Ufisadi wa tanesco kuwekwa hadharani wiki ijayo!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi wa tanesco kuwekwa hadharani wiki ijayo!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Oct 3, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,179
  Likes Received: 5,595
  Trophy Points: 280
  Sadick Mtulya

  RIPOTI ya uchunguzi wa ufisadi ndani ya Shirika la Umeme (Tanesco) inatarajiwa kuwekwa hadharani siku yoyote kuanzia wiki ijayo.


  "Baada ya kumalizika kwa mkutano wa 55 wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola, nitaweka hadharani matokeo ya ripoti ya uchuguzi wa tuhuma za ufisadi zilizoripotiwa ndani ya Tanesco," alisema jana Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja katika mahojiano na gazeti hili.


  Waziri huyo aliunda tume hiyo kuchunguza tuhuma hizo siku chache baada ya mbunge wa Sumve (CCM), Richard Ndassa kuibua tuhuma hizo za ufisadi bungeni ambazo zilimgusa moja kwa moja Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Dk Idris Rashid.


  Ndassa alidai bungeni kuwa shirika hilo liko katika harakati ya kuiuza nyumba namba 13 katika Mtaa wa Toure/Chaza, Oysterbay jijini Dar es salaam kwa Sh60 milioni baada ya kukarabati wa kwa Sh 600 milioni.


  Sambamba na ufisadi huo, mbunge huyo pia alilituhumu shirika hilo, kutumia Sh1.4 bilioni kukarabati nyumba sita za wakurugenzi wake kinyume na taratibu.


  Ndasa alitoa tuhuma hizo, wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini iliyowasilishwa katika mkutano wa 16 wa Bunge na Waziri Ngeleja.


  Kwa mujibu wa Ndassa, fedha hizo ambazo ni sehemu ya mkopo wa Sh280 bilioni zilizokopwa benki kwa ajili ya kuendeleza miradi ya maendeleo ya Tanesco, zilitumika bila idhini ya bodi ya wakurugenzi.


  "Tanesco kuna matatizo makubwa yanayotokana na usimamizi mbovu na matumizi mabaya ya fedha. Shirika halina vipaumbele; linatumia vibaya fedha za umma.


  "Mwaka 2007 shirika lilikopa Sh280 bilioni kutoka benki mbalimbali kwa ajili ya miradi ya maendeleo, lakini badala ya kutekeleza vipaumbele, limeamua kukarabati nyumba za wakubwa kwa Sh1.4 bilioni," alidai Ndasa.


  Jana Waziri Ngeleja ambaye yupo katika mkutano wa CPA, mjini Arusha aliliambia gazeti hili kuwa mara baada ya kumalizika mkutano huo, atakuwa katika hali nzuri ya kutangaza hadharani matokeo ya uchunguzi huo.


  Akinukuliwa na gazeti hili hivi karibuni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Kigoma Malima alisema Waziri Ngeleja ana wajibu wa kuitangaza au kutotaingaza ripoti hiyo.


  Malima alisema bodi ya Tanesco ndiyo iliyotakiwa kuchunguza ufisadi huo, hivyo baada ya kazi yao kukamilika waziri ana mamlaka ya kutoa taarifa juu ya ufisadi huo.


  "Niko katika mkutano wa CPA, lakini kuhusu ripoti hiyo, nikitoka hapa narejea Dar es Salaam na nitaitolea ufafanuzi hiyo ripoti," alisema Ngeleja.


  Siku moja baada ya Ndassa kutoa tuhuma hizo, Ngeleja aliliambia gazeti hili kuwa asingeacha tuhuma hizo zipite bila kuzifanyia kazi kwani tuhuma ni nzito.


  Ngeleja ambaye hakutaja idadi ya wajumbe wanaounda kamati hiyo, wala muda watakaotumia kukamilisha kazi, alisema uchunguzi huo usingetumia muda mrefu.


  Akihitimisha mjadala wa wizara yake ya Nishati na Madini, Waziri Ngeleja aliliambia Bunge kuwa tuhuma hizo ni changamoto kwake na kwamba anajipanga kuzishughulikia mara moja.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  huyo ngeleja mwenyewe ni fisadi.
   
 3. Jambazi

  Jambazi JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2017
  Joined: Jan 18, 2014
  Messages: 14,420
  Likes Received: 12,565
  Trophy Points: 280
  Thread haina wachangiaji kabisa...
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2017
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,269
  Likes Received: 22,029
  Trophy Points: 280
  Uleteni ubaoni huo ufisadi wa Tanesco tuuone na pia watakaotajwa wafikishwe mahakamani fasta kwa uhujumu uchumi
   
Loading...