Ufisadi wa Sabaya: Mwenge wakataa mradi aliosimamia, Mabaunsa wake walikuwa Wajumbe wa Kamati

Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Luteni Josephine Mwambashi amekataa kuweka jiwe la msingi kwenye kituo cha afya kilichopo wilayani Hai kwa madai kuwa ujenzi wa kituo hicho umegubikwa na rushwa...
Kufuatia hali hiyo, Kiongozi huyo wa mbio za mwenge kitaifa, ameagiza ofisi ya TAKUKURU mkoa wa Kilimanjaro wafanye uchunguzi, ili kama kuna ubadhirifu watu wote waliohusika wapewe haki yao ya kikatiba.!
 
0738-150110 ,Tunakuomba ufike huko Hai, kuangalia huo miradinwa dispensary, uliokataliwa kufunguliwa na kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru. Tunaomba majibu ya uchunguzi huo yawe wazi kwa wananchi wote ili wasikatishwe tamaa kuchangia miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao.
Ifike mahali uchoke kutetea Jambazi. Mama SSH so kwamba hana taarifa za kutosha kumpiga hili Jambazi chini. Jihadhari kutetea ujinga.
 
Mkuu, ni wazi unaonekana umekubali kwamba Sabaya ni tatizo, lakini ni kama vile unapata shida kuweka wazi, tunajua hiyo ni kwa sababu ya mapenzi kwa mwendakuzimu. Lakini umeeleweka.
Kiongozi wake wa mbio za mwenge,ameponda mradi wa huko,sasa yeye elitwege atasema nini

Ova
 
Mbowe hatasamehewa na watanzania kwa kitendo chake cha kuangushwa na konyagi alafu akaitangazia dunia amepigwa na wasiojulikana ili kumchafua mwendazake.

Uongo uongo tu
 
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Luteni Josephine Mwambashi amekataa kuweka Jiwe la Msingi kwenye Kituo cha Afya kilichopo wilayani Hai kwa madai kuwa ujenzi wa kituo hicho umegubikwa na rushwa. Awali katika hotuba ya ufunguzi ilielezwa kwamba aliyekua mkuu wa wilaya hiyo Lengai Ole Sabaya ndiye aliunda kamati ya kukusanya fedha kutoka kwa wadau mbalimbali ili kufanikisha ujenzi wa kituo hicho.

Sabaya aliviagiza vyama vya ushirika wilayani Hai vichangie jumala ya TZS 600M ambapo katika hatua ya awali viliweza kuchangia TZS 338M na kuahidi kuendelea kuchanga kadri ujenzi unavyoendelea. Wadau wengine wakiwemo wafanyabiashara na wawekezaji walichangia jumla ya TZS 169M.

Sabaya aliunda kamati ya fedha ambayo ilimjumuisha yeye kama Mwenyekiti, mabaunsa wake wawili kama wajumbe, na watu wengine wawili ambao si watumishi wa umma. Kamati hiyo ndiyo iliyohusika na kutoa pesa kwenye akaunti ya ujenzi wa kituo hicho. Hii ni kinyume na sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2011 ambayo inataka pawepo na watumishi wa umma katika kamati hiyo.

Hadi sasa zaidi ya 369M zimeshatumika lakini hakuna maandishi yoyote yanayoonesha fedha zilitokaje bank na zilitumikaje. Pia hakuna nyaraka yoyote inayoonesha "signatories" wa kutoa fedha hizo kati ya wajumbe watano wa kamati hiyo.

Hata vyama vya ushirika ambavyo ni wadau wakubwa katika mradi huo hawakushirikishwa kwenye kamati ya fedha ili kujua fedha zao zimetumikaje. "Waliambiwa wachangie na walipomaliza kuchangia, hawakuhusishwa kwenye kamati iliyoratibu ujenzi, hivyo hawajui fedha walizochangia zimetumikaje" amesema Luteni Mwambashi.

Kufuatia hali hiyo, Kiongozi huyo wa mbio za mwenge kitaifa, ameagiza ofisi ya TAKUKURU mkoa wa Kilimanjaro wafanye uchunguzi, ili kama kuna ubadhirifu watu wote waliohusika wapewe haki yao ya kikatiba.!

Credit: Malisa GJ

My Take
Wafuasi mna kazi kubwa ya kutetea jizi
Duh hii kesi ingine na Itakuwa ya kwanza serikali kumshtaki
 
Back
Top Bottom