Ufisadi wa kutisha serikalini: Bakwata, masheikh, makanisa, maaskofu - kauli zenu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi wa kutisha serikalini: Bakwata, masheikh, makanisa, maaskofu - kauli zenu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dudus, Apr 23, 2012.

 1. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,770
  Likes Received: 6,103
  Trophy Points: 280
  Suala la ubadhirifu serikalini lilipofikia na kwa jinsi Serikali inavyolichukulia linahitaji sasa kuvuka mipaka ya kisiasa. Si suala la CHADEMA, NCCR, CUF, TLP, UDP peke yao - ni suala pana zaidi. Linatakiwa kuhusisha makundi mbali mbali ya kijamii na kiimani ili kuwa na nguvu za pamoja za kupigana nalo.

  Ninategemea kusikia BAKWATA wakikemea kwa nguvu zote kupitia misikiti yote nchini. Ninategemea Sunni wote, Bohora wote, Shia wote, n.k. wafungulie vipaza sauti vya misikiti yao bila hofu kukemea uovu huu.

  Ninategemea makanisa yote - Katoliki, Lutheran, Anglican, Walokole wote kuanzia maaskofu wao, wachungaji kwa wainjilisti wakemee na hata ikibidi kupiga mayowe kukemea wizi huu uliotamalaki.

  Ninategemea asasi zote za kiraia, vyombo vya habari (of course baadhi) vikemee ushenzi huu badala ya kuviachia vyama vya siasa peke yao.

  Suala la wizi (wanaofanya watendaji serikalini) sio suala la kisiasa ni jinai na inapaswa kukemewa na wote bila kujali itikadi, imani, au mlengo wa kisiasa unless unafaidika na uchafu huo. Vinginevyo ni usaliti na unafiki wa hali ya juu kukubali kutumiwa na wanasiasa nyakati za uchaguzi kwa manufaa binafsi au ya kichama badala ya maslahi ya taifa.

  Kardinali Pengo, Sheikh Mkuu bin Simba, Askofu Malasusa, Askofu Mokiwa, Sheikh Ponda, Sheikh Bassaleh, Askofu Gamanywa, Askofu Mwingira, masheikh wote, maaskofu na wachungaji wote, watanzania na waumini wenu tunasubiri kauli zenu!
   
 2. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Hapo usiwahesabie UDP na BAKWATA katika kukemea suala lolote la ufisadi. After all huu ni upepo tu utapita na wabongo watasahau kama epa, richmond, meremeta nk
   
 3. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,770
  Likes Received: 6,103
  Trophy Points: 280
  Mkuu kosa alilowahi kufanya kiongozi mmoja ndani ya taasisi fulani isiwe kosa la wote au la taasisi nzima. Naamini UDP na BAKWATA kuna viongozi wengi sana wachukia rushwa na ufisadi kama ilivyo kwa taasisi nyingine kama makanisa n.k. Vivyo hivyo wasaliti wachache wako kila mahali mkuu na hawatakaa waishe hadi ukamilifu wa dahari. La msingi ni nguvu ya pamoja ya wenye haki ambao ndio wengi.
   
 4. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #4
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono hoja!!

  It's either they speak now,or never!!!
   
 5. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,770
  Likes Received: 6,103
  Trophy Points: 280

  Exactly! Hata mimi nitawashangaa viongozi wa dini kama hawatakemea na kulaani tena kwa sauti pana wizi na ufujaji huu wa kutisha wa mali ya umma. Hili ni muhimu kuliko kuja kuzungumza nyakati za kampeni na uchaguzi.
   
 6. kalagabaho

  kalagabaho JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,292
  Likes Received: 2,113
  Trophy Points: 280
  WW assemblies of God mambo ya bakwata yanakuhusu nini?
   
 7. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Waislamu wana swala Jangwani ijumaa wiki hii ya kulaani wabunge ambao wamekataa kusaini ishu ya kutokuwa na imani na Pinda
   
 8. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #8
  Apr 23, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,770
  Likes Received: 6,103
  Trophy Points: 280

  Great! Hayo ndio mambo ya kulaani, masula mazito yanoyoligusa taifa zima. Taasisi nyingine nazo zifanye vivyo hivyo - ibada, kwa wasomi - makongamano na mihadhara, na kwa wanasiasa - maandamano na mikutano ya umma. Kwa pamoja tunaweza kutokomeza ufisadi serikalini.
   
 9. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,198
  Likes Received: 10,539
  Trophy Points: 280
  Ijumaa kuna dua itasomwa pale jangwani na Waislam kwa hiyo ni vyema ukajoengea hapo siku ikifika
   
 10. n

  ngozimbili JF-Expert Member

  #10
  Apr 23, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 824
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 60
  bakwata ndo walimu wa ufisadi wanauza viwanja kama hawana akili nzuri na wanalindwa na dola.hata kama watauza mara mbili kiwanja kimoja suala la bakwata kukemea ufisadi liondoeni
   
 11. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #11
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,011
  Trophy Points: 280
  Mimi binafsi kwa kuwa nimeushuhudia uovu wa wale waliopewa dhamana ya kutuongoza dhidi ya wanyonge, sitaacha kuiomba zaburi ya 58 juu ya watawala wa taifa hili mpaka Mungu atakapoiachilia haki ya mwenye haki. Watu wote wenye mapenzi mema nao wajuao jinsi nafsi iliyodhulumiwa haki ya kuishi na kunyang'anywa fursa ya ushiriki tunu ya taifa inavyotaabika, basi naomba popote pale mlipo msiache kuiomba zaburi hii dhidi ya utawala wa Tanzania uliopoteza uhalali wa kuisimamia hazina ya nchi. Bwana ni mwema hakika kwa wakati muafaka atatujibu. Na huo wakati ni sasa; saa ya ukombozi ni sasa!
  .
   
 12. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #12
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Msichanganye DINI na SIASA
   
 13. Highlander

  Highlander JF-Expert Member

  #13
  Apr 23, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135


  Angalizo: Umejenga hoja vizuri mkuu. Unadhani credibility ya maneno yako ingekuwa kubwa kiasi gani kama ungetumia jina lako halisi humu, badala ya pen name? Je, unaweza kubaliana na mimi kwamba matumizi ya majina feki katika hili jamvi maarufu sana yanapunguza (au kuzimua kwa kiasi kikubwa) uzito wa hoja makini na muhimu kama hii ya kwako katika forum hii?
   
 14. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #14
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,770
  Likes Received: 6,103
  Trophy Points: 280
  Mkuu wangu, kwanza mimi sina na wala sitegemei kuwa na umaarufu wowote; mimi ni mwananchi wa kawaida tu nisiyefahamika katika jamii - namshukuru sana Mungu kwa ajili hiyo. Hivyo basi kama ningetumia jina langu halisi badala ya "pen name" kusingebadili au kusaidia lolote.
   
 15. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #15
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,770
  Likes Received: 6,103
  Trophy Points: 280
  Dini isiyokemea maovu na badala yake kuyanyamazia sio dini.
   
 16. Innobwoy

  Innobwoy JF-Expert Member

  #16
  Apr 24, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 980
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 60
  Siasa imeathiri mfumo mzima wa Dini watu wameacha kuhudhuria kwenye nyumba za ibada kwa sababu wako busy kutafuta mkate wa kila siku ambao haupatikani,,,:shut-mouth:
   
 17. I

  Isiri Member

  #17
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
   
 18. K

  Kimbito nyama Senior Member

  #18
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 157
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika viongozi wa dini/ madhehebu yaliyotajwa usitegemee kumsikia Lusekelo, kwani yeye ni mtu anayejifanya yuko karibu na serikali ili isitambue madhambi yake. Wakati mwingine anashiriki mikutano ya JK na Wazee wa DSM.Na akiona serikali inamwelekeo fulani nae huwa anelekea hukohuko.Sijui anachofaidi zaidi ya kuwadanganya waumini na moto wa uongo.
   
 19. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #19
  Apr 24, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,770
  Likes Received: 6,103
  Trophy Points: 280
  Mkuu umeeleza mambo mazuri na kwa uhalisia. Nafasi ya dini na taasisi zake kwa taifa letu ni ipi? Umuhimu wa dini ni nini? Nijuavyo, la kwanza na la msingi ni KUKEMEA UOVU kwa nguvu zote bila kujali aliyeutenda uovu huo ni nani au ana nafasi gani katika jamii.

  Hata kama kiongozi wa dini aliwahi kula, kunywa, au kuwa na urafiki na kiongozi fulani wa kisiasa hapo kabla; bila kujali kiongozi huyo (wa kisiasa) alisaidia au kutoa msaada gani kwa taasisi; kiongozi yule wa kisiasa anapokengeuka au kugeukia UCHAFU ni wajibu wa kiongozi wa dini kuonya na kukemea. Kwenye "Job Descriptions" zao, hili ndilo namba moja!

  Hata hivyo, ni kweli kwenye taasisi za kidini pia kuna mafisadi wachache ila isiwe ndio kigezo cha kwamba taasisi nzima imeoza na hakuna msafi - NO!

  Ujumbe muhimu kwa viongozi wa dini: WAKISHINDWA KUKEMEA HILI WANYAMAZE MILELE NA WASITULETEE UPUUZI NYAKATI ZA UCHAGUZI.
   
 20. m

  mweleka Member

  #20
  Apr 24, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  tuatakukumbuka CCM ukitutoaka kwa yako uliyoyafanya japo nitaje machache
  wizi wa rasilimali za nchi yetu.
  kutupigavirungu tunapodai haki zetu
  kutuibia kura zetu tunapochagua viongozi wetu
  kututambulisha kama ombaomba nje ya nchi
   
Loading...