Ufisadi wazidi kuitafuna Wizara ya Maliasili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi wazidi kuitafuna Wizara ya Maliasili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mnyama, Sep 16, 2008.

 1. m

  mnyama Member

  #1
  Sep 16, 2008
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pamoja na mabadiliko ya uongozi Wizara ya maliasili na utalii, ufisadi umeendelea kuitafuna wizara hiyo nyetu na kupoteza matumaini ya wananchi juu ya mstakabali wa wizara hiyo. Hali ni mbaya zaidi baada ya wale waliokuwa wakitarajiwa kutokomeza ufisadi kuibuka na kuwa vinara wa kuu wa ufisadi huo.

  Viongozi wakuu wawili wa wizara hiyo ambao wote ni kina mama hivi karibuni wamejikuta katika mgogoro mkubwa hadi kutishiana vifo kutokana na magogo ambayo yanadaiwa ni ya mmoja wa wa akina mama hao kukamatwa na kuzuiwa wakati mwanamama huyo akiwa safarini. Baada ya kupewa taarifa ya kukamatwa mwanamama huyo alimpigia simu mwenzake ili alimalize soo hilo, jambo ambalo mwanamama mwenzake hakukubaliana nalo na hivyo kuamua kufungua sheria ichukue mkondo wake.

  Kitendo cha mwanamama huyo kupuuza agizo hilo la bosi wake, kimeleta bifu kali na kuharibu hali ya hewa wizarani hapo. Inasemekana kuwa mwanamama ambaye anahusishwa na magogo hayo alimchimba biti mwenzake ikiwa ni pamoja na kumtishia kumuua. hali iliyosababisha achukue likizo ili kuepusha shari zaidi. Hata hivyo haikuweza kufamika mara moja ni kwa nini mwana mama huyo alitupilia mbali magizo y
  la bosi wake huyo ili hali na yeye ni fisadi aliyekubuhu.

  Habari za kutishiwa kifo mwana mama huyo aliziripotiwa ikulu, na siku za hivi karibuni watu wanaodaiwa kuwa usalama wa Taifa wamekuwa wakionekana kuzunguka mara kwa mara katika ofisi za wizara hiyo zilizoko mtaa wa samora. Haikuweza kufahamika mara moja wanausalama hao wamekuwa wakifanya nini. Baadhi ya watumishi wa wizara hiyo wameonekana wakisononeshwa na sakata hilo huku wakimtaka raisi JK kuingilia kati na kumuuondoa mmoja wao kabla hali haijawa mbaya zaidi.

  "Watauana hawa kweli ohooo" alisikika mmoja wa watumishi hao akiongea. Mtoa habari alizidi kunyetisha kuwa, ugomvi kati ya kina mama hao, ulianzia katika swala la kuhama jengo. Mmoja wa akimama hao ambaye anahusishwa na magogo alitaka wizara hiyo ihamie kwenye jengo lake ambalo limeshakamilika lakini mwenzake alipinga kuwa hakuna kuhamia mpaka furniture mpya zinunuliwe. Inasemekana mama huyo alisha chonga dili la ununuzi wa furniture mpya kwa jengo zima mbazo zina gharimu mamilion ya fedha na hivyo kupata chajuu.
  Hatua hiyo ya kulazamisha kuhama jengo inaelezwa ilimchukiza mwana mama huyo na huenda ndo sababu ya kumfanyia fitna mwenzake kwenye swala magogo.

  Mimi kilichonishangaza hapa ni jinsi mwana mama huyo alivyo hodari wa kuchangamkia ufisadi. Muda mfupi tu mwana mama huyo kuingia ofisini tayari ameshaanza biashara ya magogo! Loh kweli fisadi ni fisadi tu

  Bahati mbaya sina inzi wa kumtuma kuleta details. Wenye inzi tafadhali watumeni inzi wenu watuletee habari zaidi.
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  hata hii uliyoleta umeficha mambo mengi sana. Unataka watu wajadili 'mwanamama' au 'wanamama'? Unaogopa nini kuwataja?
   
 3. BadoNipo

  BadoNipo Senior Member

  #3
  Sep 16, 2008
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 175
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Huyo mama kazoea kufanya ufisadi toka akiwa Hazina.
   
 4. Ncha

  Ncha JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2008
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mbona hamuweki vitu wazi? JF ni kusema wazi kila mtu ajue kama ni kweli au majungu
   
 5. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  ...Marvellous!!!!!!!!!!!!!!!
   
 6. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  ....Udaku??? Hana Jina??? Mnatupotezea stimu nyie watu!!!!!!
   
 7. M

  MpiganajiNambaMoja Member

  #7
  Sep 16, 2008
  Joined: Sep 20, 2007
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maliasili katibu mkuu ni Blandina Nyoni na Waziri ni Somebody Mwangunga nimesahau jina la kwanza, labda ndo hao wanaongelewa. Na aliyekuwa hazina ni Mama Blandina Nyoni. So kwa mujibu wa maelezo hapo juu magogo yanahusishwa na waziri na Nyoni ndo alitia ngumu. I think so..
   
 8. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  why keep us guesing? kama ndio hao mleta hoja aeneleze ieleweke ili watu wenye michango zaidi waimwage
   
 9. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2008
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  Tafadhali acha mambo ya jikoni. JF ni kusema ukweli bila kuficha. Habari yako haina utamu wala radha tokana na kunyimwa vibwagizo.
  Taja majina ya wahusika kamili bila kuogopa lakini ukisema wakina mama ama mwana mama inaonesha wazi unaogopa ama hauna uhakika na unacholeta hapa JF.

  Kwa kukusaidia hapo wizarani kuna Shamsa Mwangunga ambaye ni waziri na Blandina Nyoni ni katibu mkuu. Sasa leta habari inayoeleweka.
   
 10. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #10
  Sep 16, 2008
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Acheni udaku nyie mwageni nyuzi hizo.....................................
   
Loading...