Ufisadi wa Waziri Wassira akiwa Wizara ya Kilimo

MVUA GAMBA

Senior Member
Apr 13, 2011
102
63
Wana Jf
Leo nilikua Wizara ya Kilimo na Chakula Idara ya Uhasibu katika mambo ya ambayo nimesikitika ni uzembe na Ufisadi wa waziri huyu akiwa katika serekali ya Awamu ya Nne .

Wazira wasira akiwa waziri Mwaka jana mwezi 4 alitakiwa kwenda mwanza kufungua kikao cha BODI ya Pamba jamaa akakatiwa Tiketi ya Ndege Precision jamaa akalala akapitiliza matokeo yake wizara ikabidi Imkodishie Ndege ndogo wizara ikaamua kumkodishia Single engine small flight akagoma wizara ilikua ilipe Dola 8000 kwa safari hiyo kwa aina hiyo ya Ndege.

Waziri akalazimisha akodishiwe Ndege ndogo yenye Engine mbili kwa Gharama ya Dola 13,000 hii ni fedha za walipa Kodi pia Waiting Charge na Gharama za kurudi. Ambazo kwa ujumla wizara ililipa Jumla ya Dola 19,870.

Tukio la Pili ni Ufisadi wa Ununuzi wa Gari ya wizara. Mwaka Jana (2010) mwezi Juni alinunuliwa Gari VX V8 ambayo ilikuwa haina Friji ndani kwa Gharama ya Milioni 250 akalikataa akataka zuri zaidi lenye madoido akataka la Thamani ya milioni 350 likaletwa mwezi September ambalo alilitumia kwa miezi 2 kabla ya uchaguzi.

Tukio la Tatu ni Kuibeba Kampuni inayoitwa SIMON GROUP kampuni hii ilipewa Miradi yote ya Kusambaza na Kuchukua Vyakula kutoka SGR za serekali bila kutangaza Tenda, Miradi hii Mwaka Jana Peke yake walipewa Miradi Ifuatayo. SONGEA 23.5bn, Iringa 19.2bn, Rukwa 39.5bn lakini pia ikumbukwe kampuni hii ndio iliyopewa kinyemela UDA kwa bei ya KUTUPA, kampuni hii ndio iliyonunua NYUMBA ya Familia ya MARIALE kwa 1bn masaki kampuni hii ilipewa Mradi mkubwa wa kuingiza Matrekta ambayo halmashauri zimelazimishwa kununua Matreka ya aina ya POWER TILER ambayo hayana uwezo wa kufanya kazi na mengi yamekwama. TUJIULIZE SIMON GROUP NANI YUPO NYUMA YA HII KAMPUNI?

Wana JF nimeleta uchafuu huu tuujadili na tuangalie huy wasira ambae anafanya kazi kwa karibu na MKULU.
 
mjomba hiyo familia ya marealle naifahamu walikuwa wafugaji wazuri sana wa kuku lakini ishu yao inaingiaje na huyu mzee labda ungefafanua kidgo hapo maana nimeshindwa ku connect swala la kuuzwa kwa nyumba na ufisadi wa wasira.????
 
Wana Jf
Leo nilikua Wizara ya Kilimo na Chakula Idara ya Uhasibu katika mambo ya ambayo nimesikitika ni uzembe na Ufisadi wa waziri huyu akiwa katika serekali ya Awamu ya Nne .

Wazira wasira akiwa waziri Mwaka jana mwezi 4 alitakiwa kwenda mwanza kufungua kikao cha BODI ya Pamba jamaa akakatiwa Tiketi ya Ndege Precision jamaa akalala akapitiliza matokeo yake wizara ikabidi Imkodishie Ndege ndogo wizara ikaamua kumkodishia Single engine small flight akagoma wizara ilikua ilipe Dola 8000 kwa safari hiyo kwa aina hiyo ya Ndege.

Waziri akalazimisha akodishiwe Ndege ndogo yenye Engine mbili kwa Gharama ya Dola 13,000 hii ni fedha za walipa Kodi pia Waiting Charge na Gharama za kurudi. Ambazo kwa ujumla wizara ililipa Jumla ya Dola 19,870.

Tukio la Pili ni Ufisadi wa Ununuzi wa Gari ya wizara. Mwaka Jana (2010) mwezi Juni alinunuliwa Gari VX V8 ambayo ilikuwa haina Friji ndani kwa Gharama ya Milioni 250 akalikataa akataka zuri zaidi lenye madoido akataka la Thamani ya milioni 350 likaletwa mwezi September ambalo alilitumia kwa miezi 2 kabla ya uchaguzi.

Tukio la Tatu ni Kuibeba Kampuni inayoitwa SIMON GROUP kampuni hii ilipewa Miradi yote ya Kusambaza na Kuchukua Vyakula kutoka SGR za serekali bila kutangaza Tenda, Miradi hii Mwaka Jana Peke yake walipewa Miradi Ifuatayo. SONGEA 23.5bn, Iringa 19.2bn, Rukwa 39.5bn lakini pia ikumbukwe kampuni hii ndio iliyopewa kinyemela UDA kwa bei ya KUTUPA, kampuni hii ndio iliyonunua NYUMBA ya Familia ya MARIALE kwa 1bn masaki kampuni hii ilipewa Mradi mkubwa wa kuingiza Matrekta ambayo halmashauri zimelazimishwa kununua Matreka ya aina ya POWER TILER ambayo hayana uwezo wa kufanya kazi na mengi yamekwama. TUJIULIZE SIMON GROUP NANI YUPO NYUMA YA HII KAMPUNI?

Wana JF nimeleta uchafuu huu tuujadili na tuangalie huy wasira ambae anafanya kazi kwa karibu na MKULU.
"Zamadamu" anakula kama mchwa. Ana digestive system ya herbivores" akipanua mdomo jengo la kitega uchumi linazama kinywani Hayo ni magamba bana. Chama cha majambazi at work. Sasa kweli uweke huyu na jangili aliyepewa utendaji wa chama tutabaki kweli! Tuamke jamani! Mwe!!!
 
Kuna ghorofa alilijenga maeneo ya Njiro Msola kwa miezi miwili sasa hivi liko sokoni anayetaka kununua au kupangisha amuone Tyson.
 
Yani ugonjwa wa malale anaougua mzee huyu unalipa taifa hasara ya dollar 19,870?

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Nasikia huyu mzee ni mkorofi sana, yeye na ngumi mkononi ukimkatalia anachotaka kufanya hachelewi kukushambulia' jamaa walio karibu naye wanasema ni mbabe kupita kiasi. Je ni kweli?
 
nasikia huyu mzee ni mkorofi sana, yeye na ngumi mkononi ukimkatalia anachotaka kufanya hachelewi kukushambulia' jamaa walio karibu naye wanasema ni mbabe kupita kiasi. Je ni kweli?

Nchi inahitaji mtu wa hivyo kunyosha mambo
 
Mimi huyu jamaa nikisikia habari zake hasira zinanipanda!!!!!!!!!!!!! Eti huyu naye yuko kwenye list watakaogombea kwa tiketi ya ccm nae anaitwa potential/mtaji kwa ccm,hivi hii nchi imelaaaniwa??kwa sababu yasiyoweza kutokea duniani kote yanatokea tanzania,waziri mwingine wa elimu hajui hata historia ya nchi yake philipo mulugo 'tanzania ni muunganiko wa visiwa vya pemba na zimbabwe' huyu ni waziri wa elimu na alishawahi kuwa mwalimu wa somo la historia hakika msiba mkubwa kwa taifa.
 
Wanasiasa wa Tanzania hasa wa ccm wanajua kuwa kumbukumbu za Watanzania ni fupi. Anaweza kufanya ufisadi leo, baada ya siku chache akakuambia yeye ni msafi na si fisadi. Nakumbuka wakati wa campaign ya uraisi ccm walituhumiwa kutumia vibaya ndege ya serikali ambapo mke wa raisi aliitumia kufania campaign. Alitokea Kinana na risiti iliyogushiwa akaiambia umma kuwa walikodisha ndege hiyo. Pamoja na yote hayo na mengine mengi, leo tumatangaziwa kuwa yu muadilifu,,,wapi na wapi!
 
Back
Top Bottom