UFISADI wa ZADOCK na ofisi ya Meya KIMBISA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UFISADI wa ZADOCK na ofisi ya Meya KIMBISA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Game Theory, Feb 28, 2009.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Ndio nimerudi tena nanajua kuna wengine mtasema ohhh GT umeshikwa na nini lakini ukweli ni kuwa:

  Usalama wa taifa umekaa kimya huku ZADOCK akifanya uhuni mji hapa Dar. Kuna taarifa kuwa huyu jamaa single handedly ameingia contract na Meya wa mji eti anaweza taa za bara barani kwa sharti ataweza mabango yake kwenye hizo nfuzo za taa....ukweli ni kuwa:

  NGUZO anazo weka Zadock zinaonekana ni cheap quality na ni kwa ajili ya residental area badala ya bara barani

  NGUZO ni nyembamba mno hata zikigongwa na piki piki sinapinda kirahisi

  NGUZO taa zake ni hafifu sana na hazimuliki vizuri bara barani kwa sababu ni taa kama alizoweka MBOWE nje pale Bilicanas

  Naaamini kuwa standards na guidelines hazikufuatwa ndio maana tumejaziwa taaa zenye cheap quality mji mzima...halafu tangu lini mtu binafasi akapewa authority ya kufanya kazi za jiji namna ile? maana leo tunaweza kuona ni sawa je kesho mtu binafsi akija kuambiwa aweke taa na nguzo kwenye ofisi mpya za USALAMA WA TAIFA itakuwaje? naamini watampa tuuu.

  Kwa nini jiji wasiweke taa kama zilizowekwa na WACHINA kuleee bara bara ya SAMNUNJOMA tokea MWENGE ? zile NGUZO zinaonekana ni strong na taa zake ni powerful na naamini zinatumia solar badala ya kumpa huyu fisadi ZADOCK ambaye anafanya uhuni na kutujazia taka left and right
   
 2. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #2
  Feb 28, 2009
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,701
  Trophy Points: 280
  Inabidi nikutafute baadae kidogo jioni.

  Umerejea ukiwa full naona. Welcome back mate. Mwite Masatu mkuu, tunamwitaji sana hapa
   
 3. S

  SkillsForever Member

  #3
  Feb 28, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nami naunga mkono huu ni uhuni kabisa zile sio taa za barabara kubwa jamani...hazina nguvu na hy alminium inachekesha zile zafaa kwenye fensi ya nyumba za watu campus na etc si barabarani.
   
 4. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  unajua ukienda kule Mwenge ile bara bara ya SAM NUNJOMA usiku utafikiri uko SHANGHAI kwa jinsi ilivyopendeza taa zote zina waka kasoro kipande cha Milimani City -Mwenge ...halafu ukitazama taa za anazoweka FISADI Zadock huku bara bara ya Airport-Bibi titi ushavu na vichekesho vitupu

  I mean its a disgrace...hapo bado sijaongelea lile MTARO mbele ya HAIDERY PLAZA na yale maji machafu kwenye mtaro wa Petrol station ya posta mpya
   
 5. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #5
  Feb 28, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Gt haya makampuni ya matangazo yanapewa sana tenda za ajabu ajabu bila kuangalia watu wake wakoje mfano kampuni ya brooklyn nao nasikia wanataka kuanza kuweka mabango wanachukuwa pesa za watu na matangazo hawaweki mwenye kampuni ya brooklyn ni mfanyakazi wa oryx na mume wa dada wa miss tz wa zamani pamoja na buzines dev manager wa kampuni hiyo anayefanyakazi tbl wote upande wa pili ndio wanatumia hiyo brooklyn kuendesha michezo michafu

  hivi unamjua sarah na obrian watoto wa huyo zodiak wakowapi siku hizi
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Feb 28, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Welll, well, well... Thats a good one GT;

  Yes they may be substandard, but even those sub-standards were not there a few months ago na jiji limeshindwa hata ku-repair za zamani. My big questions is "do we have to remove them or reject them rather?" au tukubali nusu shari at least ma-bar maids wetu wasibakwe ? na wasafiri wa usiku waweze kubadilisha tyres na kuongeza maji kwenye rejeta zao?

  YEs, ni sub-standard... lets propose alternative na tufanye upembuzi wa gharama halisi kisha tuziweke;

  Tanzanians never stop to amaze themselves, Tiles na vifaa vingi vya ujenzi nyumbani from china substandard, magari - used, ndege - used, treni - used, meli/vivuko - used, majumba - substandard, lami barabarani - substandard...Duh

  GT nice try buddy!! ...connecting the dots, hasa nikikumbuka ulimuulizia Nambua, sasa na hili la kimbisa, then Zaddock probably we'll end to one small guy in Dar [thats where you are heading!!]

  Regards to Zabein
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Mar 1, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  GT;

  YOu have been quiet on this one and as a tanzanian i would like to learn more... mbona kimya ndugu.... salamu zilifika?
   
 8. Mama Subi

  Mama Subi Member

  #8
  Mar 2, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 88
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 15
  Hivi maana ya "Fisadi" ni nini hasa?
   
 9. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mkuu GT,

  Hiyo tenda ya kusambaza taa ilitangazwa? TBS wamepitisha ubora wa hizo nguzo na taa zenyewe? au ndo mambo ya dumping kwenye shamba la bibi?
   
 10. O

  Ogah JF-Expert Member

  #10
  Mar 2, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  ....That is what we call "value for our money....oopps......value of our brains rather"............
   
 11. Zalendohalisi

  Zalendohalisi Senior Member

  #11
  Mar 2, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Value for our greed ...

  ZalendoHalisi
   
 12. K

  Kaka Mdogo Member

  #12
  Mar 2, 2009
  Joined: Aug 4, 2008
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwenye issue ya quality inawezekana ni kweli kwamba quality siyo nzuri sana na labda Halmashauri hazikuliangalia vizuri suala hilo kwenye mikataba yao. Issue ya kwanini kapewa zadock tofauti na mtoa hoja labda kama ana sababu zingine za kibinafsi mie sioni kama ni tatizo. Na hakupewa na Jiji na meya kimbisa, mpango wa kuweka taa za barabarani ni mpango wa halmashauri husika i.e. kinondoni, ilala, temeke, mwanza, tanga, arusha nk. Na pote huko zadock (kwa sababu tumeamua kumtaja yeye kwa jina lakini ukweli halisi ni kampuni ambaye yeye ana hisa A1 outdoor) ndio wana mkataba wa kuweka Taa za barabarani na halmashauri. Kwanini mtu binafsi?? Kuna kitu kinaitwa PPPA (Public Private Partnership Agreement). Mtu kama una idea yako na una uwezo wa kifedha basi unaifuata serikali au halmashauri husika na kukaa mezani na kukubaliana. Sababu ni kwamba halmashauri hazina uwezo mkubwa na zingine vyanzo vya mapato ni kidogo na wakati huo huo matumizi ni makubwa kuliko mapato. Kwahiyo A1 kupewa mkataba wa kuweka taa, sijui nani kapewa wa kuweka mapipa ya taka, kuna mwingine ana vibanda vya kusubiria dala dala etc ni bomba tu kwa sababu mji unabadilika. Ila suala la quality nakuunga mkono sana kwa sababu nafikiri hawakukubaliana quality gani na nani atathibitisha hiyo quality kabla ya taa kufungwa. Lakini vilevile nachelea kuamini kwamba quality ilikubalika lakini mtumishi wa halmashauri naye hashindwi kuvuta chake na kuruhusu nguzo mbovu kufungwa
   
 13. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #13
  Mar 2, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Hivi wewe bwana mdogo una matatizo gani? GT kaleta suala la Zadoc na tender za ajabu ajabu na jiji wewe unaanza kutuchanganya na taarifa zako za udaku, kwa nini huwa unapenda kufuatilia maisha ya watu?wewe kazi yako nini haswa na unaifanya kwa maslahi ya nani? kama hauna cha kuchangia si bora ubaki msomaji.
   
 14. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #14
  Mar 2, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145

  BABA NIMEKUSOMA!ni lazima tufanye maamuzi hapa ili hili swala lisiwe REPITITIVE!either WE REJECT THEM?or WE REMOVE THEM.

  T.B.S na wataalamu wao WANAABUSE PROFFESSION YAO!
   
 15. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #15
  Mar 2, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Burn,achana naye huyo dogo,ndivyo alivyo,ana matatizo huyo
   
 16. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #16
  Mar 2, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu jaribu kuwa mstaraabu kidogo....
  Kisha soma sheria za jamii forums naona wewe ni member mpya hapa jamvini na nachelewa kusema sheria za hapa jamvini huzijui kabisa.
   
 17. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #17
  Mar 2, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Nimekusoma mkuu,hilo la ugeni dont be so sure labda ni ugeni kwa jina hili.Ila sometimes watu wengine wanaboa saana hata uvumilivu na kanuni vinapita kushoto.Hebu fikiria watu wanaongelea issue tete kama hii, halafu mtu anauliza watoto wa zadok wapo wapi tena anawataja majina kabisa kabisa, hiyo inafaida gani katika mjadala huu? GT anapoongelea ubovu wa taa zinazowekwa barabarani anaongelea maisha ya watanzania yanayoweza kupotea kutokana na viwango duni vya taa hizi. Hivi unafikiri hili ni jambo la kuletea mzaa au ni mahala pa mtu kuingiza chuki zake. Mkuu fidel sheria zimewekwa na watu ili ziwatumikie watu inapofikia mahala tunalea uvundo kisa sheria tutakuwa hatuzitendei haki hata hizo sheria zenyewe.
   
 18. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #18
  Mar 2, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  kuna mtu kaongelea TBS hii ni kweli kabisa niliwasahau hawa

  Hivi kwa nini tuandikie mate wakati wino upo?

  Nendeni Sam Nunjoma road mtazame taa ziliziwekwa kule na wachina na nashauri jaribuni kupita Usiku mtazame :

  QUALITY YA MLINGOTI

  QUALITY YA TAA ZENYEWE

  MTAONA KUNA CLEAR ROAD SIGNS

  bila kusahau kuwa hakuna UCHAFU wa matangazo kama yaliyojazwa na ZADOCK et al kwenye barabara zingine

  then fananisheni milingoti ya iliyowekwa kule HAILE SELAISE road au milingoti ya Zadock na wenzie bara bara ya kutoka AIRPORT kuja mpaka ALI HASSAN MWINYI ...Freeman Mbowe naye naona kaweka milingonti pale nje ya BILICANAS lakini ukweli ni kuwa ile ni public area na ile milingoti haifai kwa sababu ni yta residental area...anaweza kutuambia kuwa katufanyai service lakini ukweli ni kuwa kuna tatizo la standards ndio maaana ugomvi wangu umerudi kwa MENYA KIMBISA na GENGE LAKE LA MAFISADI

  Kuhusu PPP sikatai lakini uwepo utaratibu na iwepo PUBLIC CONSULTATION kabla ya kubwaga mabango left and right mpaka residental areas as if kila mzazi anataka mwanawe akiamka asubuhi kwenda shule bango la kwanza analokutana nalo ni la matangazo ya ulevi

  Pili hata hizo PPP zenyewe lazima USALAMA wa taifa wazipitie ili kuwa na uhakika kuwa ni katika PUBLIC INTEREST na hautaki 10 yrs down the line walipa kodi walazimishwe kutoa pesa za kurekebisha taa zilizo kuwa substandard
   
 19. K

  Kolo New Member

  #19
  Mar 2, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  I know Zadoc to be a man of very good quality products. How can anything related to him be of such poor quality. Na hao inspectors na ma engineers wa City, how could they accept such poor quality product. It really leaves one guessing there could be a hand of Ufisadi somewhere. Hey Tanzania, we are past this now tuendelee tuache ubinafsi so obvious
   
 20. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #20
  Mar 2, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hivi watanzania naomba niulize; kuna kitu kilichonunuliwa ambacho hakina ufisadi?

  Hapa cha kuzungumzia ni ubora wa hizo taa maana kuna mengi hatuyajui kuhusu makubaliano ya halmashauri husika na A1 outdoor, maana taa zipo hata airport, za mwanza wamejenga madogo wengine na si zaddok na zenyewe ni mafafa, \baadhi ya maeneo ya dar si za kwake

  Halafu naona GT kaona hii ya taa imekaa kivile naona sasa amehamia mabango ya haile selasie na mbowe.... taratibu tutakukuta kwa barafaa unapiga mbinja

  Wallah wakutumwa hana haya
   
Loading...