Ufisadi watafuna Tanzania Daima,wahariri hoi,nini hatima??

HuXiang

Member
Apr 13, 2008
36
1
Ndugu wana jf mimi na kama wana jf wengine tuishio nje ya nchi ni mara nyingi sana tunategemea haya magazeti yanayopatikana online katika kupata news na mambo yanayojiri nyumbani,na katika yote kuna hili gazeti la Tanzania daima ambalo lina sehemu ya maoni na makala kadhaa,sasa nina hoja yangu...
Hawa jamaa kwa sasa nadhani mafisadi wamewavamia na kuwafanya washindwe kuupdate habari zao hata kwa siku nne,munaweza tembelea tovuti yao GONGA.
Mimi kwa ufahamu wangu mduchu ni kuwa hizi habari sio kama ni bure ndio maana mzee mwana kijiji huwa anatuambia tuwe tunagoogle site yake kwani huwa wanalipwa kutokana na idadi ya watu wanaotembelea site,hii ni wazi kwani hutumika kwa analysis katika matangazo.
Sasa nini nataka kusema ni kuwa sisi tunalipia internet service then tunalogin kwa hawa jamaa tunawaongezea idadi ingawa muda tunaotumia ni mchache lakini number inakuwa kubwa then wao hawatupatii huduma,je nao si mafisadi??? au mafisadi ni lazima wawe wanachukua pesa cash??
naombeni michango yenu..nitarudi tena kwa sasa naenda Duolojie kupata jiaozi.
 
hao!
jamani jioneeni maoni ya watanznaia juu ya gazeti hili.

MHUSIKA WA GAZETI HILI. SASA HAIELEWI NI GAZETI LA TAREHE IPI AU MEI MOSI HAMKUTOA GAZETI.
NI GAZETI LENYE WAANDISHI WENYE KUSAHIHISHA JAMII.
LAZIMA KWANZA MJISAHIHISHE. KUCHELEWA KWA GAZETI HILI NI UZEMBE, KUKOSA MASHINE MUHIMU AMA NINI?
KABLA YA KUKOSOA WENGINE LAZIMA UONESHE MFANO WA UWAJIBIKAJI. NI AIBU KUSOMA GAZETI LA JANA WAKATI WAHARIRI WENGINE WAMEISHA TOA HATA MAGAZETI YA KESHO!!

na Homa ya Jiji - 2.05.08 @ 15:33 | #9655

Mtanzania Daima mnaboa, yaani sa hizi ndo mna-publish gazeti kwenye Internet. Haya bwana, nyie mmeshika mpini wakati sisi tumeshikilia makali.

na Mtanzania Kweli - 2.05.08 @ 15:40 | #9660

Ndugu mhariri na moderator wa mtandao huu, naungana na waliosema kuwa gazeti la mei mosi halikutoka kwenye mtandao sehemu ya habari mpya.

Pamoja na kuwa sikubaliani na kutowekwa kwa gazeti la mei mosi kwenye habari mpya, sikubaliani na wazo la kusema habari mpya ziondolewe mapema. Inabidi kutoa muda wa kutosha kwa ambao sababu ya majukumu ya kazi maofisini wanashindwa kutoa maoni yao lakini pia kusoma maoni ya wengine.

Muda wa kutosha wa gazeti jipya kuwepo kwenye mtandao unasaidia wananchi wazalendo tuendelee kutafuta dawa ya ufisadi kupitia kubadilishana mawazo na kukemea ufisadi. Wajua gazeti likiondolewa kwenye habari mpya na kupelekwa gazeti la jana hakuma maoni mapya na mtu hashiwishiki kuangalia maoni kwenye gazeti la jana.

na Kawala, Ubelgiji, - 3.05.08 @ 12:05 | #9749

Kwa kweli Tanzania Daima hamtutendei haki wasomaji wenu. Kitendo cha kutuwekea gazeti la jana hadi dakika hii kinakera sana. Tumeshasoma gazeti la kawaida, na mida hii tumekuja kutoa maoni kwenye Internet, cha ajabu hadi sa hizi hamjapublish gazeti jipya. hatutoi maoni bure, tunalipia kwenye hizi Internet. Kwa hivyo basi zingatieni haya maana mnatuumiza sisi. Tunao taka kutoa maoni kiuchumi.

na Jamal Kileo - 3.05.08 @ 15:35 | #9763

KAMA MAMBO NDO HIVI BASI TANZANIA DAIMA TUWEKEENI HATA MAGAZETI YA MWAKA 1990, MAKE HATAKI KWENDA NA WAKATI!!!! SASA TULUDISHENI NYUMA TUWAELEWE!!

na JUMA, DAR, TZ, - 3.05.08 @ 15:54 | #9765

Gazeti hili litakuja kusomwa na wavuta tumbaku wapate karatasi la kutengeneza misokoto. LINACHELEWA MNO NA KUDHALILISHA WANA HABARI WAKE KWANI HABARI ZAO ZINAKUWA ZIMECHAKAA SABABU YA MAGAZETI MENGINE YANAYOWAHI.
MHARIRI WA GAZETI HILI AWE MNYENYEKEVU NA KUJITANGAZA TUMTAFUTIE UFADHILI.

na Madaha - 3.05.08 @ 20:09 | #9771

'Tanzania-Daima' mbele ya mafisadi sasa kwisha kazi.Mafisadi wamewaingilia mpaka jikoni hadi mmeshindwa kwenda na wakati.Ogopa mafisadi,ni kama mazungu ya unga.Poleni sana mhariri na kwa kheri Tanzania Daima!

na Johnson, Dsm, - 4.05.08 @ 12:59 | #9783

Kusema kweli mimi sasa sioni haja ya hawa watu wa Tanzania Daima kukemea mafisadi kwani wao wenyewe nao ni mafisadi,Tunapozungumzia utawala bora ambao kikwete hajautekeleza na na hili nalo watu wa Tanzania Daima lazima mulibebe kuwa munatufisadi kama baba yenu kikwete,Sio kama tunasoma magazeti bure,najua munalipwa kutokana na namba ya watu wanaologin kwenye site yenu sasa iweje ninyi mukawa munatumia pesa zetu burebure??? Tumechoka so sasa ni muda wa kutambaza sumu kote.

na FisadiDaima, Temeke, - 5.05.08 @ 08:52 | #9793

Mimi nadhani kipindi tunakemea ufisadi ni heri tukagusa anga zote,kwani hawa jamaa huwa Active kipindi kuna skendo kubwa then hupotea,so inawezekana wanatumiwa na mafisadi hawa kuwapumbaza raia kivipi ? wenye fikira watakuwa washabaini nini ninamaanisha...
Zaijian
 
gazeti kutokuwa mtandaoni siku moja au mbili unaweza kuelewa, lakini kwa zaidi ya siku tatu!!!??? (kwa tone ya wagosi ya kwaya
 
yale yale .Jamani JF we can also spin if we want thus we need no spinnesrs.Hii habari ina udaku mwingi sana .Hatuhitaji habari za ain hii hapa JF .
 
Hawa jamaa naona utendaji kazi wao unasua sua naona itakuwa labda mtaalamu wao kaachishwa ndo maana wanashindwa ku update news kila siku.Ngoja tuwapigie cmu wanatuboa sana hawa jamaa.
 
yale yale .Jamani JF we can also spin if we want thus we need no spinnesrs.Hii habari ina udaku mwingi sana .Hatuhitaji habari za ain hii hapa JF .
LUNYUNGU CHUKUA TANO NAKUUNGA MKONO EBU,MWANAKIJIJI,MWAFRIKA WA KIKE NA MKUU LUNYUNGU LETENI ISSUES HAPA TUJADILI.
 
Kimsingi hawa Tanzania Daima wanaboa mno maana unajua kwa mtu aliyewahi kufuga mbwa (ni mfano tu) halafu ukamzoesha kumpa chakula saa sita mchana kila muda huo ukifika lazima aanze kujilamba na ukipita kidogo anaanza kufanya fuju bandani. Hawa jamaa TD walikuwa wametuzoesha kutupa chakula chetu asubuhi kila siku sasa hivi hawatoi hii ni kutukosesha haki yetu ya msingi ya kupata habari. Ndiyo maana watu wanaojua namna ya kutengeneza maneno wansema ni ufisadi wa habari. Kama kuna tatizo they have announce kwamba sasa hali iko hivi.

Hii kwa kweli mimi imenisikitisha sana maana habari za uhakika zenye maoni ya watu nilikuwa ninapata TD.
 
can somebody move this thing out of here...!?

Jamani Hii JF ni ya watz wote si mtu fulani.pia mutu yeyote anaruhusiwa kuchangia awezavyo,
Kwa ushahidi wa kimazingira tunajua jinsi gani Mwanakijiji ulivyo na masilahi na watu wa Tanzania Daima ndio maana hii habari inamuuma sasa sijui huyo mwingine nae kinamuwasha nini.
Nilipoandika imevamiwa na Mafisadi nimemaanisha nililoandika kwani ni nini maana ya Fisadi? Je webmaster ambaye analipwa mshahara huku tukikaa siku nne kusubiri habari mpya sio fisadi? Au munasubiri mpaka afikie kuwa na Vijisenti ndio muanze kupiga makelele? Mwanakijiji ni wewe uliye mstari wa mbele kupiga madongo watu wa ATC kumbe ni kwa sababu ni kwa wenzako???
Ninazidi kupata hofu kuwa kuna wakemea ufisadi wengi ni mafisadi ila kwakuwa hawakupata sheha katika hilo skendo ndio maana wanajifanya kupiga makelele hapa.Tunazidi kuwaona na kubaini Tz ni fisadi tupu kila angle.
NIna imani na uhakika kuwa kitendo cha watu kutembelea site yako huwa kuna faida unapata kwani huwa wanapima number of site visitors plus muda wanaotumia ndani ya site yako..Kwa wale wasiofahamu hiyo ndio hali halisi.Sasa sisi tunalipia net na kuwapa faida huku mukituyeyusha.
Mkuu mwanakijiji kama imekugusa basi naona ni wakati mahususi kuwaambia watu wa Tanzania Daima kuwa tumekerwa na Tutapambana nao milele.ni bora waombe kujiunga na IPP Media.
Jambo forums ni ya wote so hakuna mtu wa kutuziba midomo,tutakemea ufisadi ndani ya ufisadi,Na Moderator usiifute hii thread kwa ushabiki wa watu wachache.
Mungu ibariki Tanzania,Mungu Ibariki JF
 
HuXiang,

Tatizo hujaeleza nini unachotaka kijadiliwe, unaandika mambo mengi na kuhusisha hata yasiyo kwenye heading yako! Nimesoma yote lakini sijaona kwanini kwenye heading yako umeandika "wahariri hoi". Ndio maana wachangiaji wanauliza kwanini hii thread iendelee kuwa hapa! maana ni kama ya kizushi kidogo!

Ingevutia wachangiaji kama thread yako ingekuwa katika mtiririko huu (Kulikoni Tanzania Daima, nini hatima ya tovuti yake?), hapa ninauhakika ungepata wachangiaji wengi, tena wenye majibu ya swali lako. Lakini the way ulivyo-present ... ladha na hamu ya kujibu inakwisha!

Kwasababu wewe ni mdau wa tovuti ya Tanzania Daima, ebu twanga hizi namba za chumba cha habari TZDaima, watakuhabarisha
simu +255-22-2126233
Selula 0713 296570
 
HuXiang,

Tatizo hujaeleza nini unachotaka kijadiliwe, unaandika mambo mengi na kuhusisha hata yasiyo kwenye heading yako! Nimesoma yote lakini sijaona kwanini kwenye heading yako umeandika "wahariri hoi". Ndio maana wachangiaji wanauliza kwanini hii thread iendelee kuwa hapa! maana ni kama ya kizushi kidogo!

Ingevutia wachangiaji kama thread yako ingekuwa katika mtiririko huu (Kulikoni Tanzania Daima, nini hatima ya tovuti yake?), hapa ninauhakika ungepata wachangiaji wengi, tena wenye majibu ya swali lako. Lakini the way ulivyo-present ... ladha na hamu ya kujibu inakwisha!

Kwasababu wewe ni mdau wa tovuti ya Tanzania Daima, ebu twanga hizi namba za chumba cha habari TZDaima, watakuhabarisha
simu +255-22-2126233
Selula 0713 296570


Huyu Jamaa ana matatizo.Maana sasa anamvaa Mwanakijiji.Mwanakijiji yuko US si mwandishi wa TD sasa maslahi unayo yasema ni yapi ? Ana andika makala kama wewe unavyo andika hapa JF.Jamani personallity attacks is low .Hapa JF tuko kwa nia moja tu .Kumnyama Mnyama ila kama ukija na hoja tofauti na sisi tuko tayari kukuunga mkono kama hoja ina akili na si zaidi ya hapo .
 
Mkuu nashukuru kwa mtazamo wako.
Nadhani hapa wewe umekerwa na hiyo wahariri hoi.Kimsingi tunapozungumzia Tanzania Daima tunazungumzia Gazei zima kwa ujumla uanzia wahariri,waandishi wa habari nk.Kwanini nimesema wahariri hoi? Ni kwa maana wao ndio wenye kazi ya kuhakikisha kuwa Effective news inawafikia walengwa,sasa hebu tafakari je kwa mtindo huu kuna Effective news? Hawapo Hoi?
Nashukuru kwa mtazamo wako ila sio watu wote tuwe na mtazamo mmoja,pia vichwa va habari hutumia Lugha iliyo kwenye soko la habari kwa wakati huo.
Nadhani habari yangu kwa wenye kupenda kuchambua mambo watakuwa wameelewa nimemaanisha nini na kichwa changu cha habari hakina utata hata kidobo. Ila ni mara nyingi embapo kuna watu hapa JF huwa hawatafakari maana halisi ya habari.
Huko ndio kukua kwa Lugha yetu mwanana ya kiswahili.
 
Huyu Jamaa ana matatizo.Maana sasa anamvaa Mwanakijiji.Mwanakijiji yuko US si mwandishi wa TD sasa maslahi unayo yasema ni yapi ? Ana andika makala kama wewe unavyo andika hapa JF.Jamani personallity attacks is low .Hapa JF tuko kwa nia moja tu .Kumnyama Mnyama ila kama ukija na hoja tofauti na sisi tuko tayari kukuunga mkono kama hoja ina akili na si zaidi ya hapo .
Lunyungu next time kaa chini kabla ya kuandika na usome kwa nini nimemgusa mwanakijiji? MImi nilikuwa ni mpenzi mzuri wa TD na kulikuwa na habari nyingi za huyo Mwanakijiji ndio maana nilitumia Ushahidi wa Kimazingira.
Sasa nazidi kupata picha jinsi gani watu wanavyoumia na kushambuliwa..Tumekuwa tukiwashambulia viongozi hapa hata wengine kuwatukana..so kama mwanakijiji atakosea hatumuachi mtu hapa labda waifunge hii JF.
Musitake kubadili maana ya habari yangu na kuleta malumbano hapa.Sina muda huo...
 
Lunyungu next time kaa chini kabla ya kuandika na usome kwa nini nimemgusa mwanakijiji? MImi nilikuwa ni mpenzi mzuri wa TD na kulikuwa na habari nyingi za huyo Mwanakijiji ndio maana nilitumia Ushahidi wa Kimazingira.
Sasa nazidi kupata picha jinsi gani watu wanavyoumia na kushambuliwa..Tumekuwa tukiwashambulia viongozi hapa hata wengine kuwatukana..so kama mwanakijiji atakosea hatumuachi mtu hapa labda waifunge hii JF.
Musitake kubadili maana ya habari yangu na kuleta malumbano hapa.Sina muda huo...

Mkuu you are going emotional mie simo nakataka issue .Mshambulie mtu kwa jambo la maana .TD unajua mahala pa kuwapata .Hujajua wana matatizo gani hujachunguza unaanza kusemaje ?
 
Back
Top Bottom