Ufisadi wa ugawaji viwanja halmashauri ya Arusha - Burka Estate | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi wa ugawaji viwanja halmashauri ya Arusha - Burka Estate

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Makindi N, Nov 4, 2010.

 1. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Jamani Burka Estate, lililokua shamba la Kahawa, limegawiwa. Sitaki kuhoji kama maamuzi ya kuligawa hilo shamba na kuwa ni makazi ni sahihi. Bali Halmashauri ya Mji wa Arusha, lilitangaza watu waombe ili wapewe viwanja. Form zilitolewa na Manispaa kwa TShs. 10,000/=. Zaidi ya watu elfu 30 waliomba hivyo viwanja ambao wengi wao ni wa kipato cha kati, cha chini na wasio na viwanja kama maelekezo yalivyohitaji. Majina yamebandikwa notice board ya Wilaya ya Arusha, haya ni majina ya baadhi ya vigogo waliopo katika list ya waliopata viwanja; Lowassa, Ridhiwani Kikwete, Karamagi, Nagu, Mwanri, Ruth Mollel, Ritha Mlaki, Ole Nangole, Warioba, Iddi Simba, Tarishi, Ole Medei etc.

  Pamoja na pesa nyingi zilizokusanywa kwa walalahoi kupitia application forms, majina yao yametupwa kapuni.

  MY TAKE
  1. This is a prime area, na wametangaza, walioomba wengi ni watu wa chini na wasio na viwanja inamaana vigezo vilikuwa ni majina makubwa? Kwanini hawakusema watu wa chini wasiombe?
  2. Vigezo gani vilitumika kugawa viwanja? Halmashauri inabidi itoe majibu
  3. Ukila na kipofu usimguse mkono, hawa wakulu wamefika mbali kutungÂ’aninia mkono kabisa
  4. Hivi ni kweli hawa wakubwa hawana sehemu ya kuishi? Au ndo vile mwenye nacho ataongezewa?

  KWA OLE MEDEI (MBUNGE MTEULE) NA GODBLESS LEMA (MBUNGE MTEULE) NA FULL COUNCIL YA ARUSHA
  Ole Medei kama Mbunge mteule wa hilo jimbo na uliepata kiwanja, tupe majibu ya utaratibu uliotumika maana ni tofauti na uliotangazwa. Please NULLIFY this stupid decision at its worst.

  Kazi ya kwanza kwa Mheshimiwa Mbunge mteule (Godbless Lema) na ukweli kwamba CHADEMA ndio inaunda Full Council kufuatia kuwa na madiwani wengi, pitieni maamuzi kama haya hapo Arusha Mjini na mfanye maamuzi mapya ya busara.

  Wapenda Arusha na Tanzania yote, kwa mlio Arusha piteni hapo Halmashauri Arusha mjionee.
   
 2. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  safi sana kutujuza! Ubaya ni kwamba waliogawa viwanja hivyo ni Arusha D.C na si Arusha municipal council.kumbuka Arusha D.C bado iko chini ya chichiem (ole medeya bin edward lowassa) hivyo mambo yatakua magumu.
   
 3. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Na wamefanya hivyo kabla ya city council mpya haijaingia kazini. halafu unamwibia masikini elfu kumi na kiwanja humpi????
   
 4. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2010
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,544
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  kwani hao uliowataja sio watanzania ?? wao hawana haki ya kuvipata??? mbona vile vya gomba viligawiwa kwa watu alafu wakaviuza badala ya kuviendeleza ? acha hizo wewe . mimi ni mmoja wapo wa waliopata na ni mtu mdogo sana kwemye hii nchii.
   
 5. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #5
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  hakuna mtu mdogo pale,labda mfanyakazi ofisi ya ardhi ya wailaya.au wewe ni Dr.charles .c.KIMEI,Ufisadi haupingiki pale!milioni 11 kwa mfanyakazi wa kawaida anapata wapi?
   
 6. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #6
  Nov 5, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Ugly and vicious!!
   
 7. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #7
  Nov 6, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  kaka nakushukuru kwj post hii. mimi ni mmoga wa wahanga wa sakata hilo. baada ya kukaa foleni ndefu kwa muda wa saa kumi. hatmaye nilipata namba 1000+ kabla hajafika 1100 . nikajiuliza moyoni mwangu kuna viwanja vingapi?.jibu nililopata ni kwamba havizidi 300. maswali mengi yakaja kama ni 300 kwa nn wanaendelea kupokea fedha za watu ilhali viwanja ni vichache hakuna aliyekuwa na majibu.mpaka idadi ya waombaji ikafika elfu 30+ .wiki 2 zilizopita moja kati ya ndugu wa karibu wa diwani wa Kata ya Elelarei a
   
 8. K

  Kamongo JF-Expert Member

  #8
  Mar 25, 2011
  Joined: Mar 20, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  je viwanja bado vipo!nasikia ramani yake kama cape town
   
Loading...