Ufoo Saro wa ITV ajeruhiwa kwa risasi, mamake auawa!

Status
Not open for further replies.

Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
40,205
33,224
Mtangazaji wa ITV, kapigwa risasi.

Aliempiga yasemekana ni mchumb wake somebody Mushi, ambae pia kampiga risasi mamake Ufo Saro na kumuua na kisha yeye mwenyewe Mushi kujiua kwa risasi.

Ufo Sarro yuko mahututi

Cheki ITV breaknews.

--------------------------------
0L7C0700.JPG

---------------------------------

Alfajiri ya leo, mtangazaji wa ITV anayejulikana kwa jina la Ufoo Saro amejeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi na mchumba wake ambaye baada ya tukio hilo naye alijipiga risasi na kujiua. Akizungumza na wanahabari, Kamanda Wambura ambaye ni kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni amesema tukio hilo limetokea majira ya alfajiri ya leo.

Kamanda wambura amedai kuwa mwanaume aliyetenda mauaji hayo ni mchumba wake na alikuwa anafanya kazi katika Umoja wa Mataifa (UN) huko sudani ila bado haijafahamika kitengo alichokuwa akifanyia kazi. Kwa mujibu wa Kamanda Wambura, inasemekana kulikua kuna ugomvi kati ya wawili hao ambapo walishindwa kuelewana na ndipo walipoamua kwenda kwa mama mzazi wa Ufoo Saro(mama mkwe) ili awasuluhishe.

Baada ya usuluhishi kuanza na kuonekana kuwa tatizo liko kwa mwanaume, mwanaume huyo alimshutumu mama mkwe wake kwamba amekuwa na mazoea ya kumtetea mwanae na ndipo alipotoa bastola na kumpiga mama yake na Ufoo Saro risasi ya kichwa na kumuua papo hapo.... Alipomuua mama huyo, mwanaume huyo alimpiga Ufoo Saro risasi mbili, moja ya tumboni na nyingine ya mguuni na kudhani kwamba amemuua kumbe amemjeruhi tu kisha kujipiga mwenyewe risasi ya kidevuni na kufariki dunia hapo hapo.
sio yeye tu na mama yake mzazi ambaye ameshafariki, na muuaji amabaye anatajwa kuwa mchumba wake anayefanya kazi UN pia anadaiwa kajiua kwa risasi.
Ametoka hospital ya tumbi anapelekwa Muhìmbili. Anaendelea vizuri.

Nimesikia Breaking News ITV.Nimeshtushwa sana kusikia Taarifa hii.It's so Sad

Ufoo Saro Muda huu yupo Hospitali amejeruhiwa kwa Risasi Tumboni na Mguuni.

Mama yake amepigwa Risasi Kifuani na Huyo Mchumba wake amejipiga Risasi kidevuni na kufa papo hapo.Hali ya Ufoo Saro hadi sasa haijulikani ikoje

Jeshi la polisi limetangaza kuwa linachunguza kujua ndugu za huyo mume wake.Inasemekana ni Mfanyakazi wa UN

Tukio limetokea leo alfajiri eneo la Kimara.

=====================
MORE UPDATES:-
=====================

Mwenyekiti mtendaji wa IPP ametoka kuongea na media sasa hivi. Anasema Ufoo anaendelea vema na anazungumza.

Kapigwa risasi tumboni na mkononi na madaktari wanahangaika kuhakikisha wanaokoa maisha yake. Wameomba apumzike kwa sasa so hakuna mwandishi alieruhusiwa kuingia ndani wala ndugu zaidi ya Mzee Mengi tu.

Afande Ahmed Msangi nae amesema Ufoo anaendelea vema. Polisi wamegawanyika katika timu tatu. Moja inaongozwa na Msangi ipo Muhimbili, ya pili ipo Kibamba yalipotokea mauaji na ya tatu inashughulika mtaani kutafuta taarifa muhimu za mauaji. Soon watakutana kutoa updates.

Naweka picha za msangi na mengi wakiongea na media sasa hivi

Mengi akiongea na wanahabari nje ya kitengo cha dharula hosp ya muhimbili. Pembeni ni afande Ahmed Msangi
attachment.php

Afande ahmed msangi akizungumzia tukio hilo hopitalini muhimbili muda mfupi uliopita
attachment.php
 
Mwandishi Ufoo Saro wa ITV amejeruhiwa kwa risasi baada ya kupigwa risasi ya tumboni na mguuni huku mama yake akiuawa kwa kupigwa risasi kifuani na mtu anayedaiwa kuwa ni mume wake/mchumba wake aliyewapiga risasi ambae naye amejiua kwa kujipiga risasi.
 
Aliempiga yasemekana ni mchumbake somebody mushi,ambae pia kampiga risasi mamake ufo saro na kumuua na kisha yeye mwenyewe mushi kujiua kwa risasi.
Ufo sarro yuko mahututi
 
Kuna taarifa kwamba mtangazaji wa ITV( Ufo Saro) amepigwa risasi na kujeruhiwa vibaya huko maeneo ya Kibamba leo Alfajiri. Aliye fyatua Risasi hizo ni mchumba wa Mtangazaji huyo, anayefanya kazi shirika moja la UN, ambaye baada ya tukio hilo naye alijipiga risasi na Kujiua.

Source: Breaking News - Radio One
 
Mtu mmoja alietambulika kua mchumba wa ufuo saro ame wapiga risasi ufuo saro na mama yake..mama ufuo saro kafariki dunia huku mwandishi ufuosaro kakimbizwa hospitali mahututi
 
Breaking News from ITV - Kijana Mushi anayeripotiwa kuwa ni mume au mchumba wa Ufuo Saro mtangazaji ITV amempiga risasi ya kifuani mama mkwe wake na kupelekea kifo chake leo alfajiri. Mushi amempiga risasi ya tumbo na mguuni Ufuo ambaya mpaka sasa anaendelea na matibabu. Tukio hili limetokea Kimara.
 
Mwandishi wa ITV Ufoo Saro amejeruhiwa na Mama yake kuuawa kwa risasi

Breaking News
Mtu mmoja anayedaiwa kuwa ni mume mtarajiwa
wa Ufoo Saro Bw Mushi amempiga risasi mwandishi
wa habari wa ITV Ufoo Saro na kumjeruhi tumboni
huku akimuua mama mazazi wa Ufoo Saro na kisha
kujiua yeye mwenyewe kwa risasi huko maeneo ya
Kibamba.
Chanzo: Radio One
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom