Ufisadi waigawa Ofisi ya Bunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi waigawa Ofisi ya Bunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by friendsofjeykey, Jan 27, 2011.

 1. f

  friendsofjeykey Senior Member

  #1
  Jan 27, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  VITA dhidi ya ufisadi iliyovuma katika Bunge lililopita imewagawa watumishi wa Ofisi ya Bunge katika makundi mawili yanayohasimiana huku kila kundi likijaribu kusaidia vigogo wake kujinasua au kujijenga zaidi kisiasa na kimaslahi.

  Taarifa za uhakika kutoka ndani ya ofisi hiyo zilizolifikia gazeti hili zimeonyesha kuwa mgawanyiko huo unaenda sanjari na ule uliojitokeza kwa wabunge wa Bunge la tisa, ambapo kundi moja la wabunge lililojipambanua kupambana na ufisadi liliingia katika mvutano mkubwa na jingine lililopewa jina la mafisadi.

  Baadhi ya watumishi wa ofisi hiyo hususan wale wa Idara ya Uhasibu, wamelieleza gazeti hili kwamba wamegawanyika katika makundi mawili, moja likijipambanua kama wapambanaji dhidi ya uongozi mbaya wa taasisi hiyo na jingine ni la wanaofaidika na mfumo wa uongozi.

  “Tumegawanyika, sasa baadhi yetu hata hatusalimiani kwa sababu tunachukiana na chanzo chake ni mgawanyiko ulioanza pole pole wakati tukiwaunga mkono wabunge ambao walikuwa wamegawanyika katika makundi mawili wakati wa mlipuko wa vita ya ufisadi.

  Alisema kujiingiza katika vita hiyo ya kisiasa kumesababisha wafanyakazi hao kuhasimiana kimaslahi kwa madai kuwa wafanyakazi wanaounga mkono kundi la wabunge wanaotuhumiwa kwa ufisadi wamekuwa wakinufaika zaidi kuliko wenzao wanaounga mkono kundi la wabunge wapambanaji wa ufisadi.

  “Spika Makinda mara tu baada ya kushika wadhifa huo aliitisha mkutano wa wafanyakazi wote ambapo walitupiana tuhuma kubwa, nyingi zinahusu matumizi mabaya ya madaraka na fedha za taasisi hiyo…na kwa hiyo alisema ataunda tume ya kuchunguza malalamiko hayo,” alisema mtumishi huyo wa Bunge.

  Uchunguzi wa gazeti hili tangu kuanza kwa semina ya siku kumi ya wabunge katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam, umebaini kuwepo kwa kampeni kali za kuchafuana kutoka pande mbili zinazohasimiana baina ya wafanyakazi wa ofisi ya bunge, huku wakitaka malalamiko yao yawekwe wazi katika vyombo vya habari.

  Hata hivyo, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashillilah, alipoulizwa kuhusu mwenendo huo wa mambo alisema wafanyakazi hawajagawanyika bali wapo baadhi ambao wamekuwa wakisambaza maneno ya uongo ambayo yamekuwa yakiwachonganisha watumishi na baadhi ya wanasiasa kwa malengo yao binafsi.

  Kuhusu mkutano baina ya Spika Makinda na wafanyakazi hao, alisema ni kweli mkutano huo ulifanyika na wafanyakazi walitoa dukuduku lao lakini alisisitiza kwamba hilo ni jambo la kawaida kufanywa na viongozi wanapotaka kujua mwenendo wa mambo katika taasisi wanazoziongoza.

  “Makinda analijua bunge kiasi cha kutosha na anawajua wafanyakazi wa Bunge, hivyo ana uhakika atafanyia kazi aliyoyasikia kwa wafanyakazi kadiri ya uwezo wake na sisi tutakuwa naye karibu kuhakikisha anayapatia ufumbuzi malalamiko na kero zote za wafanyakazi wa taasisi hii.

  Ufisadi waigawa Ofisi ya Bunge
   
 2. Z

  ZenaTulivu Senior Member

  #2
  Jan 27, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 137
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Yeyote anayetetea bado serikali ya mafisadi ni ADUI WA TAIFA LETU!

  Ni adui wa azma yetu kulinda rasilmali zetu! Ni adui mkubwa wa vizazi vijaavyo vya taifa hili!! Na popote walipo wamelaaniwa hata kabla hatujaing'oa hii serikali dhalimu.

  Ama uko pamoja na sisi raia wa nchi hii tunaoteshwa sana au uko na maadui wetu mafisadi, period! Watubu sasa hivi au wanyamaze milele!
   
 3. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Makinda amewekwa pale kama spika na kundi la mafisadi na wamemuahidi kumlipia deni lake kubwa la mkopo benki kama atatimiza malengo yao; ni wazi basi atakuwa mtetezi wa kundi la wafanyakazi wa bunge wanaowatetea mafisadi!
   
 4. f

  friendsofjeykey Senior Member

  #4
  Jan 27, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sasa kuna civil war

  wengine wanapata zaidi ya wenzao
   
 5. V

  Vumbi Senior Member

  #5
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 191
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kama makundi yamefika kwenye ofisi za umma basi tusubiri vita ya ndani hivi karibuni.
   
Loading...