UFISADI wa waandishi wa HABARI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UFISADI wa waandishi wa HABARI

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tina, Sep 25, 2009.

 1. Tina

  Tina JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2009
  Joined: Jul 9, 2007
  Messages: 571
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  NIKIWA HAPA DAR nakutana na Habari ya UONGO katika Gazeti la ALASIRI.

  Nililibahatika kuwa Moshi mkoani Kilimanjaro na kwa bahati mbaya sana hakuna aliyejua kama mimi ni mwana JF ambaye ninafahamu mambo mengi ya nchi hii na kwa urembo wangu ndio kabisaa nilipokuwa katika hoteli moja pale mjini Moshi kabla ya kwenda Arusha, nimeshuhudia mambo ya aibu kwa waandishi wetu wa habari wa Tanzania ila sikuwa nikiamini kinachojadiliwa kabla ya kuthibitisha katika habari hii hapa chini. Kwa muhtasari hii habari ya Alasiri ya leo ni ya uzushi na kupandikizwa kwa malengo ya kisiasa na aliyekuwa akifadhili mkakati huu ni mmoja wa watu anayewania kuingia katika siasa katika jimbo la Moshi Vijijini. Mtu huyo ndiye aliyehusika pia katika ugawaji wa kadi bandia zenye malengo ya kuwang'oa wanasiasa kadhaa mkoani Kilimanjaro akiwamo Dk. Chami na Aloyce Kimaro.

  Jambo la kusikitisha ni jinsi waandishi wa habari kabla hata ya 2010 wanavyokubali kutunga habari kama hii. Kwanza Chami hakuwapo msibani. Pili fedha za rambirambi zilienda kufuatwa na mwandishi mmoja katika hoteli moja ya mjini Moshi na huyo mwandishi ndiye aliyekuwa akimsema vibaya Marehemu Ali Sonda (Mungu aiweke roho yake pepoeni) na kuwasema pia waandishi wenzake wa Moshi mbele ya Dk. Chami na alichofanya Chami ni kukiri baadhi ya mambo yanayomhusu kama vile marehemu kuandika habari nyingi mbaya bila kuwa na ushahidi nazo. Hii ni hatari sana na wahusika wa IPP Media na vyombo vingine waangalie, kabla vyombo vyao havijachafuliwa na UFISADI.

  Jambo la kujiuliza ni kwanini mwandishi afuate mchango kwa Dk, Chami hotelini na akae kuanzia saa moja usiku hadi saa nne? Kwanini waandishi badala ya kuchanga wao waende kwa wanasiasa na wagombea wapya? Kwanini waandishi waingilie matatizo ya kifamilia nyumbani kwa marehemu Sonda kwa kuanza kuingilia hadi ugawaji wa mali za marehemu? huu ni UFISADI mwingine katika media UMULIKWE.

  HABARI HUSIKA HII HAPA.
  ..

  Waziri akwaa kashfa msibani

  Na Jackson Kimambo
  25th September 2009


  Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Bw. Cyril Chami, amekwaa kashfa nzito baada ya kudaiwa kumsimanga marehemu kwenye msiba mmoja na hivyo wafiwa kudaiwa kumrejeshea pesa zake zote alizotoa kama rambirambi ya mpendwa wao.

  Tukio hilo, limetokana na msiba wa mwandishi wa habari, Ali Sonda (47) wa gazeti la Mwananchi mjini hapa, ambaye alifariki dunia Septemba 14 mwaka huu.

  Inadaiwa kuwa Naibu Waziri Chami, alitoa pesa za rambirambi kiasi cha shilingi 50,000 kwa mazishi ya mwandishi huyo aliyefia katika Hospitali ya KCMC mjini Moshi, huku pia akitoa maneno ya masimango yaliyowakera waandishi wenzie wa habari na mwishowe kuamua kumrejeshea pesa zake kwa njia ya simu ya mkononi.

  Inadaiwa kuwa Chami alisema anatoa pesa kwa marehemu Sonda basi tu, kwani enzi za uhai wake alikuwa akimchafua sana, kauli ambayo iliwafanya waandishi ambao ni sehemu ya wafiwa kuamua kumrejeshea rambirambi yake, kwani walidai kuwa Sonda (marehemu) ametuhumiwa na Naibu Waziri Chami ilhali ikijulikana fika kuwa hawezi kufufuka na kujitetea.

  Uamuzi wa kususia rambirambi ya Chami kutokana na msiba wa marehemu Sonda, umetolewa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Kilimanjaro, ikiwa ni baada ya Kamati ya mazishi kutamka kwenye majumuisho yaliyofanyika hoteli ya Kilimanjaro Cren kuwa haikuridhishwa na kauli alizotoa Chami ambaye pia ni Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), wakati akitoa rambirambi yake kwa marehemu (Sonda).

  Kaimu Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Lini Kamafa, alisema wao na kamati hiyo ya mazishi haikufurahishwa na kauli za Chami wakati akitoa rambirambi yake kuhusiana na kifo cha mwenzao, hivyo wanasusia rambirambi hiyo kwa kumrejeshea fedha yake yote.

  Kamafa akasema hawakufurahishwa na kauli iliyotolewa na Naibu Waziri huyo kuhusu uhusiano wake na Sonda wakati wa uhai wake na waandishi wengine wa habari mkoani Kilimanjaro kwa jumla.

  Akadai kuwa pamoja na mambo mengine, Mbunge huyo (Chami), anadaiwa kumtupia lawama marehemu huyo kwa kile alichodai kuwa alikuwa akimwandika vibaya katika magazeti.

  "Kwanza namchangia Sonda basi tu .... kwani alikuwa akinichafua... na nimeshawasaidia sana waandishi... nakutuma nenda kawaambie na ujumbe umefika, ” mmoja wa waandishi hao akasema kwa kukariri maneno ya Chami.

  Kamafa akasema wamelazimika kurejesha Sh. 50,000 na kwamba kama Chami ataona hajatendewa haki, anayo nafasi ya kuomba kukutana na waandishi hao ili kuelezea malalamiko yao.

  “Kwanza Sh 50,000 tayari tumeshazirejesha kwake kwa kutumia simu yake ya mkononi... huko alipo tayari zitakuwa zimeshamfikia, ” akasema Kamafa na kushangiliwa na waandishi wenzie wa mkoani Kilimanjaro.

  Sonda ambaye alikuwa miongoni wa waandishi wa Mwananchi Mkoa wa Kilimanjaro, alizaliwa mwaka 1962 na kufariki dunia baada ya kuugua kifua kwa muda mrefu na kuzikwa nyumbani kwao katika Kijiji cha Chekereni.

  Alasiri ilipomsaka Chami kwa njia ya simu leo asubuhi ili kuweza kupata maelezo yake, haikuweza kufanikiwa kwani simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita hadi kukatika bila kupokelewa.

  CHANZO: ALASIRI
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kama umesoma magazeti ya leo utagundua kuwa waandishi wa habari most of them ndo wanakuwa ma`campaign manager wa wagombea.

  Off records/thread... kumbe ulikuja Arusha tusitafutane mamii? ... Vibaya hivyo... Si unajua Niko Single.
   
 3. Tina

  Tina JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2009
  Joined: Jul 9, 2007
  Messages: 571
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  Kabla ya kurudi majuu, nitalazimika kupita tena Moshi nijionee mwenyewe huu uchafu. Watanzania tujipe pole maana tuna safari ndefu sana. Kwa bahati mbaya sana mhusika ni mwanamke mwenzangu. Na sasa hivi nimejulishwa kwamba ameendelea kuwasiliana na Chami huku akihamisha maneno kutoka upande mmoja kwenda mwingine. Na alichofanya kibaya zaidi anawadanganya waandishi wenzake kwamba Chami amewakashifu tena na hataki kabisa kuwaona wala kuwasiliana nao. Huu ni utoto, hakuna mwanasiasa na hata mfanyabiashara ama mtu wa kawaida tu labda mwenye akili punguani anayeweza kufanya hayo.
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,854
  Likes Received: 83,312
  Trophy Points: 280
  Mkuu PJ acha hizo!...LOL! Hebu punguza speed zako.
   
 5. Tina

  Tina JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2009
  Joined: Jul 9, 2007
  Messages: 571
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  Nilipita na boyfriend wangu ametaka kujua Tanzania, ilibidi nimtembeze kwenye vivutio vyetu vya utalii. Nikiwa hapo Moshi ndio vijana wale wakajua na mimi ni mgeni sisikii wanayoongea na kupanga, nusu nipasuke kwa hasira.
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Sep 25, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  MHESHIMIWA BAK...
  Si umeona mwenyewe mdada mwenyewe alivyotuambia kwamba yuko mrembo saaana!
  Na mimi nime`prove kwako kwamba niko single... mambo ndo kama hivyo...najaribujaribu!
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Sep 25, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Heeeee....!

  Nimekoma mie mwaya!

  Vinginevyo karibu sana Arusha, wanaJF tuko tele hapa ujisikie home. Kama kuna mahali unakwama as far as Safaris and Game -dRIVING, CAMPING AND THINGS OF THE KIND, BASI TUWASILIANE...!

  kARIBU SANA Geneva of africa
   
 8. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #8
  Sep 25, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Tina,

  Uliloandika lina ukweli 100%, hata mimi nimehakikisha waandishi wa IPPMEDIA wanapika habari. Huenda na waandishi wa magazeti mengine wanafanya hivyo hivyo ila nina uhakika na hao Nipashe.

  Habari zao nyingi wanazoziandika kuhusu Mbeya ni za kupikwa. Kwa kiasi fulani, wao wamesaidia kukuza mgogoro wa uongozi mkoani Mbeya kwa kuandika habari za uchonganishi.

  Inasikitisha sana kuona vyombo vya habari vimefikia mahali hapo. Wengi wanalipwa kwanza kabla ya kuandika habari. Kuna mifano mingine ambayo mimi naijua ambapo habari huandikwa na mwanasiasa na kisha mwandishi wa habari kuweka jina lake kabla ya kuituma.
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Sep 25, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,854
  Likes Received: 83,312
  Trophy Points: 280
  Ni ukweli kwamba kuna waandishi wa habari wengine ambao ni wahuni tu na kuwaharibia wenzao ambao wanafuata maadili ya fani yao, lakini pia katika vita dhidi ya ufisadi Waandishi wa habari wamesaidia sana kuyajua mengi ambayo kamwe Watanzania tusingeyajua.

  Katika ufisadi uliofanywa na Mkapa, wa EPA, katika ufisadi wa ujenzi wa Twin Towers, ufisadi wa Richmond/Dowans, Barrick, Rites, TICTS n.k. Hivyo katika kundi la waandishi wa habari wengi ambao wamesimama kidete katika kufichua ufisadi wa kutisha dhidi ya nchi yetu, hawakosi wachache ambao ni wahuni tu na wanataka kutumia nafasi zao ili kujinufaisha.
   
 10. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #10
  Sep 25, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180

  BAK You are very right.

  Na katika taaluma yoyote, hapakosekani

  wanataaluma-uchwara. Hujaona huko Kariakoo Maghorofa

  yakiporomoka?

  Fani zimevamiwa ...Fungueni macho.
   
 11. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #11
  Sep 25, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sijaipata hii imekaaje maana sielewi kabisa kuhusu haya mambo au ndio Kampeni ndio zimeanza tayari
   
 12. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #12
  Sep 25, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kaka umenena. Katika kila fani kuna matatizo, lakini uandishi ni fani nyeti sana sawa na udaktari. MWandishi, daktari, polisi na usalama wa taifa wakifanya ufisadi ni HATARI SANA kwa mustakabali wa Taifa letu. TUPAMBANE KUKABILIANA NA MAMBO HAYO.
   
 13. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #13
  Sep 25, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Chondechonde waandishi wa habari msiidhalilishe fani yenu kwa uroho wa utajiri.
   
 14. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #14
  Sep 26, 2009
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,274
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Wewe uko upande gani???????????????????????
   
 15. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #15
  Sep 26, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Tina,

  Alasiri ni GAZETI LA UDAKU, kwa hiyo huandika habari zake ki-udaku-udaku. Wewe ulidhani hawa ni MAINSTREAM MEDIA? Mengi asitudanganye. Nilishawashtukia hawa watu muda mrefu sana, ndio maana sina imani na gazeti hata moja la Mengi! Hata moja!

  Sishangai wao kuandika namna hiyo. Chami akiamua kuwapeleka mahakamani atashinda kesi, na wao wanajua. Ila hana muda nao. Kwanza kwa kumchafua ndio wanamjenga!

  ./Mwana wa Haki
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #16
  Sep 7, 2013
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,611
  Trophy Points: 280
  Yote usemayo hapa ni kweli ila tanguliza neno "baadhi!"
  1. Ni kweli kuna "baadhi" ya waandishi wanapika habari ila sii wote!.
  2. Wengi wanalipwa kwanza kabla ya kuandika habari ila sio wote!. Wako wengine wanaandika kwa kujitolea tuu na hawalipwi chochote na yeyote!. Wako wanaondaika kwa kuajiriwa na wanategemea mishahara yao halali tuu, ila pia nakiri "petty cash journalist pia wapo!".
  3. Hili la "habari huandikwa na mwanasiasa na kisha mwandishi wa habari kuweka jina lake"-hii kali!.
  Pasco wa jf ni mwandishi wa kujitegemea kwa kujitolea!.
   
Loading...