Ufisadi wachukua sura mpya ;Mengi asema waliochukua pesa walaaniwe

Mugishagwe

JF-Expert Member
Apr 28, 2006
300
58
Bwana Mengi leo katika taarifa ya habari ITV na kwa niaba ya media owners wa TZ ametoa tamko kali dhidi ya walio chukua pesa kwa Lowasa na Rostam ili wawasafishe majina yao .Aliendelea kudai kwamba kwenye soo la Richmond kuna wakubwa kibao wamebaki na sasa wanatumia pesa kuwazima waandishi na wengine kuomba kuandikwa vyema .Mwenye full statemet tafadhali aiweke .

Je kujotokeza kwa Mengi hadharani ni move mpya ya watu kuumana ?
 
Mengi kaja juun ya jina la walio owners wa vyombo vya habari . Je hana ujume mahususi ? Mbona magazaeti yake mara zote huwa yanaficha ukweli na hata alishindw akuandia majina na picha za wale waliotajwa na akina Slaa ?
 
Jamani huyu mengi naye si nilisikia kipindi cha nyuma alikuwa na saga ambalo hakulitolea ufafanuzi, la pesa za AIDS sijui zilizotolewa bank kwa jina lake naye akasema hajui mpaka hilo suala likazua utata kati yake na basaleh? Liliishia wapi?
 
Mimi najua pesa za Vilema na ushuru wa Benzi nk .Lakini pamoja na hayo ndiyo asikemee ujinga huu ?
 
Inakubalika katika mitazamo ya watu kadhaa,kwamba vyombo vya habari ni mhimili wa nne wa dola. Ni dhahiri mhimili huu ukiendelea kuliwa na mchwa(ufisadi,rushwa au takrima na ukengeufu kimaadili)dola itaporomoka na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu litakalowatesa raia wasio na hatia hadi siku watu wema watakapoamua kuingila kati kwa nguvu zao zote.
Mlio na dhamana ya kuuendesha mhimili wa nne hatutegemei muisaliti jamii kwa manufaa ya mafisadi wachache. Eti nini,mwapewa vihela ili msafishe majina yao! Kabla hamjavipokea,mwogopeni Mwenyezi Mungu aliyewaumba watanzania,fikirieni madhara ya tendo hilo kwa watu milioni 40 walio hai na wengine watakaozaliwa baadaye, angalieni msishiriki dhambi ambayo si yenu ili hukumu halisi itakapoanza mpate pa kuponea.
Watanzania hawajashindwa kuamua kutonunua magazeti yatakayojaribu kuwaambia eti fulani msafi ilihali uchafu wake unaonekana kwa macho pasina miwani. Anayetaka usafi atokeze hadharani atubu dhambi zake alizoutendea umma wa watanzania.
Watanzania hawajashindwa kususia kupeleka matangazo ya biashara na mengine katika vyombo vya habari vitakavyoendeleza usaliti.
Tufike mahali vyombo vya habari vyote, nasema vyote viwe mstari wa mbele katika vita dhidi ya wanaoliangamiza taifa.
Aidha haitatosha tu kuwa na habari na mijadala juu ya ufisadi huu ama ule bila hatua kuchukuliwa. hapa naukumbuka usemi usemao, Njia pekee inayouwezesha uovu kutamalaki ni watu wema kutofanya chochote. Asomaye na aelewe.
 
Deo Balile ni mmoja wa hawa walio chukua chao mapema kwa Fisadi yule amwagiwe laana japokuwa ni Mhaya mwenzangu .
 
Naomba kuelimishwa,

Hivi Kulikoni na ThisDay sii mali ya IPP?

Mbona mengi sana huandikwa ktk haya magazeti kupinga rushwa?
 
mugishagwe huyu ni FISADI LAANIKA tena kama possible wambenene kabisa maana hawa wanauwezo mkubwa wa kuiua jamii ,,yalaaaa
DEEEEEEEEEEEOOOOOOOOOOOOOOOO HUONIIIIIIIII AIBUUUUUUUUU
UNAAIBISHAAAAAAAAA WAHAYAAAAAAAAA WENZAKO AFADHALI HATA UNGEKUWA DEMU TUNGEJUA ASILIAAAAAAAAAAA INASUMBUAAAAAAAAA NA SI SHIDA YA HELAAAAAAAAAA HATA WEWE SEMEEEEEJIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII
HAYA
 
Mengi ametoa ujumbe kwa waandishi wa habari kuwa mwandishi yeyote aliyepokea hela ni masaliti kwa Taifa na alaaniwe. Tunaweza kumjadili mengi kwa mapungufu yake, lakini ukweli unabakia uamuzi aliouchukua ni wa busara sana na kwa kweli una umuhimu mkubwa kwa Taifa. Binafsi naungana naye waandishi waliokula pesa kuwasafisha wanarichmond walaaniwe na kulaanika.
 
Mengi ni mtu muhimu kama watu wakigundua hilo na kumpa support.Yeye pia ana nafasi ya kuwakosoa mafisadi bila woga wa kumwagiwa tindikali!Anajua everything..waandishi wanampa nyeti na anajua vitisho wananavyovipata pamoja na unyanyasaji na hali ngumu ya mzingira wanaofanya kazi huku wakikwamishwa na sheria mbovu ambazo haziwalindi!kwasababu ana empathy na knowledge ya kufahamu issue hizopamoja na namna ya kudeal na situation kama hiyo kwa manufaa ya wananchi walio wengi ambao unyonge wao hauwezi kuwasaidia pale wanapokumbana na mafisadi!Na kwamba uhuru kamili wa habari ndio silaha madhubuti ya myonge dhidi ya mafisadi!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom