Ufisadi wa Sh48 bilioni waitikisa nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi wa Sh48 bilioni waitikisa nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Saint Ivuga, May 16, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  May 16, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,465
  Likes Received: 19,847
  Trophy Points: 280
  Sunday, 15 May 2011
  Gazeti la Mwananchi


  [​IMG]

  Boniface Maana, Tunduru na Felix Mwagara

  UFISADI unaoonyesha kuwa zaidi ya Sh48 bilioni zimetafunwa na wajanja umeendelea kulitikisa taifa baada ya kampuni za kigeni kufungua kesi zikidai fidia ya Sh3 trilioni za fidia kutoka kwa wanunuzi wa pamba kwa kushindwa kutimiza masharti ya mkataba.Madai hayo mapya yanakuja wakati serikali ilitoa fedha katika utaratibu wa mpango wa kuhuisha uchumi (stimulus package) na Bunge lilipitisha bajeti ya dharura ya Sh1.7 trilioni.

  Akizungumza kutoka Mbinga jana, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Kabwe Zitto ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Fedha alisema kuwapo kwa kesi hiyo kunadhihirisha kwamba taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwamba kuna zaidi ya Sh48 bilioni ambazo ameshindwa kuzithibitisha kama zilitoka kwa taratibu zinazotakiwa ni sahihi.


  Kabwe alitoa kauli hiyo akirejea habari iliyotolewa jana na gazeti dada la Mwananchi, The Sunday Citizen kuwa sekta ya pamba nchini inaweza kuanguka baada ya wanunuzi wa nje kudai fidia ya dola 2 bilioni sawa na Sh3 trilioni kutokana na kuvunjwa kwa mkataba.


  Aprili 15 mwaka huu, Zitto aliibua madai hayo ya ufisadi huo wa zaidi ya Sh 48 bilioni alipombana Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, katika kipindi cha maswali na majibu bungeni. Alisema kwa mujibu wa taarifa ya CAG, fedha hizo zilipotea katika utaratibu wa mpango wa kuhuisha uchumi (stimulus package).


  Kutokana na ushuhuda huo, Kabwe aliitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) pamoja na CAG kufanya uchunguzi wa kina kwenye matumizi ya fedha za mpango wa kuhuisha uchumi."Tunataka majibu kabla ya kikao cha bajeti kwa sababu kama nilivyosema awali, hizi ni fedha nyingi," alisema Kabwe.


  Zitto alisema kwamba serikali ilimnyima taarifa muhimu ikiwamo orodha ya watu na kampuni ambazo zilifaidika na mpango huo wa matumizi ya Sh48 bilioni na kwamba kesi iliyofunguliwa sasa ni uthibitisho kwamba wafanyabiashara wa pamba walikuwa hawapaswi kufidiwa kwa sababu hawakupata hasara yoyote kama inavyodaiwa.


  Alisema kesi hiyo inaonyesha kwamba wafanyabiashara wanauza bidhaa zao katika masoko ambayo yana faida kubwa.Gazeti la Sunday Citizen, jana liliripoti kuwa wasindikaji na wauzaji waliingia mkataba wa kusafirisha tani 260,000 za pamba lakini walisafirisha tani 162,000 tu ikiwa ni sawa ni asilimia 62 ya kiasi walichokubaliana.


  Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania (TCB), Marco Mutunga alisema baadhi ya kampuni za kigeni zilifungua kesi kwa Liverpool Cotton Association (LCA) ambalo ni Shirikisho mama zikidai fidia kwa kushindwa kutimiziwa mkataba kama ilivyokubaliwa.


  Mutunga alisema kushindwa kwa wanunuzi hao wa pamba kutimiza masharti ya mkataba, kulisababishwa na sababu zilizo nje ya uwezo wa wasafirishaji pamba wa ndani na wa nje kama vile hali mbaya ya hewa, usimamizi mbovu wa mfumo wa vocha za malipo kwa wakulima na hali mbaya ya uchumi ulimwenguni mwaka 2008 ambayo ilisabaisha bei ya pamba duniani kuwa chini pamoja na kuvurugika kwa uzalishaji wa ndani.


  Wakili wa kampuni ya uwakili ya Matata ya Mwanza, Chama Matata anayewatetea baadhi ya wanunuzi wanaosafirisha pamba nje alisema suala hilo lilifikishwa LCA sababu mamlaka yake na hukumu ndiyo pekee zinazotambuliwa na mikataba hiyo.


  Ingawa Sheria Nambari 225 ya LCA haitambui kushindwa kutekelezwa kwa mkataba kwa visingizio mbalimbali vikiwamo majanga ya asili, hiyo ina maana kuwa mzigo wote wa lawama unawaangukia wanunuzi suala lililowaingiza wanunuzi hao katika matata.


  Mbowe ajibu tuhuma za ukabila

  Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa hakuna chama cha siasa kinachoweza kutawala kwa dini moja Tanzania hivyo CCM kiache kuwadanganya wananchi kuwa viko vyama vya udini na ukabila nchini.

  Akihutubia wananchi wa Tunduru katika Uwanja wa Baraza la Iddi, Mbowe alisema kuwa CCM na CUF vimekuwa vikihubiri kuwa Chadema ni chama cha kidini na kikabila kitu ambacho hakimo na wabunge wa chama hicho wanadhihirisha hilo.


  Mbowe alisema kuwa vyama hivyo vinataka kuwagawa wananchi kwa udini na ukabila wakati wananchi wote ni wamoja na wanachohitaji ni maendeleo.


  "Msidanganywe ndugu zangu. Tunachotaka ni maendeleo, inashangaza kiongozi mkubwa anatoka na kusema kuwa Chadema ni chama cha Wachaga, hakuna kitu kama hicho kwa kuwa haitatokea nchi ikatawalika kwa kabila moja na dini moja," alisema Mbowe.


  Alisema kuwa inashangaza kuona kuwa wananchi wanalishwa sumu ya udini na ukabila na kusahau matatizo yao wakati hao wanaotoa sumu hiyo maisha yao ni bora na watoto wao wanakula vizuri na kusoma kwa raha.


  Mbowe alisema Mkoa wa Ruvuma ambao Tunduru imo, wanawachelewesha Watanzania kwenye maendeleo kwa kuendekeza ushabiki wa kisiasa, udini na ukabila kitu ambacho kinahatarisha maendeleo yao na Watanzania kwa ujumla.


  "Leo nitawaambia na muachane na tabia hiyo. Asilimia 86 ya wakazi wa Ruvuma hawajawahi kutumia umeme, amkeni mnawachelewesha wenzenu katika maendeleo ambayo yako mbele yenu," alisema Mbowe.


  Alisema Chadema kitapambana kwa kuwa CCM kimewanyima umeme, barabara, maji na maendeleo mengine kwa kufanyia kazi matumbo yao na ndugu zao."Wana-Tunduru mna shida sana. Hata watoto wenu wana hali ngumu hasa kwenye elimu, barabara na tutawasaidia kwa kupambana ndani na nje ya bunge," alisema.


  Mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere aliwaambia wananchi wa Tunduru kuwa udini ambao wamekuwa wakidanganywa nao, utawasababishia umaskini kadri siku zinavyozidi kwenda."Mimi nashangaa kwa nini mnadanganyika kiasi hiki, tuungane tupambane pamoja kufikia maendeleo kama nchi za wenzetu," alisema Nyerere.


  Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Mariam Msabaha aliwalaani viongozi wa dini wanaohubiri udini na ukabila wa vyama: "Udini, ukabila wa nini jamani? Sisi ni maskini halafu bado tunasikiliza ya hao!"
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  May 16, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,465
  Likes Received: 19,847
  Trophy Points: 280
  nimeamini ccm wapo kwa ajili ya matumbo yao tu
  na hapo kwenye red, kwa nini walimnyima hizo details? ni kinyume na sheria za nchi?
   
 3. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #3
  May 16, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,631
  Likes Received: 904
  Trophy Points: 280
  Mh. Zitto Kwanza nakupongeza kwa ushujaa wa kumkomalia Huyu Waziri wa Madeni (fedha).

  Mh Zitto, sisi watanzania wazalendo tupo nyuma yako, ila inasikitisha kuwa serikali imekunyima nyaraka muhimu. Mh Zitto, endelea kudai hizo nyaraka za majina ya makampuni yaliyopewa fedha za stimulus packages.

  Kama hawataki kutoa nyaraka, kuna ufisadi mkubwa na inabidi Waziri wa Madeni ajiuzulu.

  Huyu waziri akikataa kujiuzulu, basi inabidi serikali nzima ijiuzulu.

  Nguvu ya Umma iko nyuma yako Zitto na Viongozi wote wa CDM. Mungu awape Nguvu na Ulinzi watetezi wa Wanyonge.
   
 4. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #4
  May 16, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Sizani kama nitaweza kuvumilia mpaka uchaguzi ujao.
   
 5. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #5
  May 16, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,016
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Huwa najiuliza kama Zitto alikuwa Undercover, kama ni kweli basi kafuzu ujasusi. Kazi aliyotumwa na CDM kaimaliza. Matokeo yake ndo magamba yanaporomoka.
  Kudos Zitto!
  [​IMG]
   
 6. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #6
  May 16, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,016
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Tukutafutie mabomu ya kujitoa muhanga tuwategee magamba wakikaa NEC uondoke nao,
  You will die a National Hero, a Matyr.
   
 7. z

  zamlock JF-Expert Member

  #7
  May 16, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  yani roho inaniuma alafu akina mkama wanajikosha hapa na nape wake waende zao uko
   
 8. N

  Nonda JF-Expert Member

  #8
  May 16, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Ajilinde na alindwe.

  Wakiona anazidi "unoko" "watamkolimba", "watamsokoine" ",watammalima"au "watamchachawangwe", Tanzanian politics!

  Hivyo "vijisenti" vimewekwa kwenye akaunti iliyopo nchi ipi?

  Shamba la bibi limejaa mazao
   
 9. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #9
  May 16, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Msiumie sana maana mnafikiri Watoto wao watafungulia nini Makampuni makubwa?

  Mnafikiri watanunua nini MAJUMBA huko Majuu na kununua magari ya bei mbaya kututesa nayo mitaani?

  Kazi kwetu sasa Watanzania. Au tuache wale kama ambavyo Mavuvuzela ya Mukama yanasema hapa au tule nao sambamba.
   
 10. k

  kiloni JF-Expert Member

  #10
  May 16, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Jamani Wana chama cha magamba mliotumwa humu kataeni hili.
  Msisubiri kuja na Slaa ana vimada!/wanawake!
  Slaa analipwa fedha nyingi!
  CDM imenunua mafuso ya mbowe!
  Wake up tunamalizwa pamoja na wewe unaevaa tisheti ya kijani na kofia yake, chini ndala zimekatika! unadanganywa ovyooo!!!
  Wewe unaedanganywa kuwa Ukweli kama huu unahatarisha amani! ya matumbo ya mafisadi.
  POLENI
   
 11. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #11
  May 16, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Richmond,Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ,EPA,TANESCO,RADA, ATC n.k..Hizo ni SAMPLES tu za ufisadi wa chama tawala CCM ,JK na serikali yake hali hii ndivyo ilivyo kila sekta ya umma.HII NDIYO SIRI YA UMASIKINI WETU!!!!!MUNGU IBARIKI TANZANIA
   
 12. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #12
  May 16, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  hongera Mhe Zitto kwa kazi hiyo ya kufunua ufisadi, lakini watatoa ushirikiano kwa CAG na TAKUKURU ili ukweli uanikwe maana wengi waliolipwa kwenye stimulus package waligombea ubunge wengine walishindwa na wengine walishinda.
   
 13. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #13
  May 17, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Siku zote nasema na nitasema tena...
  UFISADI ni agenda ya kudumu................
  Kuchokonoa mafisadi ni best strategy na endelevu kwa ukombozi tunaoutaka!
   
 14. mundo

  mundo JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 200
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mh zitto komaa nalo suala hili mpaka kieleweke
   
 15. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #15
  Mar 11, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,631
  Likes Received: 904
  Trophy Points: 280
  Hizi ndo Billion 48 ndo wamekopeshwa hawa wawekezaji wa Maua Arumeru?
   
 16. J

  John W. Mlacha Verified User

  #16
  Mar 11, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  wanazifanyia nini? wanaliam maua au?
   
Loading...