini na wapi. Lilikuwa tukio la ujambazi au ni nini kimesababisha majeraha pamoja na kifo cha mama yake.

Mwisho usisahau kutujulisha chanzo cha taarifa hii.
 
kama alikula pesa zake,shauri yake na huenda mama yake alishirikishwa pia.
 
Poleni wafiwa, get well soon Ufro

Sent from my BlackBerry - jamiiforums
 
Pole sana mdogo wangu Ufo, this is a crazy world kama alivyo imba marehemu Lucky Dube. Mshukuru Mungu bado una uhai kwa sababu bnadam wanauwa wenzao kama inzi.
 
Kwa taarifa za uhakika ni kwamba mtu mmoja anaesadikika kuwa mume mtarajiwa wa Ufoo Saro Bw. Mushi amemjeruhi mwandishi huyo wa Itv na mchumba wake kwa kumpiga risasa ya tumboni na kisha kumpiga mama mzazi wa Ufoo Saro na kufariki hapohapo kisha yeye mwenye kujiua.

Source RADIO ONE Breaking news
Kisa ni nini?
RIP Mama yake Ufoo Saro.
 
Breaking News
Mtu mmoja anayedaiwa kuwa
ni mume mtarajiwa wa Ufoo
Saro Bw Mushi amempiga
risasi mwandishi wa habari
wa ITV Ufoo Saro na
kumjeruhi tumboni huku
akimuua mama mazazi wa
Ufoo Saro na kisha kujiua
yeye mwenyewe kwa risasi
huko maeneo ya Kibamba.
Chanzo: Radio One
 
ni wivu wa mapenzi, amepigwa risasi na mtu anaedhaniwa kuwa ni mchumba ama mume wake,katika eneo la kibabmba

mchumba/mume huyo,amempiga risasi na kumuua papo hapo,mama mzazi wa ufuo saro,na kisha kujipiga na yeye mwenyewe,na kufa papo hapo pia
 
Breaking News
Mtu mmoja anayedaiwa kuwa
ni mume mtarajiwa wa Ufoo
Saro Bw Mushi amempiga
risasi mwandishi wa habari
wa ITV Ufoo Saro na
kumjeruhi tumboni huku
akimuua mama mazazi wa
Ufoo Saro na kisha kujiua
yeye mwenyewe kwa risasi
huko maeneo ya Kibamba.
Chanzo: Radio One

mmmh wivu wa mapenzi au nini
 
Status
Not open for further replies.
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom