George Smiley
JF-Expert Member
- Oct 24, 2011
- 471
- 266
Sitoandika mengi leo lakini kuna harufu ya ufisadi wa kutisha kuhusu hii meli ya MV LIEMBA ambayo serikali ya Ujerumani walikuwa tayari kutoa pesa ili itengenezwe ili iendelee kutoa huduma kwa wananchi kwenye ziwa Tanganyika.
Meli hii ambayo historia yake mnaweza kuipata hapa:
MV Liemba - Wikipedia, the free encyclopedia
cha ajabu mbunge wa Kigoma bwana Zitto Kabwe ambaye sasa yuko huko Ujerumani naye amekuwa kimya kuhusu hatma ya hii meli ambayo ni kiungo maalim kwenye jimbo lake na pia tusisahau kuwa ofisi ya waziri Mwakyembe nayo imekataa huu msaada wa BURE toka serikali ya Ujerumani.
Habari za uhakika ni kuwa Ofisi ya waziri Mwakyembe wanataka wapewe chochote ili kupata huu msaada toka kwa serikali ya Ujerumani, na kimya cha Zitto nacho kinaonyesha kuwa haoni kama huuu usafiri una manufaa kwa nanachi wa Jimbo lake.
Lakini pia inaelekea kuwa huku kununa kwa serikali yetu kuna weza kukawa kuko linked kwa namna moja au nyingine na ile issue ya Serengeti (lakini hili hapa si mahala pake) ila ukweli usiopingika kuwa kuna hata TTB wako bize ku promote maeneo ya ziwa Tanganyika na hasa ukizingatia tayari upo usafiri wa anga kati ya Kigoma na Sumbawanga, na hii meli ingetengenezwa ingekuza uchumi wa visiwa na maeneo mengine yaliopo kwenye hili ziwa.
Taarifa zinasema kuwa tayari serikali ya Kenya na Kenya Tourist Board tayari washa lobby kuwa hizo pesa zipelekwe kwao kama Tanzania hatuzitaki ili ziwasaidie kwenye maeneo mengine ya utalii.