UFISADI: Waziri Mkuu amsimamisha Mhazini wa TPA na wengine. CAG aagizwa kufanya ukaguzi haraka

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,806
12,221
Leo tarehe 27/12/2020 Waziri Mkuu ambaye ni Mbunge wa Ruangwa amefika katika bandari ya Dar es Salaam

More to follow

=====

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwenda kufanya ukaguzi maalum katika bandari za Dar es Salaam, Mwanza, Mtwara, Tanga na Kyela kutokana na kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha za umma.

Pia Waziri Mkuu amewasimamisha kazi Mkurugenzi wa Fedha wa TPA, Bibi Nuru Mhando pamoja na Meneja wa Matumizi ya Fedha wa TPA, Bibi Witness Mahela ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha zinazowakabili.

Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo baada kupokea ripoti ya Ukaguzi Maalum uliofanywa na CAG katika hesabu ya Bandari ya Kigoma kwa mwaka 2017/2018 na 2018/2019. Lengo la ukaguzi huo lilikuwa kujiridhisha kuhusu matumizi mabaya ya fedha za umma.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Jumapili, Desemba 27, 2020) katika kikao chake na Waziri na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Bodi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania na Menejimenti ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) kilichofanyika katika ofisi za TPA jijini Dar es Salaam. Amesema taasisi hiyo imebeba taswira ya uchumi wa Taifa, lazima kazi ifanyike vizuri.

Mheshimiwa Majaliwa ameitaka Bodi ya Bandari Tanzania ihakikishe kwamba mamlaka hiyo inafanyakazi kwa weledi na isisite kuchukua hatua kwa mtumishi atakayebainika kutenda makosa na isimbebe kwa namna yoyote.
 
Leo tarehe 27/12/2020 Waziri Mkuu ambaye ni Mbunge wa Ruangwa amefika katika bandari ya Dar es Salaam

More to follow

Akitoka hapo aanze ziara za nchi nzima kuzindua viwanda 100@mkoa, vilivyojengwa kwenye awamu hii ya Tanzania ya viwanda. Hii itasaidia wale watanzania 12.5m wa kura za kwenye mabeg wawe na uhakika wa ajira.
 
Leo tarehe 27/12/2020 Waziri Mkuu ambaye ni Mbunge wa Ruangwa amefika katika bandari ya Dar es Salaam

More to follow
Amesahau Bandari ya kwao mtwara,bandari imegharimu mabillioni ya sh lkn korosho zoote kutoka mikoa ya kusini yaani Lindi na Mtwara na Ruvuma zinalazimishwa kupitia bandari ya dsm.

Wana kusini watajivunia kitu gani kwa kuwa wazalishaji wa korosho na kuwa wenyeji wa bandari iliyo boreshwa na yenye kina kirefu hapa Tanzania?
 
Akitoka hapo aanze ziara za nchi nzima kuzindua viwanda 100@mkoa, vilivyojengwa kwenye awamu hii ya Tanzania ya viwanda. Hii itasaidia wale watanzania 12.5m wa kura za kwenye mabeg wawe na uhakika wa ajira.
We dogo najua umeumia sana Chadema kupigwa down,sababu mligeuza siasa ni biashara ya kuwashibisha. Kubali yaishe utakaa unalialia mpaka lini?
 
We dogo najua umeumia sana Chadema kupigwa down,sababu mligeuza siasa ni biashara ya kuwashibisha. Kubali yaishe utakaa unalialia mpaka lini?

Ule haukuwa uchaguzi bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura, sasa hapo naumia nini? Na huyo PM akitaka alale kabisa hapo bandarini, lakini ukweli wa kuwa hali ni mbaya, uko wazi hadharani.
 
Hali mbaya kivipi? Nini kimekwama?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom